.TIPWA TIPWA NA MR MARVEL. SEHEMU YA 14
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Licha ya kukataliwa mara kadhaa, Salmon hakukata tamaa. Alikuwa anamfuata Noela chuoni kila mara ili ambembeleze. Pia alikuwa anampigia simu na kumtumia sms kiasi kwamba Noela akaamua kubadilisha namba ili aache kusumbuliwa🥱.
Na Kuhusu Iris, Salmon alimsahau kabisa. Uhusiano wao ukazidi kuwa mbaya maana kichwa cha Salmon kilijaa Noela tu na sio mwanamke mwingine👌
Katika yote haya, Noela akazidi kupendeza. Alibadilika sana hata kwenye mavazi yake. Alikuwa anavaa vizuri sana nani kwa sababu Mr. Marvel alijua kumchagulia nguo na viatu vizuri.
Pia alikuwa anatumia simu mpya na Kila wiki alikuwa anabadilisha hairstyle. Alipata pia marafiki wapya waliompenda na aliowaamini.
Kwa hiyo Noela wa zamani na Noela wa sasa walikuwa watu wawili tofauti. Noela wa sasa hakuruhusu watu wamtumie kwa sababu ya wema wake plus Wanafunzi wenzake darasani walimpenda sana.
Siku moja jioni baada ya vipindi, kama kawaida Noela akaingia kwenye gari na kuondoka eneo la chuo. Hakujua kuwa Iris alikuwa anamfuatilia nyuma kwa pikipiki😤.
Iris alitaka kujua Noela anaishi wapi na ni nani huyo mwanaume anayemhudumia hivyo. Alikuwa na hamu sana ya kujua kwaiyo alimfuata kila mahali, kuanzia alipopitia supermarket na sokoni kisha ndipo hapo Noela akaelekea nyumbani.
Nyumba aliyokuwa anaishi Noela ilikuwa nzuri sana na ya gharama kama nilivyosema mwanzo. Iris alipoiangalia akajaa wivu na hasira. Hakuamini kama Noela anaishi kwenye nyumba nzuri kiasi kile.
“What? Anaishi hapa? kwenye nyumba hii nzuri hivi? Mungu wangu, mimi bado niko hostel, nabembeleza mapenzi ya Salmon! Wallah Siwezi kubali kabisa. Huyu mwanaume anayemhudumia Noela lazima nimfanye wangu ili na mimi nianze kuishi maisha mazuri kama yake. Hilo lazima litokee….”😡
Akaamua kusubiri pale ili aone kama ataweza kumuona huyo mwanaume. Alijificha nje ya nyumba kwa masaa mawili au matatu kama sikosei.
Baadaye kabisa kuna gari lilifika aina ya G wagon! Ndani yake alikuwa yupo Mr. Marvel. Lili ingia ndani kisha Mr Marvel akashuka akitembea taratibu kuingia ndani.
Apo Iris anajitaidi kuchungulia mpaka akamuona alieshuka kwenye gari ni nani. Kwanza alishangaa, sababu ni mtu ambae uso kama anamfahamu au kuna mahali fulani alishawai kumuona.
Akafikiria kidogo ni wapi amewahi kumuona mtu huyoo ndipo kumbukumbu zikamrudisha siku ya birthday ya Salmon. Yule mwanaume alikuwa pale ndiye yule yule aliyemuona nyumbani kwa akina Salmon.
“Waiiiiit………si baba yake Salmon yuleeee!”😳
Hakuamini macho yake kuona kuwa mwanaume anayemhudumia Noela ni baba yake Salmon. Akajikuta Anacheka coz hakuamini kwamba Noela anaweza kuwa na mahusiano na baba pamoja na mtoto.
“Kumbe huyu siyo malaika kama nilivyodhani. Kwanza alikuwa na mtoto, sasa amehamia kwa baba. Lakini huyu baba yuko vizuri. Kama ningejua anapenda wasichana wadogo hata nisingepoteza muda na mwanae. Lakini hakuna kitu kitashindikana. Kwa huu utajiri na jinsi alivyo handsome lazima awe wangu….! Subiri mtaona…..”😠
Akajiapiza pale kisha akaondoka zake maana tayari alishajua alichotaka kujua.
Wakati huo, Noela alikuwa jikoni anaandaa chakula cha jioni. Alikuwa na furaha na alipanga kumpikia Mr. Marvel chakula kitamu👌.
Akiwa jikoni akahisi uwepo wa mtu pale jikoni. Akatabasamu na kugeuka, akamuona Mr Marvel amesimama mlangoni.
“Good evening, Noela! Siku yako ilikuwaje?”
Noela akajibu “Ilikuwa poa sana. Wewe je?”
“Niko sawa, ila nilikuwa na kazi na mikutano mingi sana leo”
“Aaaaaah ndiyo maana hukunipigia hata simu” Noela akajikuta ananuna! Kwa mbali alishaanza kuwa na kawivu na Mr Marvel🤣
“Sorry, nilikuwa busy sana Lakini haimaanishi nimekusahau. Nilijua tu ungekasirika ndiyo maana nimekuletea zawadi!” Akamwonyesha boksi zuri, ndani kulikuwa na mkufu pamoja na hereni zake.
“Itakua ni ghali sana”
“Hapana ni bei ya kawaida tu”
Noela akasema “Hapakuwa na sababu ya kuninunulia zawadi. Maelezo yako ya kwamba ulikua busy nimeyaelewa mbona”🙈
“I know lakini hii ni njia yangu ya kukuomba samahani. Basi fanya kama hii ndo zawadi yako ya kwanza ya birthday yako”
“Birthday yangu? Umejuaje inakuja?”
Mr. Marvel akatabasamu “Najua mambo mengi kukuhusu”😊
“Unanitisha sasa”
“HahahahahHahaha, usiogope. So una mpango gani na birthday yako? Unaonaje tukapumzike Zanzibar kidogo?”
“No! Birthday yangu itakua kwenye kipindi cha mitihani, nitakuwa busy sana”😔
“Sawa! Basi Zanzibar tutaenda wakati utakapokuwa free. Lakini siku ya birthday yako lazima tutoke, Huwezi kunikatalia”
“Sawa Maana najua hata nikikataa hutakubali”
Noela akatabasamu, kisha akaendelea kupika. Baada ya dakika chache, chakula kilikuwa tayari. Akaandaa mezani, Wakakaa pamoja na kula.
Baada ya chakula kama kawaida, wakaangalia movie, wakapiga stori nyingi wakawa hadi wanajisahau.
Mr Marvel alikuwa anamtazama Noela kwa hisia fulani iviii za mapenzi. Alitamani hata amlambe busu lakini alihisi bado ni mapema, kwa sababu Noela alikuwa bado hajapona vizuri maumivu ya mapenzi.
Uzuri baba wa watu alikuwa tayari kusubiri. Na kitu kizuri ni kwamba aliona matumaini kuwa wanaweza kuwa pamoja na hilo ndilo lililompa subira.
Sasa Siku iliyofuata, Mr. Marvel alikuwa na mkutano muhimu asubuhi sana, hivyo akaamka mapema akaondoka. Alikuwa na mkutano kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa tano. Baada ya hapo akaenda kula, kisha akarudi ofisini. Akiwa ofisini, secretary wake akaingia na kumwambia kuna mgeni anataka kumuona.
Mr. Marvel akamuuliza “Ni nani huyo?”
“Simfahamu lakini anasema anakujua. Ni rafiki wa mwanao”
Mr. Marvel akashangaa, “Rafiki wa mwanangu? Kwa nini aje ofisini kwangu?”😳
“Sijui ila anaonekana ana jambo muhimu sana la kukuambia”
“Sawa, mwache aingie”
Secretary akatoka na baada ya dakika chache akarudi na yule mgeni. Mgeni huyo hakuwa mwingine bali ni Iris. Dada ana heka heka huyuuu🙌
Je nini kitaendelea?
Nakuja……..
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni