Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo

𝑺𝒆𝒂𝒔𝒐𝒏 𝒕𝒉𝒓𝒆𝒆  𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:  11
Gonga94 · Stories

𝑺𝒆𝒂𝒔𝒐𝒏 𝒕𝒉𝒓𝒆𝒆 𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 11

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.


niahidi utakuwa sawa tu.”

Nilikuwa natokwa na machozi nikisema “dada unaongea kama unaniaga vile, hakuna kibaya kitatokea. Utakuwa salama, niahidi utatetea uhai wako.”
Dada alitabasamu na kusema “Nakuahidi, sikia mdogo wangu. Nampigia simu shemeji yako, ila hapokei simu yangu. Nenda kwake. Mwambie hali yangu pengine atakuja.”
Nilitabasamu na kusema “Usijali, nitafanya hivyo. Sasa jiandae mimi nitakuwa nje nakuombea sitaondoka mpaka ujisikie nafuu.”
Dada yangu alitabasamu, aliniambia “nashukuru mdogo wangu nitakuwa sawa.”

Nakumbuka nilitoka katika kile chumba nikilia, hata boss wangu aliponiona alinihurumia sana, alikuja na kunikumbatia akisema “totoo, unaweza ukaacha kulia tafadhali. Unapolia unaniweka katika wakati mgumu sana. Moyo wangu unavuja damu na jasho. Nakuomba sana kipenzi, nakuomba mno Ndeana wangu, usilie, acha kulia.”

Nilikumbatia nikisema “dada alikuwa sahihi, tungeacha kwanza baba apone. Nitawapoteza wote sasa, vipi kama wote wakiniacha.”

Aliniziba mdomo akisema “Unaongea nini Ndeana, unaongea upumbavu gani tukiwa katika wakati wa majonzi namna hii. Wote wanapata tiba kipenzi. Wote wanatakiwa kupona. Wangebaki bila matibabu ndiyo hatari zaidi.”

Nilimuuliza nikisema “dada yangu, dada yangu hatokuwa mama tena si ndiyo.”

Nakumbuka aliniambia “Ndeana, yeye atashindwa kubeba watoto lakini wewe utaleta watoto na watamuita mama. Ndeana dada yako atakuwa mama kwa namna yoyote ile ila lazima ataitwa mama. Mungu anapofanya jambo fulani, anakupa na namna ya kukufanya upate amani juu ya mambo hayo. Sikia mpenzi, Unanipenda?”

Nikawa namuitikia tu kwa kichwa, na yeye aliniambia “kama unanipenda basi unatakiwa uniamini pia. Dada yako atapona, na baba pia atapona kwasasa tunatakiwa tuondoke hapa ili usishihudie ya hapa tukirudi hapa kila kitu kipo sawa.”

Nikamuuliza nikimtazama usoni “ina maana hutoondoka?”

Aliniambia hivi kwa upendo “nitaondoka Ndeana ila sio sasa wala usiwe na haraka. Hata ikinibidi nikae pembeni yako usiku mzima ili wewe upo sawa nipo tayari.”

𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 112

Nilijikuta natabasamu machozi yakonitoka na kumkumbatia nikisema “Nakupenda sana, wewe ni mwanaume wa pekee sana. Nakupenda mno. Stewart, baki na mimi, Nakupenda.”

Alinikumbatia na kuniuliza “Unaweza tena kurudia hayo maneno?”

Nikasema nikiwa nimemkumbatia kwa nguvu nikilia “Nakupenda sana.”
Akaniambia kwa utani “Totoo, kwani kulia si ni haramu?”

Nikajikuta natamani kucheka ila siwezi nina huzuni sana, huku nalia nilisema “ni haramu baby wangu, dini hairuhusu..”
Akaniuliza “umeniita baby!!!!”

Nikamtazama na kusema “Kipenzi, unaweza kunisindikiza huko kwa mpenzi wa dada?”
Akaniambia “bila shaka, tukirudi hapa mambo saafi.”
Tukiwa tumeshikana mikono kwa pamoja tulitoka mimi na yeye tena kwa upendo mkubwa sana.

Tukiwa barabarani kiukweli sikuwa naweza hata kuzungumza. Sikuwa na utulivu, mara nisali kimoyomoyo, mara nilie, mara nifumbe macho mara nijikumbatia. Watu wangu muhimu wawili sasa wapo hospitali, siku moja, nitafanyaje mimi peke yangu. Mungu wangu!!, nachanganyikiwa.

Boss wangu yeye alikuwa ananihurumia tu, kuna muda alinishika mkono na kuniachia, kuna muda alinitazama kwa huruma lakini angefanya nini.Hakuwa na la kufanya zaidi ya kukubali tu lile ambalo linatokea mbele ya macho yake.

Nakumbuka tulifika mpaka anapoishi shemeji. Mpenzi wangu mimi yaani My boss, alishuka kwa gari ila hakusogea. Alikuwa ananitazama tu huku mimi nikiwa naenda kwa huyo shemeji, yaani mpenzi wa dada.

Nilishtuka sana baada ya kufika mlangoni, usiku ule nikawa nasikia ndani sauti za vicheko kati ya mwanamke na mwanaume. Nilishika moyo wangu shemeji asiwe ana msaliti dada yangu. Katika hali ile ya maumivu asifanye hivyo. Niligonga mlango. Aliuliza “nani?”

Kwakuwa nilitaka atoke, basi sikujibu nikagonga tena , akatoka. Aliponiona alishtuka sana. Kabla sijasema kitu mwanamke pia alitoka na upande wa kanga kwani mwanaume alikuwa na taulo tu. Nilitabasamu huku moyoni ni kama vile kisu chenye ncha kali kimenipitia. Hata boss wangu kipenzi alikuwa ameona hilo. Alianza kusogea.

𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 113

Nilifumba macho na nikawa naona dada yangu anavyopambana hospitali na mwanaume wake yupo na mwanamke mwingine wakati yeye mpaka dakika za mwisho anamuwaza. Nikajikuta nasema “So, ndiyo maana hupokei simu za dada kwasababu upo na mgeni?”
Akatabasamu kuzuga akisema “Ndeana karibu sana. Karibu ndani.”

Nikasema “sina haja na karibu yako, hata kitu nilichotaka kukuambia naona hapa sio sehemu sahihi. Endelea na mgeni wako.”
Yule dada akaniuliza “kwani kuna nini hapa?”

Nikamwambia kwa ukali na hasira “muulize huyo mwanaume wako ambaye hana hata aibu, shemeji nilikuona mtu wa maana sana. Kumbe ndiyo walewale kasoro majina. Sawa ila utamkumbuka dada yangu mjinga sana wewe.”

Mpenzi wangu wangu wa moyo alinifikia. My Boss, Mr Tarick. Mbele yao aliniuliza “My sweet person, kuna nini hapa?”

Nikalia kwa uchungu nikisema “Anamsaliti dada yangu, yaani dada yangu anampenda sana mpaka dakika za mwisho anamuwaza mwanaume ambaye yupo kifuani kwa mwanamke mwingine. Ni tabia gani hii?”

Yule mwanaume aliingia ndani akabaki yule dada, alibaki anatutazama tu. Baby wangu alinikumbatia na kusema “imekuwa vizuri hili limetokea totoo, tumejua mapema kuwa hampendi, kwahiyo huyu sio sahihi kwake. Mwanaume anayekupenda hawezi kukusaliti.

Mwanaume anayekujali hawezi kufikia hatua ya kuleta tena mwanamke mwingine ndani anapokuwaga na mpenzi wake. Huyu hana adabu wala heshima. Tuondoke hapa. Acha kulia na usimwambie dada mpaka atakapokuwa sawa.”

Nilimtazama na kusema “roho inaniuma sana, anawezaje kumfanyia hivi dada anavyompenda namna ile.”

My boss alinitazama na kunishika mkono kisha tukaingia ndani ya gari akisema “kipenzi, Ndeana wangu. Mtu akitaka kukuumiza. Hakuchagulii namna ya kuumia haswa kwenye mapenzi.

Hajali kama unampenda na kumjali. Kwasababu yeye haoni furaha kwako, haoni thamani yako wala hawezi kukufurahia kabisa. Ndiyo maana anakuumiza na hawazi lolote. Mbaya zaidi hujiona mjanja sana. Ndiyo hivyo.”

Nilimtazama tu nikafuta machozi nikisema “tupite nyumbani sasa tuchukue nguo.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 114

Akaniambia kwa upole “sawa mumy wangu.”
Kivivu nikatabasamu.
Akatabasamu pia akisema “kwani totoo kuigiza ni haramu?”

Nikamuuliza “Kuigiza tena?”
Akaniambia “ndiyo tuigize kama hakuna matatizo.”
Nikamtazama na kusema “kivipi sasa?”
Akacheka akisema “nimemiss husu kwakweli?, ina maana huwezi hata kunibusu hata kidogo tu.”

Nikashusha pumzi nikisema “huoni nina matatizo lakini?”
Alinitazama na kusema “Sio mimi totoo, nikiwa na wewe nakua tu sina akili. Nimemiss busu lako kwani ni haramu?”

Nikajikuta nacheka kivivu kisha tukaendelea na safari hata tukafika nyumbani. Nilimkaribisha nikisema “karibu sana hapa ndiyo nyumbani kwetu. Mimi, dada yangu na baba yetu. Karibu sana.”

Alitabasamu na kusema “Wewe huyo wakati mdogo, tabasamu vilevile. Ndeana huyu ni nani?”

Nikatabasamu na kusema “ni mama yangu.”
Akatabasamu akisema “mimi na baba ni sawa sawa kwenye kuchagua. She was so beutiful.”

Nilitabasamu na kuanza kupapasa picha ya mama nikisema “mpole na mkarimu pia. Mama alikuwa na huruma na mcheshi sana. Yeye na baba walikuwa marafiki sana. Baada ya mama kufariki, baba aliteseka sana. Ila tupo hapa kumchangamsha. “ Nikavuta pumzi na kusema “naomba nisubiri narudi sio muda.”

Nilimuacha akiendelea kushangaa ndani kwetu. Atajua yeye kama alikuwa anashangaa ile Tv ya chogo na deki yetu ambayo mlango upo wazi muda wote. Au kama alikuwa anashangaa kabati la vyombo pale sebuleni ambalo vioo vyake vyote vimetoka au sabufa yetu ya mchongo.

Sijui, labda vile viti vyetu ambavyo vitambaa vimechakaa hata godoro la ndani linaonekana au usafi wa nyumba yetu, maana kwenye usafi tupo vizuri na wala hatuna shida ndogo ndogo tunakula, tunavaa na kulala safi kabisa. Labda kama alikuwa anashangaa stuli zetu zenye miguu mipana. Sisi wala hatuna shida wacha asafishe macho.

Mimi nikiwa napanga baadhi ya nguo simu yangu iliita. Alikuwa ni Joan. Basi nikamsimulia naye alisikitika na kunipa pole nyingi sana huku akisema “Sasa kipenzi naweza kuja hapo hospitali nikupe kampani maana upo peke yako.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 115

Nilitabasamu na kusema “sipo peke yangu. Usijali kuhusu hilo Joan. Nipo na mpenzi wangu. Kwasasa wewe pumzika kesho ukiwa na nafasi utakuja.”

Aliniambia kwa upole “sawa kipenzi. Kesho asubuhi nitawahi ibadani na kisha baada ya hapo nitakupigia. Kukiwa na chochote unahitaji niambie sisi ni marafiki.”

Yaani akisema hivi naumia, unajua huyu kavuliana nguo na mwanaume wangu ila nitafanyaje sasa ndiyo tumependana kama marafiko na vile akisimulia lazima boss atajwe huwa natamani kumwambia acha kumsema Baby wangu ila nakosa nguvu kabisa. Sasa ndiyo basi tena.

Nilitoka na kukuta bado anatazama picha ukutani tena ile ambayo tupo na baba na mama. Alikuwa kama analia hivi. Nikamtazama na kusema “nimemaliza sasa, tuondoke?”

Alitabasamu na kusema “Nyumbani kwenu ni pazuri sana. Najua nimefika hapa bila utambulisho rasmi ila naamini nikirudi tena hamtonifukuza si ndiyo.”

Nikasema “Hata sasa umefanya mengi sana kwangu na familia yangu. Karibu sana jisikie upo nyumbani ingawa ni heshima mbaya hii wewe kuja bila utambulisho.”

Akatabasamu na kusema “nipo tayari, nijitambulishe ili nije kuona furaha za nyumba hii. Tazama hii picha. Baba Yenu ni baba mzuri sana, na mimi natamani kuja kuwa baba mzuri sana kwa watoto na mke wangu.”

Nikatabasamu na kumuuliza “baba yako yuko wapi?”
Alinitazama na kisha alitabasamu akisema “alifariki.”
Nikamwambia “pole sana. Baby tuondoke sasa.”

Akanitazama na kusema “Mpenzi wangu, najua unavyojisikia. Ila naomba nikubusu, mimi akili inatamani busu lako.”
Nikalalamika “Lakini baby!!”

Akanivuta akisema “My sweet person, usiwaze kingine chochote nataka ujisikie vizuri. Naomba midomo yako mitamu please. “

Nikamtazama yeye akanikumbatia na kunisogeza karibu yake, na kisha alianza kunibusu na ulikuwa ni usiku sana.Kidogo nilisahau maumivu, maana akili ilizingatia busu. Wakati ananibusu simu yake ikaita. Haraka aliniachia akisema “itakuwa dokta nilimwambia apige simu akimaliza.”
Nikasema kwa hamu ya kutaka kujua “anasemaje, pokea, pokea.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 116

Ndipo alipokea na kuweka sauti ya juu ili kusudi na mimi nisikie. Nilimsikia dokta akisema “Tunashukuru Mungu, watu wa upasuaji wamemaliza salama na mgonjwa wetu katoka salama. Ingawa kwa sasa bado amelala ila mnaweza kumuona.”
Nilijikuta napiga magoti nasema “Asante Mungu, Asante Mungu wangu.”

Huku mpenzi wangu anavyohangaika utafikiri yule ni dada au ndugu yake. Alipomalizana na dokta tulijikuta tunakumbatiana kwa furaha huku nikisema “tuondoke sasa, tuondoke.”
Boss alitabasamu na kusema “nipe kabusu kafuraha sasa.”

Basi nilimkumbatia na kuanza kumbusu usoni, macho, bua, shingo, mabega, kichwani, midomo, kidevu, kifuani yaani mimi nambusu kila mahali hata alianza kucheka akisema “nilikuambia atapona, sasa nikufanyie nini kingine unibusu kila sehemu yaani sehemu zote.”
Nikamtazama na kucheka nikisema “Mjinga sana wewe. Sehemu zote ndiyo nini sasa.”

Tukacheka, tunaondoka tukiwa na furaha yaani sisi tumeshikana mikono hatuna habari hata tumesahau dada kasalitiwa. Hakika mapenzi ya kweli na mazuri hata katikati ya maumivu huleta furaha.

Tulifika hospitali na kweli tulienda kumuona dada yangu. Dada yangu alikuwa amelala tu bado hakuwa ameamka.

Nilimshika dada yangu nikisema “Nimefurahi sana dada yangu, najua sasa utakuwa sawa kabisa. Najua Mungu atatupa namna nyingine ya kufurahi. Asante kwaajili yangu. Nakupenda sana dada, nilichanganyikiwa, nilijua sitakuona tena unajua.”

Mpenzi wangu alinitazama na kusema “totoo, inatosha usiongee sana.”
Nilimtazama na kusema “sikuwaza siku nitakuwa na wagonjwa wawili. Twende kwa baba. Nimechoka sana.”

Alinishika mkono na nikamwambia “tangulia kwa baba mimi naenda kwa dokta nikazungumze naye.”

Taratibu nilielekea kwa dokta. Lengo nikajue gharama nianze kupunguza. Nilipofika kule dokta aliniambia “mpenzi wako amemaliza kila kitu. Kuanzia bill ya baba na ya dada. Hapa labda tutajua mpaka mwisho itakuaje ila kwasasa kila kitu safi. Huna deni hapa.”

Nilitoa macho na kuuliza “Kalipia kila kitu.”
Alinitazama na kutabasamu akisema “hakika. Kila kitu tayari.”
Nikamtazama Dokta na kusema “karibu sana.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 117

Nilitoka nikitamani kulia kwa furaha, ni mwanaume gani anajali wazazi wangu familia yangu tena kwa mara ya kwanza. Angekuwa mwingine angeniuliza nina kiasi gani au familia iko wapi. Huyu kafanya tena bila kutaka asante yangu na hajasema kitu. Nilikuwa najiambia tu “Asante Mungu, asante Mungu.”

Nilifika mpaka chumbani kwa baba, nilikuta Boss anaongea na baba. Ila baada ya mimi kuingia aliacha akawa anacheka tu. Nikamtazama nikisema “Unamwambia nini baba yangu?”

Alitabasamu na kusema “ninavyokupenda.”
Nikatabasamu na kusema “naona hata baba sura walau sasa imechangamka. Kesho inaweza kuwa siku nzuri sana.”
Alisema “kabisa, dawa zinafanya kazi vizuri, wala usiwe na shaka atakuwa sawa.”

Baba alikuwa anatazama tu ila haongei. Nilitabasamu kwa huruma na kusema “baba lala sasa. Mimi nipo nje hapo.”
Baba alitazama tu. Basi mimi na baby wangu tulishikana mikono na kutoka nje.

Tulikaa kwa benchi pale nje. My boss alinilaza mapajani mwake akisema “unatakiwa kupumzika kidogo. Ni usiku sana sasa na umekuwa busy mwezi mzima huu utaumwa totoo.”

Nililala mapajani nikisema “napenda harufu ya mwili wako. Unanukia vizuri sana.”
Alitabasamu na kusema “Na wewe utapenda haya marashi.”
Nikajibu kwa upole “ndiyo, yananukia vizuri.”
Akasema “sawa kipenzi, pumzika kwanza. Nakupenda sana.”
Nilijibu “nakupenda pia huku nikiwa nasinzia kwa maana nilikuwa nimechoka sana.

Asubuhi palikucha. Ila Niliamka nikiwa chumbani kwa dada pale hospitali. Na dada hakuwa ameamka. Nikiwa namsalimia dada yangu, alikuja Boss, alinisalimia akisema “Morning my sweetperson.”

Nikatabasamu. Akaniambia “Asubuhi uzuri wako unazidi. Unawaka sana mpenzi.”
Nikatabasamu tena na kusema “kwani ulinibeba?, nimefikaje hapa?”
Akacheka na kusema “baba anakuita, ameamka vizuri leo.”
Nikasema “unasema kweli?”
Akatabasamu. Nami nikatoka pale haraka kwenda kwa baba yangu.

Nilipofika nilikuta baba yangu anafanyiwa vipimo. Nilifika na kumtazama na yeye alinitazama akitabasamu. Niliita “Baba!!”
Na yeye aliitikia kwa upole “Ndeana wangu!!”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 118

Mpenzi wangu aliingia na kututazama tu. Kisha nilimkumbatia nikisema “nimefurahi sana umeamka baba. Nilikuwa nakuwaza sana.”
Baba alisema kwa huruma “nisamehe nawasumbua wanangu.”

Nikamtazama nikisema “hata hunisumbui, kwanza unakula nini baba. Utakuwa unanjaa, ule unywe dawa.”

Niliona baba akimtazama Stewart akisema “mwanangu alishaleta chakula, kanibadili nguo ina maana hunioni. Wewe ulichoka sana na sasa muda umeenda sana.”

Nikajikuta namtazama Stewart kwa upendo sana, nikamwambia “Asante sana. Mungu akubariki.”

Alinijibu kwa tabasamu “Nashukuru, lakini leo nakuacha kidogo. Nina kazi nyingi ila nakuahidi nitarudi mapema.”

Nikasema kwa huruma “hapana, nenda kapumzike kidogo. Kisha baada ya hapo utakuja jana hujalala ujue na leo umewahi kuamka.”
Akatabasamu. Kisha baba aliniambia “Msindikize mwenzio mwanangu.”
Nikatabasamu.

Nakumbuka nilitoka na Stewart mpaka kule ambako gari lilikuwa limesimamishwa. Kabla hajaingia kwa gari nilimshika mkono na kusema maneno haya machozi yakishuka taratibu kwa hisia za upendo zinazowaka ndani yangu, ninayakumbuka sana “Stewart mpenzi wangu. Sina neno zuri la kuelezea hisia zangu juu yako kwa haya yote ambayo umeyafanya kwangu na familia yangu. Wewe sio mpenzi tu ila ni maisha yangu pia.

Sijui bila yako peke yangu ningefanya nini. Ninakupenda kwa kiasi ambacho siwezi na sitaweza kusema nikaeleweka. Siku zote umekuwa ukisema unanipenda. Naomba sasa iwe zamu yangu.

Stewart moyo wangu ni nyumbani kwako, hisia zangu ni chakula chako. Nipende kama ninavyokupenda. Mapenzi yetu yawe yenye furaha na amani. Asante kwa kila kitu, asante kwa kufanya maisha ni marahisi pamoja na wewe, asante kwa kuwa na mimi nyakati ngumu, asante kwa kubeba familia yangu kama yako, asante kwa kunichagua na kunipenda, asante umekuwa wangu, wangu wa maisha, wangu peke yangu. Nakupenda sana Stewart.”

Alinikumbatia akisema “mimi nilishasema yote. Nakupenda kuliko mwanamke yeyote hapa duniani. Ndeana wewe ndiyo Penzo langu la kwanza na la mwisho.

𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 119

Sitakuja kupenda tena nasikia raha na amani kuwa kando yako. Familia yako ni yangu pia. Na yangu ni yako pia. Nataka tuwe kitu kimoja kama familia.

Nilikuambia nafsi mbili zikielewana kila kitu kinakuwa sawa. Nafsi yangu na yako, yako na yangu zimefungamana, zimeshikana, yaani zimeungana na kuwa nafsi moja.

Hakuna mimi Stewart bila Ndeana.”
Nikatabasamu nikisema “Hakuna Ndeana Bila Stewart.”
Akatabasamu na kusema “nenda kwa baba sasa.”
Nikatabasamu na yeye akanifuta machozi.

Alipomaliza, nilianza kuondoka. Nilipiga hatua chache akaniita “My sweet person!!”
Nikageuka, akaniambia “utahitaji chochote?”
Nikamwambia “no, labda wewe tu.”
Akatabasamu na kusema “dada akiamka mwambie asijali. I will make her happy.”
Nikacheka tu, kisha akaniambia kwa tabasamu “Nakupenda.”
Nami nikatabasamu na kurudi kumkumbatia.

Kisha baada ya hapo alinong’ona masikioni, wenzio wamekuja kukuona wanatushangaa. Nikashtuka. Kugeuka nyuma naona wasichana watatu wa kazini akiwepo na Joan. Yeye wala hakujali, aliwasalimia na wao wakamjibu kwa nidhamu tu. Kisha Stewart akasema “totoo, see you.”

Nikatabasamu tu kwa aibu maana wenzangu walikuwa wanatazamana tu ingawa moyoni nilipata furaha kiasi ni kama sifichwifichwo tena. kisha niliwakaribisha wenzangu tukaingia ndani.

Niliwapeleka kwa baba yangu. Baba aliwasalimia nami nikawatambulisha kwa baba yangu. Baba alifurahi sana. Na kisha nikawapeleka na kwa dada yangu ambaye tayari aliamka. Bado hakuwa sawa muda mwingi machozi yanamtoka ila hakuwa na budi kuyakubali tu. Wageni waliona sio wakati mzuri kuendelea kuwepo pale. Hivyo waliniaga nami nikawasindikiza.

Tukiwa nje, Joan alinivuta pembeni nakumbuka alinitazama na kusema “mbona hukasiriki, hunichukii na una mahusiano na Boss.”
Nikamtazama na kumuuliza “sasa kwanini ninune. Yamepita ilikuwa zamani na sasa ni wakati wangu.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 120
Joan aliniambia “nisamahe sana Ndeana. Laiti ningejua wala nisingefanya hivyo. Pia hongera sana. Natamani niseme naomba namba ya mganga wako ila nitakuwa nachekesha. Yule mwanaume mwanamke hamrudii na hajawahi kuhangaika na mwanamke. Sasa mwenzetu umempa nini.”
Nilitabasamu tu, na kisha nilisema “Ni Mungu tu, sijui ya Mbele ila Tunapendana sana.”

Alinitazama na kusema akitabasamu “sasa naelewa kumbe ndiyo maana alikuwa...”
Nikacheka nikisema “nendeni sitaki umbea mimi.”

Nilibaki nawatazama wakiondoka huku nikiwa na hakika kuwa habari zangu zitaenda kutapakaa kazini. Nilikuwa natabasamu tu maana penzi ni kikohozi alifichiki katu.

Nilitoka nikarudi kwa dada yangu, nilipofika akanitazama na huzuni akaniuliza “Yupo hapa?”
Nikamtazama tu na kutikisa kichwa changu.Dada yangu akauliza tena “ulienda?”
Nikamjibu “nilienda lakini nikamkuta..”

Kabla sijajibu alijibu yeye mwenyewe “na mwanamke, mjinga ni mimi, nimekuwa nikimfumania mara nyingi anaomba radhi namsamehe tena. Ona sasa akijua hata sina uwezo wa kuzaa atafanya nini, si ndiyo atasema kabisa hanitaki.”

Nikashangaa na kuuliza “kwani dada bado unasubiri kuambiwa hakutaki. Utabadilika lini dada ujinga gani hata kwenye mapenzi. Sikia dada wewe ni mzuri sana. Utapata tu mwanaume mzuri sana.”

Dada yangu akalia kwa uchungu sana, alilia akilalamika kuwa nani atampenda na hana uwezo huo wa kuzaa.

Haukuwa wakati mzuri kwangu kabisa. Maana tena ilinibidi nikaongee na baba. Ila tofauti pengine baba aliumia moyoni tu. Zaidi alinitazama na kusema “Nipeleke kwa binti yangu nikamuone.”

Nikachukua kiti mwendo kwa maana baba bado hakuwa na nguvu vizuri. Nilimsukuma mpaka kwa dada. Nilipofika dada alianza kulia kumuona baba yake. Ilinibidi nitoke maana najua tena baba na mtoto.

Nilikaa nje peke yangu nikitia huruma tu. Hakuna kitu kigumu kama kuuguza. Yaani mimi siku ya pili ndiyo inaanza ila nipo hoi maana wagonjwa wewenyewe wana maumivu sana. Ila nitafanyaje.

Muendelezo sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005

Maoni

You're not logged in


Tangazo - boss Enzo fully stories
boss Enzo fully stories
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

𝑺𝒆𝒂𝒔𝒐𝒏 𝒕𝒉𝒓𝒆𝒆 𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 11



niahidi utakuwa sawa tu.”

Nilikuwa natokwa na machozi nikisema “dada unaongea kama unaniaga vile, hakuna kibaya kitatokea. Utakuwa salama, niahidi utatetea uhai wako.”
Dada alitabasamu na kusema “Nakuahidi, sikia mdogo wangu. Nampigia simu shemeji yako, ila hapokei simu yangu. Nenda kwake. Mwambie hali yangu pengine atakuja.”
Nilitabasamu na kusema “Usijali, nitafanya hivyo. Sasa jiandae mimi nitakuwa nje nakuombea sitaondoka mpaka ujisikie nafuu.”
Dada yangu alitabasamu, aliniambia “nashukuru mdogo wangu nitakuwa sawa.”

Nakumbuka nilitoka katika kile chumba nikilia, hata boss wangu aliponiona alinihurumia sana, alikuja na kunikumbatia akisema “totoo, unaweza ukaacha kulia tafadhali. Unapolia unaniweka katika wakati mgumu sana. Moyo wangu unavuja damu na jasho. Nakuomba...

👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/season-three-jamani-boss-mi-naona-aibu-11

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral #fictionwriter
#ShortDrama #fblifestyle

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi season-three-jamani-boss-mi-naona-aibu
𝑺𝒆𝒂𝒔𝒐𝒏 𝒕𝒉𝒓𝒆𝒆 𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:  90
𝑺𝒆𝒂𝒔𝒐𝒏 𝒕𝒉𝒓𝒆𝒆 𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 90
𝑺𝒆𝒂𝒔𝒐𝒏 𝒕𝒉𝒓𝒆𝒆 𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:  95
𝑺𝒆𝒂𝒔𝒐𝒏 𝒕𝒉𝒓𝒆𝒆 𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 95
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50

1.22K
*AFANDE MILLAN😎* *Sehemu ya 51 na 52*

*AFANDE MILLAN😎* *Sehemu ya 51 na 52*

737
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 39  na 40

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 39 na 40

250
SHAMIRA Sehemu ya 48

SHAMIRA Sehemu ya 48

100
BARUA ZA KAKA YANGU; Nikikupenda Mimi Inatosha!

BARUA ZA KAKA YANGU; Nikikupenda Mimi Inatosha!

32
Enzi zetu Radio Free Africa ilikuwa ndiyo bonge moja la station yani unapata full vibe hakuna kubadilisha station.

Enzi zetu Radio Free Africa ilikuwa ndiyo bonge moja la station yani unapata full vibe hakuna kubadilisha station.

13
#TBT 2014 nilijiunga na SAHARA MEDIA GROUP LTD. January niliripoti ofisi za Adda

#TBT 2014 nilijiunga na SAHARA MEDIA GROUP LTD. January niliripoti ofisi za Adda

5
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50

ZIMESOMWA ZAIDI

‎TUNDA LA  DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

‎TUNDA LA DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

11.69K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

7.41K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya tisa.  👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya tisa. 👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

3.82K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya sita.  👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇  Shemeji inauma utanichana.

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya sita. 👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇 Shemeji inauma utanichana.

3.31K
MY WANGU❀ sehemu ya 119 na 120.

MY WANGU❀ sehemu ya 119 na 120.

2.91K
MY WANGU❀ sehemu ya 108

MY WANGU❀ sehemu ya 108

2.84K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 20.  👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 20. 👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

2.69K
MY WANGU❀ sehemu ya 116 na 117

MY WANGU❀ sehemu ya 116 na 117

2.68K
MY WANGU❀ sehemu ya 106 na 107

MY WANGU❀ sehemu ya 106 na 107

2.64K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 16.  👉 nakupenda pia...👇

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 16. 👉 nakupenda pia...👇

2.57K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

Hakuna Ratiba kwa sasa

Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
#TBT 2014 nilijiunga na SAHARA MEDIA GROUP LTD. January niliripoti ofisi za Adda Post Mpya
#TBT 2014 nilijiunga na SAHARA MEDIA GROUP LTD. January niliripoti ofisi za Adda
@majario LIVE

Estaste, Kinondoni baada ya HR Mkuu Mzee Shilatu na msimamizi Steven Diallo kuning'oa kutoka Ebony FM, Iringa. Nikapokelewa na Tom Chilala, Wiltrudies Mutembei @wiltrudiesmutembei kisha wakanikabidhi kwa "Semaji"...

*AFANDE MILLAN😎* *Sehemu ya 51 na 52* Post Mpya
*AFANDE MILLAN😎* *Sehemu ya 51 na 52*
@majario LIVE

Daaaah nilishangaaaa sana kwamba aya mambo yamekujaje kujaje, na mbona sielewi, nikasema mama sijaelewa yani kwamba umesema? , mama akanmbia nilishaongea sana na wewe millan, juu ya suala la wewe...

SHAMIRA Sehemu ya 48 Post Mpya
SHAMIRA Sehemu ya 48
@majario LIVE

Wassap;0742443214 Mwandishi; lissa wa huru media Akasema mimi pia nimekula njoga nikaoge basi chapi chapu. nikase​ma sawa. Kweli mwanaume akaenda kuoga nikabaki nimetulia tu na baada ya mda akatoka akanifata...

Enzi zetu Radio Free Africa ilikuwa ndiyo bonge moja la station yani unapata full vibe hakuna kubadilisha station. Post Mpya
Enzi zetu Radio Free Africa ilikuwa ndiyo bonge moja la station yani unapata full vibe hakuna kubadilisha station.
@majario LIVE

Binafsi nilikuwa napenda sana vipindi vitatu pale RFA , 1 - Sindano 3 za moto, asubuhi na Fredwaa...!! 2 - Sitosahau na Sky Woker 3 - Showtime bongo moja ya show za...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 39  na 40 Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 39 na 40
@majario LIVE

39 MPAKA 40 🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌 Mwandishi; lissa wa huru media Nilitukana kweli kweli kwemye gari umo. Ila barka hakunijibu alikuwa busy na kuendesha gari. Akawa ananipeleka mlandizi ukoo. Nikasema wewe mjinga unaenfa...

BARUA ZA KAKA YANGU; Nikikupenda Mimi Inatosha! Post Mpya
BARUA ZA KAKA YANGU; Nikikupenda Mimi Inatosha!
@majario LIVE

Nikikupenda mimi inatosha, acha kuwa na presha, acha kuhangaika na ndugu zangu, kama wakikupenda ni ziada tu lakini haibadilishi chochote! Nani alikudanganya kuwa wanapaswa kukupenda! Mimi mwenyewe sina uhakika kama...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50
@majario LIVE

🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈 Basi bwana penzi likanoga mpaka mwezi ukakata, apo zena alikuwa na wasi wasi kuwa ntamuacha ,ila mi wala sikuwa na ayo mawazo kichwani kwangu ata kidogo, kila siku namuona...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50
@majario LIVE

🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈🊈 Basi bwana penzi likanoga mpaka mwezi ukakata, apo zena alikuwa na wasi wasi kuwa ntamuacha ,ila mi wala sikuwa na ayo mawazo kichwani kwangu ata kidogo, kila siku namuona...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 48 na 49 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 48 na 49
@majario LIVE

Daaah mchumba ndo kashanikatia simu mi nafanyaje sasa ,basi nikaweka simu pembeni tu, kisha nikapanda kitandani, nikavuta shuka , nikapumzika na asubih sana nikaamkia kazin na mwanangu lbraa,ibra akaniuliza...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 38  na 39. Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 38 na 39.
@majario LIVE

kipande cha 38 🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌 Mwandishi; lissa wa huru media Basi ndo hivyo . Nikaikosa ndoa na bwana barka.na nikawa busy na maisha yangu . Na mambo yangu. Na nikazidisha mapenzi tu kwa...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 36 na 37 namba zilikosewa endelea kusoma. Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 36 na 37 namba zilikosewa endelea kusoma.
@majario LIVE

36 MPAKA 37 🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌 Mwandishi; lissa wa huru media Maua akasema khaaa yani unanitukana mimi. Kwaiyo mimi naweza kuolewa na kaka yangu. Nikasema yaa unaweza sasa kisebengo cha nini. Nakuona sana tangu...

SHAMIRA Sehemu ya 47 Post Mpya
SHAMIRA Sehemu ya 47
@majario LIVE

Wassap; 0742443214 Mwandishi; lissa wa huru media Basi shost alivyotoka kuoga akanmbia shamira shoga yangu nisamehe kwa yale maneno nilokwambia basi. Nikasema yapi? Akasem si yale ya kukwambia ukatoe mimba...

SHAMIRA Sehemu ya 46 Post Mpya
SHAMIRA Sehemu ya 46
@majario LIVE

🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀 Mwandishi; lissa wa huru media Nikaona aisha kakasirika akanambia sawa kama unataka kulea iyo mimba na kuzaa. Ile kulea mtoto ni gharama umae ukielewa hilo suala mapema . Mana sio...

*AFANDE MILLAN😎* *46&47* Post Mpya
*AFANDE MILLAN😎* *46&47*
@majario LIVE

Nakumbuka kuna kipindi ,nilisafiri na ibraa kikazi kwenda moro , apo nilishamuaga zena kuwa mm nasafari naenda moro kikazi, ntakaa siku 2, akanmbia hakuna shida, basi mm nikawa...

SHAMIRA 44 kwa 45 Post Mpya
SHAMIRA 44 kwa 45
@majario LIVE

🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀 Sehemu ya 44 Mwandishi; lissa wa huru media Aseeee tulichoka mno na shoga yangu asa mimi jamani.nafanya nini na hili tumbo na mwanaume hanitaki. Na ameshakana kuwa hii mimba sio yake...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest