UTAMU WA KULA KUKU NA MAYAI YAKE SEHEMU YA 19 - 20
ENDELEA.......
Madame Yustar alitoa amri mimba itolewe ili kuepusha laana kwenye ukoo wao.
"Hapana siwezi kutoa mimba hata iweje" Mellisa alimvimbia mama yake. Saa ngapi asilukiwe akaanza kutembezewa kichapo.
Nae hakukubali apigwe kilahisi, walijikuta mama na mtoto wanapigana mie nilikuwa nimesimama pembeni nawaangalia yaani najionea maajabu haya yaani mama na mtoto wanapigana kisa mwanaume.
"Nakwambia lazima utoe hiyo mimba labda kama mimi sio mama yako" Madame Yustar akiendelea kuongea huku anamshushia kipigo mwanae na Mellisa nae hakukubali alikuwa anajitutumua kumludishia mashambulizi mama yake japo ilikuwa ngumu kwake kwasababu mama yake alimzidi nguvu.
Niliingilia ugomvi kuwaamulia, waliachiana kila mmoja alikuwa mwenye hasira kali sana.
"Mimi ndiye chanzo cha huu ugomvi. Nimeamua kuondoka kwenye maisha yenu, naombeni mnisamehe ila sisi wote tuna makosa. Madame wewe ndiye ulilazimisha kuwa na mahusiano na mimi kwankunitishia nisipokubali basi utanifukuza kazi.
"Hivyo hivyo hata kwa Mellisa ulinitishia pia. Mimi ni mtoto wa masikini niliyekuwa nimekata tamaa na maisha. Sehemu yenye unafuu wa maisha ndipo nilikutana na vikwazo vyenu. Niliamua kukubali yote kwasababu ya maisha na sio tamaa za kimwili. Kiukweli nyie wote wawili sijawai kuwapenda, ila keasababu mlilazimisha ilibidi nikubali tu" Niliongea hayo.
"Leo unaongea nini?, unamuogopa mama kusema kweli kama unanipenda. Hivi unajua ukweli umuweka mtu huru?"
"Ukweli wangu ndo huo. Naweza kuondoka muda huu nikapambane na life kwengine"
Wote walianza kulia. Aiseee hawa watu walikuwa na kichaa cha mapenzi. Nilishangazwa na namna walivyokuwa wanalia.
Kila mtu alisema ananipenda na hayupo tayari kunipoteza. Nilijuta hata kwanini nilikubali kujiingiza kwenye huu mkenge nilitamani siku ziludi nyuma niwakatae wote wawili ila ndo hivyo jambo lishatokea.
Madame alitoka chumbani kwa mwanae tulibaki mimi na Melissa.
"Leo nakupenda usinikatili namna hii. Baki na mimi mwenye kiumbe chako. Kwanza uliwezaje kutembea na mama mbona ni sawa na mama yako mzazi jamani?"
"Wote mlilazimisha mapenzi kwangu, ningefanyaje na mimi nilikuwa sina kitu na nyuma yangu nins familia inayonitegemea nitafute niwapelekee chochote kitu. Mellisa labda nikwambie ukweli tu ambao sikutamani muujue wote wawili wewe na mama yako.
"Ukweli gani huo unaotaka kumwambia na ambao ulituficha wote?" Madame Yustar aliingia chumbani tena huku akinitwanga na swali.
"Nitasema Leo"
"Hebu kwanza njooni sebleni" Madame akituambie twende sebleni. Tulikaa hapo sebleni huku ukimya ukitawala.
"Leo zungumza chochote ili nikuelewe na naweza nikakuacha uendelee na maisha yako kama nitakuelewa tofauti na hivyo utaendelea kuwa mtumwa kwenye nyumba hii na hakuna sehemu unaweza kunitoroka"
"Haina haja ya kuniwekea vizuizi tena. Kwa namna yoyote ile siwezi kuishi nanyi tena"
"Ukiwa na maana?" Madame Yustar aliniuliza.
"Ninaondoka leo hii"
"Hautatoka hapa bila ridhaa yangu"
"Hauwezi kunilazimisha niendelee kukupenda. Moyoni mwangu yupo mwanamke mmoja tu ninayempenda ambaye ni mama hinaya mke wangy"
"Una mke?" Melissa aliuliza kwa mshangao, mama yake nae alinitazama kwa viulizo.
"Ndiyo nina mke tena wa ndoa kabisa"
"Ya kweli hayo leo?" Madame aliniuliza.
"Huo ndo ukweli"
Madame alifoka kwanini nilimdanganya siku zote mpaka kuzama mazima moyoni mwangu. Mellisa na alipaniki wote walijikuta wanalia tena kwa uchungu.
Mellisa alienda chumbani kwake. Huko alijifungia ndani alilia sanaaa. Mie sikuwa na sababu ya kuendelea kubaki. Niliingia chumbani kwangu nilifungasha vitu vyangu huyo nikatoka.
"Hapa ukikuja ukiwa huna kitu na unatakiwa kuondoka kama ulivyokuja" Madame bakinikazia.
Sikumpinga niliachia begi na uzuri hakukuwa na kitu cha maana zaidi ya nguo na viatu tu. Pesa zangu zote nilikuwa naweka kwenye accont ya bank na nyengine nilikuwa namtumia mke wangu. Nilinyangamywa mpaka simu ila sikujali kwasababu mimi sio masikini tena kama walivyodhania.
Madame alijiaminisha naweza kukubali kuendelea kuwa mpenzi wake kwasababh mimi ni masikini nisiye na akili kumbe mwenzie nishajipata muda mrefu nina nyumba nzuri na biashara bado account yangu inasoka.
Alininyang'anya mpaka simu ili tu aniwekee vikwazo ila alifeli niliondoka. Huo ndo wakati wangu wa kutulia na familia yangu sasa. Kabda ya kufika kwangu nilipitia kanisani.
Nikienda kanisani kwaajili ya kufanya toba. Nilimueleza mchungaji yote wala sikumficha. Mchungaji aliniongoza sala ya toba. Baada ya kutubu nilijihisi nipo huru sasa kimwili na hata kiroho.
Nilipitia bank kutoa pesa baada ya hapo nilienda kufanya shopping kwaajili yangu na familia yangu kwa ujumla.
Huko shopping nilikutana na Madame Zuri. Alianza nae ujinga. Niliamini hili ni jaribu ambalo MUNGU amelileta mbele yangu baada ya kufanya toba.
Madame Zuri alifanya mbwembwe za kila aina ila nilimkataa, pesa sijui nini. Yaani slifanya jitihada zote ili nimkubali nikalale nae ila nilikataa kata kata.
Baada ya kukutana na Madame Zuri ndipo nilikumbuka kuhusu afya yangu.
"Nisije nikampelekea mke wangu maradhi. Inabidi niende hospitali kupika ukimwi kwanza"
Nilienda hospitali kujua hali ya afya yangu, namshukuru MUNGU nilikuwa salamaπ₯Ήπ.
Niliondoka mpaka mwangu. Ujio wangu wa gafla ulimshamgaza mke wangu ila kwa furaha alinipokea kwa bashasha.
"Sitokaa mbali nanyi tena. Nakupenda sana my wife. Wewe ndo mwanamke wa maisha yangu, mwanamke ambaye ni kipaumbele changu, mwanamke wa ndoto zangu, mama watoto wangu. Tambua haupo na mimi mwilini tu bali mpaka moyo wangu umeutawala wewe" Niliongea hayo kwa hisia mke wangu alinikumbatia kwa nguvu.
Kiukweli tunapendana sana na mke wangu. Mwanamke aliyenivumilia nyakati za shida na maangaiko. Kuna wakati tulilala njaa kwa kukosa chakula ila sikuwai kusikia wala kuhisi amenisaliti.
Upande wa Mellisa baada ya kuchoka kulia sasa alitoka chumbani kwake alienda chumbani kwa mama yake alimkuta mama yake anakunywa pombe.
"Mama nipo tayari kutoa mimba" Alizungumza akiea serious kabisa. Mama yake alifurahishwa na maneno ya mwanae. Aliamini kama Melissa atagoma kutoa mimba na akazaa basi itaendelea kuwa laana ya kizazi na kizazi. Mama na mtoto walisamehana kiroho safi.
"Ila nina ombi moja" Mellisa alimwambia mama yake.
"Ombi gani?, niambie binti yangu"
"Baada ya kutoa mimba sihitaji kuendelea kuwepo hapa nchini. Nahitaji kuendelea na masomo nje ya nchi"
"Hilo tu. Limepita mwanangu" kabda Usiku haujawa mkubwa walifanya mchakato wa kutafuta dawa ya kutoa mimba changa"
Mellisa alifanikiwa kuharibu mimba na baada ya hapo aliondoka nchini.
Upande wangu na familia uangu maisha yaliendelea vizuri biashara yangu ilizidi kukuwa nilifaniliwa kufungua duka lengine la spea, nilinunua gari, Hakika leo nimekuwa Leo na sio jana tena.
Madame Yustar ananitafuta sana ili tuendelee na mapenzi yetu ya siri ila hajawai kufamikiwa kunipata. Alishaenda mpaka pale nilipokuwa nakaa awali kwenye chumba cha kuoanga cha giza ila hakufanikiwa kunipata mpaka leo hii na laini ya simu nilibadili.......Huu ndo UTAMU WA KULA KUKU NA MAYAI YAKE. Nimefanikiwa japo nikichezewa sana uwanaume wanguπ₯Ήπ₯Ήπ₯Ήπππ.
Natarajia kuitwa baba wawili, kwa sasa mke wangu ni mjamzito. Yes kila siku namuambiaga MUNGU hakika njia zako hazichunguziki japo nilikukosea ila nilikumbuka toba na kwakuwa wewe ni MUNGU wa rehema ukanisamehe BABA. Endelea kuyagusa maisha yangu, endelea kuigusa familia yangu, mke wangu na watoto wangu.
............MWISHO............
IMEANDIKWA NA MTUNZI NURU HALISI..........
ASANTENI WOTE MLIOFUATILIA MKASA HUU WA KUSISIMUA MWANZO MPAKA MWISHO. MUNGU BABA AZIDI KUWABARIKI SANA β€οΈπππ.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni