VYOTE NDANI GONGA94
JAMANI BOSS๐ฅ๐ SEHEMU YA 01...02
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Mimi ni Binti wa miaka 27 nimezaliwa mkoani Tanga mama yangu ni msambaa alafu baba yangu nasikia ni mpemba simjui wala sijawahi kumuona..
Nimelelewa na bibi mama aliniacha kwa bibi baada ya yeye kuolewa na baba yangu wa kambo ikabidi yeye aende akayaanze maisha mapya mimi nikabaki na bibi yangu Tanga..
Ndoto ya mama yangu ni mimi kusoma hadi chuo kikuu na nipate kazi...yeye aliishiaga njiani baada ya kubeba mimb yangu..
Mungu ni mwema sikumuangusha nilisoma hadi nikamaliza elimu ya juu na nilifaulu vizuri sana...mama alifurahi sana
Baada ya kumaliza chuo shida ikabaki kwenye kupata kazi nyie nilizunguka kwenye ma office ya watu mpaka basi miaka 4 yote natafuta kazi bila mafanikio..
Mwishoni nilichoka nikaamua kuachana na habari za kuatafuta kazi nikajiajili menyewe
Nilianza kufanya biashara ya vitafunwa mwanzo ilikuwa ni nzuri na yenye faida ila sijui akaingia mdudu gani nikawa siuzi kabisa
Mwanzo nilikuwa nauza chapati maandazi vitumbua na sambusa lakin ilifika mda vyote vikafa nikabaki nauza maandazi tena na yenyewe nilikuwa nauza siku mbili na mda mwingine yanabaki hadi siku ya 3 tunaamua kula wenyewe
"Ile hali iliniumiza sana kiukweli nilianza kukata tamaa mdogo mdogo nikawa sina mudi ya biashara tena"
"Sikia mjukuu wangu hasara ni jambo la kawaida kwenye biashara huwezi kupata faida kila siku ndio maana Kuna jua na mwezi kiangazi na masika hivyo hutakiwi kukata tamaa kabisa "
Ni maneno ya bibi hayo๐๐alivyoona nakata tamaa akaamua kuhakikisha ananipa ushauri ili nipate moyo wa kuendelea mbele..
"Hata usihangaike kutafuta misamiati bibi kazini siendi"
"Sawa pumzika basi "
Maisha yaliendelea nakumbuka siku moja mama alinipigia simu akaniambia Nina habari njema mwanangu"
"Umenishtua nikajua Kuna tatizo"
"We unawazaga matatizo tu"
"Okay niambie habari gani hizo "
"Nimeota umepata kazi tena yenye mshahara mzuri sana "
"Kumbe umeota nikajua unaniambia nimepata niende "
"Hiyo ndio shida yako huna Imani kabisa "
"Imani?mama ni mara ngapi umesema kuwa Mungu kakwambia kuwa napata kazi ?"
"Mwanangu Mungu huwa hadanganyi siku sio nyingi utapata kazi"
"Mmmm haya amina "
"Amina mwanangu sasa nakutumia Hela ukanunue nguo za kazin sawa"
"Ila mama na wewe sasa unanitumiaje Hela wakati kazi yenyewe haijapatikana "
"Imani ni kuwa na hakika na mambo ya tarajiwayo"
"Amina tuma mama"
Alikata nikaweka sm pembeni nakuendelea kulala
Nilikuja kuamka nikakuta mama katuma 150000 ili nikanunue nguo
Nyie mama yangu ananipnda basi tu natamani nipate hiyo kazi ili namimi nimpe maua yake angali bado hai.
Mungu anitunzie mama yangu ili aje afaidi matunda ya mwanae
Baada ya kumaliza kazi zote niliamua kukaa zangu chumbani kwangu nikawa bz napitia picha za mimi na marafiki zangu kipindi tukiwa chuo
Nilijikuta njisikia vibaya kwani marafiki zangu wote walikuwa wanamaisha Yao mazuri tu na kazi nzuri na baadhi yao walikuwa tayari wameshapata wenzi wa maisha yao
Ila mimi sasa sina kazi Sina mchmb Wala msebure miaka ndio hiyo inaenda..dah mawazo yalikuwa mengi sana
Nikiwa katika ndimbwi la mawazo nilishitushwa na sm yangu ilikuwa inaita
Haraka niliichukua na kuangalia alikuwa ni rafiki yang Tuli
"Hallo Tuli".
"Nyooo baada ya kukupigia ndio unajifanya kunichangamkia hello Tuli"
"Aaaa bwana usiniambie umenuna"
"Nisinune vp wakati hata sim hutaki kunipigia sijui ndo ushapata rafiki mwingine kwaiyo umenisahau"
" Aaa weee naanzaje kukuacha rafiki yang kipnzi "
"Mh hay bhn ,haya tuachane na hayo sikia nimekupigia kukupa habari njema "
"Usiniambie unaolewa"
"We nawe unawazaga kuolewa tu"
"Sasa kimebaki nini kama wewe umesha soma na kazi tayar "..
"Bibi wewe niache kula bata eti nikimbilie kuolewa hivi unadhani ndoa mchezo we zisikie kwa watu tu na uziache hivyo hivyo,
hembu ngoja niende kwenye point, ni hivi hapa kazini Kuna nafasi za kazi za watu wa 5 wawili wa kozi yko na hawa wengine wakitengo kingine sasa hapa nimeshakenua meno kwa meneja ili upate nafasi"
"Weeee usiniambie "
"Ndio hivyo mpnzi kwaiyo kesho nakuomba ufike Dar mapema ili kesho kutwa ukafanye interview"
"Ndio maana nakupnda T wangu Mungu akuweke my dr "
"Usijali maa utoke sasa maana umeshachoma maandazi hadi ukipita unanukia hiliki tu"
"Hahhahaha mshnz wewe asante sana "
"Poaa basi nakungoja Dar.."
Tuliagana nikakimbia nje huku nikishangilia na kwenda kumkumbatia bibi akiwa zake bz kufuma mikeka
"Wewe unataka kunivunja mabega yangu"
"Bibi na wewe jitahidi kuwa mzungu hata kwa mda basi hapa ulitakiwa usema hey be careful and why you're so happy, sio unataka kunivunja ๐คฃ"
"Nimekosa nn hadi niwe mzungu "
"Achana na hayo ni hivi nnimepigiwa sm na Tuli anasema Kuna nafasi ya kazi huko dar kwaiyo natakiwa kuondoka kesho "
"Mama yako ameshaniambia"..
"๐ณ Mama amekwambia ๐ค"ilibidi niiulize kwanza kwani mama kajuje T amempigia hapana T hawezi kumpigia mama
"Alisema kuwa Mungu kamwambia "
"Oooo! Basi ndio hivyo "
"Kwaiyo kesho nabaki pekee yangu " bibi aliongea kwa unyonge nilijikuta na jisikia vibaya nikamkumbatia na kumwambia
"Hapana huatakuwa peke yako niko na wewe japo kimwl hatutakuwa wote ila kiroho Niko na wewe"
"Kwaiyo tutoke kwenye huu mwl tuishi kiroho"
",Wewe tena hata sijui babu alikupataje"
"Eee muache Mpnz wangu"
"Bibi yangu ni comedian๐๐"
Basi tulipiga story pale ilipofika jioni nilimwaga nguo zote nikachagua zile nzuri Kisha nikaziweka kwenye begi
Mara sim ikaita kuangalia ni mama
"Hello dada Vanessa"niliongea kimatani, huwa nimezoea kumtania basi akiwa vibaya ananichambaga mpaka basi ๐
"Koma wewe nani dada yako"
"Hahahahahaha wamesha kuvurugwa tayari "
"Mbona hujaniambia kama unaenda kufanya interview kesho kutwa "
"Hee mama we siumeshajua kabla yangu "
"Hata kama ungeniambia "
"Sawa dia mama nisamehe "
"Haya umeshajiandaa"
"Ndio mama "
"Na nguo ulinunua'"
"Hapana nitanunua nilifika huko huko "
"Kwaiyo kwenye hiyo interview utaenda umevaa
nini "
'" nguo za kuvaa zipo nyingi"
"Haya utajua mwenyewe,ila jitahidi kwenda ukiwa smart"
"Hilo tu usijali"
"Haya jioni njema"
"Haya mama byee"
"Alafu uoshe hizo nywele usije kwenda kwenye office za watu na minywele inanka "
"Mama bhn ushaanza mambo yako"
"Mambo yangu yamefanya nn we osha hicho kichwa tena ikiwezekana ukasuke kama huna hela sema nikutumie "
"Kusuka tena ๐ bora nioshe tu"
"Osha na usuke nakutumia hela ukasuke sasa ole wako bibi yako aniambie hujasuka".
"Sasa mama nasuka sangp wakati safari ni kesho asubuhi "
"Sasaivi unanynysha au uko mazishini"
"Eeee haya nitaenda "
"Na uoge vizuri "
"Tena ๐คฃ khaa haya mama"
Hakutaka hata kuaga akakata sm
Basi niliosha nywele mda huo muamala ukasoma mama kasha tuma hela huyu mwanmk nyiee hahahaa kwani anataka nikamteg Boss au๐
Baada ya kumaliza kuosha nywele nilienda kusuka kwa dada mmoja hivi jirani yetu
Kesho yake niliamka asubuhi nikaongozana na bibi hadi stendi tukaagana Kisha nikapanda gari na safari ya kuja dar ikaanza
Je huku Dar ilikuwaje?? Alipata kazi?. Itaendeleaaaaaaa
Tume toka mbali na nyumbani kuja kwenye miji ya watu kutafuta maisha
Mwanangu Mungu ndio anae jua
Sikiliza Wimbo Kamili
Umesoma kwa utulivu ยท dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi jamani-boss-sehemu-ya