Nikasoma tu na kuvuta pumzi huku nikishika kichwa changu kwa kuchoka maana hata sielewi. Kusema ukweli, kazi naitaka, Hotel ile ni kubwa sana yaani mimi kufanya kazi ni ndoto yangu, ila tayari boss anataka penzi na mimi.
Nitafanyaje sasa. Miguu yangu ilikuwa mizito, nguvu ziliniisha. Ilinibidi nitafute mahala nikae. Ndani ya moyo wangu nasikia sauti ikisema “usitoe utu wako kupata kitu, ipo siku utapata kilichobora zaidi.”
Kila nikisikia sauti hii machozi yananitoka roho inaniuma kuikosa Hotel kubwa namna ile. Picha za jengo, furaha ya kufika pale kwa mara ya kwanza, namna nilikuwa nasubiri kwa hamu kufanikiwa kunajirudia kichwani.
Roho inaniuma sana kwa maana sipo tayari kutoa mwili kisa kazi nzuri. Nikiwa nawaza ujumbe tena uliingia kwa simu yangu. Nilipotazama alikuwa ni boss wangu Stewart. Aliniandikia hivi “Ndeana mrembo wangu. Vipi ushaondoka. Mar ameniambia haupo vizuri nami sipendi kukuona au kukuharibia siku yako. Tafadhali naomba kukuona.”
Nilisoma na bila hata kutaka kufikiria haraka haraka nikajibu “nimeondoka.”
Ujumbe mwingine uliingia na kusema “Kumbe hata wewe ni muongo Ndeana. Ninakuona hapa unaniambia umeondoka. Please haipendezi.”
Sikujibu sasa badala yake nikageuza twiga kwa kuinua shingo yangu na kuanza kuangaza huku na kule pengine ningeweza kumuona ila haikuwa hivyo. Sikumuona.
Wakati nataka nimtumie ujumbe nimuulize alipo. Nilishtuka naguswa bega na naitwa kwa sauti yake nzuri sana “Ndeana.”
Nikatulia. Nilitulia kwa maana tayari nimejua yuko pale na pia nimetulia kwa maana nashindwa na sijui hata nifanye nini.
Akaniita tena “Ndeana.”
Nikainua kichwa changu na kumtazama. Sasa mimi moyoni ninao uchungu ambao nashindwa kujizuia kabisa. Nina uchungu unaofanya machozi yanitoke na nishindwe kujizuia kabisa yaani.
Ilinibidi niinue uso wangu kumtazama. Ile namtazama tu machozi yananitoka na hasira juu yake. Nikajikuta namuuliza “Ina maana unanifuatilia si ndiyo, unanifuatilia.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:22
Boss wangu, alitazama huku na kule na kusema “kuwa mstaarabu basi Ndeana. Kwani wewe ni mswahili hivi?, relax ingia kwa gari na tuzungumze.”
Nikavuta pumzi na kusema “Stewart sina haja ya kuingia ndani ya gari yako. Tumemalizana. Kama ambavyo nimesema kuwa siwezi kutoa utu wangu kwaajili ya kazi ndiyo ipo hivyohivyo. Tumemaliza.”
Stewart akatabasamu, kiasi nikaona hata ule mwanya wake. Nikainama chini na na kisha Stewart aliniambia “Sikia Ndeana, mimi sitaki kukuumiza na ndiyo maana nilipoambiwa upo hapa ikabidi nikufuate. Ndeana mimi siwezi kukufanya kitu kibaya mtoto mzuri kama wewe.
Sikia kama unaona mimi nitakudhuru. Chukua simu yako, kisha mwambie mtu ambaye unamuamini kuwa upo na mimi. Ikiwezekana chukua picha kabisa mtumie ili ukipotea niwe wa kwanza kuulizwa.”
Nilimtazama, na kisha akaniambia “simama sasa. “
Nikasimama.
Baada ya kusimama yeye akatoa simu yake na kupiga picha akisema “tazama, hapa hata haina yale makeke yenu watoto wa kike picha inawaka namna hii. Ndeana, wewe ni msichana mzuri.”
Akanitumia ile picha na kisha akanishika mkono mpaka kwa gari yake.
Alinifungulia mlango wa gari yake, niliingia na kukaa hata sina raha ya kufanya lolote wala kuzungumza lolote. Baada ya kuingia tu alianza kuzungumza akinitazama usoni na kusema “ Ndeana, nisamehe sana.”
Nikamtazama na yeye aliendelea akisema “nisamehe Ndeana. Sikujua kama utachukizwa na hisia zangu. Nafahamu kama unawaza mambo mengi sana katika kichwa chako. Sikatai ni kweli huenda hizi ni tabia za wanaume wengi sana.
Ndeana mimi Stewart sifanyi hivi ili nikupe kazi. Ndeana trust me or not. Tangu siku ile ambayo dada yako Mar aliponitumia picha, uliukamata moyo wangu. Uzuri wako, upole, macho yako, midomo ya pekee sana ni vitu ambavyo kila nikitazama nashindwa jizuia.
Pengine unachukia hata kusikia haya maneno. Ila wacha niendelee kuomba msamaha kwa maana sitaacha kusema nakupenda. Ndeana mimi nakupenda kweli kweli haki ya Mungu.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:23
Nimekutana na wengi sana, ni kweli nimeona wengi mno ila umeushika moyo wangi na akili yangu kwa namna ya pekee. Sipendi kukuona unachukia, na kukosa furaha ila kama kusema neno nakupenda kwako ni chukizo la moyo wako ni sawa kwa hili sitazuia kuchukia kwa maana neno nakupenda litakuwa ni Wimbo mzuri wa kutoka katika moyo wangu. Kipenzi, ninaposema haya maneno, ninasikia
amani ya ajabu. Ninaona ajabu sana, mimi Stewart napenda kiasi hiki, sijui umenifanya nini wewe mtoto, ila amini usiamini wewe ni mke wangu. This time next year utakuwa mafhabahuni ukisema Yes I do.
Nakupenda Ndeana na natala kuwa mwanaume wako utakayetumia maisha yako yaliyobakia duniani pamoja na yeye. Ndeana ina maana wewe hunipendi hata kidogo kweli, Ndeana tell me please?”
Ungekuwa wewe fikiria ungemjibu nini Stewart, kwanza anaongea kama kajipanga ville. Utulivu na kwa makini sana. Sauti imetulia haina kelele. Maneno yake kayapangilia ipasavyo. Nikajikuta nainamisha tu kichwa chini kwa maana maneno yake yananifikia, yananigusa na kusisimua kwa namna fulani mwili wangu. Ila haki ya Mungu sitaki kuwa na mahusiano naye na kazi ninaitaka.
Akanishika juu ya paja langu, nikashtuka fulani hivi na yeye akatabasamu akisema “Ndeana zungumza kidogo.”
Taratibu nikainua uso wangu, na kumwambia kwa upole “Boss!!!”
Akatikisa kichwa akisema “no!!, noo totooo, Stewart. Kwani jina langu ni baya namna hiyo?”
Nikavuta pumzi na kusema “Stewart.”
Basi akawa anatabasamu, sasa huyu mwanaume wa makamo akitabasamu tabasamu lake ni kama lina uchawi. Ushawahi kukutana na mtu mwenye tabasamu zuri. Ni kama umuombe muda wote awe anatabasamu tu. Kwa maana unaona uzuri wa ajabu kuhusu Mungu kwa watu hawa. Sasa Stewart ndiyo mtu wa namna hiyo. Mpaka nimefika hapa sijawahi kuona tabasamu la pekee kama la Stewart.
Nikajikaza na kumuuliza “ina maana Stewart, siwezi kupata kazi mpaka niwe mpenzi wako?”
Stewart akaniambia kwa kushika mikono yangu “haina maana hiyo, ila mimi nakupenda nataka uwe mpenzi wangu. Ingekuwa ni hivyo basi wale wasichana wote wa kazini wangekuwa wapenzi wangu. Si ndiyo?”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:24
Nikavuta pumzi na kusema kwa upole “lakini mimi sitaki kuwa na uhusiano na boss wangu.”
Stewart akaniambia akitabasamu ni kama vile kajua lile tabasamu lake ni zuri hivyo anafanya kusudi “mimi na wewe hatujuani. Siyo boss wako. Mimi ninakupenda Ndeana. Ndeana I love you so very much , please Ndeana Accept my love.
Wewe ni mwanamke ambaye nataka kulala na kuamka naye maisha yangu yote. Wewe ni mwanamke ambaye najua watoto wangu watakuwa salama na amani wakiwa kando yako. Ndeana wewe hapo, ni wewe hapo peke yako. Fikiria kuhusu mimi.
Sitaki kuzungumza sana ukaniona muongo, leo mimi ni dereva wako sasa nataka nikuzungushe, uone jiji hili zuri kwa uzuri sana na tena uone na hotel zingine na kisha uone ile hotel yetu na wewe ukiwa ndiyo mama Stewart si utakuwa mmiliki nikikuoa. “ Akatabasamu
Mimi natamani kumwambia sitaki ila nashindwa. Huyu mwanaume ni mwanaume sio wale wanaume kuhusu mapenzi hayui chochote. Huyu anaonekana mpenda mapenzi yaani anayajua mapenzi.
Kwa maana anavyozungumza, anavyojali kuhusu furaha na mambo kama hayo. Nikisema mwanaume presentable nadhani tunaelewana.
Huyu ni wale wanaume ukienda naye sehemu basi watu watajua kuwa hiyo sehemu kweli mwanaume kaingia. Huyu ni Yule mwanaume hujielezei sana kumtambulisha kuwa ni mwanaume wako.
Maana kuna wanaume unajielezea wewe kisha ni mpenzi wangu inakuwa mwishonu. Ila huyu unaweza kutamani sana mtu akuulize ili ti useme he is my man and i love him. Kwakweli ni mwanaume safi sana.
Msafi, mcheshi, handsome, ana mvuto na sifa nyingi kumuhusu. Mwanaumr hasifiwi sana ila ndiyo namuelezea sasa na kubwa kuliko ni Boss wa Hotel kubwa ambayo mimi ninatamani sana kwenda kufanya kazi. Kusema ukweli ninatamani sana hata iwe kesho.
Basi aliweka nyimbo hizi za Injili kwa gari. Nikashangaa na kumuuliza “Unasikiliza injili pia?”
Akaniuliza “why not?”
Nikatabasamu na kusema “wanaume wengi hawapendi kujiweka karibu na Mungu. Hata hivyo watu wenye pesa wao hujihisi tayari wana kila kitu hawajui tena kuhusu Mungu.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:25
Akatabasamu na kisha alisema “totooo, mimi nimeumbwa na Mungu. Tena kila nikimfikiria Mungu ninaogopa sana. Nampenda na tena hata hivyo Ndeana mimi nimetunzwa na kulelewa katika familia ya kumpenda na kumjua Mungu sana. Ndiyo maana na mimi nampenda Mungu.”
Nikashangaa sana, na kusema “Hongera sana.”
Akaniuliza “vipi wewe unampenda Mungu Ndeana?”
Nikatabasamu na kusema “yeye ndiyo kabla
ya kuanza jambo lolote, na Mungu huyohuyo ndiyo baada ya jambo lolote. Kifupi mimi huwa naanza na Mungu na huwa namaliza na Mungu.”
Akasema “waaaaooo, interesting!!, sasa Ndeana kama ni hivyo. Kanuni ni nzuri sana na rahisi. Basi hata hili langu kabidhi kwa Mungu, Nina hakika asilimia mia. Mungu atafanya njia. Wewe ni wangu, wangu peke yangu. Muombe Mungu juu ya hili.”
Nikamtazama usoni tu. Kisha yeye aliendelea kuendesha gari huku anaimba ile nyimbo ambayo ilikuwa inapigwa pale tena anaimba kwa uzuri kabisa kama vile na yeye ni msanii. Mimi nikawa nashangaa sana.
Alikuwa ananizungusha huku na kule huku anaimba. Ananitazama anatabasamu mwenyewe hana hata shida. Nakuambia kumbe jiji hili ni zuri sana. Wewe pengine unaona tu hapo unaishi na mazingira jirani na pengine kazini. Kwahiyo kuna sehemu tu umezoea kwa maana ndiyo unazopita kila siku. Ila ni nzuri sana. Basi nikiwa na dereva wangu ambaye ndiye Boss wangu simu yangu iliita na alikuwa ni dada yangu. Nikapokea, dada alianza na kusema “sasa mbona kimya mimi nimekaa nina hamu ya kusikia wewe tena upo kimya.”
Nikacheka kidogo kumfanya dada asiwe na wasi na kusema “nakuja!!, nakuja dada wala usiwe na shida.”
Dada akaniambia “fanya haraka sasa. Mimi hamu inaniua.”
Nikajikuta nacheka.
Dada akakata simu. Stewart akaniuliza “nani tena anamfurahisha Ndeana wangu.”
Nikasema “ni dada yangu.”
Akajibu “Mar!!”
Nikamwambia kwa upole “hapana huyu ni dada yangu wa kuzaliwa kabisa. Amenikumbuka inabidi niwahi nyumbani.”
Akaniambia “ondoa shaka boss, dereva wako nipo hapa nitahakikisha kila kitu kinaenda sawa.”
Nikajikuta natabasamu hata nacheka. Akauliza “umecheka, kumbe na wewe hucheka.”
Soma muendelezo kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005.