FATE TO LOVE YOU π 5 MTUNZI UHURU MEDIA Alipokuwa njiani alimpigia simu Mishely. " Hallow Mishely... " Lina mbona kama unalia?
" Uko wapi?
" Nipo nyumbani.
" Nataka kuonana na wewe nina matatizo rafiki yangu.
" Sawa niambie uko wapi nikufuate?
" Natoka nyumbani kwake Maxwell .
" Nitakuwa hapo baada ya dakika chache nisubiri hapohapo.
" Sawa.
Lina alisimama kumsubiri huku akiwa na hasira na Stephen.
" Nitahakikisha nafanya juu chini kupanua maisha yangu siwezi kuvumilia hizi dharau.
Baada ya dakika kadhaa kuna gari nyekundu ilifika na kusimama mbele yake. Lina alikuwa akiangalia kwa makini, mara kioo cha gari kiliteremshwa na Mishely ajachungulia.
" Lina fungua mlango uingie.
" Mishely ni wewe? Aliuliza lina kwa mshangao huku alifungua mlango wa gari. Akapandishwa begi lake siri ya nyuma kisha akaenda kupanda siri ya mbele.
Mishely aliwasha gari wakawa wanaelekea nyumbani kwake.
" Lina nini kimetokea?
" Siwezi kuishi kwenye ile familia ya kishenzi iliyojaa dharau na masimango.
" Nilijua tu hautadumu kwenye ile nyumba. Ila usijali kazi zipo nyingi sana si unaona mimi nilivyopiga hatua baada ya kutoka pale.
" Kwanza nataka kujua hili gari ni lako au umeazima?
Mishely wakicheka sana .
" Lina ndio maana nilikwambia kukaa kwenye ile nyumba ni kuendelea kuwa masikini . Hii gari ni gari yangu na maisha yangu safi .hata wewe ukitaka unaweza kuwa kama mimi.
" Nawezaje wakati sina elimu ya kusema niajiriwe na kupokea mshahara mkubwa?
" Achana na hiyo elimu , haya maisha yanahitaji akili tu, kikubwa ni utayari wako.
Walifika kwenye nyumba ya Mishely , lina alibaki mdomo kwa mshangao.
" Mishely hapa ndipo unapoishi?
" Sio kuishi tu ni nyumbani kwangu, hii nyumba wamiliki mimi.
" Umewezaje kupata hivi vyote?
" Ni rahisi tu. Alijibu Mishely huku akikaa kwenye kochi lake la gharama.
Lina hakuwa na la kuongea zaidi ya kuangaza macho kila upande wa ile sebule.
" Kaa Lina , naweza kukufanya ukawa kama mimi.
" Tafadhali Mishely nisaidie niweze kufika hapa ulipo.
" Kama utakuwa tayari kesho nitakupeleke.
" Nipo tayari kipenzi.
" Sawa.
Mishely alipeleka mabegi chumbani kisha akaenda kuandaa chakula .
Usiku ule walikula pamoja huku akili ya Lina ikiwa inawaza mafanikio tu.
Upande wa ili Tasha alipokuwa ameondoka Stephen alianza kumtafuta Lina. Alipita kila kona hakumuona. Alimfuata shangazi yake akamuuliza.
" Nilikuwa nina shida na Lina sijui yuko wapi?
" Lina hayupo.
" Ameenda wapi?
" Ameenda na hatarudi tena.
" Kivipi?
" Ameacha kazi
" Kwa ruhusa ya nani? Alimuacha nani wakati anaondoka?
" Ni maamuzi yake hivyo hakuna mtu wa kumpinga , alafu huu ni mwisho wa mwezi hamumfai .
Stephen aliondoka kwa hasira , alijaribu kupiga simu ya Lina lakini haikupokelewa .
" Huyu msichana ni mshenzi sana, anaondoka je sasa ?
Aliongea Stephen akiwa amepaniki.
Kesho yake asubuhi Lina alikuwa amejiandaa akijua ndio muda wa kupelekwa kazini .
" Vipi bado haujajiandaa? Lina alimuuliza Mishely
" Kujiandaa kwenda wapi?
" Jana tukiongeza nini?
" Tukiongeza mengi.
" Kuhusu kujipeleka kazini.
Mishely aliachia tabasamu, alinyanyuka alipokuwa amekaa akaenda kumshika begani.
" Sio muda huu kipenzi alafu huwezi kwenda ukiwa upo hivi .
" Sijakuelewa.
" Taratibu utanielewa tu.
Ilimbidi lina awe mpole na kusikiliza kile atakachoambiwa na mwenyeji wake.
" Stephen alinipigia sana simu .
" Anataka nini?
" Sijui na wala sikutaka kujisumbua kupokea.
"Achana nae.
Ilifika jioni Mishely alienda kwenye chumba cha Lina akiwa na nguo mkononi pamoja na viatu.
" Unatakiwa kujiandaa sasa. Unatakiwa kujitenga ili upendeze maana huwezi kupata kazi ukiwa rafu.
Lina aliangalia nguo alizokuwa amepelekewa.
" Hizi nguo ndio natakiwa kuvaa?
" Ndio. Lina alionekana kuwa na wasiwasi kidogo.
" Mishely ni kazi gani ambayo naenda kufanya nikiwa nimevaa nguo za kuniacha maungo wazi , kama hii mgongo wote utakuwa wazi.
" Lina unataka kuwa kama mimi au hautaki?
" Nataka .
" Basi jitoe , fumba macho. Unaenda kukutana na mwanaume mwenye pesa usiku mmoja tu unaweza kupata hela ya kulipa kodi na wewe unaenda kuishi kwako.
Lina alijikuta akishusha pumzi ndefu hakujua akubali au akatae.
Akiwa anafikiria mara iliingia messege kwenye simu yake.
Alifungua na kukuta ni Stephen kamtumia.
" Unajifanya jeuri na hauna kitu, umeamua kwenda kijijini kuzalishwa kama sungura huku ukisurubishwa na jembe kama mtumwa , jua kali likiupiga mgongo wako.
Kweli masikini ni watu wa ajabu sana yani hata akili zenu haziwezi mambo makubwa inawaza umasikini tu.
Lina alipomaliza kusoma alifyonza kwa hasira kisha akasema.
" Nipe nafasi ya kujiandaa.
Mishely aliachia tabasamu kisha akatoka.
Lina alienda kukaa mbele ya kioo cha dressing table na kuanza kujiremba, alivaa nguo zake na kusimama mbele ya kioo akiangalia kisha akaachia tabasamu.
" Hapa hakuna cha kuongeza wala cha kupunguza .
Alitoka ndani ya kile chumba na kwenda sebleni, Mishely alipomuona alisimama na kusema
" Waoooo .... Lina umejua kuniacha mdomo wazi, umependeza sana .
" Asante.
" Sasa tunaweza kwenda.
Walitoka na kwenda kupanda kwenye gari ya Mishely.
Safari ilianza mpaka kwenye hoteli moja ya kifahari.
Usiku huo ulikuwa na kibaridi kilicho penya kwenye mwili wa Lina.
" Shika hii kadi ukifika pale mlango muonyeshe mlinzi atakupeleka mpaka kwa huyu mtu.
Lina alipokea ile kadi na kuiangalia ilikuwa imeandikwa jina la Jovin peter.
" Huyo mtu ndio mtu ambae atabadilisha maisha yako siku ya leo.
Full 1000
Whatsp
0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi