*AAAAAASH BOSS ENZO* *season two* *SEHEMU Ya tisa*
Kwanza kitendo cha pully kumuona mama yake mzazi kwenye eneo ilo Tena gafla alijikuta akishtuka sana na pasi na kutalajia akajikuta akimuuliza kwa jazba.
"Mama umekuja kufanya nini hapa?"
Kila mtu akashtuka na kwa pamoja wakauliza.
"Mama...?"
Ooooh nimewapeleka mbele sana eeeh, najua mnataka kujua nimewezaje kumtoa mama amina mgahawani kwake na kumleta mpaka kwenye eneo ilo anyway Ngoja niwaambie ilikuwa hivi.....
Baada ya Mimi kuzungumza na Suzy na akaniambia Habari za birthday party, ndugu yenu nikapata wazo na sikutaka kupoteza muda kabisa, muda huo huo nikafunga safari na kwenda kwenye mgahawa wa mama amina kule manzese.
Kiukweli huyu mama anisamehe tu Maana nilimdanganya Kuwa Binti yake anataka kumfanyia surprise kwenye siku hiyo muhimu ya kuzaliwa, mwanzo alikataa akidai Kuwa mwanaume hayuko Dar Bali yuko Dodoma, aiseeeh nilitumia akili nyingi sana kumuaminisha Kuwa amina Ndio amenituma nimfuate na baada ya maelezo mengi Ndio akakubali kuongozana na Mimi mpaka NYUMBANI Kwa Enzo na hivyo ndivyo ilivyokuwa my zangu, pully Sijui amina ameanzisha na Mimi. namaliza.
Kwakuwa niliona drama limeanza vizuri kabisa na Mimi Ndio nimelianzisha, moja kwa moja nikasogea mpaka kwa MC na kumuomba maiki kisha nikaanza kuzungumza.
"Hello pully"
Hapo Kila mtu akanigeukia Mimi na kumuangalia kwa mshangao wa hali ya juu, msisahau Kuwa nachukiwa kwenye hii familia, Yaani ni Kama Nilijivika mabomu kwa wakati huo.
"Huyu mpuuzi ameingiaje hapa?"
Aliuliza madam groly kwa hasira uku akinisogelea na kutaka kuchukua maiki.
"Madam groly subili kwanza Basi nimalize
kilichonileta, najua sijaalikwa hapa lakini Nipo kuwasaidia mjue ukweli wa huyo mkwe wenu, Sijui pully, Sijui pulizo anajua Mwenyewe
Muda huo huo Enzo akanisogelea na kwa SAUTI ya utulivu akaniuliza.
"ISHANI unafanya nini eeeh? Acha Bwana, umekuja kufanya nini hapa "
Aaah kwa wakati huo, akili yangu ilikuwa ni kumzalilisha pully tu na sio kingine hivyo kwa haraka nikazungumza.
"Nimekuja kuwaambia ukweli Kuwa, huyu. mwanamke mnayemjua Kama pully, Jina lako la
kweli ni Amina, na mama yake mzazi ni huyu hapa anauza chakula manzese"
Hapo kwanza Kila mtu akashtuka na Kila mtu akamgeukia pully wa mchongo na mama yake fake.
Enzo akaona haya mambo Mbona yanakupa magumu kwa Namna yake, haraka akanipokonya maiki na kutangaza Kuwa shughuli imeisha na watu watawanyike tu, Kiukweli niliharibu sherehe ya watu, lakini siwezi kusahau Kuwa pully au kwa Jina lingine Amina aliharibu Bishara yangu kwa makusudi kabisa.
Baada ya muda Kila mtu akatawanyika na familia Kama familia ikakutana sebuleni kwaajili ya mazungumzo, Sawa Mimi sio mwana familia lakini Kwakuwa Ndio msema ukweli nikajikuta nikiungana nao kwenye kikao cha familia Yao.
"Nini kinaendelea hapa?"
Madam groly alimuuliza Antie Asu, aaah sikuwa nimewatambulisha Antie asu, anti Asu ni mama
Pesa sana na ni mtu wa Karibu sana na familia wa mchongo wa Pully na ni mwanamke Mwenye ya kina Enzo.
Ila Mimi ni mpashukuna jamani, imagine ameulizwa mtu mwingine lakini Mimi Ndio nikadakia.
"Mimi Nitakuambia "
Madam Groly akaniangalia kwa hasira na kunifokea.
"Funga Mdomo wako we chokolaa wa kinyakyusa"
Kaaaaaaaha Kwahiyo Mimi chokolaa, Sawa bwnaa.
"Antie Asu, Kama huyu ni Amina, Binti yako Pully yuko wapi?"
Aliuliza Suzy, hapo kidogo ata Mimi nilishindwa kuelewa Yaani Antie Asu Ana Binti yake anaitwa Pully? Na Kwanini amtumie amina kwenye Jina
la Mtoto wake.
Baba mzazi wa Enzo, akasimama kiume kabisa na kumsogelea mama amina muuza chakula na kumuuliza.
"Kwahiyo huyu ni Binti yako na anaitwa amina?"
"Ndio, kwanza Mimi mnanichanganya tu, Binti
yangu huyu ni Mwanangu ni mwana chuo Uko Dodoma halafu Saa Hizi mnaniambia ni Mke wa mtu ni nini kinaendelea hapa? We amina
umeolewa lini? Hiyo Mahari yako amekula Nani 20
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni