FROM BANGI TO BABY ππ SEHEMU YA 9
Nikamuona D anatoka kwenye geti nikamwambia Boda tuondoke Boda akatimka hata hajui naenda wapi, sikuwa tena hata na mood ya kwenda kazini .
Nikanyoosha mpaka kwa Tinner, alishangaa kuniona asubuhi asubuhi tu nyumbani kwake
"We kwemaaa!!!??"
"Hata sio kwema embu nikaribishe hata ndani basiii daah" nikapitiliza ndani moja kwa moja nikajitupa kwenye kochi li pochi nikatupa hukoo akili ilikuwa imechoka mnoo
"Enhee nambie mwenzangu" Tinner akaja kukaa pembeni yangu huku shingo kaichachamaza kweli anataka nimwambie
"Mh!!! Hata sio ya kuongea"
"Umeanzaaa..... hivi hapo unataka nikubembeleze weeee yaani nikurambe rambee ndo uongee"
"Hahah ushaanza mambo yako, Mwenzangu jana mie huyo nimekupuka mbio mbio naenda kwa D tenaa, Nimemiss mkong'onto wa dudu ...."
"Mhuu!" Tinner akajitengeneza vizuri na mikono akailea ka anasubiri mkate wa bwana
"Yaani hata sijui nianzie wapii ninalizie wapi "
"Embu endelea bwana "
"Mwenzangu D nimemkuta na wanawake watatuuu upoo tena wotee analala nao yeye maana walivyokuwa wanampeti peti na kwa ile pichaa wale watu wanajuana yaani ndio tabia yake mjinga yule kalewa chakariii ......"
"Mungu wangu, D huyuu chaufupi wako?? Mbona namuona mstaarabu sana kumbe na pombe ana kunywa"
"Eh...... mie ndo nimeona juzi na jana sijawahi hata kumuhisi kuwa pombe anakunywa na anafanya ujinga wa kiwango cha lami vile .... mie ndo kuanzisha ugomvi tena dadaa D huyo kanifukuza mbio mbio, kumwambia Veda aniondoe, Tinner nimelia mie jana Roho imeniumaa Basi tu yaani D huyo hata sikumdhania kabisaaaa ...."
"Daaah ... pole sanaa ila wanaumeee sijui wanajikuta kina nani tu jamani dah pole, Enhee ikawaje Ukatembea na Veda tena"
"Mwenzangu Veda kanibaka "
"Hahahah Hapo ndo napatraaaaakaaa nipe hizo nyuuuuz maana naona uso hadi una nuruu hahaha kwa hilo fumanizi ungekuja hapa leo unalia hadi kamasi ila umekuja na uso wa bashashaa hahaha embu nipe nipe mamaa nipo lelee lelee hapaa"
"Hahaha Mjinga wewe .... yaani nilikuwa nahasiraaa basi Veda nae amekazana et kunifukuza nje daah wacha nianze kumtukanaaa ........" wakati namuhadithia Tinner alikuwa anachekaaa yaani anacheka mpaka anaishiwa pumzi anaanguka kwenye kochi anainuka ikabidi tu na mie niwe nacheka kila nikimuelezea Veda alivyoniingilia bila ridhaa yangu jamani ndio najikuta sasa najenga picha mpya kichwani kuhusu Vedaaa nyie anabonge wa mkono ila alivyokuwa ananipapasa sasa uwiiiihhh
Nikajikuta natamani kumuona hapo sasa hiviii yaani nikawa kama nina hamu nae hatari ...
"Weee kifupi kaka ma bangi Fundiiii "
"Hahaha acha mambo yako bwanaa, Sio sanaaa ila anajitahidi"
"Sema ukweli D na Veda nani anajua kulicheza sebele mazuka vizuri "
"Hahaha Vedaaa haha ile sio ndio namsifiaa useme namtakaa aah wapiii Mie na Mvuta bangi ni mbali mbaliii"
"Mie kuanzia leo Veda ndio shem languuuu yaani Mitano tena kwa kaka Veda na nikipita hapo nikimuona namuita kabisa Shemmmmm hahah'
"Afu Tinner sitaki ujueee"
"Usinambia tu unampango wa kurudi kwa huyo jifupi nyundo wako na kitambi chake kaa anashambuliwa na minyoo"
"Hahaha leo hiyo Tinner, "
"Aah kanikeraa afu nilikuwa tu namvumilia kwasababu ndo shemeji nitafanya ninii ila mmh aende huko mfyuu, Vero usije kurudi kwake huyo sio mwanaume ni mshenzi huyoo achana nae mungu kakuonesha mapemaaa sasa jifanye atajirekebisha shauri yako ...kama shida ni kodi ikikushinda hama hapo maishe yanaendelea..."
Nikashusha pumzi ndefu maneno ya Tinner ukiacha utani wake yaliniingia kichwani, kama anaweza kulala na wanawake watatu usiku mmoja atashindwa kunipa ma ukimwi kwa maksudi kwelii?? Nilijifiriia kidogo haswa kuhusu kulipa kodi maana pale yeye ndie alinipangia baada ya kunihamisha nilipo kuwa anaishi mwanzo ndio akanipangia na kila kitu yeye ndio anajumuika kwangu ..
Lakini nina kazi yangu na nilikuwa naishi kabla yake kwahiyo hata akienda nitaishi tu bado hizi picha mbili nilizo ona zinatosha kabisa kunitoa kwenye giza ..
"Nitakaa hapa kwako hii wiki najua atasafiri wiki hii hii tu akiondoka na mie nitarudi kwangu kodi ikiisha nitahama "
"Hamaa njoo tukae hapa wote hata usiende kupanda si unaona hii nyumba ilivyo kubwa afu nipo tu mwenyewe "
"Aah wee sifanyi hiyo kazi bwana"
"Ndo kama kawaida yako hutaki uswahilini"
"Sio hivyo ila ukiachwa tunaanza tena kuhangaika na mzigo aah sitaki!"
"Hahaha we mwehu kweliii......"
Siku enyewe nilipiga tu simu kazini nikaomba ruksa ya dharula kuwa naumwa gafla tu homa imenishika asubuhi basi nikapewa ruksa ya siku mbili, Ila siku ikaisha nipo tu ndani kwa Tinner, D alikuwa anapiga simu mara kwa mara ila hata sikujiangaisha kupokea wala kuzima na alikuwa hajui nipo wapi uzuri ndani kwangu nilikuwa nimefunga nilicho acha wazi ni geti tu kwahiyo sikuwa na ma shaka na usalama wa kwangu ....
Siku ikaisha ikaja siku inayofata niliamkia pale pale kwa Tinner, Jioni Tinner akanambia embu twende ukatembee tembee huko sio kukaa tu ndani kama utumbo twende ukapate hewa upunguze mawazo yako ..
Basi tukatoka tumashusha kile kilima alinambia twende akanunue mboga, Ile namaliza tu kushusha kilima hapa na hapa Veda huyu anatokeza akaenda kukaa kwenye Bench chini ya mti, Jamani moyo wangu hati hati miee, Muda wote upo juu juu kama umepanda ndege
ITAENDELEA....
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni