Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya โ€“ Gonga94 Semajambo

EPS 1 SIMULIZI;MCHEPUKO WA RAIS
Gonga94 ยท Stories

EPS 1 SIMULIZI;MCHEPUKO WA RAIS

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
EPS 1
SIMULIZI;MCHEPUKO WA RAIS
________________________________
CHAMA HURU MEDIA

**
UTANGULIZI
Saa tatu na dakika ishirini usiku,ndani ya Chumba cha hoteli namba 45 yenye hadhi ya nyota tano,alionekana mwanaume (37) akiwa amesimama pembeni ya kitanda huku mikono yake na suti nyeusi aliyovaa imetapakaa damu,mwanaume huyu anafahamika kwa jina la Grayson Mwailubi,kifua na mwili wake umejengeka kwa mazoezi,macho yake yalikuwa yanatazama juu ya kitanda kilichopo ndani ya hiki chumba.

Mbele ya mboni za macho ya Gray alionekana mwanamke mrembo akiwa amelala chali huku damu zinamtoka tumboni ,mwanamke yule alikuwa amevalia shela nyeupe ya harusi ambayo nayo ililowana damu zinazotoka tumboni kwake.

Gray akaitazama mikono yake kwa hofu kubwa kisha akasema
"Leyla nisamehe,hakuna mwanaume ambaye angelivumilia upuuzi ulioufanya,utanisamehe" (akavuta pumzi na kuishusha)

Leyla (30) alikuwa amepoteza maisha baada ya kuchomwa kisu mara nane tumboni na mume wake Gray, tukio hili limetokea masaa machache baada ya wawili hawa kufunga ndoa na kuwa mwili mmoja.

Wakati Gray akiwa anautazama mwili wa marehemu mke wake Leyla, mlango wa chumba alichopo ukaanza kugongwa,Gray akayatoa macho mithili ya mjusi aliyebanwa na mlango.

{"Ngo.. Ngo...ngo"}ร—3
Gray akautazama mwili wa mke wake uliolala kitandani, akautazama mlango huku akihema kwa hofu kubwa,akajitazama suti yake akaziona damu nyingi zikiwa zimetapakaa,Gray akashusha pumzi halafu akajikaza kupaza sauti.

"We nani?"

Sauti ya kiume ikasikika upande wa pili
"Mimi ni Mohamed rafiki yako,njoeni basi ukumbini tunawasubiri tumalizie sherehe yetu"

Gray akageuka tena kuutazama mwili wa marehemu mke wake,akavuta pumzi na kuishusha ili Kupunguza hofu.
"Sawa mohamed nakuja"

"OK,mwambie na shemeji awahi"

"Poa"

Sauti ya hatua za miguu ya mohamed ikasikika,bila Shaka alikuwa anaondoka eneo hili,Gray akashusha pumzi baada ya mohamed kuondoka nje ya mlango wa chumba alichopo ,Gray akasogea haraka kitandani alipolala marehemu mke wake,akakichukua kisu kilichotumika kufanyia mauaji,kisu kile kilikuwa kando na mwili wa Leyla,Gray akakitupa kisu uvunguni Mwa kitanda halafu akaanza kukusanya nguo zake ili akimbie.

Akiwa anajiandaa kutoroka eneo hili mara ghafla ving'ora vya magari ya askari polisi vikaanza kusikika kwa nje,Gray akapatwa na mshituko mkubwa maana amefanya tukio la mauaji ya mke wake dakika chache zilizopita,kabla hajakimbia, ving'ora vya askari vimeanza kusikika nje ya hoteli aliyopo.

**
TUANZE SASA........
Magari ya askari polisi yapatayo sita yalifika hotelini,askari polisi wakashuka ndani ya Gari wakiwa wamebeba silaha zao,Mkuu wa hii operesheni, Inpekta Alexander Dickson (40) akatoa amri kwa askari polisi wazunguke hoteli na wengine waingie ndani ya hoteli.

Hoteli hii ilikuwa ya kifahari na imejengwa kwa ghorofa nne kwenda juu ,ghorofa ya kwanza ni Mapokezi,ya pili ni Sehemu ya kupata Chakula,ghorofa ya Tatu ni ukumbi wa mkutano pamoja na sherehe, kwenye hii ghorofa ya Tatu ndio kulikuwa na sherehe inayoendelea ya Gray na Leyla.

Wageni waalikwa hawakuwa wanafahamu kilichotokea ghorofa ya Tatu kwa Bwana na Bibi harusi,wao walikuwa bize kuucheza muziki huku wakiwasubiri Bwana na Bibi harusi wafike ukumbini kwa ajili ya kuendelea na sherehe,Meza kuu ilipambwa kwa Maua mazuri pamoja na picha za Gray na Leyla wakiwa wamevalia mavazi ya Harusi tena katika 'pozi' la Mahaba.

Askari polisi walikuwa wamefika ghorofa ya pili ambapo kulikuwa na watu mbalimbali wakipata Chakula na vinywaji.Inspekta Alexander Dickson aliwaondoa hofu wateja maana wameogopa baada ya kuona askari polisi wametapakaa kila kona.

"Naitwa Inspekta Alexander Dickson, ni mkuu wa kitengo cha upelelezi wa mauaji,niwaondoe hofu lakini hakuna mtu anayeruhusiwa kutoka nje mpaka pale uchunguzi wetu ukikamilika,Asanteni" Inspekta Alexander Dickson akaelekea zilipo ngazi,akapanda kuelekea juu,wateja walipigwa na butwaa, kila mmoja alikuwa na maswali mengi imekuwaje Inspekta Alexander Dickson afike hapa,jina la Alexander Dickson ni miongoni Mwa majina mashuhuri nchini Tanzania kutokana na utendaji kazi wake.

Alexander Dickson akafika ghorofa ya Tatu ambapo kulikuwa na sherehe inayoendelea,akakuta askari polisi wenzie wameshafika muda mrefu na wamewaambia wageni waalikwa watulie,muziki ulizimwa Kama disko linavyoingiliwa na Masai.

Inspekta Alexander hakutaka kupoteza muda ,akapanda ngazi haraka Sana kuelekea ghorofa ya nne ambayo inavyumba vya wageni maalumu (V.I.P),na kwenye moja ya chumba yupo Gray na mwili wa marehemu mke wake Leyla.

Alexander akafika mpaka kilipo chumba namba 45,chumba ambacho muda si mrefu kuna mauaji yametokea,Alexander Dickson aliwakuta askari polisi wenzake wapatao nane wakiwa wamesimama pembeni ya mlango huku wamezielekeza silaha zao kwenye mlango wa chumba namba 45.

Alexander akapaza sauti.
""Tumekuzingira. Tafadhali toka nje kwa mikono juu na usalimishe silaha yoyote uliyonayo,tunataka kumaliza jambo hili kwa amani,nakupatia sekunde 30."

Ukimya ndani ya chumba ukaendelea kutawala,Alexander Dickson akatoa amri ya ishara kwa askari wenzake waingie ndani maana sekunde 30 zimepita,Askari polisi watatu wakausogelea mlango kisha wakaupamia,Mlango ulipofunguka askari polisi wakaingia ndani ya chumba namba 45,cha ajabu hawakumkuta Grayson bali walikuta mwili wa Leyla ukiwa umelala kitandani.

SEHEM

"inaonekana kapita dirishani" (sauti ya askari polisi mmoja wakati akichungulia nje ya dirisha)
Ghorofa ya nne,haikuwa rahisi kwa Grayson kuruka kutoka juu asipoteze Maisha.

Alexander Dickson akatoa simu (Redio za mkononi),akasema
"BOLO" (Be on the lookout) ikiwa na maana ya kutoa taarifa kwa askari polisi wote waliopo eneo la tukio kuwa makini na kumtafuta mhalifu,kitu ama Gari alilotumia kutorokea.

Askari polisi wakawaamru watu wote wakae chini ili wafanye uchunguzi wao,watu wote wakatii agizo liliotolewa na askari polisi.
Alexander Dickson akashuka haraka mpaka ukumbini,akakuta watu wote wamekaa chini,wengine wakiwa wamelala kifudi fudi kwa uoga,Alexander akapaza sauti akisema
"Naomba wazazi wa Bwana harusi wasimame"

Alexander akawa anatazama huku na kule,Bibi mmoja mwenye umri wa miaka karibia sitini na tatu akasimama kwa hofu,alikuwa ameshona nguo zake kwa kitenge, kwa mwonekano anafanana fika na Bwana harusi Gray.

Alexander akamuona Bibi yule
"Wewe ndiye mzazi wa Bwana harusi?"

"Ndi...ndiyo" (Bibi alijibu kwa sauti iliyojaa wasiwasi)

Alexander akashusha pumzi,akamsogelea mama Gray.
"Mwanao anatuhumiwa kwa kesi ya mauaji"

"Mauaji...?mwanangu ni Bwana harusi,tena yupo huko juu tuna..." (Kabla mama Gray hajamalizia sentensi yake Insp.Alexander akasema)

"Mama sisi siyo vichaa,mwanao amemuua Bibi harusi tunaomba utuambie sehemu gani tunaweza kumpata" Kauli ya Alexander ikaibua minong'ono ya sintofahamu kwa wageni waalikwa pamoja na wazazi wa Leyla,hakuna ambaye aliamini anachokisikia kutoka kwa Alexander Dickson.

"...hey,naombeni mkae kimya"

Baba mmoja mwenye asili ya kiarabu akiwa amevaa kanzu yenye rangi ya dhahabu na baraghashia kichwani akasimama kwa ghadhabu,
"Unataka kusema mwanangu ameuawa..!!"

Alexander akajibu
"Ndiyo,na mtuhumiwa wetu ni Bwana harusi, askari polisi wamezunguka hoteli yote naimani watampata,ushirikiano wenu tunauhitaji"

"Uwiii.... Mwanangu weeee" (Mama yake na Leyla akaanza kulia maana leyla ni mtoto wake wa pekee)
Mama yake Leyla ana asili ya kitanzania,ile aliolewa na Muarabu ndio wakampata Leyla,sherehe imebadilika na kuwa msiba ndani ya dakika moja tu.

Alexander Dickson akaacha maagizo kwa askari wake wampeleke Baba Leyla ndani ya chumba alichopo mwanae kwa ajili ya utambuzi wa mwili,hawakutaka kumpeleka Mama Leyla maana angelizidi kuumia,Alexander Dickson akashuka ghorofa ya chini kwenda kuongea na meneja wa hoteli,lengo lake ni kupata picha za CCTV kamera ambazo zitawasaidia kufahamu alipo Gray.

Ingawaje mauaji yametokea ndani ya chumba alichokuwa Gray,lakini maswali mengi Sana yanaibuka miongoni mwa watu waliokuwa hapa,imekuwaje tukio litokee ndani ya dakika chache halafu askari polisi wafike haraka.?,na kwa nini walipita moja kwa moja mpaka kwenye chumba namba 45 alichokuwepo Gray na Leyla bila ya kuuliza kwa wenyeji..!.

**
Askari polisi waliokuwa nje ya hoteli wakakaa chonjo endapo Gray akionekana wamkamate,cha ajabu Gray haonekani ilihali ni dakika chache tu zimepita tangu askari polisi wafike hotelini.

Mageti yote mawili ya hotelini yakafungwa,waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari hawakutaka kupitwa na jambo,kila mmoja aliparangana kupata maudhui ambayo angeliweza kuyachapisha.

Upande wa pili kwa inspekta Alexander Dickson alikuwa amefika kwa meneja wa hoteli,bahati nzuri meneja alikuwepo usiku wa Leo tofauti na siku nyingine ambazo huwa anaenda kupumzika kila usiku na kumuachia msaidizi wake.

Meneja wa hoteli hii anafahamika Kama Musa,wengi hupenda kumuita 'BIG'(mkubwa) kutokana na umbo lake la unene na kitambi alichonacho,Meneja Musa aliongozana na inspekta Alexander pamoja na askari wawili mpaka ndani ya chumba kinachotunza kumbukumbu zote za CCTV, ndani ya kile chumba kulikuwa na kompyuta kubwa tatu ambazo zilionesha mbashara matukio yote yanayoendelea ndani ya hoteli,vilevile kompyuta hizi hutunza kumbukumbu za matukio yaliyopita.

Inspekta Alexander akamgeukia askari wake mmoja.
"Hebu pekua Kama tunaweza kumuona huyu mpuuzi"

"Sawa kamanda" Askari polisi akasogea kwenye kompyuta zile,akaanza kutazama kamera moja baada ya nyingine kuangalia Kama wanaweza kumnasa Gray.

Wakati askari anaendelea kupekua kompyuta,Inspekta Alexander akamuuliza meneja Musa.
"Leo ni siku ya jumapili,siyo rahisi Sana kumuona meneja akiwa eneo la kazi tena usiku,kulikoni..?" (Akamtazama kwa kumkazia macho)

Meneja 'BIG' akapatwa na kigugumizi.
"Aah..aa..unajua eeh..Leo nime..nimepata mwaliko kwenye sherehe iliyokuwa inaendelea ghorofa ya tatu"

"Ok,mchango ulikuwa shingapi?"

Swali la inspekta Alexander Dickson likamfanya meneja 'BIG' akae kimya maana hafahamu mchango wa harusi na wakati amedai kwamba alikuwa na mwaliko.

Askari polisi aliyekuwa anapekua pekua CCTV kamera akakatiza maongezi ya inspekta Alexander na meneja 'BIG'(Musa)
"Mkuu ,matukio yote ya nyuma yamefutwa,inaonekana muuaji alikuwa amejipanga kulifanya tukio hili"

Inspekta Alexander akatikisa kichwa
"Sasa kwanini amuue mke wake.! Tena siku ya Furaha Kama hii..! Kwanini asingemuua kabla ya ndoa yao kufungwa!!" (Inspekta Alexander alikuwa na maswali mengi Sana kichwani kwake)

"...Twendeni nje tukaendeleze msako,huenda tukafanikiwa kumpata muuaji" Alexander na askari wengine wawili wakatoka ndani ya chumba kinachotunza kumbukumbu za CCTV kamera, wakamuacha meneja BIG akiwa anakuja kwa nyuma.

Baba Leyla aliumia Sana baada ya kumuona mwanae akiwa ameuawa,machozi ya huzuni yakamtoka.
"Mwanangu..., mwanangu" Baba Leyla alizidi kuumia kila alipomtazama mwanae.Madaktari na wahudumu wa msalaba mwekundu wakaingia chumbani kwa ajili ya kuandika mambo ya kitabibu na kuuandaa mwili kwenda mochwali.

Baba Leyla akavuta pumzi ,macho yakamtoka kwa ghadhabu, akatoka nje ya chumba kwa hasira na kuwaacha askari polisi na wahudumu wa afya wakiwa wanakamilisha taratibu zao,moja kwa moja Baba Leyla akashuka ngazi Mpaka alipowaacha wageni waalikwa,akakuta wameruhusiwa kukaa kwenye viti vyao na askari, Baba Leyla akatupa macho kwa mama Gray ambaye alikuwa amesimama karibu na askari polisi aliyeshika kalamu na karatasi,Mama Gray alikuwa anaulizwa maswali kadha wa kadhaa na askari polisi kumhusu mwanae.

Baba Leyla hakufikiria mara mbili,machungu ya kumpoteza mwanae yakamfanya asiamue maamuzi mazuri,Baba Leyla akakunja ngumi Mpaka misuli yake ikakakamaa,akaanza kupiga hatua kusogea eneo alilopo mama Gray.

Baba Leyla anataka kwenda kumpiga makonde(ngumi) Mama yake na Gray kwa sababu mtoto wake Gray amesababisha kifo cha mwanae Leyla.

Itaendelea.....
????KWANINI GRAY KAMUUA MKE WAKE SIKU YA HARUSI..?KUNA SHIDA GANI?
????BABA LEYLA ANATAKA KUMSHUSHIA MAKONDE MAMA GRAY AMBAYE UMRI WAKE UMEENDA????
????WATAFANIKIWA KUMPATA GRAY(BWANA HARUSI)?
Muendelezo mpaka mwisho sh 1000
Unaweza ukaipata kupitia WhatsApp 0781858056

Maoni

You're not logged in


Tangazo - CEO usinivue mi nimchumba wa mtu mwanzo wa simulizi Hadi Mwisho wa simulizi
CEO usinivue mi nimchumba wa mtu mwanzo wa simulizi Hadi Mwisho wa simulizi
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

EPS 1 SIMULIZI;MCHEPUKO WA RAIS

EPS 1
SIMULIZI;MCHEPUKO WA RAIS
________________________________
CHAMA HURU MEDIA

**
UTANGULIZI
Saa tatu na dakika ishirini usiku,ndani ya Chumba cha hoteli namba 45 yenye hadhi ya nyota tano,alionekana mwanaume (37) akiwa amesimama pembeni ya kitanda huku mikono yake na suti nyeusi aliyovaa imetapakaa damu,mwanaume huyu anafahamika kwa jina la Grayson Mwailubi,kifua na mwili wake umejengeka kwa mazoezi,macho yake yalikuwa yanatazama juu ya kitanda kilichopo ndani ya hiki chumba.

Mbele ya mboni za macho ya Gray alionekana mwanamke mrembo akiwa amelala chali huku damu zinamtoka tumboni ,mwanamke yule alikuwa amevalia shela nyeupe ya harusi ambayo nayo ililowana damu zinazotoka tumboni kwake.

Gray akaitazama mikono yake kwa hofu kubwa...

๐Ÿ‘‰ Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/eps-1-simulizi-mchepuko-wa-rais

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral #fictionwriter
#ShortDrama #fblifestyle #BeautyBattle #AfricaVsWorld #Tanzania #Kenya #Congo #Rwanda #Burundi #SouthAfrica #USA #VoteNow #DebateTime #Trending <br>

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu ยท dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi eps
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 15
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 15
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 14  ยฉ GAMBO ELVIS
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 14 ยฉ GAMBO ELVIS
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 23
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 23
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 24
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 24
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 17
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 17
.BABAMKWE epsd 19.
.BABAMKWE epsd 19.
NI WANGU PEKEANGU epsd   16.
NI WANGU PEKEANGU epsd 16.
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 18
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 18
MAPENZI NI HISIA TAAM SANA epsd 5.
MAPENZI NI HISIA TAAM SANA epsd 5.
NI WANGU PEKEANGU epsd 3.  Franco alipomtupia Vanessa kitandani akataka aje kwa juu
NI WANGU PEKEANGU epsd 3. Franco alipomtupia Vanessa kitandani akataka aje kwa juu
MAPENZI NI HISIA TAAM SANA epsd 6.
MAPENZI NI HISIA TAAM SANA epsd 6.
 NI WANGU PEKEANGU epsd  5.  Alipoingia Franco akaubana mlango na kumwambia Vanessa
NI WANGU PEKEANGU epsd 5. Alipoingia Franco akaubana mlango na kumwambia Vanessa
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 19
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 19
NI WANGU PEKEANGU epsd  15
NI WANGU PEKEANGU epsd 15
NI WANGU PEKEANGU epsd  4.  Fred aliwapeleka Erica na Vanessa
NI WANGU PEKEANGU epsd 4. Fred aliwapeleka Erica na Vanessa
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 25
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 25
MAPENZI  NI  HISIA TAAM  1-----2 epsd 1.
MAPENZI NI HISIA TAAM 1-----2 epsd 1.
NI WANGU PEKEANGU epsd 20
NI WANGU PEKEANGU epsd 20
BABAMKWE  epsd 3...4
BABAMKWE epsd 3...4
BABAMKWE epsd 11.
BABAMKWE epsd 11.
NI WANGU PEKEANGU epsd 14.
NI WANGU PEKEANGU epsd 14.
NI WANGU PEKEANGU epsd  11.
NI WANGU PEKEANGU epsd 11.
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 30
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 30
EPS 2 SIMULIZI;MCHEPUKO WA RAIS
EPS 2 SIMULIZI;MCHEPUKO WA RAIS
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 28
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 28
NI WANGU PEKEANGU epsd  7.  Franco akapiga goti chini kisha akaanza kumwambia
NI WANGU PEKEANGU epsd 7. Franco akapiga goti chini kisha akaanza kumwambia
SIKU YA KWANZA  EPSODE 1
SIKU YA KWANZA EPSODE 1
NI WANGU PEKEANGU epsd  17.
NI WANGU PEKEANGU epsd 17.
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 26
MASTER MISTAKENLY SLEEPS WITH HIS HOUSEMAID CHAPTER 26
NI WANGU PEKEANGU epsd 18.
NI WANGU PEKEANGU epsd 18.
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 62 na 63

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 62 na 63

1.42K
AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž *season 3*  *64&65*

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž *season 3* *64&65*

560
JOGOO WA KIENYEJI 1----5

JOGOO WA KIENYEJI 1----5

259
SHAMIRA Sehemu ya 65&66

SHAMIRA Sehemu ya 65&66

214
MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ) EP 11.

MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ) EP 11.

212
*MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ) EP 12.

*MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ) EP 12.

196
SHAMIRA Sehemu ya 60&61

SHAMIRA Sehemu ya 60&61

195
SHAMIRA 62 63 na 64

SHAMIRA 62 63 na 64

192
*MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ)  EP 13.

*MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ) EP 13.

186
*MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ)  EP 14.

*MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ) EP 14.

148

ZIMESOMWA ZAIDI

โ€ŽTUNDA LA  DADA โ€Ž โ€ŽSEHEMU YA KWANZA

โ€ŽTUNDA LA DADA โ€Ž โ€ŽSEHEMU YA KWANZA

11.76K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

7.47K
๐Ÿ™„ NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA๐Ÿ”ฅ  sehemu ya tisa.  ๐Ÿ‘‰ Akaanza kunipamp sasa...๐Ÿ‘‡

๐Ÿ™„ NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA๐Ÿ”ฅ sehemu ya tisa. ๐Ÿ‘‰ Akaanza kunipamp sasa...๐Ÿ‘‡

3.84K
๐Ÿ”ฅ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ  Sehemu ya sita.  ๐Ÿ‘‰ Aaaaaaaaa chomoa...๐Ÿ‘‡  Shemeji inauma utanichana.

๐Ÿ”ฅ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ Sehemu ya sita. ๐Ÿ‘‰ Aaaaaaaaa chomoa...๐Ÿ‘‡ Shemeji inauma utanichana.

3.33K
MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 119 na 120.

MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 119 na 120.

2.95K
MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 108

MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 108

2.91K
MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 116 na 117

MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 116 na 117

2.74K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ  Sehemu ya 20.  ๐Ÿ‘‰ Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...๐Ÿ‘‡

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ Sehemu ya 20. ๐Ÿ‘‰ Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...๐Ÿ‘‡

2.72K
MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 106 na 107

MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 106 na 107

2.67K
๐Ÿ”ฅ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ  Sehemu ya 16.  ๐Ÿ‘‰ nakupenda pia...๐Ÿ‘‡

๐Ÿ”ฅ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ Sehemu ya 16. ๐Ÿ‘‰ nakupenda pia...๐Ÿ‘‡

2.6K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

Hakuna Ratiba kwa sasa

Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
*BILLIONS OF LOVE๐Ÿ’“๐Ÿ’“*  "1__5" Post Mpya
*BILLIONS OF LOVE๐Ÿ’“๐Ÿ’“* "1__5"
@majario LIVE

SEHEMU YA "1"๐Ÿ’“๐Ÿ˜ฝ BY BABIE LOVE "Alikuja kama muuza chai kumbe ni Billionea๐Ÿ’ต" Nyie njooni niwaambie kitu โ€ฆโ€ฆโ€ฆ mnazijua chapati? Sambusa je ? ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ nani hazijui halfkeki ? Wote mnazijua ? Ona sikilizeni...

Nargis and Sunil Dutt were not just legendary stars of Hindi cinema, but also one of the most respected and inspiring couples in Bollywood Post Mpya
Nargis and Sunil Dutt were not just legendary stars of Hindi cinema, but also one of the most respected and inspiring couples in Bollywood
@majario LIVE

. Nargis was known for her natural acting and powerful screen presence. Films like Mother India made her a timeless icon, and even today she is remembered as one of...

SHARON 1 mpka 5 Post Mpya
SHARON 1 mpka 5
@majario LIVE

๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ *SHARON* Sehemu ya 1 Kwa majina naitwa sharon hillary, mm ni mtoto wa 3 kuzaliwa katika familia ya watoto watatu, so mm ni wa mwisho kuzaliwa wa kwanza ni kaka yetu anaitwa...

Mwamuzi wa mchezo wa Esparance dhidi ya Al Ahly,Issa Sy ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ณ Post Mpya
Mwamuzi wa mchezo wa Esparance dhidi ya Al Ahly,Issa Sy ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ณ
@majario LIVE

Mara baada ya filimbi ya mwisho akatoa kadi yake nyekundu,anataka kumuona mtu amfuate kuhoji maamuzi yake. Kuna afisa mmoja wa benchi la Al Ahly alitaka kwenda,baada ya kuona kadi nyekundu imeshikwa...

SHAMIRA 71  MPK. 78. ( MWISHO S3) Post Mpya
SHAMIRA 71 MPK. 78. ( MWISHO S3)
@majario LIVE

๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€ SHAMIRA Sehemu ya 71 Mwandishi; lissa wa huru media Nikamwambia sawa nashukuru kama mimi ndo kiboko yako. Basi mchumba akaenda kuoga akatoka mwepesi kabisa akavaa kisha akachuku pochi aknihasabia laki 8 .akanipa...

๐Ÿšจ SIMAMA KWANZA USIPITE! ๐ŸŒ BATTLE YA WAREMBO WA DUNIA Post Mpya
๐Ÿšจ SIMAMA KWANZA USIPITE! ๐ŸŒ BATTLE YA WAREMBO WA DUNIA
@majario LIVE

Tanzania ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ, Kenya ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช, Congo ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฉ, Burundi ๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ฎ, Rwanda ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ, South Africa ๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฆ na USA ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ธ Wote wamevaa rangi za nchi zaoโ€ฆ lakini NANI AMEUA STYLE ZAIDI? ๐Ÿ‘‘๐Ÿ”ฅ โš ๏ธ CHAGUA NCHI MOJA...

SHAMIRA 67 to 70 Post Mpya
SHAMIRA 67 to 70
@majario LIVE

62 MPK 70 (SEASON THREE) ๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€ SHAMIRA Sehemu ya 67&68 Wassap; 0742443214 Mwandishi; lissa wa huru media Basi nikiwa nawaza sana pale akaingia husna .akagonga mlango...

NAKUPENDA BILA MIPAKA 1 - 12 Post Mpya
NAKUPENDA BILA MIPAKA 1 - 12
@majario LIVE

:01 Natafuta ni wapi nianzie na ni wapi nimalizie, sijui kabisa yaani kwa maana moyo wangu, roho yangu, na hisia zangu vyote kwa pamoja vimejawa na furaha isiyo kifani. Maisha yangu ni...

*MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ)  EP 14. Post Mpya
*MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ) EP 14.
@majario LIVE

Alinilegesha jamani king anajua kuandaa, anajua kutia sio Polepole jamani, nilijikuta nimempa yote bila kumbania, jamaa kumbe kiu ilikuwa kubwa na Mimi nilikuwa naukata kweli make kufanya hii kitu na...

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž *season 3*  *64&65* Post Mpya
AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž *season 3* *64&65*
@majario LIVE

๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ Basi nikapata na kipaji cha kubembeleza huu usiku mana zena hakuwa sawa kabisaa, na alikuwa na stress mnoo maskini na ni baada ya kumkubusha ya nyuma uko maskini, tulibembelezena mpka...

*MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ)  EP 13. Post Mpya
*MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ) EP 13.
@majario LIVE

Tulifika nikakuta mke mwenzangu tayari yupo ukweni na anamimba japo ilikuwa haionekani, nilitukanwa matusi yote, Mimi tasa, maskini sina msaada wowote, nilikuwa niwakulia tu ukizingatia, sijawai tumia hats uzazi wa...

*MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ) EP 12. Post Mpya
*MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ) EP 12.
@majario LIVE

MTUNZI: SMILE SHINE Baada ya king kuzimia,ilibidi apate huduma ya kwanza, Mimi ilibidi niludishwe kwenye Sheree, tulimaliza saa Saba usiku, nilikuwa nimechoka mno, nilioga nakuingia kulala, hata vicram pia alikuwa hoi,...

JOGOO WA KIENYEJI 1----5 Post Mpya
JOGOO WA KIENYEJI 1----5
@majario LIVE

๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“ sehemu ya 1 Mwandishi:lissa mwalla Naitwa Talya jones,ni mtoto wa pili katika familia ya watoto wawili,wakwanza kakangu tommy na mie ndio last born sasa,baba yetu alikua mwanajeshi na mama yetu ni nesi.baba...

MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ) EP 11. Post Mpya
MY HOT PILOT* (rubani wangu๐Ÿ”ฅ) EP 11.
@majario LIVE

MTUNZI: SMILE SHINE Mama alipokea nikamuita atoke nje,vicram alibaki tu akinishangaa, mama alitoka akatukalibisha ndani, niliomba niongee nae pembeni, tulitoka nililia Kwa mama mpaka na mama nae akaanza kulia, badae nikaamua...

SHAMIRA Sehemu ya 65&66 Post Mpya
SHAMIRA Sehemu ya 65&66
@majario LIVE

Wassap;0742443214 Mwandishi; lissa wa huru media Nilimuangalia sana nikamuuliza unamuongeleaa mtoto gani kwanza .akanambia ahaa si mtoto wangu ambae ulikuwa unakujaga nae nyumbani kuomba msada ama.nikasema sawa kumbe unakumbukumbu. Unahisi...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest