Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

6 - 10🚩🚩🚩🚩🚩🚩 𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞

2nd Aug, 2025 Views 7

:06

Dada alisema “mimi ninamuamini sana yule dada. Sio mtu wa polepole. Hawezi kunidanganya tena baada ya kumuonesha picha yako alikusifia sana kuwa unafaa sana na alipenda mno ngozi yako. Mimi ninayo imani tumpe muda. Ila mdogo wangu, kamwe tusije msahau huyu mzee hapa.”

Nilitabasamu nikisema “siamini hata, tusubiri kesho tu.”
Dada alicheka akisema “sasa lala, kesho tutampigia atuambie nini kinaendelea.”

Nikamkumbatia dada yangu, kisha nikashika mikono ya dada yangu na kusema “Asante sana dada yangu. Nakupenda. Nashindwa kuongea ila una moyo mzuri. Unapenda mdogo wako nipate. Unanipambania sana.”

Dada alitabasamu na kusema “wewe ni mdogo wangu, sisi ni damu moja, tumelala tumbo la mwanamke mmoja. Na mimi ni kama mama na wewe pia ni mama yangu. Tunaleana. Nakupenda sana Ndeana wangu.”

Nikatabasamu tu dada yangu alikuwa akitoka akiwa na furaha huku akisema ulale sasa mrembo wa familia.
Mimi nikacheka tu.

Siku ile nikalala nikiwa nina hamu ya kufika siku mpya. Yaani ninalala ni kama naota siku inayofuata vile. Niliamka kwa kuchelewa kidogo nilikuta dada kafanya kazi basi nami nikamuandalia baba chai. Baada ya hapo nikamuuliza dada “kuna hata dalili dada?”

Dada akacheka akisema “alisema saa tano na wewe ndiyo kwanza unauliza saa mbili. Acha mambo yako.”

Nikamtazama dada kwa kudeka nikisema “si nauliza tu dada unajua sijalala mwenzako usingizi nimepata asubuhi ndiyo maana nimechelewa kuamka.”
Dada akacheka akisema “uvivu tu huna lolote subiri hiyo saa tano.”
Dada akaniacha nikaendelea na kazi zingine.

Nikikumbuka natamani hata kucheka yaani, kwasababu nilianza kujipa kazi ambazo hata sikutakiwa kufanya ili mradi tu muda uende. Mpaka saa tano inafika dada hakusema lolote lile. Nikamwambia dada “mmh mpaka sasa kimya nilijua tu zile sehemu wanapeana sana kazi.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:07

Dada hakujibu badala yake akapiga simu. Simu ile iliita na haikupokelewa na baadaye ukaingia ujumbe. Dada akasoma na kisha akanipa na mimi nisome. Ujumbe ulitoka kwa dada Posta ndiyo dada yangu alimsave huyo dada, nami nikasoma. Aliandika “nakukumbuka kipenzi, nimetingwa kidogo hapa ila usikae mbali na simu yako.”
Nikatabasamu. Dada akaniuliza “mbona tabasamu.”
Nikasema “itakuwa safi eenh mbona usikae mbali na simu.”
Dada akacheka akasema “ndiyo tusubiri tujue mbivu na mbichi.”
Nikatabasamu.

Basi hata muda ambao simu ya dada iliita nikijua ni huyo dada Posta haikuwa kiasi hata dada alisema “tulia mdogo wangu, usipopata tutatafuta kwingine. Najua ni ndoto yako ila kuwa na utulivu.”

Mimi nilimtazama tu dada na kuitikia huku ndani ya moyo wangu nikisema “Mungu naomba usonipite kwenye hii nafasi.”

Hata sikuwa naelewa vipindi vya Tv yetu ndogo ya chogo vilivyokuwa vinaendelea pale sebuleni. Mara nyingine tena simu iliita. Dada alinitazama na kusema “anapiga.”
Nikashtuka haraka nikatoa sauti kwa tv nikisema “weka loudspeaker dada.”
Dada alipokea na kusema “niambie rafiki yangu.”

Nikamsikia akisema “aisee mdogo wako ana nyota kali. Unajua boss wa hiyo Hotel leo ndiyo nimemtafuta na nikaenda kukutana naye.”
Dada sasa akawa anatabasamu huku mimi natetemeka, dada anasema “eenh niambie shoga imekuaje.”

Yule dada akasema “nakuambia nilipomuonesha tu picha, akaniuliza huyu mdogo wako, na anapenda mambo ya hotel. Sasa mbona husemi. Hawa ndiyo vivutio kwa wateja.”

Dada yangu akasema “wewe usiniambie, ina maana amekubali?”
Yule dada akachrka akisema “unajua nilipokuwa nakuja nilijua ataniambia habari za Corona ila huwezi amini, unajua alichosema?”

Mimi hapo natetemeka, naogopa natamani nipige kelele za furaha. Dada akawa anachekelea akisema “niambie sasa, niambie Boss kasemaje?”

Yule dada akasema “hongera sana una mdogo ana mvuto sana. Boss amesema kama ana muda leo leo nimepeleke pale. Nimkutanishe na meneja na kisha meneja ndiyo atajua cha kufanya.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:08

Dada akauliza “hivyo tu basi?”
Yule dada akacheka akisema “na vyeti vyake tu, ni hivyo tu kwahiyo mpe mrembo wetu namba yangu kama ana muda leo leo aje. Kama hana basi siku nyingine.”
Kwa furaha nikajikuta najibu “nakuja dada, nakuja.”

Wakaanza kucheka huku wakiambiana namna nimechanganyikiwa. Nyie, nyie jamani. Kupata kazi ni amani, ni raha sana. Nilifurahi nikimkumbatia dada yangu, nilitokwa machozi nikipiga kelele za asante Mungu. Hakika ilikuwa ni furaha sana huku dada na yeye alipomalizana na shoga yake alikuwa akiniambia “hongera mdogo wangu, kajiandar sasa.”

Nilimtazama dada nikisema machozi yakitoka “siamini eti dada, nimefurahi sana,”
Dada alinikumbatia tena na kusema “Ndeana wewe ni msichana mzuri sana. Nakuambia kila siku na unaipenda hii kazi. Niamini utafanikiwa sana.”
Basi nilimkumbatiana dada na Asante nyingi sana.

Dada yangu aliniambia “kajiandae sasa unachelewa sana.”
Nikamuuliza “baba yuko wapi sasa nimuambie.”
Dada akacheka “baba yako umkute saizi kweli. Nenda kajiandae kwanza.”

Nikakimbilia chumbani kwa haraka, nikavua nguo na kuvaa kanga na kisha nikatoka mpaka kwenda bafuni. Haraka haraka nikaoga na nilipotoka nikachagua moja kati ya gauni ninazopenda sana nikavaa, nikavaa na viatu vyangu mchuchumio, nikabeba na pochi mtoto wa kike.

Ingawaje vitu vyangu havikuwa vya bei ghali ila vilinikaa, nikapendeza nakumbuka hata dada yangu aliponiona alisema “wacha wacha wacha, mdogo wangu katika siku umependeza wewe umependeza sana. Nimefurahi.”

Nikatabasamu tu. Dada akanipa maelekezo yote muhimu, kisha aliniambia “njoo nikupe baraka mdogo wangu.”

Nilisogea na dada alinikumbatia, namjua dada yangu alikuwa ananiombea kimoyomoyo tangu nikiwa mdogo hupenda kufanya hivyo na alipomaliza nikajibu “Amen dada Vee.”
Akatabasamu.

Kwa namna nilipendeza hii siku haikuwa ya kupanda daladala kusema kweli. Nikajikakamua nipande bajaji kwa kukodi. Kwa maana nilikuwa poa sana.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:09

Hii bajaji ilinifikisha mpaka mahali yule dada alisema tukutane kwa maana alisema yupo nje kikazi siku hiyo. Hivyo nami nikafuata maelekezo.

Nilifika hiyo sehemu aliponiona tu, alitabasamu na kuniita “Ndeana!!”
Nami nikaitikia “dada!!”

Akaniangalia akitabasamu nami nikimsogelea. Nakumbuka aliniambia “kumbe kuna wasichana wazuri hivi. Ndeana wewe ni mrembo.”

Nikamjibu kwa upole “Asante sana dada.”
Akaniambia “Naitwa Martha, niite dada Mar”
Nikatabasamu tu na yeye akatabasamu.

Tukawa tunaelekea kwenye gari na yeye akaniambia “nimekupenda, unaonekana upo makini sana. Mwingine angejivuta tupigiane simu mpaka. Ndeana ukiendelea hivi utafanikiwa. Nidhamu ndiyo kila kitu kwenye haya maisha.”
Nikamwambia kwa tabasamu “nashukuru sana dada Mar.”

Akanitazama tu na tabasamu akaanza kuendesha gari huku tukiongea kuhusu dada Vanessa na tukajikuta tunacheka kama vile tunajuana zamani sana. Nakumbuka sana, tulifika maeneo ya ilr hotel ya ndoto. Kabla hatujaingia alisema “Usiwe muongeaji sana, mimi ni dada yako mtoto wa shangazi wako. Hivyo tu mdogo wangu.”

Nikaitikia huku natetemeka. Sehemu naiona kwa picha sasa naenda na nitafanya kazi hapa. Sio ndoto ni kweli. Mpaka tunashuka kwa gari siamini natazama huku na kule, naangalia huku na huku. Aiseee!!, Aiseeee!!! Tanzania hii ina majengo, kuna watu wanalala pazuri sana. Mandhari ya sehemu hii ilizidi furahisha macho yangu.

Basi mimi namfuata tu huyu dada. Yeye pale anaonekana mwenyeji sana. Kwa maana anasalimiana vizuri na watu wa pale na mambo kama hayo, Kisha moja kwa moja tukaelekea ofisini kwa meneja.

Meneja aliponiona akawa ananishangaa. Huyu dada Mar akauliza “mbona kushangaa hivyo, mgeni wenu huyu. Mimi nina haraka. Naomba mpeleke kwa boss wako. “

Kisha akanitazama na kusema “mdogo wangu kama ambavyo nilikuambia leo sijatulia nna kazi nje ya ofisi. Tafadhali kuwa mtii, sikiliza na kisha utaambiwa utaratibu.”

Nikatabasamu tu. Kisha huyu dada mzuri akaagana na meneja ambaye pia kiumri ni mkubwa kwangu na tulianza kuelekea ofisi nyingine ni mwendo wa lift tu. Mimi nafuata tu maana nashangaa kila kitu.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:10
Tukiwa kwa Lift huyu meneja akaniuliza “unaitwa nani?”
Nikamjibu “Naitwa Ndeana.”
Akaniambia “una jina zuri sana. Una ahadi na boss,”
Nikamjibu “Ndiyo.”
Akaniambia “sawa, karibu.”
Nikamjibu tu “asante.”

Tulifika mpaka korido la hiyo ofisi. Aliniambia nisubiri nje kisha yeye akaingia huku mimi nampa habari dada yangu kwa simu. Na baada ya muda kidogo, alitoka na kusema “Unaweza kuingia sasa.”
Nikatabasamu na kusema “Asante.”

Basi yeye akaondoka na mimi nikavuta pumzi na kuingia. Ooh!!, ofisi ni safi, imepangwa vizuri sana. Pananukia mno. Na kuna mwanaume alikuwa amekaa tu kwenye kiti ameinama. Niliingia taratibu. Kisha kabla sijasalimia, huyu mwanaume aliinua kichwa chake.

Eeenh!!, wacha nivute pumzi. Huyu mwanaume ni bonge la bwana, yaani anakuaje bosi mbona kama bado mdogo ingawa kwangu mkubwa kama miaka kumi na zaidi hivi, ila kuwa boss wa Hotel ile ni inawezekana vipi.

Nikawa nashangaa namna alivyo na muonekano wa kuvutia. Na hata yeye niliona uso wake ukinisaili kuanzia chini mpaka juu. Kisha kwa sauti ambayo ni wazi alitoa hila kukusudia alisema “waoooh!!, waooo!!”

Yaani tunashangaana kiasi hata sasa naogopa, ilibidi nisalimie “shikamoo!!”
Akatabasamu, uwiii!!, anao mwanya fulani hivi na meno meupe, anatabasamu sijawahi kuliona. Ni zuri sana tabasamu lake, akaniambia akijibu salamu “Marahaba beutiful, karibu sana.”
Nikasema “nashukuru sana.”

Huyu mwanaume aliniambia “unaweza kuketi sasa.”
Nikaketi. Nilipoketi alisema “Naitwa Stewart, and you?”
Nikamtazama kwa tabasamu nikajibu “Ndeana.”

Akanitazama kwa muda akitabasamu na kisha alianza kutaja jina langu mfululizo “Ndeana!!, Ndeana!!, Ndeana!!. Unajina la kushangaza kama ulivyo wewe. Karibu sana.”
Nikatabasamu, na yeye akatabasamu akiniambia.....
eeemh itakuaje sasa🤣🤣🤣🤣💃🏻💃🏻💃🏻.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

6 - 10🚩🚩🚩🚩🚩🚩 𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞  >>> https://gonga94.com/semajambo/6-10-jamani-boss-mi-naona-aibu
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest