TIPWA TIPWA NA MR MARVEL SEHEMU YA 7
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Bila kusema neno lolote, Mr. Marvel aligeuka akaondoka. Basi Salmon alitakiwa kusimamisha party lakini kabla hajafanya hivyo alimwangalia Noela akamwambia
“Ondoka! Unasubiria nini tena?”😒
“Hutanipeleka hostel?”
“No, sina muda”
“Kwa nini? Nitarudi vipi jamani?” Noela alitia huruma
“Ni juu yako. Chukua taxi au pikipiki utajua mwenyewe”😒
Noela akavuta pumzi kwa huzuni kisha akamwambia
“Kwa nini unanifanyia hivi na Nimeshakuomba msamaha”
“Tutazungumza kesho” kisha akamwacha Noela pale na kuondoka.
Alirudi kwa marafiki zake kuwaambia kuwa party imeisha na kila mtu akaanza kutawanyika. Kwa kua Salmon alikataa kumrudisha hostel, Noela akaamua kumtafuta Iris ili warudi pamoja.
Cha kushangaza hakumwona Iris popote. Basi Hakuwa na namna nyingine zaidi ya kurudi hostel peke yake.
Alitembea taratibu hadi akafika nje ya geti akisubiri taxi au pikipiki, lakini kwa kuwa ilikuwa giza na muda umeshapita, ilikuwa ngumu kupata usafiri. Akiwa pale, akasikia kama kuna mtu nyuma yake.
Kugeuka tu anakutana uso kwa uso na Mr. Marvel.
“Unataka nini?……….pia Sijisikii vizuri kukuona baada ya kile kilichotokea”
“Kile kilichotokea hotelini kilikuwa kosa”
“Ndiyo, lilikuwa kosa la kusahaulika and please usimwambie Salmon. Nampenda, sitaki kumpoteza” Noela aliomba🙏
Mr. Marvel akatabasamu “Sitomwambia chochote. Lakini Salmon ni mwanangu, namfahamu! Sidhani kama anakufaa and i know Mwishoni lazima utaumia”
“Sijaomba ushauri wako maana kinachoendelea kati yangu na mwanao hakikuhusu. Kaa ukijua Tunapendana” Noela akamjibu kwa hasira😡
“I know that! But Sitaki kukuona unaumia because itanivunja moyo. Nakupa onyo Noela, be careful”
“Asante, lakini sihitaji onyo lako” Noela Akageuka akiondoka Kwa hasira maana alihisi Mr Marvel anamchefua tu.
Alitembea kutoka kwa akina Salmon akielekea kwenye kituo cha daladala mpaka akahisi miguu inataka kuingia tumboni. Kila akitembea anaona kama hafiki alafu mbaya zaidi hapakua na boda wala Tax inayopita🥺.
Bahati nzuri kuna gari likapita na kusimama mbele yake. Dereva akashusha kioo akiwa ana smile taratibu
“Hellow! Nimetumwa na Mr. Marvel nikurudishe hostel”
“Sitaki! Sijaomba kupelekwa!” Alikataa
“Hapa mpaka ufike kituo cha daladala utasota sana! Pia sio salama maana kama juzi kuna sista alikabwa apo mtaa wa chini na nusu wambake! So utaingia nikupeleka ama nikuache uende??”🤔
Noela kusikia vile akaogopa, akajitafakari na kuona kweli anahitaji usafiri. Kwaiyo akaweka kiburi pembeni, Akazunguka upande wa pili na kukaa siti ya nyuma kimyaaa🤐.
Imagine Boyfriend wako anakataa kukupeleka nyumbani na hata usafiri hakuitii, ila baba ake anatoa private car speacial for you ikupeleke hadi mlangoni! How romantic💕💕
Hapa kweli Noela inabidi afungue macho yake lasivyo atalia sana.
Basi, Safari ikaendelea mpaka wakafika hostel. Noela akamshukuru dereva then akashuka na kuingia ndani hakutaka hata maneno mengi.
Baada ya kuhakikisha Noela ameingia ndani Salama, dereva akampigia Mr. Marvel kumpa taarifa kuwa ameshakamilisha kazi yake.
“Boss, tayari! Kafika salama”
“Good job George! Nina kazi nyingine nataka kukupa. I want taarifa zote kumhusu Noela, kuanzia Familia yake, marafiki na anachofanya kila siku. Umenielewa?”
“Nimekuelewa boss” kisha simu ikakatwa.
Ukweli ni kwamba Mr. Marvel hakuwa tayari kumuacha Noela. Moyo wake ulimwambia Noela ndiye mwanamke anae takiwa kuwa nae kwaiyo kumtoa kichwani na moyoni ni ngumu sana🥰.
Basi alisimama taratibu ili aende chumbani kwake kupumzika, ila kabla hajafika mbali, alisikia kelele toka chumba cha Salmon.
“Party imeisha, watu wote wameondoka hizi kelele ni za nini?”
Alisogea mpaka mlangoni mwa chumba Cha Salmon, akafungua na kuingia ndani. Alichokiona kilimkasirisha sana. Eti Salmon na Iris walikua wakifanya mapenzi kitandani bila hata uoga.
Aiseeee hasira zikampanda Mr Marvel vibaya mno
“Upuuzi gani huuuuu!” Alipiga kelele🗣️🗣️🗣️😡
Haraka Salmon akamsukuma Iris pembeni na kusimama kwa uoga maana hasira za baba yake anazijua vizuri kabisa.
Mr. Marvel akamwangalia Iris akamwambia
“Ondoka nyumbani kwangu! Get out….”🗣️
“Lakini nitaenda wapi usiku huu?” Iris aliuliza
“Unadhani najali??? I said get outtttttt (toka njeee)”
Weeeh Iris akaona hapa kachokoza nyuki, fasta fasta akachukua nguo zake, pochi na viatu akatoka spidi kama hana akili nzuri.
Huku nyuma alimuacha Salmon akiwaza ni namna gani atajitetea kwa baba yake.
“Ni upuuzi gani unafanya ndani kwangu Salmon???? Are you crazy? (Wewe ni kichaa)”😡
Salmon akajitetea “Lakini Dad sijafanya kosa”
“Unaona ulichofanya ni sahihi? Umenitambulisha kwa yule binti ukasema ni mpenzi wako, now nakukuta na mwingine and then unasema hujafanya kosa!”
“I know Dad! Noela ni mpenzi wangu lakini siwezi kukaa na msichana mmoja kila wakati. Mimi bado kijana nataka kuonja na wengine”
“Fanya unavyo fanya ila Sitaki kuona wasichana wengine ndani ya nyumba yangu Unanisikia?…….”
“Ndio Dad” 😔
“Also Hiyo tabia ni mbaya, kama unajua wazi unampotezea binti wa watu mda ni bora umuambie mapema!”
“Nimekuelewa Dad! Sorry…….haitatokea tena”
“I hope so” Mr Marvel hakutaka kuendelea kuongea, akaondoka zake.
Mpaka pale akaona kuna umuhimu wa kuongeza nguvu ili kumpata Noela ikiwa kijana wake haonyeshi nia yeyote ya kua nae. Ali smile taratibu mpaka anafika chumbani kwake😊.
Je nini kitatokea?
Nakuja………..
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni