Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo

*KISASI CHA SINDELE BAADA YA KUAMBUKIZWA UKIMWI KWA MAKUSUDI*😭😭😭. *1-4*
Gonga94 · Stories

*KISASI CHA SINDELE BAADA YA KUAMBUKIZWA UKIMWI KWA MAKUSUDI*😭😭😭. *1-4*

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.

*_________________________________________*

*Sehemu Ya 1*

Ndani Ya hospital Moja kubwa wanaonekana Vijana wawili Wakiwa Wanasubiri Majibu Ya vipimo ambavyo Tayari walikuwa wamepima.

"Hivi Sindele kwa mfano ikatokea Mimi nimekutwa nimeathirika utanioa au utaniacha!?"

"Uuuuu Tatu Hapo kiukweli Sijui, Kwani Wewe Vipi ikibainika Mimi nimeathirika utafanyaje!?"

"Hahaaaa Sindele Hii Ndoa lazima itokee kivyovyote, Si unajua wazazi Wetu Ndo wanaitaka, kwa Hiyo Hata nikikuta umeathirika nitaolewa na Wewe ila hatutashiriki tendo Yaani itakuwa Ndoa Jina"
Yalikuwa mazungumzo ya vijana Hao Ambao nyuso Zao zilikuwa zinaelezea Mambo mengi Muno, kwa jinsi tu wanavyo angaliana walionekana ni vijana Ambao hawapendani ila kuna kitu kipo nyuma ya Pazia ambacho kinawalazimisha kuoana!.

Basi Baada ya Muda kuwadia waliitwa kuchukua Majibu Yao.
Hakika Mule ndani kuligeuka Msiba, Daktari alifanya Kazi ya kunyamazisha kile kilio na Yote Hiyo ililetwa na majibu yaliyo onesha kwamba kijana Sindele hajaathirika yupo Safi Bali Binti Wa kuitwa Tatu ana UKIMWI kama Wote😆😆😆😆!.
Aisee Yule mtoto alilia Muno Huku akijiuliza huo UKIMWI kaupatia Wapi wakati hajawahi lala na mwanaume maisha Yake Yote.

Kwanza Tatu alisema hayaamini Yale Majibu walienda hospital Nyingine Huko pia nako walikuta Mambo ni Yale Yale!.
Hapo Sasa Majibu ilibidi yarudishwe nyumbani kwa wazazi kile kilicho tokea Huko hospital!.

Wazazi Wa Tatu na wazazi Wa Sindele walikuwa ni Wabia kwenye kampuni Moja, yaani walikuwa wanamiliki kampuni Moja Huku ndani Yake kukiwa na biashara kibao zinazo endelea ambapo zingine zilikuwa halali na zingine haramu, na familia hizo kuna makubaliano ya mikataba ambayo Wao walikuwa washaiweka na Sijui ilikuwa ya Aina Gani ila tutajua mbeleni!.

Basi Baada ya majibu Yale Aisee wazazi walikataa kuairisha Ndoa, Neno Lao lilikuwa ni lazima Ndoa ifanyike na kwa Jinsi walivyo yapokea Majibu Bila Shaka hawakushitushwa yaani walikuwa wanategemea yatakuwa Vile!.

"Heeeee Mama si nimekwambia Tatu kaathirika mbona unasema Ndoa ipo pale pale Hiyo ipoje kwani!?"

"Sindele kuhoji maswali mengi sitaki Wewe tambua kwamba lazima Wewe na Tatu muoane kivyovyote Vile na mzae mtoto Baada ya Hapo Sasa Ndo mtajua Nyie mnaachana au inakuwaje!"

"Heeeee makubwa Mama kwa Hiyo unataka Mimi nimuoe Mtu kaathirika, kama una Shida na mjukuu nitafutie mwanamke mwingine ila Siyo Tatu!"

"Sindele nisikilize unataka Tatu utamuoa na hutaki utamuoa nimemaliza!" Yalikuwa mazungumzo Kati ya kijana Sindele na Mama Yake, kwanza Sindele hakuelewa kwa Nini analazimishwa kumuoa Huyo Tatu, aisee Sindele alimwangalia Mama yake Huku akiwa haishiwi kujiuliza maswali!.

"Hivi Huyu ni Mama Yangu Kweli!?? Au Bibi alinidanganya tu!?" Ni Swali Ambalo Sindele alijiuliza Bila kupata majibu!.
Huku nyumbani kwa Kina Tatu vilio kwa Binti Tatu vilikuwa havikomi, ilibidi wazazi Wake wamwambie ukweli Binti Huyo, kumbe aisee mtoto Tatu alikuwa kazaliwa na virusi ila wazazi Wake miaka Yote walikuwa wanaogopa kumwambia mpaka Siku aje ajipatie Majibu mwenyewe Kutoka kwa Daktari!.

"Sasa Baba kama mlijua nimeathirika kwa Nini mkubali kwamba Mimi niolewe na Sindele!?"

"Tatu Mwanangu lazima Hilo litokee, Bila hivyo Haya makampuni Yote na utajiri tulio nao utapotea, Hiyo Ndo Njia pekee Ya kufanya Mali Zetu ziendelee vizazi na Vizazi!."yalikuwa majibu ambayo yalimfikirisha Muno Tatu.
Binti Yule alisimuliwa mengi muno na wazazi Wake alipangwa akapangika na baada ya Hapo naye alijisemea kivyovyote Vile kwa Yale aliyo elezewa na kusimuliwa lazima Sindele amuoe!.

Basi Siku kadhaa zilipita kijana Sindele alihisi ni utani Lakini aliona lile swala ni kama lipo serious Hivi, Sindele alikuwa analazimishwa na kupewa vitisho ilimladi amuoe Binti Tatu.
Sindele aliamua kwenda kwa Doctor kupata ushauri, Basi kijana aliambiwa inawezekana akaishi na Mtu Mwenye UKIMWI na Yeye asipate huo UKIMWI kama atafuata ushauri Wa kitaalamu.
Kutokana na Hilo Sindele alikubali kumuoa Tatu na Ndoa Ya Bomani ilipita, Baada ya Hapo ilipangwa bonge la parti kufanyika kusherekea Ndoa Hiyo!.

Lakini kabla Ya Hiyo parti, Siku Hiyo Tatu na Sindele walichukuliwa na kupelekwa Sehemu, Ilikuwa ni mbaali Mwendo wa Masaa zaidi ya Kumi kutokea pale Mjini na ilikuwa vijijini ndani ndani kabisa.
Baada ya kufika kwenye Moja ya Kijiji walipaki Gari na kuanza kutembea kwa Mguu maana huko mbele Gari ilikuwa haiwezi kutembea Tena!.

"Mama mbona siwaelewi tunaenda Wapi!??" Sindele akiwa Haelewi kitu aliuliza, Binti Tatu Yeye alionekana anajua kinacho endelea maana kila kitu alikuwa ashasimuliwa na wazazi Wake kwa Hiyo alikuwa Hata Hashangai.

"Sindele nimekwambia Acha maswali! Tukifika tunako enda Ndo utaelewa!"

Basi walitembea zaidi Ya Nusu Saa walijikuta wapo porini kabisa, Huko porini kulikuwa na Magofu Ya nyumba za kale Muno.
"Vueni Viatu!" Ilikuwa ni Kauli ya Mama Yake na Tatu Baada ya kuwa wameyafikia Yale Magofu, ni kweli Wote walivua kisha waliingia ndani ya lile Gofu!.
Baada ya kuingia kuna ishara Mama Tatu na Mama Sindele walizifanya na kutamka maneno ambayo Siyo Sindele Wala Tatu Ambao waliyaelewa, Muda Huo Baba Tatu na Baba Sindele Wao walikuwa wapo kimya tu.
Baada ya Zile ishara kuna Mlango Wa Ajabu ulifunguka na Wote waliingia kule ndani! Aisee kulikuwa kunatisha Huko ndani hapana mchezo, Mbele Yao alionekana Babu kikongwe akiwa amekaa tena alikuwa amekaa anaelea hewani, ulikuwa ni uchawi Wa Hali ya Juu Kutoka kwa Yule Mzee!.

"Heeeee Mama Huku ni Wapi!?" Sindele aliuliza kwa Uoga Lakini Mama Yake alimpatia ishara ya kukaa Kimya.
Basi ilibidi wakae kwenye vigoda ambavyo vilikuwepo pale Bila Shaka utaratibu walikuwa wanaujua!. Basi Pasina kuongea Neno lolote Yule Mzee alisogea Kisha alitoa ishara kwamba Sindele na Tatu wasogee mbele na kweli walisogea.
Yule mtaalamu alichukua Damu ya Sindele na Damu ya Tatu Kisha alizitia kwenye kibuyu Baada ya Hapo walitulia kusikilizia Majibu, Muda Huo kila kitu kwa Sindele kilikuwa kigeni.

"Hizi Damu haziendani kuna kitu mumekosea!" Yalikuwa maneno ya mtaalamu akiwa kawatumbulia macho wazazi Wa Tatu na wazazi Wa Sindele tena akionekana kuwa na hasira.

"Babu Mbona hatujakosea Popote, labda ni kwamba Huyu Binti ni mwathirika ila Huyu kijana ni mzima labda inaweza kuwa Ndo Sababu!?" Mama Yake na Sindele aliuliza!.

"Kwa Nini mnakuwa wazembe kuzingatia masharti, nilisema kama ni wazima Basi Wote wawe wazima na kama wana ugonjwa Basi wote wawe wagonjwa, Mnapewa nafasi ya Mwisho lasivyo tusije laumiana"yalikuwa maneno ya mtaalamu ambayo yalifanya Wote watazamane, Baada ya Hapo waliamua kurudi nyumbani ili wakalimalize Hilo Tatizo!.

"Sindele Hapa haina Namna ili tufanikiwe inabidi uwe kwenye Hali kama ya Tatu yaani Hiyo ni lazima Siyo Ombi" yalikuwa maneno ya Mama Yake na Sindele ambayo yalimshangaza kijana Sindele, kwanza alitumbua Macho akiwa haamini yule ni Mama Yake kweli au alidanganywa na Mtu aliye mlea!
Sindele bila kuuliza Chochote Wala kuongea chochote alipitiliza chumbani Kwake kwanza maana alikuwa anaona kama anataniwa hivi nahisi Hapa Ndo Mkasa wetu ulipo anzia

Je ilikuwaje kwa kijana Sindele na Yapi yapo Nyuma ya Pazia mpaka ilazimishwe Sindele kumuoa Mtu Mwathirika.

*Sehemu Ya 2*

Sindele bila kuuliza Chochote Wala kuongea chochote alipitiliza chumbani Kwake kwanza maana alikuwa anaona kama anataniwa hivi nahisi Hapa Ndo Mkasa wetu ulipo anzia.

"Uuuuu Hivi Huyu ni Mama Yangu Kweli au kuna Mchongo Bibi Yangu alitengeneza, maana nilicho kiona Leo! Na Yale Bibi aliyo kuwa anafanya kama vinaendana hivi!!" Sindele akiwa chumbani Kwake alijiuliza maswali Yasiyo na Majibu, Sindele alikumbuka Jinsi ambavyo Bibi Yake alikuwa anasifika kwa uchawi na uganga kijijini Kwao Basi alipo kumbukumbu na kule porini aliko pelekwa na Mama Yake alianza kuona kama kuna Vitu havipo Sawa!.

"We Sindele ebu Njoo Huku tuzungumze Hakuna Muda kabisa wa kupoteza!" Sindele akiwa anawaza gafla alisikia Sauti ya Mama Yake.

"Mama Ebu nambie unatania Basi, unataka kusema unataka niwe Na UGONJWA kama Tatu!?" Baada ya Sindele kuona kelele za Mama Yake zimezidi aliamua kutoka na Hilo ni Swali alilo uliza!

"Sindele Mwanangu mbona Waathirika wanaishi tu kama Watu wengine, Ujue tusipo Fanya Hivi kuna Vitu vingi Muno tutavikosa!?"

"Aisee nilijua unatania kumbe upo serious, Sasa ni Hivi kuanzia Leo Huyo Tatu simtaki na Ndoa yenyewe Basi kama Vipi Mimi nisiwe mwanao tu! Utamwambia Hata Mumeo kile mnacho kitaka hakitakuwa!" Basi kijana Sindele akiwa na hasira aliamua kuropoka Baada ya Hapo aliondoka nyumbani kwa hasira!.
Siku Hiyo Sindele hakurudi nyumbani kabisa maana hasira ambazo alikuwa nazo zilikuwa Siyo za kawaida, Huwenda Sindele angejua kitakacho tokea Basi angepotea Moja kwa Moja na asingerudi tena!.

Siku iliyo fuata asubuhi na mapema kabisa Sindele alirudi nyumbani, na alimkuta Mama yake na Mume Wa Mama Yake wakijichekesha chekesha tu!.

"Sindele Mwanangu ule Jana ulikuwa utani Hata Mimi nimeamini nilikosea!" Basi Mama Sindele akiwa anajichekesha aliongea, Baada ya Hapo Sindele naye alitabasamu akiamini ni kweli ulikuwa utani maana kiuhalisia Mama hawezi kufanya Vile kwa mtoto Wake!.
Kijana Sindele akiwa Hana Hata wasiwasi alitengewa supu Safi na chapati changanya mayai, Basi Sindele Meno Yote yalionekana akiamini ule Ndo upendo Sasa wa Mama kwa mtoto Wake!.

Sindele alipiga ile supu na chapati mpaka alivimbiwa Lakini Baada ya kushiba tu alihisi kama kizunguzungu, yaani alianza kuona Vitu Viwili Viwili!.
Baada ya Hapo kijana Sindele alizidiwa na kuzimia!.

"Pumbavu zako ulihisi sikio linaweza kuzidi kichwa! Sasa Hapa Baba Dayo Mpigie Simu Doctor Faraja tumalize Kazi!" Baada ya Sindele kuzimia tu hayo yalikuwa maneno ya Mama Sindele akimwambia mumewe!! Na inaonekana kabisa Sindele alikuwa Siyo mtoto Wa Mume Wake, je kipi kipo nyuma ya Pazia kuhusu Sindele kuwa mtoto Wa Mama Huyo hayo Yote tutayajua tu kaa kwa kutulia.

Basi ni Kweli Yule Baba kama alivyo ambiwa alimpigia doctor Simu na baada ya Nusu Saa doctor alikuja Kisha walimpigia Simu Binti Tatu naye aje pale nyumbani, kilicho fanyika kilifanyika Damu ya Tatu ilichukuliwa kimakusudi kabisa na Sindele aliwekewa tena kwenye mshipa kabisa!.

"Shoga Yangu Mama Dayo Hapa Sasa nimeamini Maneno Yako kwamba hutavunja ahadi kwa Njia yoyote ile!" Basi Mama yake Tatu Baada ya lile zoezi alimpongeza Mama Sindele!.

Masaa yalisogea, Siku ya Kwanza ilipita Siku ya Pili ilipita, kila Sindele akizinduka alikuwa anakutana na Sindano kisha anazimia Tena!.

Zilipita karibia Wiki Mbili Sasa Hapo Sindele akiwa kazimia alibebwa na Safari ya kuelekea kwa mtaalamu ilianza!.
Sindele alikuja kuzinduka Yupo kwenye Gari wanaelekea kwa Mtaalamu, alipo angalia pembeni alimuona Mke Wake Tatu, pia aliwaona wazazi Wa Tatu na wazazi Wake!.

"Ma!ma!ma!.. Mama!!, nini kinaendelea!??" Kwa taabu Sana Sindele Sauti ilimtoka!.

"Ebu tulia Sindele utajua mbele kwa mbele!!" Yalikuwa Majibu ya Mama Yake na Sindele!.
Basi Baada ya safari ndefu walifika kwa yule Yule Mzee ambaye walienda mwanzo, Baada ya Yule Mzee kachanganya Damu alicheka kwa Sauti kubwa na ya kishindo!.

"Hahaaaa ili tumalize na kufunga ukurusa! Kilicho bakia ni Hizi Damu mbili kuleta kiumbe ambacho kitakuwa Sadaka!" Hayo yalikuwa maneno ya Yule Mzee ambayo yalifanya Sindele atumbue Macho!.
Basi Baada ya kukamilisha kilicho wapeleka kwa mtaalamu Huyo walirudi Mjini!.

Sindele alikuwa haelewi Hata kimoja kinacho endelea, yaani alikuwa anaona tu Mwili Wake umetobolewa masindano ila ukweli alikuwa hajui lolote!.
Basi Baada ya kufika Mjini sherehe kubwa ya kusherehekea Ndoa ya Sindele na Tatu iliandaliwa, Watu maarufu walialikwa na sherehe ilifana kweli kweli!.
Baada ya sherehe wazazi Wa Sindele na wazazi Wa Tatu walifanya mpango Wa kuwatafutia wawili wale chumba ili Sasa wakapelekeane Moto, maana Lengo la wazazi alikuwa ni mtoto atakaye zaliwa Kati ya Sindele na Tatu!.

"Tatu hakikisha unamshawishi Sindele kwa Njia yoyote mpaka mnafanya Mapenzi Sawa eee!?" Hayo Ndo yalikuwa maneno ya Mama Tatu akimsisitizia Binti Yake!.
Na kweli Muda uliwadia wa wanandoa hao kushirki tendo kwa Mara ya Kwanza!.

"Tatu Ebu acha kunitania kwa Hiyo unataka kunipaka maradhi Siyo!? Sipo Tayari kufanya huo upuuzi Hata kwa bunduki!" Basi wakiwa chumbani Sindele pasina kujua kama naye anao Tayari aliamua kumpa ukweli Tatu!.
Binti Tatu kiukweli alijaribu kila Njia kumshawishi Sindele Lakini mtoto Wa kiume alikaza, Tatu alijaribu Hata kukaa uchi mbele ya Sindele Lakini haikusaidia!.
Tatu uvumilivu ulipo mshinda aliamua kuropoka!.

"Sindele Mimi sioni Hata unacho lingia maana kama ni Umeme Hata Wewe unao! Bora tufanye tu!" Yalikuwa maneno ya Tatu ambayo yalifanya Sindele atumbue Macho, pale Pale kuna kitu kilipita kichwani kwa Sindele fyaaa!.
Japo ulikuwa Usiku Lakini Sindele aliamua kutoka na kwenda hospital kupima.
Aisee Sindele hakuamini alipo ambiwa ameathirika, alibadilisha hospital kama Tatu lakini kote aliambiwa Majibu Hayo Hayo, hakika ulikuwa Usiku Mgumu Muno kwa kijana Sindele!.

Akiwa na hasira Sindele aliamua kurudi pale Hotelini alipo muacha Tatu, na kweli alimkuta Tatu anajigeuza geuza kitandani!.
Kipigo alicho kipata Tatu aisee mbona aliropoka Yote, maana baada ya Sindele kuingia tu kule ndani wala hakuuliza alianza kushusha kipigo, mpaka Tatu aliropoka Namna Sindele alivyo wekewa Damu!.
Kwa hasira tu kupooza Machungu Sindele aliamua kufanya mapenzi na Tatu tena alikuwa anafanya kwa hasira kama anakomoa hivi, Lakini ukweli ni kwamba Hapo Ndo alikuwa anafanikisha mipango ya Watu!.

Japo Tatu aliondoka na manundu ilipo fika asubuhi Lakini kile alicho kuwa anakitaka kilifanikiwa!.
Sindele alipo rudi nyumbani alimuuliza Mama Yake ni Kitu Gani kafanya Lakini Mama Yake aliishia kumjibu kwa mkato!.

"Kwani aliye kwambia Waathirika Siyo Watu nani!? Acha mawazo ya zamani Wewe ni mtoto Wa Kiume kaza!" Hayo Ndo Yalikuwa majibu ya Mama Sindele!.
Ndugu msomaji wiki nzima Sindele hakupata usingizi, kibaya zaidi Pale Mjini Sindele Hata angesema akimbie kwa Mama Yake alikuwa hana pa kwenda kwa Hiyo ilibidi tu atulizane pale kwao Japo ilikuwa kwa maumivu makali Muno.
Tatu naye alikuwa anaishi nyumbani kwa kina Sindele maana alikuwa ni Mke Wa Sindele!.

Kadri Siku zilivyo zidi kusogea Ile Hali Sindele alianza kuizoea na kuona kawaida tu, Tatu Tayari alikuwa ni mjamzito.
Maisha yalikuwa Ya kawaida kwa Sindele pale nyumbani ila Mambo yalianza kubadilika Baada Ya Tatu kujifungua!.

Mtoto akiwa na Siku Tatu tu alichukuliwa na wazazi Wa Sindele Pamoja na wazazi Wa Tatu na waliondoka Naye kwenda kwa mtaalamu, Hata walivyo Rudi walirudi bila Huyo mtoto Huku nyuso Zao zikiwa za furaha kuonesha kuna kitu kikubwa wamefanikisha!.
Binti Tatu Yeye Wala hakuuliza mtoto Yuko wapi maana alikuwa anajua kinacho endelea, ila Sindele Sasa Ndo alikuwa gizani maana alikuwa hajui lolote!.

Manyanyaso kwa Sindele yalianza aisee Baada ya kuwa lao lishafanikiwa, Hata Tatu alirudi nyumbani kwao hakuendelea kukaa pale kama Mke Wa Sindele!.
Kijana Sindele kulala na Njaa alianza kuona kama kawaida, ilifika kipindi alianza kuona Yule Siyo Mama Yake kwa Yale aliyo kuwa anafanyiwa!.
Binti Tatu Naye alipata mwanaume mwingine tena msomi mwenzake na Mwenye Pesa Zake, na Tatu alimtaka Sindele amuandikie Taraka!.

Sindele alikuwa anaona kama mapicha picha kwenye maisha Yake, maana baada ya kutoa tu Taraka kwa Tatu haikupita Hata mwezi Pale Kwao alifukuzwa.
Sindele ni Nani na ilikuwaje Yupo Hapa, Je yapi yapo nyuma ya Pazia kuhusu wazazi Wa Sindele na wazazi Wa Tatu.

Turudi Miaka ishirini na Tatu Nyuma kabla Sindele hajazaliwa Hapa Ndo Mkasa wetu unaenda kuanzia

Miaka 22 iliyopita......

Alionekana Binti Wa Miaka 17 akiwa analia kweli kweli Huku akiwa kavaa nguo za Shule, Binti Huyu alikuwa kabaini ana ujauzito ingali Bado Yupo Shule na alikuwa yupo Kidato Cha Tano Tena alikuwa ni Binti anaye tegemewa na ukoo mzima kuja kuwa mkombozi, maana Ndo alikuwa anaonekana kuwa na akili kwenye ukoo mzima!.
Jina lake ni Panina Binti Huyu Baada ya kugundua ana ujauzito tena ukiwa ujauzito Wa Baba Mtu mzima kiukweli aliamua kufanya maamuzi magumu ili kunusuru aibu na kunusuru masomo Yake!?

Je unahisi alifanya maamuzi Gani!? Na huyu penina ni Nani!?? Na Je kijana Sindele ilikuwaje tunamuona alipo!? Kisasi Gani Cha Sindele kinazungumziwa!?? Nadhani Hapa Ndo Hadithi Yetu inaenda kuanza Huko kote ulikuwa ni utangulizi!.

Tukutane sehemu Ya 3


*Sehemu Ya 3*

Jina lake ni Panina Binti Huyu Baada ya kugundua ana ujauzito tena ukiwa ujauzito Wa Baba Mtu mzima kiukweli aliamua kufanya maamuzi magumu ili kunusuru aibu na kunusuru masomo Yake!?.
Penina alipewa ujauzito na Mpishi Wa Shule tena Mpishi Huyo alikuwa ni Mzee, Vishawishi vya Hapa na pale Ndo Vilifanya penina kuingia kwenye mahusiano ya Siri na Yule Baba!.

Penina Kwao maisha yalikuwa ya kawaida Muno, na wazazi Wake walikuwa wajasiriamali wa kawaida tu, kwa Hiyo kila Senti wanayo ipata walikuwa wanawekeza kwa kumsomesha penina, alafu Leo Hii eti ana ujauzito, hakika penina aliona Zile taarifa wazazi Wake wakizipata Basi aisee anaweza akatengwa Hata na ukoo!.

Penina Baada ya kugundua Hali ile hakumwambia Hata rafiki Yake Mmoja, Pia hakumwambia Hata Yule Baba aliye mpatia ujauzito, yaani kimya kimya penina aliamua kubeba Begi lake Bwenini na kutoroka pale shuleni.
Japo nyumbani kwa kina penina ilikuwa ni pale pale Mjini na ilikuwa Siyo mbaali Kihivyo na Shule ila penina alikuwa anakaa bwenini maana Ndo yalikuwa masharti ya Shule kila Mwanafunzi kukaa bweni, penina alikuwa anarudi tu kwao Siku za weekend!.

Baada ya penina kutoroka pale Bwenini alienda mpaka Stendi na kupanda Gari, ilikuwa ni basi iliyochokaa Bila shaka ilikuwa inaelekea Huko vijijini!.
Penina alikuwa kama kapagawa maana Hata maamuzi Yake alikuwa hana uhakika nayo!.

Safari ilianza penina akiwa Hana uhakika na anako elekea, ilikuwa ni safari ya Masaa zaidi ya Kumi na kitu!.

Mida ya Saa Kumi na Mbili Jioni penina aliamua kushuka kwenye Gari Huku akiwa katikati ya Kijiji ambacho Hata hakijui!.
Penina alianza kupita nyumba Moja Baada ya Nyingine akiwa anaomba msaada Huku anatoa maelezo ya Uongo, kwa maelezo Yake ni kwamba alikuwa ametelekezwa na Mumewe na hajui Hata Hilo ni Eneo Gani!.

Wengi Wao walionekana kumkatalia kiasi kwamba penina alijikuta katembea umbali mrefu Muno kutoka barabarani, yaani alijikuta yupo vijiji vya mbaali kabisa!.
Ikiwa Imefika Saa Nne za Usiku bahati iliyoje penina Baada ya kutoa maelezo kwa Bibi Mmoja Hivi alifanikiwa kupewa hifadhi!.

Ilikuwa Siyo hifadhi Ya Siku Bali miezi kadhaa, Yule Bibi hakuwa na hiana kuendelea kuishi na penina pale Kwake, Japo Bibi Yule kutokana na utaalamu Wake aligundua Yote aliyo yaongea penina ni Uongo ila aliamu kukausha, maana huwenda Naye kuna Faida alikuwa kaiona kutokana na ule uongo wa penina.

Upande Wa Huku Mjini penina alikuwa katafutwa kweli kweli na wazazi Wake kushirikiana na walimu mpaka taarifa zilifika polisi Lakini penina hakupatikana!.

Miezi kadhaa ilipita upande Wa Huku Kijijini Muda Wa penina kujifungua ulifika, na bahati iliyoje penina alijifungua vizuri tu mtoto Wa kiume!.
Aisee huwezi Amini mtoto hakuonja Hata Ziwa la mama Yake, ukiwa ni Usiku Sana penina aliamua kumterekeza mtoto mchanga kijijini na kumuachia Yule Bibi msala!.

Katika Kijiji hicho hakuna ambaye alikuwa anamjua penina Wala aliko tokea, kwa Hiyo Hata pa kwenda kumtafutia walikosa!.
Yule Bibi Yeye aliona ni Sawa tu maana Hata hivyo kapata Mrithi Wake atakaye rithi mikoba Yake ya uchawi na uganga na Ndo Faida ambayo Bibi Yule alikuwa kaiona Tangia Penina anafika Kwake.

Panina Baada ya kurudi Mjini alitoa maelezo ya Uongo Kwamba alitekwa na Watu asio wajua na walikuwa wamemfungia sehemu Huku wakimtesa!.
Basi Binti penina alipewa pole nyingi Muno na wazazi pia walimu shuleni na wanafunzi wenzake!.

Penina aliendelea na masomo Japo kuwa alikuta wenzake washafika Kidato Cha Sita, alijitahidi kufundishwa masomo ya binafsi na vipindi vya ziada ili alingane na wenzake na hatimaye Kweli Wote kwa pamoja Baada ya miezi kadhaa walimaliza Kidato Cha Sita.
Bahati Mbaya au nzuri Maksi ya Penina ilimruhusu kwenda Diploma na Siyo Chuo kikuu!.

Upande Wa Kijijini Yule mtoto mchanga aliendelea kulelewa vyema na Yule Bibi akiwa amepewa Jina la Sindele, kwa Lugha ya Pale Kijijini Sindele maana Yake ilikuwa inamaanisha Mrithi Wangu, kwa Hiyo Bibi Huyo alitoa hilo Jina kwa malengo!.

Siku hazigandi hatimaye miaka kadhaa ilipita penina alimaliza masomo Yake ya Diploma na alipata Kazi kwenye kampuni Moja hivi Kubwa linalo jihusisha na Maswala ya kuuza Vyombo vya Moto Nchi nzima na lilikuwa kampuni kubwa Muno, kwa kuwa penina alikuwa kasomea maswala ya Masoko Basi aliwekwa kwenye hicho kitengo.
Akiwa anafanya Kazi kwenye kampuni lile Kwa Mara ya Kwanza penina alikutana na mwanaume ambaye alikuwa mhasibu Wa Pale hakika wawili hao walitokea kupendana Muno!.

Pia Yule Mwanaume kwa Jina la Ibrahimu alikuwa na Rafiki Yake ambaye alikuwa pia na kacheo cheo kwenye Hilo kampuni!.

"Penina Ujue Mimi na Rafiki Yangu Bedo kuna mpango kabambe tupo nao Sijui na Wewe utakuwemo kwenye Huo mpango, maana Bedo kasema Demu Wake kakubali!" Siku Hiyo penina aliletewa Mpango Fulani na kipenzi Chake Ibrahim, na ulikuwa Mpango wa kulichukua lile kampuni, yaani walikuwa wanataka kumpora Mzee Mwenye lile kampuni!.
Hakika penina aliona ule mpango unamfaa maana Hata Hivyo familia nzima ilikuwa inamtazama Yeye na Huku mshahara ukiwa ni mdogo!.

Unahisi mpango ulikuwaje na ulifanikiwa!? Na ilikuwaje mpaka tunaona Watu wapo kwa mganga!??

*Sehemu Ya 4*

Hakika penina aliona ule mpango unamfaa maana Hata Hivi familia nzima ilikuwa inamtazama Yeye na Huku mshahara ukiwa ni mdogo!.

Mpango wa Watu Wanne kupora kampuni ulianza, Yaani Ibrahim na mpenzi Wake penina, pamoja na Bedo akiwa na Mpenzi Wake!.

Hakika walikuwa wamejilipua maana Mtu wanaye panga kumdhurumu Naye alikuwa Siyo mnyonge na alikuwa Mtu Maarufu!.
Hatua kwa Hatua walikuwa wanasuka Mambo iliwachukua Mwaka Mzima kukamilisha, Siyo kampuni tu Bali Utajiri na Mali zote za Tajiri Huyo walifanya mipango na ulaghai walizitia mikononi, yaani Documents zote za umiliki zilidondokea mikononi Mwao!.

Yule Mzee ambaye kaporwa Mali alijaribu kuleta Chokochoko Lakini alitumiwa Watu na kuuawa.
Ndugu Wa Baba Yule walijaribu kupeleka kesi mahakamani kudai Mali za ndugu Yao Lakini ilisemekana ashauza kila kitu na Alikuwa Hana Mali, yaani penina na wenzake walijikuta wanamiliki utajiri Wa Mabilioni gafla, na Wale ndugu walipo Zidi kuleta Chokochoko nao waliuawawa Wote.

Basi Ibrahim alimuoa penina pia Bedo alimuoa Yule Demu Wake ambaye Tayari alikuwa kazaa Naye, na familia hizo mbili ziligawana asilimia Hamsini za Hisi kwenye ile kampuni na Mali zote!.
Lakini Baada ya miezi kadhaa tu kutoka wachukue ile kampuni Mambo yalianza kwenda kombo Huku kampuni ikiwa inaporomoka kwa Kasi, kila Njia waliyo ifanya kuokoa kampuni ile ilishindikana, Basi Hapo ilibidi waende kwa mtaalamu maana waliamini wanafanyiwa figisu!.

"Mali zote za Yule Mzee zilikuwa za kafara na ushirikina kwa kuwa kafariki Basi Mali zote zitapotea! Na Mbaya zaidi Nyie mnaweza kuwa Kwenye matatizo maana zile Roho za Watu alio watoa Yule Mzee zitaanza kuwaandama Nyie!" Hayo Ndo yalikuwa maelezo ya yule mtaalamu!.
Basi penina na wenzake waliomba awasaidie kunusuru Yale majanga.

Yule mtaalamu aliwaelekeza sehemu ambayo wanaweza kupata msaada, pia aliwapa maelekezo Namna ya kufika!.
Hapo Sasa penina na wenzake Ndo waliamua kufunga safari na kwenda kule porini tuliko ona mwanzo akina Sindele wanapelekwa!.

Hakika walifika Huko walikutana na masharti mazito Muno.

"Ili kunusuru majanga yanayo enda kuwatokea na kubakisha Mali Salama mnahitajika mtoe kafara, na kila Mmoja wenu atoe kafara ya Watu Watatu anao wapenda na ndugu Wa karibu Baada ya Hapo litabakia Sharti Moja Ambalo mtakaa Miaka kumi na Tano Ndo mtarudi tena kulikamilisha!" Hayo Ndo yalikuwa masharti ya yule mtaalamu!.
Hakika ilihitajika roho Ngumu, kwa kuwa walikuwa wameyavulia Maji Nguo waliamua kuyaoga!.
Huwezi Amini penina aliwatoa wazazi Wake wawili pamoja na Dada Yake kafara yaani alijikuta anaingia kwenye Tamaa ya Utajiri kuliko kawaida mbaya zaidi walikuwa wameonja maisha ya utajiri kwa Hiyo hawakuwa Tayari kuyaacha.

Kila Mmoja Wao alitoa kafara ya ndugu Zake anao wapenda Watatu, Baada ya Hapo Sasa Mambo yalianza kunyooka na kampuni ilirudi kwenye uimara Wake tena Mara dufu!.

Upande Wa Huku Kijijini Tayari mtoto Sindele alikuwa kakuwa kuwa kafikisha Miaka kama Sita Hivi, Hapo ilibidi apelekwe Shule na kuanza Darasa la Kwanza!.

Siku hazigandi miaka ilisogea hatimaye Sindele alimaliza Darasa la Saba na hakufanikiwa kufaulu, kwa Hiyo alibaki kijana Wa pale pale kijijini!.
Kero Moja kwa Sindele ilikuwa ni uchawi na uganga wa Bibi Yake, na kila Siku alikuwa anakumbushwa na Bibi Yake kwamba ajiandae kurithi ile mikoba, maana Bibi Huyo alikuwa kazeeka Muno ni miaka tisini alikuwa anaikaribia!.

Sindele maswala ya uchawi alikuwa hayapendi kweli kweli sema Basi tu Bibi Yake alikuwa mchawi!.

Miaka ilizidi kusogea hatimaye Sindele alifikisha miaka ishirini Sasa Hapo Kasi ya kulazimishwa kurithi mikoba ilizidi, na ilifika kipindi Sindele alianza kutishiwa na Bibi Yake pamoja na wachawi wengine kwamba akikataa Basi anaweza kufa!.

Kijana Sindele Aliona ya Nini kujitesa kuendelea kuishi sehemu wanayo Amini uchawi, Sindele aliamua kutoroka pale kwa Bibi Yake , na safari ilikuwa ni kwenda Mjini Ambako Vijana wengi wa Kijijini huwaga wanaamini kuna maisha mazuri na Pia Pesa zipo Nje Nje!.

Sindele alifika Mjini kwa Mara ya Kwanza Huku Akiwa hana mbele wala nyuma, alikuwa haelewi atakula nini na kulala Wapi, ila kutokana na kero za Bibi Yake aliona Bora tu akapambane Mjini!
Baada ya kufika Mjini Wiki nzima Sindele alilala sitendi, yaani alijikuta anajifunza upiga Debe Bila kupenda!.

Hakika maisha yalikuwa magumu Muno kwa kijana Huyu, Baada ya kuona kupiga Debe hakuna Tija Sindele aliamua kuanza kutembea Mtaa kwa Mtaa kuomba Kazi kwenye majumba Ya Watu!.

Turudi upande Wa Huku kwa Penina, Tayari penina na Mumewe Ibrahim walikuwa Wana watoto Wawili maana Tangia waoane ni zaidi ya Miaka Kumi na Kitu ilikuwa imepita!.
Maisha Yao yalikuwa mazuri Muno Huku Shida zikiwa Siyo Sehemu ya maisha Yao yaani Pesa ilikuwa inaongea!.

Mtoto Wao Wa kwanza kwa Jina la Dayo alikuwa anasoma Shule ya kitajiri na alikuwa na miaka Kumi Na nne, mtoto Wao Wa Pili nae hivyo hivyo alikuwa anasoma Shule ya kitajiri alikuwa na Miaka Kumi, Yaani Wote walikuwa wanasoma shule za kitajiri!.

"Baba Dayo kwa Nini tusitafute kijana Wa kutunza mazingira ya Humu ndani, ujue naona kama Mlinzi Wa Pale Getini anazidiwa na ukijani Huku ndani umeanza kupotea!" Basi Siku Hiyo Mama Dayo ambaye Ndo penina alitoa Wazo na kweli walikubaliana watafute kijana Wa kutunza Bustani na mazingira mengine ya Mule ndani Ambapo wao walikuwa wanapaita Paradiso Yao!.
Bahati iliyoje Wakati wanawaza kutafuta kijana Wa Kazi, kama ameotea Hivi kuna kijana alionekana kuja kuomba Kazi pale na alikuwa Siyo mwingine Bali ni kijana Sindele!.

Sindele alijikuta anapata Kazi kwenye Jumba la kifahari Huku akiwa haamini, Tena kwenye Jumba la Mama Yake mzazi Pasina Yeye kujua!.

Ilikuwaje mpaka Mama Dayo akajua Sindele ni mtoto Wake!? Na ilikuwaje Sindele akalazimishwa kumuoa Binti Wa kuitwa Tatu!?

*Sehemu Ya 5*

Sindele alijikuta anapata Kazi kwenye Jumba la kifahari Huku akiwa haamini, Tena kwenye Jumba la Mama Yake mzazi Pasina Yeye kujua!.

Maisha mapya kwa Sindele yalianza, Huku akiwa kajitambulisha Kwamba anaitwa Sinde, yaani Sindele alikuwa hapendi kujiita Sindele! Alikuwa anaona akifupisha na kujiita Sinde Ndo unyama.

Sindele alianza maisha mapya ya ufanykazi, Japo yalikuwa ya manyanyaso ila alijikaza, Sindele alikuwa anaombea watoto wa Mama mwenye nyumba wasiwe wanarudi toka shuleni maana walikuwa wanampelekesha Muno tena walikuwa na Dharau isivyo kawaida!.

Basi Siku hazigandi hatimaye Sindele alimaliza Mwaka ndani ya Mjengo Ule akiwa kama mfanyakazi mtiifu Japo Ndo hivyo alikuwa anavumilia mengi, kwa mfano kuna kipindi mtoto Wa Boss amewahi kumumwagia Mkojo makusudi, yaani alikojoa kwenye kikopo na kwenda kumumwagia Sindele kwa makusudi kabisa, ila Ndo alikuwa mtoto Wa Boss, Sindele hakuwa na lakufanya zaidi ya Kujichekesha Huku Roho inauma.

Ile Miaka 15 ambayo Penina na wenzake walikuwa wamepewa na mtaalamu kwamba inatakiwa warudi Kwake wakapewe Sasa sharti la Mwisho ilikuwa imetimia na Kweli walirudi kwa Yule mtaalamu, awamu Hii walikuta kazeeka Kawa Mzee!.

Walijielezea vizuri na Kweli mtaalamu aliwakumbuka vyema!.

"Nahitaji Damu Ya mjukuu Wenu itolewe kafara na Hiyo Damu Ndo itafunga Mali zenu zisipotee!" Yalikuwa maelezo ya mtaalamu!.

"Mtaalamu Sisi Lakini hatuna wajukuu!"

"Sasa Hapo Ndo ibabidi mpate, yaani uzao Wa kwanza kutoka kwenye familia zenu mbili inatakiwa waoane na wapate mtoto ndani ya Mwaka Mmoja Kisha Huyo mtoto Ndo atafunga hizo Mali, lasivyo Mali zote mulizo Nazo zitapotea kama vumbi kwenye upepo!"

"Uuuuu Sasa uzao Wa kwanza kama Wote Wakawa Jinsia Moja hapo inakuwaje!!"

"Sasa Hapo Mimi Sijui inakuwaje ila mizimu Ndo inataka hivyo, na Bila Shaka mpaka mizimu imesema hivyo inaamini uzao wenu Wa kwanza ni jinsia tofauti!"
Kwanza ilibidi Wote watazamane!! Upande Wa Bedo na Mkewe Wao ni Kweli walikuwa Na mtoto mkubwa ambaye kafikia umri Wa kuolewa maana alikuwa Ndo katoka kumaliza Chuo akiwa na Miaka 21 na mtoto Huyo walikuwa wamempata Hata kabla hawajaoana yaani kipindi Hata hizo Mali hawajazipata!., ila changamoto ilikuwa kwa upande Wa penina na Mumewe maana mtoto Wao Wa kwanza alikuwa ni Dayo ambaye alikuwa kafikisha Miaka kama Kumi Tanto kuelekea kumi na Sita Hivi!.

"Uuuuu Sasa Dayo kumuoa Tatu Jaman si itakuwa ubakaji Huo!" Yalikuwa maneno ya penina akimuonea huruma mwanae!.

"Mtaalamu Kwani huwezi kubadilisha Sharti!??" Mume Wa Penina aliuliza!.

"Sharti Ndo Hilo Halibadiliki, Fanyeni hima maana baada ya Mwaka tu Mali kidogo kidogo zitaanza kupukutika na kumbuka Mali zikiisha basi kitakacho Fuata ni uhai wenu!" Yalikuwa maneno ya yule mtaalamu, hakika familia zilitoka pale wakiwa wamepagawa!.
Baada ya kufika nyumbani walikaa kikao na waliona ni Sawa tu inabidi mtoto Dayo amuoe Binti Tatu!!.

Haraka haraka walifanya mpango na Ndoa ya Kimya Kimya ilipita, yaani ni familia tu walikuwa wanajua, maana kwa umri Wa Dayo ilikuwa ni kama ubakaji kwa Hiyo taarifa zingesambaa huwenda Hata Sheria ingefuata Mkondo, Baada ya Hapo Sasa walienda kwa mtaalamu ili Damu zikachanganywe, yaani Damu Ya Dayo na Damu ya Tatu maana ilikuwa ni Moja ya maelezo ya mtaalamu!.
Lakini kitu cha Kushangaza Damu zile zilipo changanywa hazikuendana na mtaalamu alibaini kwamba Dayo Siyo mtoto Wa kwanza!.

Aisee Hapo Sasa Bwana Ibrahimu Ndo aliijua Siri ambayo alikuwa haijui kuhusu Mkewe kwamba amewahi kuzaa, yaani penina Naye kumbukumbu Ndo zilirudi kwamba amewahi kuzaa mtoto na akamtelekeza kijijini.
Japo Mr Ibrahim alilalamika Muno kwa Mkewe kumficha Siri Hiyo lakini Ndo yalikuwa yametokea.

Kilicho kuwa kinatakiwa ni Huyo mtoto atafutwe Ndo aje afunge Ndoa na Tatu! .
Hapo Sasa Kizazaa Ndo kilipo anzia maana ilimlazimu penina na Mumewe kusafiri mpaka kijijini kwenda kumsaka Huyo mtoto!.

Penina alikuwa anakumbuka vyema mazingira aliyo mtelekeza mtoto, kwa kuwa walikuwa wamethibitishiwa na mtaalamu kwamba Huyo mtoto yupo hai Basi walikuwa na matumaini ya kumpata!.
Lakini bahati mbaya walipo fika maelezo waliyo yakuta ni kwamba Huyo mtoto ashafariki!.

"Ila we Mwanamke Wa Ajabu kweli!? Yaani Baada ya Miaka ishirini na kitu kupita Ndo unakuja kumuulizia mtoto Wako!? Haya Huyo mtoto ashafariki!" Hayo yalikuwa maelezo ya Bibi Yake na Sindele ambaye walimkuta kajichokea, maana miaka tisini Siyo mchezo!.
Kutokana na maneno ya Mtaalamu walikuwa na uhakika kwamba Huyo mtoto yupo hai ila Yule Bibi anaficha tu!.

Basi penina alizama kwenye mkoba Wake alitoa kibunda Cha Pesa kama million mbili Hivi na kumpatia Yule Bibi! Aisee Yule Bibi alitumbua Macho kuona zile Pesa maana tangia azaliwe alikuwa hajawahi shika Pesa Nyingi Vile!.
Bibi Wa Watu alianza kufunguka kuhusu Sindele!.

"Bibi kwani anaitwa nani Huyo mtoto tukamtafute Huko Mjini!?"

"Anaitwa Sindele!!" Yule Bibi alijibu, aisee lilikuwa Jina Jipya kabisa Masikioni Mwao.
Kumbuka kijana Sindele Mjini alikuwa anajiita Sinde yaani alikuwa anapenda kufupisha kwa Hiyo Hata pale kwa Boss Wake alijitambulisha hivyo kwamba anaitwa Sinde.

Basi penina na Mumewe walirudi Mjini wakiwa na Jina la Sindele kichwani na waliamini kwa Pesa walizo Nazo Basi watampata tu!.
Baada Ya kufika Mjini kitu cha kwanza walienda kwenye maredio na magazeti kutoa taarifa kuhusu Sindele, na walitaja mpaka Kijiji anacho Toka na Jina la Bibi Yake, maana Hizo taarifa zote Bibi alikuwa kazitoa Baada ya kumwagiwa Pesa.

Japo picha ya anaye tafutwa ilikuwa haipo Lakini maelezo yalikuwa yanajitosheleza vizuri kabisa!.

Wiki nzima ilipita Huku Huyo Sindele akiwa hajajitokeza, penina na Mumewe walikuwa Wanasubiri Simu mpaka Wanasubiri tena Sana Sana walikuwa wanapata Simu za matapeli!.
Maana vijana kama Watatu walijitokeza kwamba Wao Ndo kina Sindele Lakini walipo pelekwa kwa Bibi Yule aliwakataa hawajui na wengine walikamatwa uongo Baada ya kushindwa kutoa maelezo fasaha!.

Sindele Mwenyewe alikuwa hajui Hata kama anatafutwa maana Hata Simu kwamba ataona taarifa alikuwa hana!.
Kama bahati tu Siku Hiyo Sindele alibahatika kupata chansi ya kwenda kudhurura Baada ya kuwa kamaliza Kazi!.
Katika Kuzunguka alikutana na Bango likiwa limeandikwa Maandishi makubwa na meusi*SINDELE ANATAFUTWA*.
Kijana Sindele alisogea na kuanza kusoma maelezo kwa undani, aisee kijana alipagawa alipo ona taarifa kwamba wanao mtafuta ni wazazi Wake na atakaye Saidia kupatikana kwa Sindele atapewa million Hamsini!

"Aisee Huu utajiri Walai, kama tu atakaye nipata anapewa Hiyo pesa Mimi Je!!" Sindele akiwa anakenua meno kwa furaha alijiwazia na alijua kabisa ni Yeye anatafutwa kutokana na taarifa zilizopo pale, maana mpaka Jina la Bibi Yake lilikuwa limetajwa!.
Sindele aliandika kwenye mkono Namba za kwenye lile Tangazo kisha alipo fika mbele aliazima Simu kwa Mama tu muuza mboga!.

Upande Wa Pili penina na Mumewe walipokea Simu Huku Mtu akijitambulisha kwamba Yeye Ndo Sindele, kutokana na maswali machache waliyo muuliza kwenye Simu na kuyajibi kwa ufasaha aisee walipata kimuhe muhe Cha kukutana na Huyo Mtu, maana waliona Huyo anaweza kuwa ndiyo!.
Basi kwenye Simu walipeana maelezo sehemu ya kukutana, na Sindele aliwaelezea Nguo alizo Vaa na muonekano Wake, na aliwaambia Hana Simu!.

Aisee hapa Ndo patamu!? Unahisi penina akigundua yule mfanyakazi Wake Wa pale nyumbani Ndo mwanae atachukua hatua Gani!? Vipi Sindele atafanyaje!??

Maoni

You're not logged in


Tangazo - Mimi sikuachi fully stories
Mimi sikuachi fully stories
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*KISASI CHA SINDELE BAADA YA KUAMBUKIZWA UKIMWI KWA MAKUSUDI*😭😭😭. *1-4*


*_________________________________________*

*Sehemu Ya 1*

Ndani Ya hospital Moja kubwa wanaonekana Vijana wawili Wakiwa Wanasubiri Majibu Ya vipimo ambavyo Tayari walikuwa wamepima.

"Hivi Sindele kwa mfano ikatokea Mimi nimekutwa nimeathirika utanioa au utaniacha!?"

"Uuuuu Tatu Hapo kiukweli Sijui, Kwani Wewe Vipi ikibainika Mimi nimeathirika utafanyaje!?"

"Hahaaaa Sindele Hii Ndoa lazima itokee kivyovyote, Si unajua wazazi Wetu Ndo wanaitaka, kwa Hiyo Hata nikikuta umeathirika nitaolewa na Wewe ila hatutashiriki tendo Yaani itakuwa Ndoa Jina"
Yalikuwa mazungumzo ya vijana Hao Ambao nyuso Zao zilikuwa zinaelezea Mambo mengi Muno, kwa jinsi tu wanavyo angaliana walionekana ni vijana Ambao hawapendani ila kuna kitu kipo nyuma ya Pazia ambacho kinawalazimisha kuoana!.

Basi...

👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/kisasi-cha-sindele-baada-ya-kuambukizwa-ukimwi-kwa-makusudi-1-4

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral #fictionwriter
#ShortDrama #fblifestyle

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi kisasi-cha-sindele-baada-ya-kuambukizwa-ukimwi-kwa-makusudi
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

AFANDE MILLAN😎 41 to 42

AFANDE MILLAN😎 41 to 42

913
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 43

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 43

554
TIPWA TIPWA NA MR MARVEL 19 to 20 final

TIPWA TIPWA NA MR MARVEL 19 to 20 final

369
MIRANDA (Binti Yangu)   SEHEMU YA 15

MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 15

115
*KISASI CHA SINDELE BAADA YA KUAMBUKIZWA UKIMWI KWA MAKUSUDI*😭😭😭. *1-4*

*KISASI CHA SINDELE BAADA YA KUAMBUKIZWA UKIMWI KWA MAKUSUDI*😭😭😭. *1-4*

77
Victor Osimhen alishindwa kujizuia na kutoa machozi..  FOOTBALL ⚽.

Victor Osimhen alishindwa kujizuia na kutoa machozi.. FOOTBALL ⚽.

3
🚩Rais wa klabu ya Al Ahly, Mahmoud El-Khatib, ametangaza maamuzi makali

🚩Rais wa klabu ya Al Ahly, Mahmoud El-Khatib, ametangaza maamuzi makali

2
ACHA NIKUPENDE ❤️ 3  to 5

ACHA NIKUPENDE ❤️ 3 to 5

ZIMESOMWA ZAIDI

‎TUNDA LA  DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

‎TUNDA LA DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

11.65K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

7.38K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya tisa.  👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya tisa. 👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

3.81K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya sita.  👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇  Shemeji inauma utanichana.

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya sita. 👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇 Shemeji inauma utanichana.

3.29K
MY WANGU❤️ sehemu ya 119 na 120.

MY WANGU❤️ sehemu ya 119 na 120.

2.89K
MY WANGU❤️ sehemu ya 108

MY WANGU❤️ sehemu ya 108

2.8K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 20.  👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 20. 👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

2.68K
MY WANGU❤️ sehemu ya 116 na 117

MY WANGU❤️ sehemu ya 116 na 117

2.66K
MY WANGU❤️ sehemu ya 106 na 107

MY WANGU❤️ sehemu ya 106 na 107

2.62K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 16.  👉 nakupenda pia...👇

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 16. 👉 nakupenda pia...👇

2.56K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

Hakuna Ratiba kwa sasa

Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
ACHA NIKUPENDE ❤️ 3  to 5 Post Mpya
ACHA NIKUPENDE ❤️ 3 to 5
@majario LIVE

ACHA NIKUPENDE ❤️ 3 MTUNZI uhuru media Karibu WhatsApp 0794810082 Kwa jicho aliloangaliwa na Nicky ilimbidi aondoke haraka haraka akaenda jikoni huku akiwa kachukia na machozi yalimtoka bila kutegemea. Alipofika...

*KISASI CHA SINDELE BAADA YA KUAMBUKIZWA UKIMWI KWA MAKUSUDI*😭😭😭. *1-4* Post Mpya
*KISASI CHA SINDELE BAADA YA KUAMBUKIZWA UKIMWI KWA MAKUSUDI*😭😭😭. *1-4*
@majario LIVE

*_________________________________________* *Sehemu Ya 1* Ndani Ya hospital Moja kubwa wanaonekana Vijana wawili Wakiwa Wanasubiri Majibu Ya vipimo ambavyo Tayari walikuwa wamepima. "Hivi Sindele kwa mfano ikatokea Mimi nimekutwa nimeathirika utanioa au utaniacha!?" "Uuuuu...

🚩Rais wa klabu ya Al Ahly, Mahmoud El-Khatib, ametangaza maamuzi makali Post Mpya
🚩Rais wa klabu ya Al Ahly, Mahmoud El-Khatib, ametangaza maamuzi makali
@majario LIVE

ili kujaribu kubadilisha mwenendo wa timu katika Ligi ya Misri na CAF Champions League. 🔴 Maamuzi yaliyotangazwa: 💵 Kupunguzwa mishahara: Wachezaji wote wa kikosi cha kwanza watakatwa 30% ya mishahara yao,...

MIRANDA (Binti Yangu)   SEHEMU YA 15 Post Mpya
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 15
@majario LIVE

SONGA NAYO....... Mira mie nikaanza kupiga maombi ya kuteketeza roho ya umauti niliomba sana, jasho lilikuwa likinitililika na kulowanisha kifua Changu Nilikuwa nimezama kwenye ulimwengu wa roho nikifanya maombi, ni sauti ya...

Victor Osimhen alishindwa kujizuia na kutoa machozi..  FOOTBALL ⚽. Post Mpya
Victor Osimhen alishindwa kujizuia na kutoa machozi.. FOOTBALL ⚽.
@majario LIVE

Napoli walimchukulia kama takataka na kumfanyia ubaguzi, lakini Galatasaray wanamchukulia kama familia yao .. Hadithi ipi ni yenye huzuni kwa Victor Osimhen kwenye maisha yake , hadithi yenye huzuni ni kuhusu...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 43 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 43
@majario LIVE

Mi sikufanya ajizi, nikamuuliza kwani apa majirani zako hawapo, akanmbia mmoja alisafiri na mwengine kaenda kwao leo, wote hawapo, nikaona kazi leo, nisingekuja sijuh ingekuajee, ni mungu tu aliniongoza nije...

TIPWA TIPWA NA MR MARVEL 19 to 20 final Post Mpya
TIPWA TIPWA NA MR MARVEL 19 to 20 final
@majario LIVE

SEHEMU YA 19 🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋 Asubuhi Mr Marvel alipoenda chumbani kwa Noela kama kawaida yake ili kumuamsha, anakuta chumba kipo kimya, hakuna mtu wala baadhi ya vitu vya Noela havipo😳. Anadhani labda ameenda chuo...

AFANDE MILLAN😎 41 to 42 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 41 to 42
@majario LIVE

🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈 Sehemu ya 41 Basi bwana , zena alivyoniona mnazani alisimama,hapana bali ndo kwanza akaongeza speed ya kuelekea kwake ,na mm nikawa namfata kwa haraka ili asije akajifungia, basi zena akaingia...

TIPWA TIPWA NA MR MARVEL SEHEMU YA 18 Post Mpya
TIPWA TIPWA NA MR MARVEL SEHEMU YA 18
@majario LIVE

“Dad, Ninakupa masaa 24 Uchague. Ukimchagua Noela, huta niona tena. Lakini Ukinichagua mimi, utaachana na Noela then tutaendelea na maisha yetu kama zamani” Baada ya kusema hivyo, Salmon na mama yake...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 40 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 40
@majario LIVE

Basi mimi nikaludi nyumbani nipo stressed kinoma , yani mawazo yamenijaa mnoo, nawaza inakuwaje sasa demu ndo kashanikazia ,ila naumia mnoo kwa ile hali yake na bado anaendelea kufanya biashara...

AINA ZA MIZUNGUKO YA HEDHI KWA MWANAMKE NA SIKU ZAKE ZA HATARI.👇 Post Mpya
AINA ZA MIZUNGUKO YA HEDHI KWA MWANAMKE NA SIKU ZAKE ZA HATARI.👇
@majario LIVE

Kila mwanamke ana mzunguko wake lakini hii ndiyo mizunguko ambayo kila mwanamke lazima awe na mzunguko mmoja kati ya hizi:👇 1. MZUNGUKO WA SIKU 22. Huu ndo mzunguko mfupi kuliko mizunguko yote...

Mashabiki wa Kaizer Chiefs waumizwa na Kitendo Cha Rushine kusalia Simba SC Post Mpya
Mashabiki wa Kaizer Chiefs waumizwa na Kitendo Cha Rushine kusalia Simba SC
@majario LIVE

Baada ya jana klabu ya Simba kutangaza kumuongezea mkataba mpya wa mwaka mmoja beki wao kitasa Rushine De Reuck, baadhi ya mashabiki wa soka nchini 🇿🇦Afrika Kusini haswa wa Kaizer...

UTAMU WA KULA KUKU NA MAYAI YAKE   SEHEMU YA 19 - 20 Post Mpya
UTAMU WA KULA KUKU NA MAYAI YAKE SEHEMU YA 19 - 20
@majario LIVE

ENDELEA....... Madame Yustar alitoa amri mimba itolewe ili kuepusha laana kwenye ukoo wao. "Hapana siwezi kutoa mimba hata iweje" Mellisa alimvimbia mama yake. Saa ngapi asilukiwe akaanza kutembezewa kichapo. Nae hakukubali apigwe kilahisi,...

UTAMU WA KULA KUKU NA MAYAI YAKE SEHEMU YA 17 - 18 Post Mpya
UTAMU WA KULA KUKU NA MAYAI YAKE SEHEMU YA 17 - 18
@majario LIVE

ENDELEA......... Mipango yangu iliendelea kwenda vizuri. Nilifanikiwa kufungua duka langu la spea za magari mke wangu alikuwa nsimamizi mzuri. Japo hakuwa na elimu ila alikuwa na akili ya biashara sana na...

MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 14 Post Mpya
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 14
@majario LIVE

SONGA NAYO.... Niliwaona mama na baba yangu wakiwa wanamshangaa sana yani walishangaa mpaka wakanisahau mtoto wao kama naumwa 😂 Basi mimi niipomuona Anfrey nilinyanyuka na kwenda kumkumbatia " Nasrat wangu, yupo wapi mtoto...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest