CEO SIKIMBII TENA NITAVUMILIA* *____________________________________* SEHEMU YA 3 Nilikua nipo mwenyew nazunguka tu kwenye lile kasri maan sijui niseme ni hoteli maan ni pazuri jaman mpaka
Nilikua nipo mwenyew mpaka nikaamua kuwasha tv nikawa naangalia nimekaa mpka mida ya saa 12 jioni naona namba ngeni inanipigia nikapokea nikaskia ‘mwanangu hujambo’’ nikajua kabisa huyu ni mama maan sauti yake haipotei kabisa maskioni mwangu nikasema kwa msisitizo na kudeka "mama kwanini ulikua kimya siku zote na wakat unajua kabisa mimi sipo karibu na wewe?" niliuliza kwa msisitizo mama akanijibu "ilibidi tubadilishe na makazi maan pale Buguruuni sio salama tena kwetu kwasababu wale watu uloingilia mambo yao hawashindwi kukupata na wasipokupata wewe wataumiza hata familia yako" nilishtuka kidgo nikasema "kwahy mama mpo mkoa gani na je mpo salam huko mlipo?" mama akanijibu "tupo Mwanza na tupo salama" mama akaendelea kunambia hivi wewe Nasma "nakuuliza swali?" nikasema "niulize tu mama mimi ni binti yako" akaniuliza "hivi wewe Nasma umejuanaje na huyo mkaka tajiri hivyoo?....
Maan huwezi ingilia mambo ya mtu ukiwa humjui huyoo mtu wewe unamjua", akashusha pumzi kidgo na kuendelea kusema hivi, "Nasma namby kweli mimi ndio mama ako" mimi nikamjibu nikamwambia, "mama hivi hata kama ndio niko hivyo lakin siwezi kuwa na mahusiano na wanaume wawil kwa wakati mmoja, kwanza nawapa kitu gani wakati unajua mii siezi fanya chochote ni muoga sana na hilo unalijua na ndio maana Kareem kasema kwamba ataleta posa nyumban ili anioe niwe mali yake maan anajua fika kabisa siwezi kufanya chochote bila ndoa mama", mama akawa kam vile bado hajaniamin akanambia "haya wee shauri yako hao watu wenye hela wengine wanawatoaga wapenzi wao kafara" nikacheka😌 tu nikaamua kumwambia mama napika ili tu nikate simu maan hawezi maliza kuongea asa hivi, nikawa nimemkatia simu ndio akili ya kusema niende jikoni ikaja nikaenda nikajipinda mtoto wa kike nikapika chakula pambe hatare hhh nilipika vitu vingi hadi nilivyokuaga naviona mtandaoni maan nilikua sijui Naseer atakuwa anapenda nini na kipi hapendi…
Ilikuwa mida ya saa tatu ndio Naseer akawa karudi akanikuta, akanisalimia nikamwambia "chakula kipo mezani" akanitizama akanambia "usijali nishakula" kisha akanisogelea akanipa begi, na mfuko umeandikwa woman suit dresses akanambia humo kuna nguo zako na humo ni nguo yako ya kazini nikasema sawa kisha akaondoka zake, akaenda ndani kwake na mimi nikaenda ndani kwangu siku ikawa imeisha kihivyoo……
Hatimae ni asubuhi hh😅😅 jaman nikaoga si ndy kuvaa ile nguo yangu ya kazini jaman mhhh nilipendeza na ile suti yangu nyeusi na kajimtandio changu mtihani ukaja kwenye kiatu bhana sijawahi vaa kiatu kirefu toka nazaliwa hhh😅😅 jaman ila ndy kuangalia vizuri kwenye ule mfuko nikaona kuna simple nikatabasam 😊nikavaa jaman na kusoma kwangu chuo kote lakin mambo ya fashion sijuagi kabisa yaan sio vitu vyangu kabisa …
Natoka ndani nashuka sebleni namkuta Naseer amekaa ananisubiria akanambia wewe ni "personal secretal wangu kwahy sehem, ntakayo kuwepo na wewe lazima uwepo" nikasema "okay sir" nikaongea kingereza etty hhh ila mimi🙈🙈…..
Tukapanda gari humo kwenye gari njia nzima tupo kibubu bubu🙄 hamna wa kumsemesha mwenziee bhana, hatimae tulipokua tunaenda tukafika bhaana kwenye hospitali akanambia "nifate nyuma" tukafika officine akanambia "kaa pale kwenye kiti" nikawa nimekaa tu sasa ntafanyaje , nikaskia mtu mlangoni "samahan boss naweza ingia" Naseer akasema ingia akaingia mdada yule ambae alikuja kunisafisha siku naumwa akasalimia akasema sir yale mafail uliyosema niyafanyie kazi haya hapa Nasser akayapokea na kuanza kuyakagua akasema "wow napenda wachapakazi yaani yalitakiwa kuchukua wiki kuyaandaa wewe umefanya kwa siku tatu wewe sio nesi tu yani ni genius girl" yule nesi akawa katoka , Naseer akanitizama akanambia "hii ni hospitali yangu pia namilki kampuni na pia nina kituo cha watoto yatima nilikifungua pia nina miliki migodi binafsi" , mimi nikawa namshangaa nasema moyoni "sasa ananiambia kuhusu utajiri wake mimi unanihusu? hovyoo😏😏", akaendelea kusema "pia nina miradi mingine kama maduka ya simu na nguo pia nina miliki hoteli na shule nikujikuta" namwambia "sawa nimeshaelewa" akanitazama kwa makini kisha akasema "nimekwambia hivyo sio kwasababu nataka kukuonesha mimi ni tajiri kiasi gani bali ni kwamba wewe ni secretary wangu binafsi hivyo sitaki nikiwa nakupeleka sehem unaanza kushangaa" nikasema "saw nimekuelewa" Muda ulipita sana na sasa tulikuwa tumekaa kila mtu ana kazi yake hamna anaemsemesha mwenzie , mara simu yangu ikaita nataka kupokea Naseer akasema kwa msisistizo "hakuna muda wa kuongea na simu tukiwa officine", sikujibu nikakata ile simu, ikapiga tena nikakata, hatimae nikazima simu, Naseer akanamby "officine kuna sheria kuna mambo hutakiwi fanya hasa ikiwa ni hospitali kwasabab hospitali kuna wagonjwa ambao hawahitaji kelel mlio wa simu unaleta disturbance kwao lakin kwenye office zingin tofauti nah ii ya hospitali unaruhusiwa kuongea na simu kasoro tukiwa kwenye vikao" nikasema "sawa nimekuelewa sir" akasema "unaez niita tu Naseer inatosha" nikamjibu "lakin wewe ni boss wangu: akasema "utavyojisikia kuniita niite tu hakuna shida", nikaitika nikasema sawa nikaendelea na mambo yangu, mara ghafla akaingia mdada kavaa short dress lekundu la tait kavaa kajiwigi flan , kwanza nikamshangaa😳 mbona kaingia bila hodi officine kwa watu, akanitizama kwa jicho kali kwel yaan tafkir ananijua au ashawahi kuniona sehemu Fulani 🤔 kisha akamsogelea Naseer kwa karibu….
JE NINI KITAENDELEA……..!! "
Full 1000 TU
NAMBA YA MALIPO 0755090082 MPESA JINA LA USAJILI ZAINABU SUNGITA MPESA
UKISHALIPIA NJO INBOX
WHATSAP 0755090082
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi