BETWEEN SISTERS AND SECRET Chapter 19
Mia alimuangalia Gael, alisogea karibu akajilaza kwenye kifua cha Gael.
Gael alitabasamu, akamkumbatia Mia kwa
nguvu.
Walijikuta wamelala huku wamekumbatiana.
Mida ya saa mbili asubuhi, mlango wa chumba cha Gael ulifunguliwa. Mira aliingia, akasimama mbele ya kitanda,
"Hongera sana, hongera! Nilijua tu ni lazima huyu changudoa atafanya hivi!"
Sauti ya Mira iliwashtua Gael na Mia kutoka usingizini.
"Mira..." Mia aliita kwa uoga.
"Mira umefuata nini nyumbani kwangu?” aliuliza Gael kwa kufoka.
"Gael, ivi leo unaniuliza nimefuata nini kwako.
kweli?
Kwani umesahau kama sisi ni wapenzi? Homa imekufanya upoteze kumbukumbu?" Mira aliongea kwa kulalamika.
"Mira, ondoka nyumbani kwangu!" aliongea Gael kwa amri.
Mia alitaka kuondoka, lakini Gael akamzuia..
"Hauwezi kwenda popote, Mia."
"Gael, mimi siwezi kuondoka, anayetakiwa kuondoka ni huyo malaya!"
Gael na Mia waliangaliana.
Mira alitaka kumvamia Mia, Gael akamzuia.
"Kama umechoka kuishi kwa amani, basi mguse
hata ukucha wake utanijua mimi ni nani!" Mira alimuangalia Mia kwa hasira, akaondoka.
Mia,
"Gael, kilichotokea kati yetu jana ni makosa,
naomba usahau kila kitu,
na mimi nitafanya hivyo hivyo."
Mia alivaa nguo zake, akaondoka.
"Nimekuacha uondoke, Nitakufata tena na tena,
lakini bado siwezi kukata tamaa.
siwezi kukata tamaa penzi langu kwako." Gael aliongea huku anatabasamu.
Kwa upande wa Mia, alifika nyumbani akaingia bafuni, alikaa muda mrefu.
"Shoga, mbona kama haupo sawa?" Furaha alimuuliza Mia.
"Atakuwaje sawa na unamuona alivyo, alisema Judith.
"Nauliza kwa sababu nataka kujua kilichomfanya.
awe hivyo,"
alisema Furaha.
"Eti kipenzi, umepatwa na nini? Dora alimuuliza Mia.
"Aaaah, natamani hata kuondoka kwenye huu
mji,
Mia alikaa kitandani.
"Kwanini?"
"Mimi na Gael jana tumelala pamoja, na Mira alitukuta asubuhi.
Alitaka kuleta ugomvi ila Gael akamfukuza.. Hapa sijui Mira atanifanya nini,
naogopa sana."
"Unampenda Gael?" Judith alimuuliza Mia.
"Nahisi kama nampenda.
Sikuwahi kujihisi hivyo kabla ya kukutana naye
na kuwa karibu naye."
"Kama unampenda sasa unaogopa kitu gani? Mira ameichezea hiyo bahati ya kuwa na Gael
kwa kumcheat na ex wake, na sio makosa yako wao kuachana," alisema
Dora.
"Ndiyo ni kweli, mimi nakubaliana na Dora.
Acha kumuogopa Mira na upambanie penzi
lako," alisema Furaha.
"Nyie naona mnanishauri vibaya.
Mnajua kabisa Mira ni dada yangu na mchumba
wa Gael,
na hii inamaanisha wamewahi kulala pamoja.
Afu na mimi niende pale pale kula makombo ya
dada yangu?
Kweli mimi hata sitaki,
nitajitahidi nimsahau Gael."
"Kipi ambacho hukijui tena kwa Gael? Si ni wewe mwenyewe umesema umeshalala
naye?"
Mia aliangalia chini kwa aibu.
"Acha ujinga, shoga yangu.
Mira amempotezea muda kaka wa watu,
na Gael anakupenda, na wewe unampenda.
Sasa kwanini ujitese?"
"Eti kwanini ujitese?
Embu pambania penzi hilo.
Na hata hivyo Mira hakuwa mke wa Gael,
walikuwa wachumba tu,
na wazazi wake hata hawakumkubali."
"Mnamsema sana Mira mbele yangu.
Mmesahau kama ni dada yangu?"
"Mtu akifanya mabaya ni lazima yasemwe.
Haya, twende tukanywe chai," Furaha, Dora, na Judith walielekea sebleni.
"Sijui kama nitakuwa sahihi ama la, ila ukweli ni kwamba nampenda sana Gael.
Nisamehe sana, Mira." Mia alijilaza kitandani,
alitabasamu kila alikumbuka kilichotokea kati yake na Gael usiku wa jana.
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni