๐บ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐
โTotoo, tunaweza kuondoka sasa?โ
Nikawatazama wale wafanyakazi wengine namna wanatutazama na nilimtazama My boss na kusema kwa kichwa tu maana aibu zimenijaa nashindwa hata kuinua miguu yangu.
Alinishika mikono yangu na taratibu tulianza kutembea kuelea juu. Ofisini kwake yaani. Nilifika pale na yeye alinikalisha kwa kiti chake, nilikaa kwa kiti cha boss wangu. Mimi mtu wa maisha ya kawaida tu ambaye sio kukaa tu hata kuwa na ukaribu wa huyu mwanaume wa aina hii haikuwa ni kitu cha kawaida ila ndiyo amekua mpenzi wangu. Mbali zaidi kwangu huyu mwanaume hajivuni, linapokuja suala langu haofii kufanya lolote lile.
Alizungusha kiti upande mwingine, kisha neno la kwanza alisema โSijakusaliti Ndeana. Tangu nimekutana na wewe, tangu nitamke neno Nakupenda kwako sijawahi kukusaliti.
Achana na kutamani tu nje, sijawahi hata kuwaza wala kufikiria kwamba mbali yako wewe ninatakiwa kuwa na mwanamke mwingine.
Ndeana, pumzi yangu inayoingia na kutoka, usingizi wangu ninao lala na kuamka, kazi zangu ninazofanya na kila ninapotembea au ninapokuwa ni wewe.
Nakuwaza wewe peke yako, nawaza mwanamke wangu nikupende vipi ili na wewe unipende, penzi letu liwe na furaha. Nawaza nikufanyie nini ili usihangaike nje na maisha haya.
Tafadhali Ndeana, najua usaliti ni nini, najua maana ya kupenda na kupendwa na wewe ndiyo umenifundisha. Nimekukosea kwasababu sikukuambia kuhusu Martha. Ni msunbufu tu ila siwezi kuwa naye.
Sitaki kukiri kila kitu kwako kwa maana unajua tayari nilikuwa mbaya sana. Ila yeye yupo kwaajili ya pesa bila pesa huwezi kuwa naye. Na sijui hata kwanini tangu nimekuwa na wewe kawa msumbufu sana.
Amekuwa akiniambia vitu vingi kuhusu familia yenu na kusema yeye ni bora kuliko wewe. Ila namjua sana, ndiyo maana nikakuchagua wewe. Totoo, dady loves you. Upendo wangu kwako ni upendo wa kweli kabisa.
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 130
Sikutanii na namaanisha kila kitu. I love you kama namna neno lilivyo. Nakupenda sana, Nakupenda kuliko kitu chochote. Naomba usikasirike katika siku yetu nzuri namna hii. Naomba usikasirike ili tukafurahie hizo siku nilizokuambia vizuri. Ndena Please ongea kitu.โ
Nilimtazama, mimi tena kutaka kudeka eti nami nimenuna nikaitikia tu โsawa, hakuna shida!!โ
Akanitazama na kusema โhapa serikali iingilie kati. Ndeana hivi kweli unanijibu hivyo na unataka niendelee kupumua vizuri kabisa. Unakuaje hivi mtoto mzuri, nisamehe mzee wa watu mimi nitajifia bure unajua.โ
Nikamtazama nikitamani kucheka ila hasira sasa, nilianza kuongea kwa upole maana nilitaka nianze kufoka. Nilikumbuka maneno ya dada yangu kuwa hawa viumbe hawataki kelele na wanawake wengi tuna kelele nijitofautishe nao nisifoke hawapendi kabisa kufokewa anaweza kuondoka na asirudi tena.
Nilivuta pumzi kwa kudeka nikasema โulipaswa kuniambia nikae naye mbali, maana alikuwa anaingilia mpaka maisha yangu binafsi. Na alikuwa akijifanya kuniita wizo na vitu vingine kama hivyo akinichimba. Sasa ndiyo nini hivi.โ
Akanitazama akisema โnisamehe baby wangu, nimekosa mwenzio. Umenipigisha goti mbele za watu, unafikiri mchezo, niliona wazi nakupoteza. Na sipo tayari kuyabeba hayo maumivu ya kukupoteza kwasababu ninakupenda sana Ndeana.
Huyo sio wifi yako, wala sio rafiki mzuri kwenu. Naomba achana naye, mimi nimezaliwa peke yangu. Ukitaka kuitwa wifi basi niite mimi mwenyewe.โ
Nikacheka nikisema โsio mzima wewe.โ
Akasema โwaooo!!, hilo tabasamu, futa basi machozi.โ
Nikafuta kisha aliniambia โbaby asante kwa zawadi. Mungu akubariki sana. Ingawa unajua kuwa wewe ndiyo zawadi yangu kubwa sana kwenye maisha yangu.โ
Nilitabasamu na akaniuliza โeenh, umeniletea nini?โ
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 131
Nikacheka na kusema โhakuna kufungua mpaka mimi niondoke.โ
Akacheka. Na kisha alikuja pale kwenye kiti, aliniinua mimi, akakaa yeye na kisha alinipakata. Mimi nikawa nafurahi tu maana kupakatwa nako ni raha haswa akupakate mtu anayekupenda sana na wewe unampenda sana.Ingawa huku moyoni ninajisikia vibaya sana. Maana wivu uliwaka baada ya kuona wizo wa mchongo akipambana kuvua nguo na kulazimisha busu ninalopewa mimi na yeye apewe.
Alinifungua droo na kusema โnimekununulia zawadi. Ila Sharti lake kwa mwanzo tunatumia wote.โ
Nikasema โsasa zawadi ni yangu tunatumiaje wote.โ
Akanitazama akisema โuchoyo si ni haramu baby!!โ
Nikacheka tu. Alitoa kitu cha kuchekesha kwa sisi watu wazima. Alitoa pipi, tena pipi kijiti . Kuna hizi pipi zilikuwepo kipindi fulani hivi zina umbo la love halafu zina radha tofauti tofauti. Na hizi pipi hata ile siku alinipeleka kununua vitu na hii alininunulia. Ni tamu sana. Nilimtazama na kucheka nikusema โkwahiyo umenunua moja tu na unajua ni tamu.โ
Akasema โndiyo ujue kuwa sio malaki, mamilioni na pesa nyingi zitafanya ufurahie penzi lako. Haya sasa fungua tule.โ
Nikacheka tu, nikafungua basi nikawa nakula na kisha namlisha. Ananitazama anasema โafu wewe unanyonya sana kuliko mimi.โ
Nami namwambia โaku wewe hapo ndiyo mlafi.โ
Akaniambia โbasi nipe pipi yangu!โ
Nakatalia, si akaanza kunitekenya. Basi nikaanza kucheka, yaani huko ofisini sijui kwasababu muda mwingi yupo peke yake tu sio ofisi za kuingia sana watu. Nilicheka mpaka nakaa chini. Nacheka mpaka machozi. Aliniinua na kusema โbasi basi totoo, usije ukapaliwa.โ
Nikamtazama na kusema โnalipa, nitalipa tu.โ
Alijipa ushindi akisema โAnd the winner is Mr Stewart.โ
Nikamtazama kwa kudeka tu.
Basi akacheka na kisha aliniambia โsikia, nataka uende pale kwa aunt. Katengeneze nywele vizuri. Kisha mimi nitakufuata nyumbani. Nataka upendeze sana. Nataka utokelezee. Nitakufuata nyumbani, au nitakupeleka. Sijui nina kazi hapa ila unaweza kwenda tu hakuna shida.โ
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 132
Nilitabasamu, mara akashika simu yake. Baada ya muda akaniambia โNjoo uone, unajua pale nalia nilikuwa nachukuliwa video. Basi Kaka Fabian kanitafuta hapa mpaka page za umbea wameshare.โ
Nikasema โwewe usiniambie!!โ
Akatabasamu akisoma comment anasema โwasichana wengi wanateseka sana na mapenzi. Ukiona Comment zao utajua. Mpenzi tuwaombee na wao wayapate mapenzi kama sisi.โ
Nikacheka nikisema โhakika, tuwaombee na wao wafurahie.โ
Tukacheka na alisema โeenh Mungu hawa watu wameshare sana itakuwa simu zao zimejaa lile tukio. Sasa hata najali, nasijali wala nini. Najali nini na nilikuwa natetea utamu wangu wa maisha. Wewe ni tamu yangu Ndeana, nitakutetea kivyovyote hata kama itagharimu maisha yangu ila nataka wajue kuwa wewe ni wangu. Na nakupenda sana.โ
Kabla sijajibu, mlango uligongwa. Aliruhusiwa wakati huo mimi nimesimama na Boss wangu amekaa. Akaingia yule dada ambaye ananichukia. Boss alipomuona alinitazama na kuuliza โwewe tena?โ
Sasa nikaona ni bora niwaache niondoke zangu. Nikafika mlangoni na pipi kijiti yangu. Boss akaita โtotoo, njoo mara moja.โ
Nikarudi na kisha alimtazama yule dada alisema โhuyu ni Ndeana, na ndiye mke wangu mtarajiwa. Unataka kufanya kazi kwa amanj basi sitaki kelele zote huko kazini kwenu. Unavyoniheshimu ndiyo umuheshimu. Sitaki kusikia lolote. Na kwasasa huruhusiwi kuja kwangu bila kupita kwa meneja.
Nitamwambia awatangazie maana naona mmenizoea sana. Mipaka, mimi ni Boss wenu, mbali na hilo nina familia yangu naheshimu. Kwahiyo kama ni kazi ongea, kama ni ujinga wako wa kila siku naomba uondoke eneo hili sasa hivu.โ
Huyu dada aliinamisha kichwa chake chini kwa aibu. Na alinitazama kisha akamtazama Boss akisema โlakini hata mimi Nakupenda.โ
Eenh Mungu nipe uvumilivu ndiyo nilikuwa nasema moyoni huku natazama pembeni kama nicheke vile. Kumbe hata Stewart alikuwa anajisikia kama mimi. Tulipotazama tukajikuta tunacheka halafu Stewart alisema โtoto, sasa unaondokaje, majaribu ni mengi. Nipe busu nishibe nipate nguvu ya kupambana.โ
Malizia season four kwa sh 1000
No 0743433005 iko WhatsApp
๐ต๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐ฝ๐๐
๐๐๐๐ ๐ด ๐๐๐๐ 0743433005 ๐๐๐๐ ๐จ๐ฎ๐ถ๐บ๐ป๐ฐ๐ต๐ถ
๐ผ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐พ๐๐๐๐๐จ๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ +255743433005 ๐๐๐๐๐๐๐
๐๐๐๐.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments