VYOTE NDANI GONGA94
MY TRUE LOVE STORY SEHEMU YA 19 - 20
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Yule baba alikuwa anaongea kwa upole na kwa busara ya hali ya juu, yaan maneno yake yote tuliyaelewa vyema kabisa, nabil akamuangalia baba yake wa mchongo kisha akasema “ nampenda sana mama na nakupenda sana wewe, ila naomba nikawaone hata wazaz wangu, na nitaongea nao, na ninakuhakikishia hawatakuwa na shida kabisa kwa mimi kuwa kijana wenu ila angalau tu wajue kuwa nipo hai, kwa sababu nimesikia mama yangu hajawah kuacha kulia kuanzia aliponipoteza…
Yule baba alituelewa, na tukalala, na kesho yake nabil aliamka na kupika chakula ambacho alikuwa anakipenda sana mama yake, na mama yake akafurah sana, kisha wakawa wanataniana sana, yaan mpaka utapenda maisha yao, na mimi siku hio sikujichanganya nao, maana najua mimi ndio tishio lake kubwa…
Basi baada ya siku hio nabil au kwa jina lingine omari, akataka turudi nduruma tuende tukatoe taarifa kuhusu uzima wake…
Tumefika usiku, ila tulifikia kwa akina omari, kwa sababu mimi ndio nimeshaolewa tena, na wakati tunafika nyumba yao ilishakamilika na wazazi wake wakawa wameanza kupata nuru na mwanga hata kidogo…
Mama yake alipomuona ni kama hakuamin, akaanza kulia. Ikabidi omari akamkumbatie mama yake, na baada ya muda mfupi baba yake nae akaja, alikuwa huko unguuni, wakaanza kupiga story na omari akasimulia maisha yake yote na kuwaomba sana Yule mama akishakuja kuwaona wamkatae kuwa hawampendi, sio kwa sababu labda wanataka mali, ila ni kwasababu wanataka kumtengenezea mazingira mzuri ya kuamin kuwa omari ni wakwake pekee yake, kwa usalama wa afya na akili yake….
Baba yake hakuwa na shida, ila mama yake akawa anasema kuwa hawez kumkana mwanae, kisa mwanamke mwingine, ila omari alimchukua mama yake na kwenda kuzngumza nae sana, basi mwisho mama yake akamuelewa…
Basi bana tukarudi dar, na yule mama bado alikuwa na hasira na mimi, ila sijui hata mume wake pamoja na nabil walimuambia kitu gani, akapoa akawa ananichangamkia kama kawiada, na baada ya muda flani tikaerudi tena nduruma mkoani Arusha kwenye familia ya akina omari na wamefika tu baba na mama yake omari wakaanza kuwafukuza, kumbe yote yalikuwa ni maigizo na mimi nikawa nawasema vibaya, sasa huyu mama mwingine akawa ananiona mimi ni mka mwana bora sana, nikaomba niende kwetu kuwatambulisha, na wazaz wangu walishaambiwa hali ilivyo hivyo hawakuwa na shida, basi tukarudi kuendelea na maisha yetu kama kawaida, na yule mama akawa ndio Yule mama ambae alikuwa ana upendo kuanzia nakutana nae…
Omari alikuwa anawasiliana vyema na familia yake, na alikuwa ana toa misaada sana kijijin, na kuhusu wale watu ambao walitufanyia ukatili, huyu baba wa omari wa kufikia akasema tumuachie hilo yeye atamalizana nalo…
Na kweli baada ya miaka mingi wakakamatwa, na walishajiaminisha kuwa hali ilishakuwa shwari, na baada ya kukamatwa sijui hata Yule baba alitengeneza mazingira gani kwa sababu walifungwa na kupewa hukumu za kukaa zaidi ya miaka 30 jela…
Kuhusu shenaiza wazaz wake walikuja kumchukua, ni kweli alikuwa anampenda sana omari, ila kuishi na mwanaume asiekupenda ni sumu kubwa sana, hivyo akapewa talaka kabla hata hajaguswa kimwili na mume wake, na faisal alikujaga kwenye ndoa yangu na omari na akatupa baraka zote na maisha yetu yakawa yanaendelea kwa upendo na amani ya ajabu….
SIKU ZOTE USIPOTEZE TUMAINI KWA MWENYEZI MUNGU, NA KAMA RIZKI YAKO IPO HAKUNA MTU HATA MMOJA ANAEWEZA KUICHUKUA..
MWISHO
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi my-true-love-story-sehemu-ya
