TIPWA TIPWA NA MR MARVEL SEHEMU YA 9
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Mbali na ivyo zile zawadi alizo tumiwa Noela zilimuuma vile vile. Alihisi Noela hastahili vitu vizuri wala maisha ya kifahari. Alitaka kila kitu kiwe chake, wanaume wote wawe wake. Hata baada ya kumchukua boyfriend wake bado hakuridhika, Ila Iris🙌.
Sasa Salmon alipo pata taarifa, baba wivu ukamkaba vibaya sana Akaamua kwenda hostel kwa Noela ili kujua ni nani aliyemnunulia zawadi.
Alipofika, akaingia chumbani bila kugonga. Noela akashangaa, kumuona kaingia spidi spidi hata salamu hakuna😳.
“Ni nani huyo mwanaume?” Salmon alifoka
“Mwanaume gani?”
“Ni nani aliyekununulia hizo zawadi? Unanisaliti, sivyo?”
Moyo wa Noela ukaenda mbio mbio huku akijua moja kwa moja ni Iris ndie alie mchoma.
“Nauliza huyo mwanaume ni nani Noela sitaki unipande kichwani”🗣️
“Hakuna mwanaume utakua umeelewa vibaya tu” Noela akaanza kujitetea
“Muooongo! Una mwanaume anakuhonga, ndiyo maana siku izi una kiburi hata hunisikilizi”
“Siyo kweli. Sina mtu mwingine zaidi yako Salmon elewa ilo”🥺
Salmon akacheka kwa dharau “Unajua nini? Nachukia waongo na wasaliti kama wewe. Sidhani kama naweza kuendelea na huu uhusiano. Skia, kuanzia now fanya maisha yako na mimi nifanye maisha yangu”
Noela kwanza akabaki kama ameganda
Maana kuachana na Salmon ni kitu ambacho hawezi
“Nini? Unaachana na mimi kwa sababu ya kutoelewana tu? Please usifanye hivyo Salmon……..Nakupenda sana, siwezi kukusaliti niamini…..”😭
Noela akapiga hadi magoti, akamshika miguu yake lakini Salmon hakumsikiliza. Tayari aliamua kuwa uhusiano umeisha na hakutaka mambo mengi.
Alichofanya ni kumsukuma Noela pembeni kisha huyoo akaondoka zake. Naaaaam! Hilo ndilo Iris alilotaka, wao waachane ili yeye awe na Salmon bila kumwogopa Noela.
Basi akajifanya ana huzuni, akamwambia Noela
“Shogaaa poleee, Sikutaka kukuumiza. Nilimwambia tu ili ajue ukweli ila usijali, acha nimuwai niongee nae kabla hajaondoka”
Iris akasimama akavaa slipper zake kisha akatoka mbio mbio akimkimbilia Salmon. Bahati nzuri Salmon hakua amefika mbali kwaiyo alipomfikia alimdaka mkono wake.
“Sasa Kwa nini una hasira?” Iris Akauliza
“Nina hasira kwa sababu ananicheat”😡
Iris akamtazama kwa makini “Sio hasira tu, naona pia una wivu. Salmon, usiniambie unampenda yule kipipa wako??? Lile lijitembo???”😳
“No Simpendi”
“Basi kama humpendi hakuna sababu ya kuwa na hasira. Umeachana naye, now ni nafasi yetu kuwa pamoja na kuonyesha penzi letu bila uoga”
“Bado mapema sana ndo kwanza Nimeachana na Noela dakika chache zilizopita”
“Sasa ilo linanihusu nini mimi??? Unajua nimekuwa nasubiri kwa muda gani hii nafasi? Nimechoka kuwa mchepuko, kufichwa fichwa kama sehemu za siri!……Kwani unaogopa nini kwani??”
“No one! Simuogopi yeyote”
“Vizuri” Iris akamkumbatia kwa nguvu sana akiwa na furaha.
Bhana bhana lile Kumbato lao si likaonwa na Noela. Baada ya kusubiri kwa mda mrefu na kuona Iris anachelewa kurudi nae akaamua kuja kuangalia ndo hapo akawaona jinsi walivyo ng’ang’aniana💔.
Alijiuliza, mbona wakumbatiane namna ile??? Alafu wame relax utadhani sio mara yao ya kwanza!
Sio siri ile kitu ilimchoma hadi kwenye utosi mpaka kijasho chembamba kikawa kinamtoka😰.
Uzuri Hata hakuwafuata kuwauliza kwanini walikua wakikumbatiana vile, alichofanya alirudi chumbani kama kamwagiwa maji ya baridi.
Alikaa kitandani kimya akimsubiri Iris arudi ili amueleze vizuri. Bahati nzuri dakika zile zile Iris akaingia akiwa anatabasamu.
Noela akamuuliza “Unacheka nini?”😡
“Hakuna”
“Umeongea na Salmon?”
Iris akajibu “yes nimeongea naye, lakini inaonekana alikuwa serious na alichosema. Hataki kuwa na wewe tena shosti”
“Kama hataki kuwa na mimi, kwa nini ulimkumbatia vile?”
Ghafla Iris akashtuka na kubadilika palepale. Aligundua kuwa Noela aliwaona Lakini akaamua kukataa.
“Sio kwa nia mbaya! Nilimkumbatia tu kwa sababu alikuwa anaumia na alikuwa na huzuni. Nothing else”😒
“Mtu wa kumkumbatia ni mimi rafiki yako ambae nina maumivu na sio Salmon” Noela alilalamika
“My God Ni kumbato tu madam! Acha kuhisi vibaya khaaa!”
“Unadhani kwa nilicho kiona sitahisi kama kuna kitu kinaendelea kati yenu wawili?”
Iris akacheka “Salmon ni shemeji yangu tu. Na imeniumiza sana kuona unaniwaza hivyo, Noela”
“Kama ungekuwa kwenye nafasi yangu, ungewaza hivyo hivyo”
“Daaaah! Ukweli Umeniumiza sana kuniwazia upuuzi kama huo! Sio kila mwanamke anamtaka bwana ako tena hasa mimi shoga ako!! Yani umenichefua mno kiasi kwamba leo sitalala hapa” Iris akajifanya amekasirika.
“Sasa utaenda kulala wapi??? Sorry Iris! Please Usifanye hivyo”🥺
“Hapana kwakweli umenikera vilivyo! Acha nikalale pengine”
Iris Akafungua kabati akatoa nguo zake mbili akazipanga kwenye pochi, kisha huyoo akaondoka.
Yani hakua amemkasirikia Noela wala nini, alikua anatafuta visababu vya kwenda kulala kwa Salmon maana alijua usiku mzima atakua free kwaiyo aende wakapeane kampani. Mnaona mambo hayo???
Haya…..nakuja………
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni