AFANDE MILLAN๐ Sehemu ya 28 na 29
Nikasema sikia utakaaa apa, na usiwaze kabisa kuhusu kodi, mimi nipo na sina plan za kukuacha wewe kabisaa, nakupendaa sana, nakupenda kuliko chochote zena, siwez acha kukulipia kodi ata siku moja, na apa utakaa kwa mda mfupi sana, nakuoa soon utaamia kwangu sawa zena, akanmbia sawa asante millan ni pazuri nimepapenda sana, nikasema okey ,karibu mama, basi tukaikagua sana nyumba nikiwa nae na zen alionesha kapafurhia sana pale na kapapenda , na baada ya apo nikawapeleka mpaka home kwake, kisha nikamkabizi funguo ya makazi mapya na nikamkabizi na pesa kidogo, nikamwambia kesho tu aamie makazi mapya, basi zena akanishukuru sana, mtoto wa watu, nikamwambia usijali ni ya kawaida ayoo, wewe ni mwanamke wangu, so kuwa na amani kabisa mpenzi , akanmbia sawa, apo mm ndo nikaaga kisha nikaludi kwangu
Na kesho yke niliamkia job na niliwasiliana tu na zena ,na akanmbia ameshamia makazi mapyaa, nikampa hongea na nikamwambia nikitoka kazini basi nitaenda kupaona, na kweli mm nilivyotoka kazini , nilienda kwake alipoamia sasa, mashallah, kuliko kuzuri na kumependeza sana mana alipanga vitu vyake vuzuri mnoo , basi bwanaa zikapita week 2 , nimezama kweli kweli na zenaa, yani penzi limenogaa kinoma, hizo week mbili mi nyumbani nimelala siku 3, hizo siku zengine zote nalala kwa zena, nakula kwa zena , na kuna nguo zangu nyingi tu ,nilikuwa naacha kwa zena kabisaaa, nakula utamu tenaaa, mtoto mpya mpya utanambia nini , aseee zena alikuwa na furaha sana , kwa kipindi chote, alikuwa na rahaaa mnoo, alikuwa anaonesha kunipenda na kunijali kweli kweli, aseeeee kama kuzama dada alizama, na mm kwa uo mda naenda kwa zena, mademu zangu wengine wote nikapiga chini ,ila.sasa baada ya week 2, nikawa nishamzoea namuona kawaidaaaa, na nikapunguza kwenda kwake, sikuwa naelewa nilikuaga na mdudu ama nini, ila nikishatembea na mwanamke , anapunguza kunivutia natafuta wanawake wengine
Basi ndo ikawa hivyo kwa zena , nikiwa nikitoka job sipiti kwake tena kama zamani, nanyoosha kwangu, apo visingizio kibao, mala nimebanwa sana , mala naingia shift usiku, mala.nimechoka sana kazi zilinizidia , hivyo yani, nikawa nafosi machaka mapya sasa, zena kashaliwa nafanya nini, apo zena sijawahi kumpeleka nyumbani kwangu ata siku moja na hapajui kwangu, siku iyo sasa kanipigia simu mida ya mchana, apo nna week 2 sijakanyaga kwake ,sababu kibao, mi nikapokea simu, nikasema nambie mchumba akanmbia powa , uko wapi nikasema nipo kazini zena vp, akanmbia unakuja saa ngapi uku , sijakuona mda nimekumiss, nikasema oohh zena ,leo nipo busy sana na kazi, apo bwana nilikuwa kuna demu wangu wa zamani, usiku wa hii siku nilikuwa nimepanga tukapashane nae kiporo, zena akanmbia ahaaaa sawa so hautakuja nyumbani, nikasema yaaa ,akanmbia lakini haujaja week 2 sasa kila siku ni busy tu jamani, ummy anakuulizia ,nikasema ntakuja zena mambo ni mengi ata mm nimemmis sana ummy na natamani sana kuja kumuona ila majukumu yamenizidia nielewe mama ,akanmbia basi sawa ,kisha akakata simu, yani ahaaaa , nishamtomba sana asa naenda kwake kufanya nini sasa
Basi bwana mimi sikuenda kwa uyu demu kama mwezi, namkwepa kwepa sanaaa, siku iyo zena akanitumia sms, akanmbia millan naomba leo ukutoka kazini naomba ufike,japo nishkujua kuwa ww ni mwanaume wa dizaini gani, doooh asa kama kashanijua mm ni mwanaume wa dizaini gani kwake mi naenda kufanya nn, mi nikaingalia ile sms sana ,ila nikaona ngoja tu niende nikamuoneee, basi kweli mi nilivyotoka job hii siku ndo nikapita kwa zena, basi katoto kake kakanichangamkia sanaa, yani sanaa tu, naona kalinimiss na vile sijaenda mda, ila zena wala hakuwa kanichanganmkia kabisaaaa, nikajua ayaa bwana, basi nikamsalimia zena , akaniitikia ila kiunyonge kweli kweli, nikamwambia ummy nenda chumbani niongee na mama kwanza, ummy akanyanyuka akaingia chumbani, nikamwambia zena vp mbona unanuna sasa , mi sifanyi makusidi kutokuja kwako ,ni vile nina kazi nyingi sana kazini , nakuwa nabanwa sana niamini na unielewe mama, zena akaningalia sana akanmbia una uwakika ? Nikasema yes, zena akanmbia kwaiyo upo busy mwezi mzima unashindwa kupata ata mda mdogo wa kuja kuniona si ndio
Nikasema yaaa , niko busy sana na kazi nielewe mama ,akanmbia sawa ,japo sikuamini kabisaa umechange sana millan, umekuwa mwanaume ambae sikuelewi, nisipokupigia mim simu ,we hunipigii kabisa, millan umekuwaje, unanaifanya naanza kukufikilia vibaya, na kuna mda najutia kwa kuingia katika mahusiano na wewe, why lakini baba, nikasema no unakosea , ebu nielewe tu zena ,kazi yangu kuna mda huwa inanikula sana mdaa, zena akaningalia sana akanmbia sawa , akanmbia ningoje akaingia chumbani na baada ya mda akatoka na karatasi akanitupia ,mi nikaichukua ile karatasi nikasoma, ooh yalikuwa ni majibu ya hospital ambayo yalikuwa yanaonesha zena ni mjamzito wa mwezi mmoja na siku 10, nikaona kazi ipo mtoto wa 6 anakuja, na baba bado sisomeki kabisaa, uzuri wa mm sas, mi namsikiliza mama mwenyewe anasemaje, akitaka kuzaaa fresh, akinambia anatoa poa frssh na ela ya kutolea nakupa, apa nipo mi tajeer wa watoto bwana,
Nikasema nimaona we ni majamzito sio, akasema ndio si umeona apo, nikasema yaa nimeona hongera, so wewe kama mama umeamuajee, zena akanmbia naamua nini, unazani kuna la kuamua zaidi ya kuzaa ,nikasema sawa zaa hakuna shida mi ntaudumia mimba mpaka mtoto, zena akanmbia millan ,ebu naomba basi nikupeleka nyumbani kwa ndugu zangu, ukajitambulishe na ikiwezekana unioe, nazaaje nje ya ndoa millan, nikasema ahaaaa mama tulia bwana ,aya mambo hayataki harkaa yanataka kujipnga, we lea mimba, mi najipanga, ikifikia miezi 6 basi mi nataned akwenu , zena akanmbia sawa ,ukitoka apa unaenda wapi leo, nikasema naenda kwangu, zena akanmbia sawa naomba leo twende kwako, nataka kupajua kwako, mana sasa tumeshakuwa katika hatua kubwa millan, nawezaje kubeba mimba ya mwanaume ambaye bado simjuhi vizur ata kwake tu sipajuhi , nikaona kazi ipo, nikamwambia now usiku ummy unamuacha na nani, we tulia mi ntakufata siku nyengine ata kesho , zena akanmbia hapan, leo naenda kwako, utanifata siku nyengine ni lini na unvyonambia upo busy sanaa
Alafu millan, hii si ni mimba ya kwanza unampa mwanamke ,it means unaenda kupata mtoto wako wa kwanza mbona upo kawaida sana nilitegemea utafurahi sana, mh angejua anayekuja wa sita , sijuh wa saba mana daaah๐คฃ๐คฃ๐ฅฒ๐คฃ๐คฃ๐๐๐๐, nikasema mm nimefurahia mbona , kuwa na amani kabisaa , au unataka mpka niluke luke zena, mi nimefurahi ila leo tulia plssss, zena aknambia hapana apa leo mguu wako , mguu wangu mpaka kwako nipajue tuu, ahaa mi sikuwa nataka apajue kwangu basi tu, nikaona kwakua ana mimba yangu, apa teali kuna kitu cha pamoja tunakitengeneza na nikakubali kumpeleka kwangu, basi nikamwambia sawa muandae mtoto tunaenda, kweli zena hii siku alinikomalia, akamuandaa mwanae harka harka, nikawapakiza kwenye gari yangu na safari ya gomz kwangu ikaanza, basi njiani , nikawa najalibu kumuongelesha zena ila zena wala hakuwa ananichangamkia sana naona alishaona hakuna mwanaume umu๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐๐๐๐๐๐๐
Basi bwana tukafika mpaka kwangu, mi naishi pazuri, ila shida daah nabadilisha sana wanawake sana apa, basi bwna nikaingia na zena mpkaa ndani, basi ummy akawa ananmbia baba apa ndo kwetu kupya ni kuzuri, mh mimi nikawa nacheka tu zena wala hakusema kitu nikamkalibisha kwangu, na nikamwambia aya maam apa ndo kwangu, na karibu sna, akanmbia ningejisikia raha na furaha , kma wewe mwenyewe kwa ridhaa yako ndo ungetaka mimi nije apa ,.ile umenileta baada y mimi kukufosi, nashukuru nimepaona na nimepajua naomba tu niludishe kwangu, khaa ata kukaa ahajakaa et, nikamwambia acha masihara ,asa mi nakurudishaje usiku huu tena, we lala mi asubuh na kupeleka kwako, akanmbia hapana nataka kurudi kwangu, nilitaka kupajua unaishi wapi tu, na nimeharizika, nikaona uyu ananitania uyu, nikamsogelea nikamsika kiuno, nikamwambia shida nn mama mbona kama una hasira, nikaona zena machozi yanamtoka , nikajua kumekucha apaaaK
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni