FROM BANGI TO BABY ππ SEHEMU YA 10
Veda huyu akatokeza nilikwepa macho fastaaa nikaangalia mbinguu, Tinner akanambia kwa sauti ya chiniii
"Kumbe shem sio haba nilikuwa sijamzingatia tu bonge la mwanaume jamani
"Nikashindwa kuvumilia ila nikajikaza kuchekaa sikujibu kitu midomo inatetemeka nikajikaza kweli nisimtazame Veda na ndo tukaw tumefika usawa wake .
Shingo iko ngaa inataka kugeuka kumtazama mie naikaza ile nampita tu kidogo nikajikuta nimegeukaa ..
Tukagongana macho, sijui nae alikuwa ananiangalia au bahati mbaya tu, akatabasamu lile tabasamu lake la pembeni, akanitikisia kichwa taratibu kama salamu sijui au alikuwa anamanisha nini mie sijui ila Sikujua nifanye nini shingo ikagoma kugeuka kunipa support natembea kiwili wili mbele uso wenye macho nimeacha nyuma, ikabidi nikaitikia kwa kichwa pia kisha.
Ndo akazidi kuachia tabasam mpaka nikaona vi meno kwa mbalii vyeupeee, Nyie hii nini tenaaa mie mjukuu wa babu na bibi yanguuu Huyu kijana ni nani hasa? Mbona moyo wangu unanichokoza hivi? Na umri huu jamani lakini nimekuwa kama mtoto wa form one alieanza kumendewa mendewa hajui mapenzi mie ama kweli mapenzi hayana umri haki tenaaa ..
"Shoga angalia mbele basi piki piki hiyo!!!!" Tinner akanishtua kwa kunisutaa, nikajikuta naona aibuu achaa, basi nikakaza mwendo nusu nijikwaee ...
Tukanunua mboga, Muda wa kurudi nikamwambia Tinner tubadilishe njia aisee akasema kisa nini sasa ???"
Nikamwambia "Sitaki kupita pale kila nikimuona huyo kaka nakumbuka tu alivyonibaka najisikia aibu kama alinidhalilisha "
"We naee, Sa ulibakwa hivi wakiitwa walio bakwa utaenda embu twende"
"Sitaki kuonana na huyo mjinga Tinner nielewe"
"Mh hayaa... njia ingine niya kuzunguka sana hapa mpaka boda ni mbali sana "
Bora tupite hiyo sitaki kabisaaaa kumuona huyo kakaa kama aliweza kunitumia mie bila ridhaa yangu ina maana anawatumia wengi halafu kwa Akili yangu tu ndogo niitumie kama anaongozana na Veda sehemu kama zile anashindwa vipi kununua wanawake inamaana yeye na Veda wote lao ni moja sa sitakiiii kashanitumia basi hasara kwangu, Tukachukua usafiri wa Boda tukarudi kwa njia ingine kabisaa ....
Usiku ulipofika, nikajikuta namuwaza tena, Lile tabasamu ule muda akanitikisia kichwa alikuwa anamaaisha niniii ...
Jamani huyu kakaaa nilikuwa nagala gala tu hukuu mpaka hukoo nikaanza kujuta kwanini nilibadilisha njia et haha si ningepita tu pale nikamuona Duh nikajukuta naongea mwenyewe
"Kutoka bangi⦠hadi baby? Dadeek" Nikacheka mwenyewe kitandani, nikajifunika shuka mpaka puani.
Mapenzi shikamooooo mtu mzima miee yamenirudisha utoto kabisaa ile unatamani kujipitisha mbele ya kijana hahaha wote tumepita huko eeh tumepita bwanaa .....
Basi asubuhi nikajiandaa zangu kuingia kazini na sikuwa hata na nguo maana niliondoka mwenyewe tu bila kujiandaa, nikachukua nguo za Tinner, Mwenzangu mbaba wake amemkataza kufanya kazi mwenzangu nae kweli kaacha, hayaa ngoja yamkute kama yangu atajijua mwenyewe..
Kwakua sina tena gari, Tinner akaniitia tu Boda, Basi tumefika pale chini wanakaaga wale wakaka si nikamwambia apunguze mwendo macho kupu kupuu namtafuta Veda hata hakuwepo kulikuwa na wakaka na wababa wanabishanaaa kuhusu mpira asubuhi asubuhi tu jamani sijui wanawaza nini mmh
Mie nikaenda zangu kazini, Ila ile kutokumuona Veda pale nikajikuta siku nzimaa namfikiria yeye tuu najuta kwanini sikurudia ile njiaa ...
Muda wa kutoka kazini nikaona ngoja tu niende kwangu maana D hakuwa amenitafuuta tangu ile jana nikaona amepotezea kuhusu mie, Nikarudi nyumbani ajabu nakuta Geti limefungwa mmh , funguo ninazo mie sasa nani amefunga geti, ikabidi nimpigie mwenye nyumba kumuuliza huenda ana funguo za dharula akasema mume wangu ndio kamwambia afunge na asifungue mpaka yeye atakapo sema kama nina shida ya kuishi humo ndani nimtafute yeyee duuh nilichokaaa ...
Kwa muda huo akili yangu ilikuwa imevurugika kweli kweli kwa hili swala kufungiwa nyumba, ikabidi tu nichukue Boda mpaka kwa Tinner , nimechanganyikiwa
Tinner akanishauri tumpigie tu ili nimsikilize anataka ninii kama vipi aniache nichukue vitu vyangu nimuachie nyumba yake, nikampigia kawaida hapatikani ikabidi nimpigie wasp call akapokea, tena kapokea anacheka kweliii yaani kama vile anaona ameniweza sanaa ..
Nikamwambia mie wala simuhitaji tena naomba tu nichukue vitu vyangu nikuachie nyumba yako akanambia Kwasasa nimesafiri nipo kenya ila nikija nitakutafuta sasa ole wako usipokee simu yangu, kinyonge na hasira nikasema sawa ...
Itaendelea.....
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni