UTAMU WA KULA KUKU NA MAYAI YAKE SEHEMU YA 17 - 18
ENDELEA.........
Mipango yangu iliendelea kwenda vizuri. Nilifanikiwa kufungua duka langu la spea za magari mke wangu alikuwa nsimamizi mzuri. Japo hakuwa na elimu ila alikuwa na akili ya biashara sana na ni mwanamke mwenge uchungu wa pesa.
Basi asubuhi moja tukiwa mezani kwaajili ya kifungua kinywa. Ilikuwa chai ya maziwa, mkate na mayai ya kukaanga.
Gafla Mellisa alijisikia kichefu chefu. Alikimbilia jikoni kwenye sink la vyombo alianza kutapika.
"Ana nini huyu?" Mama yake aliuliza. Wote hatukuwa na majibu, nilipata hofu moyoni nilihisi labda Mellisa nibmjamzito.
"Mama yake alimfuata jikoni alimkuta bado anatapika. Alisimama pembeni yake. Alipomaliza kutapika swali la kwanza alimuuliza.
" Mellisa una mimba?"
Mellisa mwenyewe alishtuka kwanza.
"Unashangaa nini sasa. Nakuuliza una mimba?"
"Sijui mama"
"Okay, najua huwezi kuendelea kunywa chai maana ndiyo sababu ya wewe kujisikia kichefu chefu. Nenda chumbani kwako kapumzike nakuja muda si mrefu"
Mellisa alienda chumbani kupumzika, mama yake alitoka nje ya nyumba hatukujua ameelekea wapi.
"Inaweza kuwa ni mjamzito" Misha aliniambia tukiwa mezani tunakunywa chai. Hofu ilizidi kunitanda.
Madame aliludi na moja kwa moja alienda chumbani kwa binti yake.
"Shika hiki kipimo kapime mimba" Alimkabidhi Mellisa kipimo. Melisa alienda chooni baada ya muda akitoka akiwa na kipimo mkononi, alimkabidhi mama yake.
"Unaweza kuniambia hiyo mimba ni ya nani?" Mama yake alimuuliza. Mellisa alikaa mimya kama vile hajasikia.
"Leo kama utasubutu kujifanya kiburi nitakupiga kipigo cha mbwa koko, sikumbuki kama nimewai kukupiga ila leo nitakuzibua haswaaa! Niambie muhusika wa hiyo mimba.
"Mama nakwambia ukweli ila naomba umsamehe pia yeye hana kosa mwenye makosa ni mimi. Nampenda sana mama yangu" Melissa aliongea hayo huku analia.
"Sawa niambie ni ya nani?"
"Muhusika wa hii mimba ni Leo" Mellisa aliongea kwa sauti ya chini.
"Umesema ya nani?"
"Ya Leo mama"
"Leo Huyu wangu au Leo gani?" Mama yake aliuliza kwa uoga.
"Ndiyo Leo huyu mfanya kazi wetu"
"Uwiiiiiii! Nimekwisha mimi" Mama mtu alishika kichwa na kukaa chini kabisa.
"Mama naomba usimdhuru nampenda sana Leo nipo tayari kuwa mke wake.
"Mb...wa wewe unaongea ujinga gani. Unawezaje kushare du...du na mama yako"
"Sijakuelewa?" Mellisa aliuliza kwa mshangao.
"Hujaelewa nini. Hivi Mellisa muda wote tulioishi na Leo humu ndani kusoma hujui hata picha huoni, yaani wewe huyo nae umelikalia du....du la Leo mpaka mimba umebeba?, Uwiiiii! Aibu gani hii"
Basi ni vilio tu vilitawala humo chumbani. Ilibidi mimi na Misha tuwafuate huko chumbani ili kujua shida nini.
Ile naingia tu Madame Yustar alinikwida kisawa sawa. Alinitukana matusi kama yote huku ananishushia vibao vya maana.
Sikuwa na namna zaidi ya kuwa mpole tu.
"Unaweza kutembea na binti yangu mpaka kumbebesha mimba mimi sikutosh" Misha alibaki mdomo wazi.
"Mama Leo hana kosa. Mwenye makosa ni mimi, mimi ndiye niliyempenda kabda yake na nilimlaximisha kuwa na mimi kwa kumtishia nitamchongea afukuzwe kazi. Nampenda sana Leo tafadhali usimoige" Mellisa aliongea hayo huku akiwa analia.
Mama yake aliishiwa pawa. Alikaa chini kwa mala nyengine alianza kulia, alilia sana na hakuna aliyemsogelea kumbembeleza.
Baada ya kunyamaza alimwambia Misha atoke anataka maxungumzo ya watu watatu tu. Misha alitoka.
"Umesema wewe ndiye mwenye makosa maana ulimpa vitisho Leo yaani ulitumia ubabe ili akupende si ndiyo?" Madame alimuuliza mwanae. Mellisa hakujibu zaidi ya kuinamisha kichwa chini.
"Okay basi ni hivi, hiyo mimba itolewe tena kwa haraka leo hii hii kabda jua halijazama. Siwezi kuifuga hii laana mimi" Madame aliongea hayo kwa kumaanisha.........
ITAENDELEA...........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni