VYOTE NDANI GONGA94
MY TRUE LOVE STORY SEHEMU YA 16
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Mama yake akamfata na kuanza kuongea nae, ila ni kama nabil hakuwa anajali kabisa, ikabidi mama yake amuache, ila pia shenaiza hakuwa anajisikia vizuri, yaan mbele ya mashoga zake kabisa, mwanaume anaonesha hana muda nae na anamuda zaidi na dada wa kazi, akawa anapakwa hina huku kanuna huyo, ila mimi sasa nilikuwa najiona kama malkia vile, nikawa natabasamu kila dakika kama nimeona bia za offer..
Basi nabil akafanya shughuli zake, na siku hio hata hakujali mtu, nadhan aliamua kufata moyo wake, akawa anakaa na mimi sana, anapiga story na mimi sana, na hata kulala hakutaka kuaminisha watu kuwa analalaga na shenaiza kwa sababu alikuja chumban kwangu mapema sana na hakutoka mpaka mimi nikawa nina wasiwasi sasa, ila kila wakati akawa ananisisitizia kuwa nimuamin, na hawez kuniumiza kwa namna yoyote ile kwa sababu ananipenda sana…
Kesho yake ilikuwa ndio ndoa sasa, nilimuona kamfata mama yake, na kaongea nae sana ila mama yake ni kama hakuelewana nae kabisa, akaondoka zake…
Shenaiza akanifata na kunambia “ ndio naolewa hivyo na nabil anakuwa mwanaume wangu milele daima sijui utaweka wapi sura yako…
Nikatabasamu kisha nikamuambia “ sura yangu nitaiweka kwenye moyo wa nabil, kwa sababu hata ukiwa na mwili wake utakuwa na kiwili wili chake tu ila hisia na mapenzi yake yapo kwangu, haya mama muolewaji nenda kaolewe ulie kila siku kwa kuwa na mwanaume asiekupenda hata kidogo na anakuonesha kila siku, ila unajifanya king’ang’a haya ng’ang’ania mama mpaka mwisho tuone mwisho wako ni wapi…
Akataka kuniwasha kibao, nilimshika mkono kisha nikauviringisha na kusema “ kama kuna watu ulikuwa unawaonea na kuwapiga hovyo ni hao, ila hautakaa unitamkie maneno ya hovyo kwa sababu nitakufundisha adabu na hautakaa pia uniguse hata kwa bahati mbaya, kwa sababu hapo nitakuhakikishia kuwa unachapika mpaka unaenda kulazwa…
Aliniangalia kwa hasira kisha akaondoka zake, nikawa najiambia kuwa huyu ameshazoea kuonea watu basi safari hii amejichanganya, na amejichanganya vibaya sana…
Basi harakati za harusi zikawa zinaendelea kama kawaida, mara nabil akarudi akanifata mpaka nilipo, kisha akanishika mkono na kuanza kunikokota, tukaenda mpaka msikitini, nikashangaa namkuta baba yangu hapa, nikauliza kulikoni, akaniangalia na kusema ‘ hata kama nitaoa mwanamke mwingine ila wewe lazima uwe mke wangu wa kwanza…
Nikakubali haraka haraka bila hata kufikiria mara mbili, basi tukafunga ka ndoa chetu cha chap chap, na baba akataka kuuliza kama Yule ni omari au laa, ila tukamuomba arudi nyumban, kwa sababu kumbe omari alimsafirisha kimya kimya bila hata kunambia, na akamuomba asiwaambie watu kama amemuona, awaambie tu kuwa katoka kumuozesha binti yake kwa nabil, na asiongee jambo lingine lolote lile, basi baba akaelewa kisha akaondoka zake…
Tukarudi nyumban na kila kitu kikawa kinaendelea kama kawaida, hakuna mtu hata mmoja alijua kuwa omari ameshafunga ndoa, na harakati za ndoa zikawa zinaendelea kama kawaida, na alipofika pale akafunga ndoa tena…
ITAENDELEA …
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi my-true-love-story-sehemu-ya
