MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 14
SONGA NAYO....
Niliwaona mama na baba yangu wakiwa wanamshangaa sana yani walishangaa mpaka wakanisahau mtoto wao kama naumwa π
Basi mimi niipomuona Anfrey nilinyanyuka na kwenda kumkumbatia
" Nasrat wangu, yupo wapi mtoto wangu..??"
Nilimuuliza pale tu nilipojitoa kwenye kifua chake, upande wa wazazi wangu walikuwa hawaelewi chochote kilichokuwa kinaendelea hapo.
"Mtoto wako yupo kwenye hospital nyingine tofauti na hapa, maana kule yupo chini ya uangalizi mkubwa sana maana hali yake sio nzuri .."
"Sawa naweza kwenda kumuona..??"
"Kwa sasa hali yako sio nzuri ndio kwanza umeamka, unajua toka uzimie kule Oman ni week mbili sasa yani tumekusafirisha ukiwa hujitambui kabisa..."
Habari hizo nilikuwa ngeni kwangu, nilijua tu hakuna uwezekano wa kumuona Nasrat tena ikiwa kama nipo Tanzania na Mtoto yupo Oman nitafanya nini mimi eeeh
Nilipiga magoti chini na kukusanya mikono kwa pamoja kisha nikasema
"Ee mungu, ikiwa umeandika apitie kikombe hiki cha maumivu , ninakuomba bwana umuepushie mabaya yote yaliyo mbele yake na hata yajayo
Nakuomba bwana muinue yule malaika wako, muondoe katik roho ya umauti ambayo anaipitia kwa wakati huu najua bwana unaweza na hakuna jambo lolote lile lisiloshindikana kwako
Pleas Lord, ππ"
Niliomba sana mpaka mama akaja kuniinua lakini sikuacha kusali nikimuombea Nasrat, muda ulienda nikiwa sina furaha amani wala utulivu
Nilikuwa situlii kabisa mule wodini, na siku hiyo ikapita kwa mbinde sana hata usiku sikupata kabisa usingizi, kesho yake majira ya saa nne Anfrey alirudi akiwa ameongozana na swatii
Sikuwa mwenye amani kabisa ndani ya moyo wangu, basi nikasalimiana nao pale ki kavu tu huku moyo wangu ukiwa na hamu ya kuwauliza habari za Nasrat
"Mira, unatakiwa kunywa chai harafu twende ukamuone mwanao.."
Nilitabasamu, basi chai ikaletwa nilikunywa haraka haraka vitafunwa nilikuwa navitafuna mara moja au mbili kisha nameza yani chapu chap nikawa nimemaliza π π
Anfrey na swatii wakabaki wananishangaa tu, me sikujali nilichokuwa nawaza kwa muda huo ni mtoto tu basi hayo mengine hata hayanihusu kabisa.
Basi hawakuwa na muda wa kupoteza tuliingia kwenye gari, na safari ya kuelekea kumuona mtoto ilianza, safari niliiona ndefu sana basi tuliweza kufika
Kwa kuwa akili yangu haikuwa sawa sikuweza kutambua sehemu tulipokuwa, baada ya gari kusimama nilikuwa wa kwanza kushuka kwenye gari
Nilitembea kama vile me ndio mwenyeji yani nilikuwa sijielewi kabisa, ikabidi Anfrey na swatii waongeze mwendo wa kunikimbilia π
"Mira hapa kuna itaratibu wake mama, so tafadhali sana kuwa makini tu usije kuleta vurugu.."
Anfrey alizungumza nikajibu tu sawa kisha tukaendelea na safari yetu, tulifika mapokezi tukaelekezwa vizuri tu huku kwa upande wangu nikijitahidi kutulia
Tulifuata maagizo yote ya mdada wa mapokezi kisha tukaondoka, chumba alichokuwa mtoto kilikuwa ni ghorfa ya tatu so tulitumia lift kufika huko
Kweli bana tulifika mpaka chumba alichokuwemo mtoto, nyie niliumia zaidi baada ya kumuona binti yangu akiwa bado hajazinduka na kibaya zaidi kitovu chake kilikuwa kimevimba na kutoa usaa ni vile tu walikuwa wanamsafisha kila muda π₯Ή
Nilisogea na kuanza kumshika nywele zake huku nalia dah, yani kama ikitokea nikagundua ambaye amefanya hivi walah nitahakikisha na yeye anapitia maumivu ambayo anapitia huyu Malaika
Hata kama nitakuwa nimemkosea mungu kiiasi gani ila kwa hili niseme tu samahani yani siwezi kuvumilia kumuacha huyo mtu aishi kwa amani na ikiwa binti yangu anapambania uhai
Nitamtenda kitu kibaya ambacho atakaa akijutia maisha yake yote, nilikuwa nampapasa mtoto ila mawazo yalikuwa mbali mno, basi nilikaa mle wodini huku nikiwaomba wale wengkne watoke
Kwakuwa walikuwa wanajua mimi ndio mama mzazi wa Nasrat so hawakuwa na kipinganizi, walitoka mle wodini na kuniacha mimi na binti yangu
Nilimtazama binti yangu kisha nikapiga magoti mkono mmoja nilimuwekea Nasrat juu ya paji lake la uso harafu ule mwingine niliuinua juu ........
ITAENDELEA......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni