TIPWA TIPWA NA MR MARVEL SEHEMU YA 8
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Siku iliyofuata Asubui, Noela aliamka na kitu cha kwanza alichofanya ni kumtumia Salmon ujumbe akimuomba msamaha. Alitegemea atajibiwa lakini haikua ivyo licha ya Salmon kusoma meseji zote🥱.
Sasa Dada watu akawa anawaza ni wapi anapokosea maana kila siku zinavyozidi kwenda ndivyo meli yake ya mahaba inavyozidi kuzama taratibuuuu.
Ila ghafla kuna kitu kikamjia kichwani, mnakumbuka ile siku ya Valentine? Salmon alisema baba yake alipata ajali, wakati huo Noela ndie alikua na baba yake hotelini. Hiyo ilimaanisha Salmon alimdanganya. Na kama alimdanganya Sasa alikuwa wapi? Na alikua na nani?????🤔
Noela kichwa kikapata moto sababu alipata uhakika kabisa kuwa lazima Salmon ana mchiti na mwanamke mwingine. Lakini hakujua kuwa msichana anayemsaliti naye ni rafiki yake wa karibu, Iris💔.
“Nikimjua huyo mwanamke uwiii sijui nitamfanyajee just sitaki hata kufikiria icho kitu…..” aliongea peke yake na mda huo huo Iris akaingia chumbani akiwa kachoka kama mbwa koko.
“Iris Ulikuwa wapi? Nilikutafuta jana kabla sijaondoka kwenye party” Noela akauliza
“Huna haja ya kujua”
“Unaweza kuniambia kilichotokea? Unaonekana umechoka na una hasira”😳
“Aahaaa bhana niache Sina nguvu ya kuongea. Hapa Nataka kulala tu”
“Kabla hujalala, nataka nikuambie kitu. Sikupenda jinsi wewe na Salmon mlivyokuwa mnafanya jana”
“Nilifanya nini?” Iris alijafanya kushangaa😳
“Ulikua unacheza naye karibu sana pia mlikuwa mnashikana shikana sana kama vile wewe ni mpenzi wake”
Iris akacheka kwa dharau “Jamani, ile ilikuwa party. Kwenye party watu wanacheza, Ulitegemea tufanye nini? …….. Ulielewa vibaya tu”
“Najua, lakini si sawa kufanya hivyo na boyfriend wangu. Pia sikupenda namna ulivyonicheka Iris”
“Sasa kucheka napo ni kosa? Nachoka mimi” Iris akakunja uso
“Si kosa lakini ulimcheka rafiki yako mwenyewe. Watu walinidharau lakini hukusimama hata upande wangu. Wewe na Salmon mlinicheka kama vile hamjali kabisa nitajihisije”🥺
“Sio siri kale kanguo ka kuogelea ulichokavaa kalikua kituko ila anyways kwa hilo samahani! Na wewe uache kuwa drama queen, kitu kidogo tu unachukulia serious”😒
Iris hakuonyesha kujali kabisa hata msamaha aliomuomba Noela haukua umetoka moyoni. Baada ya kusema hivyo akaenda kuoga kisha alipomaliza akapanda kitandani na kulala hata hakutia neno lingine.
Kuna jinsi Noela alihisi Iris amebadilika. Yule rafiki aliyemjua mwanzo na huyu ni watu wawili tofauti. Sikuhizi Hamjali kama zamani na wakati mwingine anaonekana kumtetea Salmon kumzidi yeye.
Kwa vile yeye sio mtu wa maneno mengi ama kulalamika sana, aliamua kupotezea na kuanza kujiandaa kwaajili ya kwenda kwenye vipindi.
Siku hiyo hata alichokua anafundishwa darasani hakua anakielewa, kila wakati alichungulia simu akitegemea atakuta sms zake zimejibiwa na Salmon, ila hapakua na chochote.
Mpaka jioni Salmon alimlia buyu dada wa watu kiasi kwamba Noela akawa mnyonge kupitiliza. Baada ya vipindi kuisha Noela alirudi hostel kupumzisha akili.
Alipofika, alimkuta Iris bado amelala Lakini alipotazama kitandani kwake akaona kulikua na mifuko minne ya shopping, maua pamoja na kadi🛍️💐
Kitu cha kwanza kilichokuja kichwani mwake ni kwamba zile zawadi zilitoka kwa Salmon. Weeeh Akafurahi sana, akarukaruka na mwishoni akaamua kumuamsha Iris.
“Iriisss amka……amkaaaa”😊
“Kuna nini? Mbona unaniamsha? Noela sipendi usumbufu nikiwa nimelala” Iris alilalamika
“Najua but kuna kitu nataka kukuuliza! Salmon alileta hizi zawadi saa ngapi?? Mbona hukuniambia?”
“Zawadi?? Unamaanisha nini?” Iris kuangalia vizuri ndo akaona zile zawadi, yani pale pale akajaa wivu maana hata yeye alijua vile vitu vimetoka kwa Salmon.
Tangu awe mchepuko wa Salmon hajawai nunuliwa hata kibakuli ila mwenzake anapata vizawadi kila kukicha ndo maana anaumia namna ile🤣
Noela wa watu hakugundua ilo, yeye ali focus na zawadi zake akiwa anafungua mfuko mmoja mmoja kujua kulikua kuna nini ndani.
Mfuko wa kwanza, Ndani alikuta kuna gauni zuri sana la rangi ya purple. Mfuko wa pili kulikuwa na boksi la viatu pair mbili na vyote ni saizi yake.
Mfuko wa tatu kulikuwa na vito vya thamani, kama hereni, cheni na pete. Alafu sasa mfuko wanne huko kulikuwa na aina tatu za perfume za gharama ambapo kila moja sio chini ya laki 6😱.
Alipomaliza kukagua mifuko akahamia kuisoma
Ile kadi ambayo ilikua ina maneno matamu sana ya mapenzi. Alipofika sasa kwenye jina la mtuma zawadi mood yote ilimuisha.
Alitegemea atakuta from Salmon, badala yake jina lilisoma from M na kakopa pembeni❤️. Akajiuliza huyo M ni nani ndipo mwishoni akapata majibu kuwa M sio mwingine bali ni Mr Marvel, baba wa Salmon.
Uso wake ukabadilika kutoka furaha hadi hasira mpaka ile kadi akaichana chana vipande na kuitupa pembeni.
Iris akashangaa mwenzake kachukia ghafla wakati sekunde mbili nyuma alikua anashangilia kama mtoto alie ona pipi.
“Vipi tena mwenzetu??? Mbona kisirani?”
“Nina hasira kwa sababu hizi zawadi hazijatoka kwa Salmon”
Iris kusikia vile kidogo akashusha pumzi kwa furaha
“Kama si zake, niza nani??”
“Kuna li mtu tu halijiheshimu hata kidogoo! Sijui watu wengine wapoje! Yani hawajui kabisa kukataliwa”😡
“Mbona sikuelewi Noela, mtu gani huyo? Mbona haujawai kuniambia kumhusu??”
“Acha tu…” Noela alikusanya zawadi zote na kwenda kuzifungia kabatini maana kama angeendelea kuziona basi angepata kichefu chefu.
“Iris please usimwambie Salmon kuhusu hili! Asije akajua jamani”🥺
Iris akauliza “Kwa nini asijue?? Au Una msaliti?”
“No! Siwezi kumsaliti”
“Basi kama si hivyo, kwa nini mwanaume mwingine anakununulia zawadi? Lazima kuna kitu kinaendelea. Na huyo mwanaume ni nani? Nataka kumjua, anaonekana ana pesa”
“Nitakuambia siku nyingine. Kwa sasa nataka kutafuta njia ya kumrudishia zawadi zake. Sitaki kitu chochote kutoka kwake naona kama hanielewi”😡
Iris akajibu “Sawa” kisha akarudi kulala.
Lakini ukweli ni kwamba ule umbea hakuweza kubaki nao moyoni. Ile ilikua karata yake ya mwisho ya kuicheza ili kusudi Salmon na Noela waachane kabisa kabisa.
Hata hakusubiri dakika mbili ziishe, pale pale alichukia simu, akaandika meseji ndefu akimsimulia Salmon kila kitu kisha akajikausha.
Je nini kitaendelea???
Nakuja………
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni