ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 76
...
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 77 Nikamuuliza βkwani ni vipi huyu dada, nimekutana naye muda ule natoka kwa Boss. Basi alinitazama kwa jicho hilo nikaogopa.β Joan alianza kucheka alicheka akisema βhao ndiyo wanaohangaika waolewe na Boss. Boss mwenyewe hacheki na kima, yeye akikupitia tu tayari si bora watulie kama mimi hapa?β Nikashtuka na kuuliza βhata wewe pia?β Akasema βndugu yangu kupata kazi sio rahisi hivyo, mtu mwenyewe ana dharau kama nini unaweza nenda naye room akaishia kukutazama tu. Ya nini mimi.β Nikacheka tu, nikisema βtuondoke, nitakula tu nyumbani.β Joan alisema βyamekuwa hayo, au unampenda Boss ndugu yangu. Kama unampenda bora usahau tu. Yile sijui hana Moyo.β Nikacheka tu nikisema βnitamuanzia wapi mimi, na usikute anaye mke nyie mnahangaika tu.β Naongea hapo moyoni kuna waka moto. Nachukia kusikia hayo maneno sana, ila nitafanyaje sasa na mtu kakiri. Nilichukia ila moyoni nasema βMungu anajua.β Basi tulienda kuchukua simu, na kubadili nguo. Nilipowasha tu simu nilikuta na semeji zake zimejipanga. Honey babe Hunny bunny Honey pot My sweet person Totooo Kipenzi Ndeana wangu, na maneno matamu matamu mengi. Nikacheka tu. Na kisha ujumbe mwingine aliandika β Nisubiri nilipokuambia, tunaenda saluni pamoja leo.β Kiukweli siku hii sikuwa na story nyingi na Joan. Basi tulipotoka tu tuliagana vizuri tu. Nilitembea mpaka hiyo sehemu aliyoniambia. Nilimtumia ujumbe kuwa nipo hapo. Hakuchelewa ndani ya muda mfupi tu alifika. Niliingia ndani ya gari na alinitazama na kuniambia βUnaonekana umenuna kuna nini totoo!!!β Nikamtazama na kumuuliza βKwani kazini umetembea na wanawake wangapi?β Akasimamisha gari na kusema βNdeana nilijua umenielewa na yameisha. Ina maana unataka nilie tena. Mumy mimi mtu mzima ujue, please nipe muda. Ningekuwa sikupendi nisingekuwa nahangaika hivi. Please jiweke mbali na hayo mambo kama ni hivyo basi uache kazi.β
...
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 78 Nikamtazama na kusema βNiache kazi kivipi sasa?β Akavuta pumzi na kuniuliza βunanipenda mimi?β Nikamtazama tu, akaniambia βnisikilize mimi, mimi nakupenda peke yako wewe tu.β Nikaitikia kwa kichwa. Akaniita βNdeana!!!β Nikaitikia βabee!!β Akaniuliza βunajua kwanini napenda kukubusu?β Nikamtazama kwa aibu na kusema βHapana, sijui?β Akniambia βkwasababu kila busu lako linaanzisha maisha mapya ndani ya moyo wangu. Mwili wote unasisimuka na kuwa na furaha. Nakupenda Ndeana.β Nikasema kwa upole βTuachane na hayo sasa tuendelee na safari.β Akatabasamu. Basi akaweka nyimbo zake kama kawaida, kwa mara ya kwanza, tangu nitoke kwenye tumbo la mama yangu. Ninaonaga kwa tv tu, ila sasa hivi yananitokea mimi mwenyewe katika maisha yangu. Nilishuka kwa gari, na Boss akashuka. Kapendeza mwenyewe, anavutia yaani hata ukisimama ukisema huyu ni mpenzi wangu, lazima upewe maua yako. Alinishika mkono, alinibebea pochi yangu. Nilikuwa najisikia aibu sana. Tulitembea mpaka saluni. Ile tunaingia tu, wadada wote wa saluni wakaacha walichokuwa wanafanya wakatutazama. Kisha Boss wangu, aliita kwa sauti ya wote kusikia βAunt, nimekuletea mkweo leo, maana kila siku unanipigia kelele haya huyu hapa, anaitwa Ndeana, ni mke wangu mtarajiwa.β Aunt sasa akashangaa akisema βStewart, usinambie unanitania, mbona mrembo hivi, nitambulishe vizuri.β Mwanaume wangu sasa, alivyo anajiachia kwa raha, si mwenzenu nilianza kutambulishwa alianza kwakusema βAunt, she is my sweet person.β Aunt sasa βumh!!, uhm!!β Aliendelea akisema βMimi namuitaga totoo, Aunt huyu sasa ndiyo roho yangu, nampenda sana huyu mrembo anaitwa Ndeana. Ni mwanamke wa pekee sana kwangu. Ndeana huyu ni aunt yangu. Rafiki kipenzi wa mama yangu. β Mimi sasa mpaka aibu wadada wengine wanavyoshangaa yaani huku moyoni nasema βNdeana mimi, sijawahi kupendwa hivi, zamani nilikuwa kama hawa wanaoshangaa.β Basi nikasalimiana na Aunt kwa furaha na kisha Boss wangu alisema βNakaaa hapa nataka nione anavyopendeza. Naomba mtengeneze vizuri sana. Vyovyote ili mradi apendeze. Totoo enjoy kipenzi.β π€£π€£π€£ππna leo mkikoment kama jana kesho mpaka miaππ»
...
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 79 Nikacheka. Akasema βBaby kwani kukusubiri hapa ni haramu.β Nikamjibu nikicheka βni haramu baby dini zote zinakataza.β Akacheka akisema βumoja wa mataifa uingilie kati nakusubiri kipenzi.β Watu wakajikuta wanacheka na kuanza kunongβonezana. Mimi na yeye tunatazamana na kukonyezana huku akiwa na pochi pembeni. Nyie mapenzi matamu mjue, mimi ndeana nawaambia. Basi tena, Aunt mkwe tena kajua mimi ni mkwe wake. Basi ananifurahia mwenyewe, ananitengeneza nywele akiwa na furaha sana.Boss wangu amekaa tu anachezea simu yake hana habari, wadada mule ndani wanapiga story wanamuangalia Boss wangu napata wivu maana wasije niibia njiwa wangu akapeperukia mbali sana. Nilipendeza sana, unajua kuna kule kupendeza mpaka wewe mwenyewe unajua wazi ya kuwa umependeza. Basi nilipomaliza Aunt mkwe alisema βmkwe wangu umependeza mno, yaani hapa sasa kila mawimbi yakivurugika njoo tunatengeneza mtindo mwingine. Hili wiki ni kama lilitengenezwa maalumu kwaajili yako. Stewart unasemaje, umemuona mwenzio.β Boss alitabasamu na kusema βnimemuona aunt, ni mzuri sana. Amependeza sana.β Akanisogelea na kisha akanishika mkono tulienda kukaa kwenye sofa pamoja. Akawa ananishika nywele zangu huku ananiambia βbaby hawa wadada wanaona wivu, itakuwa hawapendwi hawa.β Nikajikuta nacheka na akaniziba mdomo watu wanatutazama. Mimi nikamwambia βhuna akili kabisa.β Akatabasamu na kusena βNdeana wewe ni mzuri sana. Umependeza sana. Umependeza vibaya mno.β Nikamwambia βNashukuru sana. Haya uliza basi gharama nilipie.β Boss wangu alitabasamu na kusema βuna matatizo wewe. Nikusifie na Bill ulipe wewe. Hii ni juu yangu. Mwanaume akikusifia ahakikishe yeye ndiyo ana gharamia. Yaani akikusifia umevaa nguo mpya umependeza, viatu vipya ama chochote na yeye hana tatizo lolote lile, yupo tu kukuonea, anakufanyia makusudi mbinafsi.β Nikamtazama na kusema βbaby lakini mwingine kipato kidogo?β Akatabasamu akisema βkipato kidogo pia kuna vitu vidogo vya kunogesha penzi lao. Sasa baby niwe sina hela hata kijola ukose, hata kukupeleka kula mihogo nishindwe, masihara sasa.β Nikacheka na kusema βuna maneno kama nini?β
...
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 80 Aliinuka na kisha alienda kwa Aunt yake. Walizungumza kidogo kisha Aunt alinifuata na kusema βKipenzi, sasa usiwaze kuhusu nywele. Wewe njoo hapa kila ukiona nywele haifai. Njoo hapa na utengeneze. Ushalipiwa kabisa, na bill ikiisha mpenzi wako analipa hana shida.β Nikamtazama Boss na kutabaasamu kwa kushangaa yaani, kisha akaniuliza βUtanishangaa tu totoo, hutonikumbatia?β Nikacheka na kwa aibu nilikumbatia nikisema βAsante sana, Mungu akubariki.β Basi alinishika mkono mpaka kwenye kioo eti akaniambia βhaya baby jishaue kidogo nakuchukua video hapa.β Huyu mwanaume ana vituko yaani nikajikuta ninacheka. Basi tukapigana picha na tukiwa timekumbatiana huku tunaonesha picha na video za hapa na pale. Tukamaliza basi nakuambia nikabebewa pochi tena tukamuaga Aunt huku msalimie mama zikiwa nyingi, nitakuja na vitu kama hivyo. Nikafunguliwa mlango totoo mie tukaingia ndani ya gari. Mimi mwenzenu nimepata dereva binafsi, napelekwa nyumbani na nimepata furaha ndani ya muda mchache. Huyu mwanaume amenifanya nifurahie mapenzi ndani ya muda mfupi sana. Hata wiki hatujamaliza ila ananidekeza ananijali na kunitunza ni kama yaani tumejuana kwa muda mrefu sana. Ni kama vile tunajua miaka na miaka. Amenifanya nimzoee na amenifanya nijihisi huru kwake. Ninampenda, ila naona aibu nami kufunguka nahisi bado ni mapema sana. Basi mwenyewe kwa gari humo nilikuwa na furaha sana. Maana nasifiwa na kutaniwa tu huku na yeye akijisifia kuwa katika wanaume wamepata wanawake wazuri basi na yeye ni mmoja kati ya hao wanaume. Tulifika mpaka mitaa karibu na nyumbani. Alisimamisha gari na baada ya hapo alinitazama na kusema βTotoo, nimesimamisha kukuambia kuwa jambo ambalo linaenda kutokea kesho ni jambo kubwa sana. Ni jambo ambalo sikumbuki kama katika hotel yetu limewahi kutokea. Kwanza hotel itakuwa busy, kuanzia vyumba, na hata upande wa chakula. Pesa zitaingia za kutosha. Pia itatangazwa sana Hotel hii na tutapata watu wapya wengi sana. Yote haya ni kwasababu yako. Natamani nikufanyie kila kitu kizuri ndiyo uwezo sina.
Soma muendelezo kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005


Maoni