SASA NAKUPENDA Sehemu ya 21 na 22.
Mwandishi; lissa wa huru media
BASI nikapanda kitandani kwangu. Nikijutia sana nilichokifanya mana mh . Nilikuwa nasababisha ugomvi mkubwa wa wazazi mungu wangu. Yani mama yangu alikuwa anaachwa leo Atanielewa mimi. Niliwaza sana .mpaka kukapambazuka kabisa. Aseeee mama aliamkia chumbani kwangu. Niliogopa sana nikajua na mama anakuja kunipiga. Mama akaningalia sana . Akasema yani wewe mtoto umenizidi mpaka ushetani mama yako. Hivi unaanzaje lakini .unavua nguo mbele ya mwanaume unamsingia mwenzako kakubaka. Eeeeh angekubaka kweli jeeee? Mana si umejipeleka mwenyewe . Mtoto mbona mnafiki sana. Yani mimi pale ata kukuamini sikuwa na uhakika kabisa. Mana baraka ni kijana mzuri . Hana hizi tabia za kipumbavu . Tunamfanyia sisi roho mbaya tu. Kheeee nikashangaa shetani leo kawa malaika mungu wangu. Mama akanmbia nataka ukamuombe msamaha baraka mpumbavu ww unataka kunivunjia na ndoa yako mbwa sana ww. Kisha akayoka chumbani kwangu. Kiukweli ata mimi niliona nimekosea sana .man jana hali ilikuwa mbaya baba alikuwa anamuacha mama. Na baraka uyo uyo ndo kamuombea msamaha mama yangu kwa kumtuliza baba.mana daah nilijua kuyapika ya kuyapika.
Basi mama alipotoka chumbani kwangu . Na mimi nikajivuta nikaingia bafuni nikaoga. Nilipoyoka nikavaa vizuri nimawaza niende nikaongee na baraka sasa sijuh ata nimuangaliajee. Ila nikqjikaza nikaenda mpaka chumbani kwake. Ila sokumkuta baraka. Nikatoka njeee nikamkuta kakaa barazani anaongea na simu. Alaikuwa anaongea na mdogo wake wa kike anayemfuata. Nilisogea nyuma yake .nikasikia anamwambia sikia dada unajua navumilia mengi kwa ajili yenu. Na nyie msiavhe kuvumilia wadogo zangu.nikianza chuo tu. Napanga nawacchukua najua kuna pesa ntakuwa napata za boom. Naomba muwe wavumilivu wadogo zangu sawa. Sikuwa nasikia maongezi ya dada yake .ila nilijisikia vibaya nikajua kuna menhi ambayo wanapiyia yeye na familia yake. Basi alipomaliza kuongea na ndugu yake. Akakata simu . Kisha nikamuona katulia. Basi haraka nikatokea mbele yake . Nilishangaa kuona machozi yanmtoka kwenye macho yake. Aseeeee nilijisikia vibaya sana hii siku. Na aliponiona akafuta haraka machozi yake. Nikamsogelea mpaka alipo. Kisha nikakaa pembeni yke. Nikamwambia pole. Akanyamaza kimya wala hakunijibu.nikajikuta nimemsogelea nikamkumbatia tu. Aseee na yeye akanikumbatia kwa nguvu. Akawa analia maskini. Nahisi alikuwa ana machungu sana . Nikasem basinnyamaza jamani. Hakuwa analia kwa saiti ila zile kwikwi jamani .uwiiiiiiii . Yani kwiki za kutosha na machozi tu yanamshuka. Nikajalibu kumtuliza sana mwisho nikaona kanyamaza. Nikasema kaka baraka nisamehe najua nimekukosea sana na nimekusabababishia matatizo mengi . Nisamwhe kaka siludiii tena . Akaniangalia sana . Akanmbia shakira unamaanisha na uo msamaha wako. Nikasema ndio kaka namaanisha kabisa . Akasema sawa yameisha. Mh mbona kanisamehe haraka hivi .nilizani ata atanifukuza wala. Basi baada ya apo kila mtu akawa kimya sasa. Yani yeye yupo kimya na mimi kimya . Tukaaa pale kwa mda mrefu sana . Tumetulia tu. Mapaka mama akaja sasa aktukuta tumekaa pale.
Mama akawa anajichekesha oooooh jamani mtu na kaka yake mmekaa pamoja . Aya chakura teali mje kula wanangu. Mh niliona mama kabadilika sijuh baba alimpiga mikwara . Basi baraka akasema shangazi mimi kwa sasa sina njaaa nashukuru sana.heeee et mama kaanza kumbembeleza kula. Mh mbona nilibaki kushangaa ila baraka alisema kashiba anaenda kupumzika tu. Basi mimi nikaenda kula .ila baraka aliingia chumbani kwake. Basi mimi nikala niliposhiba nijaenda chumbani kwangu kupumzika. Ila nilimuwaza sana baraka. Niiliona huwenda ata wadogo zake na wao wanapitia magumu. Ndo mana anwaomba wawe wavumilivu jamani.niligisi huruma. Mpaka mtoto wa kiume analia suala dogo. Basi mida ya jioni sana nikaenda chumbani kwa barka. Nikagongaa hodi hii siku . Ila nikaona kimya nikasukuma mlango nikaingia. Mh namkuta kalala kumbe.
Nikamsogelea . Nikamtikisa . Akafumbua macho kisha akakaa .akasema vp shakira. Nikasema pow baraka. Vp upo powa? Akanambia yaa niko powa sema njaa inanuma sana kwa sasa.nikasemangoja nakufatia chakura kaka akasema sawa. Basi kweli nikaenda kumpakulia chakura nikamletea kweli. Akawa anakula uku nipo pembeni yake namuangalia tu. Alipomaliza nikaenda kumfayia na maji .akanambia s asante dada.
Basi alipomaiza kula. Akawa anataka kula tena.nikasema kwani unaumwa jamani? Akasema hapana nataka kupumzika tu. Nikasema sawa kaka na mimi nilale apa pembeni yake. Akasema karibu. Basi nikasogea nikajilaza pale. Lakini hakuna amabae alikuwa kalala. Kila mtu alikua kimya. Basi tukatulia sana pale. Sijuh kwa nn nikajikuta namuangalia sana baraka . Yani sijuh nini kimenikuta nikajikuta nimemsogelea baraka nikambusu mdomoni. Aseeee baraka akastuka mno. Akasema mbona umefanya hivyo. Nikasema kama kaka tu. Baraka akatabadamu kisha akageuka upande wapili . Mh nikaona aibu na mimi nikanyanyuka haraka nikaludi chumbani kwangu uku nacheka .ata sijielewi nini kinanichkesha sasa Mungu wangu. Mh ni nini iki tenaaaa jamani
πΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌπΌ
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni