FROM BANGI TO BABY ππ SEHEMU YA 17
Ikabidi nikae tu kwenye piki piki maana sura alivyokuwa kaikaza mmh asije kunipiga, Kimyaa kikatawala sasa mie nilijua tunaenda kwa Tinner na moyoni nilikuwa nimempangia hayo maneno Tinner eeh mbona hasira zangu zote nilihitaji kumalizia kwake ...
Nishangaa hatuenda kwa Tinner khaa nikamuuliza kwa hamaki kwani tunaenda wapii?? Hata ananijibu basii wa mbuzii yaani amekasirikaaa eeh nikawa namwambia nishushee yupo kimyaa hata hanijibu, akaongeza mwendoo ooh ikabidi nifumbe macho maana niliona hapa tunaenda kufaa sasa nikamshika kwa nguvuuu, mpaka nilipo hisi piki piki kusimama ndio nikafumbua macho naona tupo nje ya nyumba kuna geti dogo jeusi akanambia shuka hapokanishika mkono, mpaka nikaanza kumuogopa alivyokuwa amekunja sura, nikashuka
Kabla sijapiga hatua nikamuuliza kwani hapa wapi, , , wee hakunijibu alinikata jicho hilooo hee nikaanza mwenyewe kutembea naogopa ukweli ile nasukuma geti nakutana na Tinner hee nilishtukaa
"Umenichoka kwako eeh??"
"Vero .. huwezi kunielewa sasa hivi ila ipo siku utanishukuru hata kimoyo moyo, mie sipo tayari utoe mimba Vero, mie nipo natamani mtoto wewe umempata unaenda kumtoa embu ongea na Veda mpe nafasi mie naamini huyu ni mwanaume Bora kwako hajawahi kutokea mpe nafasi mbona anakupenda "
"Asante shem..." niligeuka kwa hasira nikamkata jicho Veda et anamwita shem Tinner ushem umeanza lini, Basi Tinner akaondoka Veda akanishika mkono mpaka kwenye chumba kilikuwa cha nje akaingia akafunga mlango, waooh chumba ndani kilikuwa kizuriii yaani duh kinavutia kitanda safiii hata changu cha kawaida tu, chumba akina ma vitu mengii lakini kitamuuuu hatari
Akavuta mlango wa kabati akatoa vipisi vya bange akawasha hapo hata hajaniongelesha kitu nimekaa kitandani namtazama uso wa mbuzii ...
Akaanza kuvuta moshii anavuta kwa pupaa yaani ndani ya dakika 10 alishamaliza vi pisi vitatuuu, ule moshi na ile harufu vilikuwa vinaniumiza sana mie nikaanza kukohoaa nikainuka nikafungue mlango kutoka maana mtu mwenyewe haongei kitu ..
Ile nashika mlango mgumu umefungwa na fungo kwa kiburi nikamgeukia
"Naomba funguo mie niende..." alinikata hilo jichooo weeee akatembea haraka haraka yaani ni sec tu nikashtuka nimekabwa shingo amenibana ukutanii alinikabaa sikuamini anaenda kuniua maana pumzi ziliniisha mwanzo nilikuwa napiga kelele ile unaniumizaa niachee lakini mwili ukaishiwa nguvu hata sauti ikawa haitoki tena
"Unaniuwaa..." kweli kabisa nilianza kuona nakufa kabisa, bahati nzurii mlango ukaanza kupigwa nje kwa nguvu nasikia sauti ya mmama anasema
"Vedastus fungua mlango wewe....Fungua mlangooo unamfanya nini mtoto wa watuuuu" akanisukuma huko nikaangukia kitandani naliaaa kweli Veda alikusudia kuniuwa mie auu, Siamini macho yangu shingo ilikuwa inauma sanaa nakohoa akawa anapiga ngumi za ukuta kwa hasiraaa akanikuta pale pale kitandani akanikunja nguo kifuani kama aniuwe hivii
"Kwaniniii ulitaka kumuua huyo mtoto kwanini wewe unaogopa kufa halafu unataka kuuwa mtoto wangu kwaniniiiii.....Kumbe wewe mwanamke ni mshenziii"
"Veda nisikilize utaniuwa buree, Jamani nisaidieni anataka kuniuwaaaa??" Nikaanza kupiga makelele maana kifo nakiona live hapa aisee ndo mana alisema nisitake kujua upande wake wa pili mwee Nimekoma miee ...
Yule wa mlangoni akazidi kugonga mpaka Veda akaenda kufungua, haamadi nakutana uso kwa uso na mama ake na Veda ye mwenyewe alishtuka kuniona
"Doctor, , kuna nini hapa" Veda akachukua vile vidonge vilikuwa vimeanguka pembeni akampa mama yake huku machozi yanamtoka
"Anataka kumuua mwanangu mamaa, sijui nimemkosea nini huyu mwanamke anashindwa hata kuja kuniambia kuwa ana mwanangu, Mzae basi uniachie lakini usimuue!!!" Veda anavyoongea kwa kunyenyekea kama sio yule kataka kuniua hapa sec chache nyuma, akanifanya hadi moyo uume yaani nimeonekana kama muuwaji hivi
"Mwanao?? Ana mimba?? Yaani ...tangu lini??"
Mama tulijua kumchaganya kabisa,
"Nimekutana na Vero kabla hujakutana nae, tulikuwa na mahusiano yasio Rasm, hakukua kama wewe ni mama yangu mlivyokutana hata mie sikujua kama ni Vero ndio aliekuhudumia " Veda akatoa maelezo tu kidogo
"Mungu wangu, , Faraja gani hii!!! " Mama veda sijui kwanini ila nilimuona kabisa amefurahia hilo jambo
Veda akaondoka bila hata kusema kitu mie tena uso umenishuka shuu aibu yaani maneno ya mwisho ya Veda ilikuwa kama kunisuta nikajutaa bora hata ningekuja kuongea nae maana ameonesha kama vile ana shida sana na mtoto ...
"Mwanangu...kweli una mimba??" Nikatikisa kichwa kukubali ni kweli, yule mama akapiga vigele geleeee akashangilia mweeh nikabaki nimetoa machoo ..
"Kuna kitu kibaya chochote Veda alifanya ndo maana unatoa mimba yake??" Nikatikisa kichwa kukataa yule mama akanishika mikono
"Labda kuna mahali amekukosea, kuna muda mwanangu sio mzuri sanaa lakini nimejitahidi sana kumlea aheshimu wanawake haswa alio nao kwenye mahusiano, kama kuna kitu amekosea naomba kwa niaba yake na mjukuu wangu usimpe hiyo adhabu "
"Mamaa, Veda ana wanawake kibao huko, sioni kama anafaa kuwa babaa wa mwanangu mie sitaki nianze kugombana na mtu kisa mapenzi tukae kulizana "
"Wanawakee?? Veda huyu mwanangu?? Uliwahi kumkuta na wanawake??" Mie tena uso ukanishukaaa sijawahi kumkuta nao ila nahisi anao wengi maana anaenda sana casino ....
Baada ya kuona nimebaki kimyaa akanambia "Sijui hizo tabia ameanza lini mimi namjua mwanangu hana kabisa tabia za kubadili wanawake tunachogombana mie na yeye ni bangi tu na alianza kuvuta baada ya kuachana na mkewe ..." hee nikashtuka mkeweee?? Kwahiyo aliwahi kuwa na mke??
Nikamuuliza huku nimetoa jicho wivu debee, Akanambia "Kwani hajawahi kukuambia?? Veda alikuwa na mke mdada mmoja huko Buza japo imepita miaka mingi karibu miaka 7 tangu kaachana nae "
"Waliachana kwa nini??"
"Sababu inaendana na hii yako, ndo mana Veda amekasirika sana sijawahi kumuona hivii..." mmh nikaguna kwanza
"Alitoa mimba??"
"Ndio..." uwiii niliona aibu nikainama chini uso pwee umenipauka gafla
"Kwanini alitoa labda Veda ndio alikuwa ana shida "
"Veda wangu hajawahi kuwa na shida kabisa, Sijui tu kwanini hana bahati ya kurudishiwa upendo, Veda tangu akiwa mvulana mdogo hajawahi kuwa na tabia za hovyo namjua vizuri mwanangu"
ITAENDELEA...
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni