WEWE NI WANGU SEHEMU YA 21
SONGA NAYO........
Hatimae mke wangu alijifungua baby boy, π₯° nyieeh hivi mnajua nilikuwa na furaha kiasi gani eeh yani iku hii mwanaume nilifanya kaazi mpaka ambazo nilikuwa sifanyi.
Kwanza niliingia jikoni nikapika kitu kitamu, π₯° baada ya hapo nikapiga deki nyumba nzima πππΎ mtaniona tu nimewehuka ila hakuna furaha kama kuitwa baba aiseee π₯°
Hii feeling wanaijua wale wanaume ambao wamesumbuka sana kutafuta mtoto, hii raha yake wanaijuwa walah hii siku mpaka mama alinishangaa, nilijikuta naongea mpaka kihindi pale nilipokabiziwa dume langu nyie π₯°
Mtoto wangu alikuwa mzuri bwana, ni miezi imepita toka nitoke kule mwanza so nikaoona sio mbaya kama nitamshtua rafiki yangu Jose
Basi nikachukua simu na kupiga, yani ni kama alikuwa ananisubiri ile nimepiga tu ikapokelewa
"Hello..??"
Sauti nzito na hii sauti ilikuwa ya Bony kabisa, kitendo cha kusikia sauti yake moyo ukafanya puh, nikaitoa simu sikioni na kutazama labda nimekosea namba, nikairudisha tena sikioni
"Shemu uko poa..??"
( π naota au vipi jamani, leo Bony wakuniita mimi shem..)
"Samahani nimekosea namba.."
Nilisema na kutaka kukata simu, akaniwahi
"Oya acha mambo ya kiwaki, me shemeji yako au umenisahau nasema mpe simu Lizy niongee nae..."
"Eeeh ah nampa..."
"Harafu kaa kama mwanaume bana, sasa kinachokufanya utetemeke hapo ni nini, mimi nimekubali tu uwe na dada yangu kama nisingekuwa nimekubali ningewafata huko huko..."
( π kwahiyo unazani songea ndio mwanza, we kama unataka kuja si uje ili nikuroge vizuri )
Nilijiwazia
"Unasikia naona umekaa kimya mpe simu Lizy nimsalimie hata kidogo basi.."
Nikaona isiwe kesi nikampelekea mama watoto.
"Vipi.."
Lizy aliniuliza.
"Ongea na kaka yako.."
Lizzy bila kujiuliza mara mbili mbili alipokea simu akiwa na furaha sana,
"Kakaaa"
"Lizy, umejifungua mtoto gani..?"
" wa kiume..."
" hongera sana mdogo wangu, saivi aitwa uncle..."
( ππ eti naitwa uncle, na wakati ulitaka kumtoa mtoto wangu, saivi ndio unajikuta mwema..." )
Nilijiwazia, basi mtu na kaka yake waliongea weee mpaka wakaanza kunikera sasa maana Lizy alijisahau kabisa kama ananmtoto maana mtoto alikuwa analia
Nilichofanya ni kuchukua simu na kukata kisha nikammpiga block, huyu jamaa simpendi toka ile siku yani hapa anajifanyaa amekuwa mwema ilì ananipate kirahisi hivi, mwambieni huyo ndugu yenu
Huku songea sio pakuja hovyo hovyo kabisa, sasa yeye alete uhuni wake huku aone anaondoka bila moyo.π
"Mbona umechukua simu..??"
Lizy aliniuliza.
"Unaongea na simu na kusahau kama mtoto anallia hapo, sasa basi huyu kaka yako sijui bony au nani, nakwambiaje hakuna kuongea nae tena mwisho Leo.."
"Lakini..."
"Nafikiri nimeeleweka..."
Nilimwambia na kuondoka zangu, sikuwa na amani kabisa kwa sababu tabia za bony sio nzuri hata kama ni kaka wa mke wangu aisee siwezi ruhusu kabisa akitane na lizy akiwa na mtoto.. .
***
Maisha yetu yalikuwa yenye furaha kubwa mtoti wetu alitimiza mwaka mmoja hapo sasa ndio nikafunga ndoa na Lizy rasmi akawa mke wangu
Kwa uwezo wa mungu niliweza kupata kazii kwenye shule nyinge huku songea, nilikuwa serious na kazi yale mambo ya kutongoza tongoza niliacha kabisa.
Nilimpenda mke wangu pamoja na mtoto wetu Acram, ngoja niwape sifa za mtoto wangu,
Dume langu bana lilikuwa lizuri arafu jeupe, π₯° alikua na mwili kama wa baba yake π₯° na kibaya zaidi huyu kijana alichonikera ni kuchukua tabia ya mjomba wake Bony π
Yani ukikuta kanaongea kama naongea na shemej yangu vile, japo ni mwanangu siwezi kumchukia kΓ mwe nampenda nampenda kijana wangu Acram, mungu akupe maisha marefu kijana wangu... ππ
Mpaka kufika hapa sina la ziada, mungu wabariki sana wale wote ambao mmekuwa nami katika kila hatua ya maisha yangu
Mungu awabariki sana sana tena sana, awaonyeshe njia zake za baraka na upendo....
MWISHO......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni