UTAMU WA KULA KUKU NA MAYAI YAKE SEHEMU YA 12
ENDELEA.........
Madame aliwapa taarifa Mellisa na Misha kuwa mimi sio mlinzi tena bali ni mfanya kazi wake kwenye biashara zake.
Rasmi niliajiliwa kusimamia duka kubwa la spea. Huko ndo kulikuwa na pesa kama zote. Licha ya kulipwa vizuri ila nilikuwa napata hongo kibao. Kama masihara ndani ya miezi mnne tu mimi na mke wangu tulikamilisha ujenzi wa nyumba yetu.
Haikuwa nyumba kubwa sana ila tulijenga kisasa zaidi.
Niliendelea kula kuku na mayai yake kwa siri sana huku kila mmoja akiniongo. Mellisa alikuwa ananionga pesa balaaa. Anaomba pesa kwa mama yake akipewa ananipa mimi. Mama mtu mwenyewe alikuwa ananipa sana pesa.
Niliishi nao kwa akili sana ili niuage umasikini. Kila mtu militenga nae muda wa kumlidhisha pasipo wao wenyewe kujua hilo.
Weekend moja madame Yustar aliniomba nitoke nae party ya rafiki yake. Mavazi yangu yalikuwa ya kitajiri balaaa, yaani siku hiyo niliwaka sio pouwa unaweza kusema tajiri flani hivi.
"Kwanini mama anajali sana kuhusu Leo mpaka imepitiliza sasa" Mellisa alimuuliza Misha.
"Usimuwekee mashaka mama yako japo kuna muda hata mimi nashindwa kuelewa ila tambua tu mama yako ni mtu mzuri, ana roho ya kipekeee. Ona muonekano wangu na wako.
"Kwa mtu mgeni kufika hapa kwenu hawezi dhaniaka kama mimi ni dada wa kazi kwaiyo usishangae hata kwa Leo"
"Nimekuelewa lakini hali hii ya kutoka wote mpaka kwenye party ni jambo la kushangaza. Kwanini asingeenda na mimi?"
"Yule ni mwanaume anajua namna gani ya kum care mama, kama angeenda na wewe asingekuwa na uhuru maana muda wote angekuwa anakulinda wewe"
"Ila ni kweli na anavyopenda kunichunga sasa kama vile mtoto mdogo"
"Hahahaaaa! Mtoto kwa mama akui"
Tulifika huko kwenye party ilikuwa nilibaki mdomo wazi. Yaani party ilikuwa ya mishangazi ya mjini. Yaani umri umeenda ila matendo yamesimama unaweza kusema watoto wa mwaka 2000.
Mashangazi wote walikuwa wamekamatia vibenteni wao, nilikutana na vijana wenzangu kama mimi eti ndo waume zao.
Vyakula pombe vilikuwa kibao. Madame Yustar alinitambulisha mimi kama mume wake, macho ya mashoga zake yaliwatoka.
"Ni kijana mzuri na anavutia" mmoja wa mshangazi alizungumza hayo.
"Sitaki mapapa kwenye penzi langu" Madame Yustar alizungumza kwa makasiriko kuwakanya mashoga zake wasije kupita na mimi na ushoka utavunjika.
"Kwanza ulimpata wapi huyu ni kijana mzuri sana na anaonekana ana nguvu sana kitandani,"
"Mpaka mnauona uzuri wake na nguvu zake mjue nimemwaga pesa nyingi sana kwaajili yake. Leo unaweza kujichqnganya kwa vijana wenzio mkabadilishana mawazo"
Niliondoka niliwaacha wanaendelea kunijadili. Nilijichanganya kwa vijana wenzangu wawili yulianza kupiga story za hapa na pale huku wenzangu wakinisifia kuwa nimepata mshangazi mzuri mwenye mvuto utasema kitoto cha 2000. Eti kama wangekuwa ni wao hata kuloga wangeloga maaana madame Yustar hana tofauti wa watoto wa 2000 labda umri tu.
Ni kweli wasemacho. Madame Yustar ni mwanamama mzuri, sura ngozi, shepu, miguu ya bia nywele ndefu unaweza kumfananisha na mwanamama mmoja hivi wa jua kali jina namuhifadhi.........
ITAENDELEA.............
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni