FATE TO LOVE YOU π 9 MTUNZI UHURU MEDIA Angelo alimuangalia na kutambua wasiwasi pa moja na hofu aliyokuwa nayo Lina.p
" kama nilivyojitambulisha hapo mwanzo naitwa Angelo na nimekuja hapa kwa agizo la Jerry.
" Jerry huyu Double J?
" Ndio huyo huyo.
Lina alitulia kimnya huku akiwa anajiuliza Jerry amejuaje kama yupo pale kituoni.
" Tunaweza kufuatana pamoja.
" Kwenda wapi?
" Aliniambia tukitoka kituoni tuende pamoja nyumbani kwake.
" Sawa lakini nataka kumtafuta shangazi yangu kwanza.
" Sawa fanya hivyo.
Lina alichukua simu yake na kupiga simu kwa shangazi yake. Simu iliita mara mbili kisha ikapokelewa.
" Vipi lina? Shangazi yake aliuliza kwa shauku.
" Shangazi nimetoka polisi kwa dhamana , wewe upo wapi?
" Nimechukua chumba gesti nilikuwa nafikiria kuja kudhamini huko polisi.
" Basi pumzika shangazi nitakuja huko uliko.
" Njoo sasa hivi binti yangu.
" Hapana shangazi sio saizi. Kwanza natakiwa kwenda kuonana na Boss alienitoa polisi baada ya hapo nitakuja ulipo.
" Sawa
Lina alikata simu kisha akaondoka na Angelo wakaelekea nyumbani kwa Jerry.
Lina alishangaa wanaenda kwenye nyumba tofauti na ile iliyokuwa na sherehe siku ile.
" Huku ni wapi?
" Ni nyumbani kwa Jerry.
" Anakaa huku?
" Hii ndio nyumba yake anayoishi japokuwa ana nyumba nyingi sana hapa mjini.
Walishuka kwenye gari na kuelekea ndani ya jumba la kifahari lililopangwa kwa thamani za bei ghari. Kulikuwa na walinzi pamoja na wafanyakazi wa kutosha.
Walikuja sebleni wakamkuta Jerry akiwa anaongea na mwanaume mmoja. Jerry alipomuona Lina aliachia tabasamu na kumkaribisha.
" Karibu sana Lina.
" Asante.
" Karibu ukae.
Lina aliangalia makochi kisha akamuangalia jinsi alivyo nafsi yake ikamsuta ilimbidi aendelee kusimama.
Jerry alikuwa anasafiri kwenye baadhi ya mafaili kisha akakabidhiwa yule mwanaume aliekuwa nae wakaagana.
Jerry alisogea pale walipokuwa wamesimama lina na Angelo.
" Wote mmegoma kukaa?
" Mimi sina muda wa kuendelea kukaa hapa , nimemleta Lina na sasa naomba ruhusa ya kuondoka.
" Nashukuru sana Angelo.
Angelo aliwasha kisha akaondoka na kuwaacha .
" Utasimama hivyo hivyo?
" Mmmh kwa hali yangu niliyokuwa nayo siwezi , hata hivyo nimefanya makosa kuingia ndani .
" Kwanini unajihisi umekosea?
" Nimewahi kusikia mtu akitoka jela au rumande hatakiwi kuingia ndani mpaka afanyiwe mambo fulani.
Jerry alimuangalia kisha akacheka.
" Achana na mambo ya uzushi, hayo maneno hayana maana kabisa. Nifuate.
Jerry walitangulia na Lina alimfuata, walipandisha ngazi mpaka kwenye chumba kimoja kizuri kilikuwa kuna kitanda , kabati na dressing table kubwa na zuria dogo la manyoya la rangi ya off white.
" Ingia hapo bafuni uoge naenda kuongea na dada akuletee nguo ya kubadili.
" Sawa , asante.
Jerry alitoka pale chumbani , kina alivua nguo zake akachukua taulo jeupe lililokuwa limeandaliwa kwaajili yake akajifungua na kuingia bafuni.
Aliita kwa sabuni nzuri zilizokuwa na harufu nzuri , alihakikisha anajisugua vizuri kutoa mikosi . Baada ya kumaliza alikuta kuna nguo zimewekwa kitandani .
Alisogea kwenye dressing table akachukua mafuta na kupaka kisha akavaa nguo safi . Alipomaliza alishuka chini kwenda kuonana na Jerry.
" Karibu huku.
Alipofika sebleni Jerry alikuwa dinning akamuita ili wakale pamoja.
" Najua una njaa , tule kwanza ndio tuendelee na maongezi.
" Samahani nilikuja tu hapa kutoa shukran zangu kwanza , bado nina mambo ya kuyashughulikia haraka.
"Mambo gani hayo ambayo yanabana hayatupi nafasi ya kupata chakula pamoja.
" Shangazi yangu , sijui yupo kwenye hali gani.
" Kwani unajua alipo?
" Yupo kwenye guest moja huko mitaani .
Jerry alinyanyuka na kumfuata Kina pale alipokuwa kasimama.
" Nitaongoza na pamoja na wewe.
Walitoka nje ya nyumba na kupanda kwenye gari dereva aliendesha gari mpaka kwenye guest moja ya zamani iliyokuwa na kibao kilichoandikwa Sheraton guest .
Walishuka kwenye gari wakaingia ndani na kukutana na dada mmoja ambae alionekana ndio muhudumu wa pale.
" Samahani nilikuwa nataka kuonana na mwanamke mmoja wa makamo anaitwa Elizaberth Mwamba .
Kabla yule muhudumu hawaamini is wapi kwa kumpata Lina alimuona shangazi yake.
" Basi yule pale.
Lina alimfuata na kumkumbatia shangazi yake.
" Lina imekuwaje mpaka ukapata dhamana wakati nasikia hawakufika utoke hata kwa dhamana?
" Shangazi ni story ndefu kidogo ila elewa hii dunia ina watu wenye roho tofauti sana sio kila mwenye pesa anamdhsrau na kumgandamiza mtu wa hali ya chini.
" Ni kweli.
" Jerryson Jonathan ndio alituma wakili wake akaja kunitoa.
" Asante Mungu.
" Shangazi nimekuja na Jerry anataka tuondoke hapa tukakae nyumbani kwake kwa muda mpaka pale mambo yetu yatakapo kaa sawa.
Lina na shangazi yake wakibeba mizigo na kwenda kupandisha kwenye gari la Jerry kisha safari ya kuelekea kwake ikaanza.
Siku hiyo Jerry alikuwa mkarimu sana kwao akiwa hudumia kwa kila kitu muhimu walichokuwa wanahitaji.
" Huyu kijana umenijulia wapi?
" Mimi mwenyewe nipo kwenye fumbo yani ananijua kuliko unavyotegemea.
" Mmmh..... Sasa hatma yetu ni ipi?
" Nataka niongee nae kama atanipa kazi.
" Sawa lakini mimi nataka kurudi kijijini. Kwa pesa niliyokuwa nayo nitaenda kulima na kulipa vibarua baada ya hapo nitaangalia miradi mingine ya kufanya.
" Sawa shangazi , hata mimi nilifanikiwa nitakuwa nakutumia pesa .
Kesho yake asubuhi Stephen aliamka mapema na kwenda jikoni ambako kulikuwa na mpishi mpya.
" Umeniandaoia kile nilichokuwa nimemwambia uniandikie jana usiku?
" Ndio kila kitu kipo tayari nimeweka kwenye huo mfuko.
Stephen alichungulia kwenye mfuko akaona vitafunwa na chupa ya chai. Alibeba ule mfuko na kuondoka nao.
Alianza safari kuelekea kituo cha polisi kwaajili ya kumpelekea Lina chai.
Alipofika kituoni alimkuta mama yake ameshafika.
" Inawezekana vipi na mimi nilisema asitokewe hapa?
" Mr Maxwell dhamana ilikuwa ni haki yake na isitoshe alikuja wakili wake.
" Acha kunifanya wakili anamtoa wapi yule mpaka hoi?
Stephen alisogea mpaka alipo mama yake.
" Mama kuna nini?
" Lina hayupo , eti wakaniambia katoka kwa dhamana na alikuja kutolewa na mwanasheria, hivi inakuingia akilini kweli?
" Mwanasheria Lina Kampala wapi?
" Tena sio mwanasheria wa kando kando ni mwanasheria mkubwa sana anayesimamia kesi za watu wa kubwa Angelo. Aliongea askari mmoja.
Stephen na mama yake waliangaliana kwa mshangao.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi