UTANIITA SHEMEJI. SEHEMU YA 17
SONGA NAYO...............
Mda ulienda jioni ilipofika akatoka kazin ,baada ya kufika nyumbani tu salamu ya kwanza aliingia chumbani na kufungua kioo na kutoka kwenye kibalaza kilicho pembezoni mwa chumba chake .
Alifika na kusimama huku macho yote akielekeza kwenye chumba changu, alisimama karibu nusu saa bila kuniona akatoka na kurudi chumbani .
Alibadilisha nguo na kutoka hadi nje akaangalia kama ataniona ila sikuwepo nje , akarudi tena ndani na kupanda ghorofa ya mwisho na kusimama juu kabisa akawa anaangalia pande zote ila bado hakunionaπ₯.
Moyo wake uliingiwa na huzuni sana ,maana alitamani kuniona ila bahati haikuwa upande wake π₯ masikini kinyonge alishuka na kurudi chumbani kwake.
Akaingia bafuni na kuoga ,baada ya kuoga akatoka na kurudi kukaa kibalazani , mda ulienda ikafika hadi saa tano usiku bado sijaonekana machoni pake.
Ngoja kwanza kabla sijaendelea naomba niulize hivi vile visehemu vya wazi ambavyo viko kwenye nyumba za ghorofa ambavyo watu hutumia kupumzika .
Au vingine ndo hivi vimekaa upande wa chumbani yaani unakuta chumba kina mlango wa kuingilia lakini bado kuna mlango wa kioo ambao unafunguliwa kwa kuslide si ndo vinaitwa kibalaza au?
Nisije kuwa natamka tofauti nikafikili naeleweka kumbe nawalisha matango poriπ₯², ila nahisi mnanielewa bhna .
Basi bwana kijana wawatu baada ya kukaa kwa mda mrefu alichoka na kuamua kuingia chumbani na kulala, usiku ukapita kesho yake asubuhi na mapema aliamka na kujiandaa kwaajili ya kwenda kazn.
Alivyo maliza alitoka akiwa na matumaini ya kuniona nje lakini alivyo pita hakuniona , akajiambia ataniona jioni , lakini hata jioni alivyo rudi pia hakuniona π₯.
Bado akajipa tumaini ila siku iliisha nyingine ikaingia na kuisha akiwa bado hajaniona π₯, moyo wake ulikosa raha kabisa π₯ akabaki akiwaza nini afanye ili tu anitie machoni π₯.
Baada ya kuwaza sana alipata jawabu, tabasamu lilopotea usoni likarejea π₯² kwa kujiamini akainuka na kuingia jikoni akachukua mfuko na kuja hadi getini kwetu akagonga.
Nikiwa nimekaa zangu ndani huku sina hili wala lile nilisikia geti likigongwa , haraka nikainuka na kwenda kufungua hapo akili mwangu najua ni kaka wa mifugo maana alikuwa katoka kidogo.
Ajabu nilifika nafungua nashangaa ni Samuel, nilimuangalia kwa mshangao huku nikijiuliza amefuata nini π€ , Samuel kuona namuangalia bila kumkaribisha akasema.
"Mambo" nilijishtukia na kusema.
"Aaaam poa ,karibu "
"Asante , nahitaji mayai sijui nitapata !?"
"Ooh yeah yapo karibu " niliongea na kumpisha apite nae bila kuchelewa alipita nikafunga geti na kuongoza kuelekea ndani .
Huku nyuma alikuwa akiangalia namna nyama zinavyocheza π€ moyoni anasema huyu ndo mwanamke sasaπ€mimi nae bila kujua naangaliwa mzigo π nikaendelea kuchapa mguu.
Basi alikaa kwenye sofa lilokuwa balazani me nikaingia ndani ,kufika yalipo mayai nikakumbuka sijauliza anataka mangap ikabidi nirudi na kumuuliza .
"Samahani unahitaji kiasi gani?"
"Trey moja au hayatoshi?"
"Hapana yapo " nilijibu na kurudi ndani nikamfungia kisha nikatoka na kumpatia akapokea na kunipa hela yangu .
Nilimshukuru tukaongozana hadi getini akatoka nikafunga na kurudi ndani , baada ya hapo ikawa kama utaratibu kila juma moss lazima aje kununua mayai .
Sikuwaza wala kufikilia kwamba anakuja kununua kwaaliji yangu me nilihisi ilikuwa ni kawaida yao ,japo nilikuwa nawaza sana wanatumiaje mayai hadi kila wiki lazima wanunue trey. π€
Uliza upande wa pili mayai yaliyokuwa yananunulia kila wiki yalikuwa yanaenda wapi π, ila wanaume wakiwa na jambo lao wanapambana hadi wafanikiwe π .
Yaani mtu anakuja kununua mayai unahisi anenda kula na familia yake kumbe anachukua hapa na kwenda kuuza mtaani kwa rafiki yake π .
Kwa hiyo anachukua si kwasababu anayahitaji ila nikwasababu anataka kuniona ,wote tusema okay π π .
Haya muuza mayai niliendelea kuuza mayai miezi ikakata , ikawa mara moja moja ananiona nje nikiwa bize na kazi zangu au usiku nikiwa kwenye kibalaza cha chumbani kwangu.
Mdogo mdogo miezi ilikata , mtoto wawatu nikazidi kunawili π mapenzi kwa boss wangu yakazidi siku hadi siku ,nikawa naishi si kama mfanyakazi bali ndugu yaani ni full maupendo π₯°.
Sasa bwana baada ya kupita miezi kadhaa siku hiyo nikiwa nimetoka msikitini kuswali ,nilifika nyumbani nikaitwa na boss akidai anamaongezi na mimi.
Kusikia hivyo nilishtuka nikihisi nimeyavurunda niniπ₯, eee Mungu saidia niwe sijakosea kitu maana kibarua kikiota nyasi itakuwa tatizo kubwa.
Basi nilikaa huku mapigo ya moyo ya kienda mbio , boss baada ya kuona nimekaa na niko tayari kumsikiliza akanambia.
"Wardah mwanangu , nimekuita hapa nikitaka kuongea na wewe vitu viwili tu.
Kwanza naomba nikupongeze kwa ufanyaji kazi wako, kwakweli umeni surprise maana kwa jinsi nilivyo kuona kwa mara ya kwanza tu nilihisi hapa hamna mfanya kazi.
Ila umethibitishia kuwa sitakiwi kumhukumu mtu kwakumuangalia usoni, kwa hiyo nakushukuru sana kwa hilo pamoja na kuwa rafiki bora kwa wanangu.
Sasa ukiachana na hili kingine nilichotaka kuongea na wewe ni hiki , aaam ninataka nifungue duka hapo nje na kwakua hakuna mtu wa kusimamia nikaona ngoja niongee na wewe kwanza.
Ili kama ukiwa tayari uwe wewe kwasababu humu ndani sioni kama kuna kazi nyiingi kiasi hicho na pia wewe tunakufahamu vyema so haitakuwa vizuri kumpa kazi hii mtu mwingine ile hali we upo.
Kwa hiyo kama uko tayari unaweza kubeba majukumu yote ,me nitakuongezea pesa ila kama utaona huwezi kufanya yote basi nitafute mwingine. "
Weeeeπ€©nilifurahi nikatamani kumrukia , jamani hii ni neema ya pekee, yaani nimepata kazi juu ya kazi mshahara juu ya mshahara π₯²aaa Mungu wewe nikupe nini mimiπ₯°π.
Bila kufikilia wala kunjing'ata nilijibu ndio niko tayari π boss akasema poa na kunitajia kiasi cha pesa atakacho kuwa akinipa kwa mwezi .
Kwa moyo mmoja nikasema asante mama π₯²π na kukaa tayari kwaajili ya kuanza kazi mpya , aka dada mshika mawili π sasa sijui wahenga watapita na mimi au ndo nitawashangaza π
Embu tukutane kesho jamani.......π
ITAENDELEA
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni