TIPWA TIPWA NA MR MARVEL SEHEMU YA 10
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Maeneo ya pale pale chuoni, Salmon alikuwa amepanga nyumba kubwa ya peke yake. Wakati akiwa chuo ndo alikua anaishi hapo, ila siku za weekends kama hana mambo mengi ndo anaenda nyumbani kwa baba yake Mr Marvel.
Basi mda huo Salmon alikuwa anakunywa pombe na kumfikiria Noela. Kuna time akawa anajilaumu kwanini amesema waachane lakini sasa kiburi kilikua kinafanya aone alichokifanya ni sawa.
Akiwa bize na pombe mlango ukagongwa. Akatabasamu na kuhisi ni Noela kaja kuomba msamaha ndo maana akaenda kufungua mlango kwa spidi namna ile.
Ila wala hata hakua Noela bali alikua ni Iris! Pale pale mchizi tabasamu lote likayeyuka, akauliza
“Unafanya nini hapa?”😠
Iris akajibu “Nimekuja kulala hapa leo” huku akiingia ndani kwa nguvu pasipo kukaribishwa.
Alienda akajitupa kwenye kochi kama vile yeye ni mama mjengo, kitendo kilicho mkera Salmon
“Una akili kweli Iris??? Vipi kama Noela akipata habari uko hapa? Unajua ni hatari kiasi gani?”😳
“Kwa sasa sijali kuhusu Noela, Kitu pekee ninachojali ni kwamba nakupenda na hii Ni nafasi yetu kuwa pamoja. Nashindwa kuelewa kwanini unapinga?
“No sipingi! Nahitaji muda kupona na kurekebisha mambo”
Iris akamtazama kwa mshangao “Usiniambie unataka kurudiana na yule tembo wako. Salmon, yule msichana Anakusaliti na mwanaume mwingine. Muache aende zake, Mimi nipo hapa kwa ajili yako. Ama Sitoshi?”
“Unatosha ila mimi bado sipo sawa, pia kumbuka hata mimi nina msaliti Noela so sipaswi kukasirika namna hii!”🥺
Iris kabla ya kumjibu akasimama kumfuata Salmon alipokua. Kwa kipindi alichokua nae karibu alijua ni sehemu gani amshike ili jamaa atulie. Na icho ndicho alichofanya! Alimpapasa taratibuu akimwambia
“Najua hauko sawa ndio maana nipo hapa kukufanya ujisikie vizuri. Nakujali baby, alafu pia nime kumiss sio mchezo” akamkonyeza kidogo Kisha akaanza kumbusu shingoni.
Yani Salmon mwenyewe akapagawa na kuanza kutoa ushirikiano. Dakika za kuhesabu akambeba Iris na kuhamia chumbani kwenye uwanja mpana🥱
Upande wa Noela alikuwa bado analia. Kila kitu kwake kilikuwa kinaenda vibaya na yote yalianza kwa Mr. Marvel.
Licha ya yote hayo hakuwa tayari kuachana na Salmon wala kumpoteza mwanaume anayempenda. Baada ya kufikiria kidogo, akaamua aende kwa Salmon ili waongee.
Ila Kabla hajaondoka, simu yake ikaanza kuita. Alipoangalia akaona namba ni ngeni lakini hakuacha kupokea.
“Hello?”
Sauti upande wa pili ikasema “Hi, ni Mr. Marvel. Umeziona zawadi zangu?”
Noela akakasirika “Kwa nini uniletee zawadi? Niliwahi kukuambia ninataka zawadi zako?” 😡
“Nilijiskia kukununulia kitu so nikafanya hivyo. Tatizo liko wapi?”
“Tatizo ni kwamba hatuna uo ukaribu wa kununuliana zawadi. Mimi ni mpenzi wa mwanao na kilicho tokea kule hotelini baina yetu ni bahati mbaya. Na sijui namba zangu umetoa wapi na sitaki kujua ila please Kuwa na heshima!”
“Ninakuheshimu ndio maana nina uvumilivu na wewe Lakini sidhani kama nitaendelea kuvumilia”
“Unamaanisha nini?”😳
“Nataka uwe mwanamke wangu. Nimejaribu sana kukutoa kichwani lakini imeshindikana. Niko tayari kufanya chochote ili uwe wangu Noela! I want you….”
“Ndio maana uliniletea zawadi?? ili Salmon azione na aniache? Now anasema ninamcheat na yote nikwa sababu yako!”😡
Mr. Marvel akatabasamu “Kwa nini aachane na msichana mzuri kama wewe kisa sababu ndogo hivyo?”
“Embu please hili ni jambo serious na sioni sababu ya wewe kutabasamu!….Unafurahia kuvunja uhusiano wangu? Also nimegombana na rafiki yangu kisa wewe wewe!”
“Listen Noela, nilifanya nilichofanya kwa sababu nilitaka. Lakini nikuambie kitu, mwanangu na rafiki yako hawaaminiki. Wanafanya mambo nyuma yako na ukigundua utaumia sana. I promise nitakuwepo kukupunguzia maumivu. Usisahau hilo”
Noela hakuelewa Akauliza “Unamaanisha nini?”
“Good night Noela! Take care” Kisha akakata simu.
Maneno ya Mr. Marvel yalimtisha kidogo Noela, lakini akahisi labda anataka kuzidi kuwagombanisha ivyo akaamua kumpuuza. Alijiandaa vizuri kuelekea nyumbani kwa Salmon.
Huko, Salmon na Iris bado walikuwa chumbani waki enjoy bila wasiwasi wowote. Tena ndo kwanza Iris alikuwa analia kwa sauti kuonyesha mambo yalikua bam bam😰😭.
Sasa Noela alipofika pale akapokelewa na izo sauti za ajabu ajabu. Binti wa watu akaanza kutetemeka huku machozi yakianza kumtoka.
Alipofungua mlango, ulifunguka kwa sababu Salmon alisahau kuufunga na funguo. Yani ukisikia siku ya kufa kwa nyani miti yote huteleza ndo hii sasa.
Basi aliingia sebuleni akakuta kuna nguo zimetapakaa tapakaa chini, na juu ya sofa akaona pochi ya Iris. Acha joto la mwili lisimpande???? Alihisi kuzimia sio kuzimia, kichefu sio kichefu yani tafraniii.
Hakutaka kuamini kwamba msichana anayelia chumbani ni rafiki yake Iris. Noela Alikuwa tayari kumkuta Salmon na mwanamke mwingine yeyote lakini sio Iris maana ingemuuma mpaka kesho🥺.
Ili kujihakikishia kwamba yaliyomo yamo, alienda mpaka chumbani akawaona kitandani tena ni yule yule rafiki yake Iris
Kwa presha akasema “Nini?” Na wote wakashtuka.
Wa kwanza kumsukuma mwenzie ni Salmon ambae
Aliruka futi 50 utadhani sio yeye mzinifu💔.
Ila kwa Iris ilikua tofauti, hakua akijutia kabisa tena Noela alivyo wafuma ilikua jambo jema kwake.
“Noela hapa huna haja hata ya kuumia. Wewe na Salmon si mmeachana tayari?? kwa hiyo sasa ni zamu yangu” alisema Iris
“Nini?” Noela hakuamini alichokua anasikia! Alitegemea ataombwa msamaha lakini haikua ivyo
“Yeees! Ilikuwa inaniumiza kukuona na Salmon wakati mimi nipo kama mchepuko tu! But kwakua mmeachana, imenipa nafasi ya kuwa na Salmon bila kujificha jificha tena”
“Kumbe wewe ndio ulikuwa unacheat na mpenzi wangu?………Kwa nini ufanye hivyo Iris? Wewe ni rafiki yangu tena zaidi ya dada…..why……. Nilikupenda na kukuamini! Tulikuwa tunashare kila kitu ila ukaamua kulala na mpenzi wangu?”😭
Iris akatabasamu “No! No! si kulala tu, Tulikuwa kwenye uhusiano sema tulifanya siri ili usijue”
“Kwa nini ulifanya hivyo?…….ni toka lini…..whyyy???”😭
“Toka Valentines!… na huna haja ya kulaumu coz tunapendana, also Mimi na Salmon tunaendana. Embuuu kwanza Angalia wewe ulivyo! Mnene, tipwa tipwaa, unaonekana kama nguruwe. Ukitembea na Salmon njiani mnaonekana kama mtu na shangazi yake!! Hahahahahhahahahahahahhahah! Kama hukua unajua ndo ujue sasa kuwa Salmon alikua ana kuhurumia tu”
Salmon akadakia akisema “No! Its not true! Noela nakupenda jinsi ulivyo wala sijali kuhusu mwili wako! Just imetokea tu mimi na Iris tumejikuta tupo kwenye mahusiano”
Noela akacheka kwa uchungu “wooooow!!!!! Kumbe ni kweli ulikuwa unadate naye kwa siri? Kwa nini Salmon?……Nilikupenda mno….. kwani Nilikosea wapi mimi?”😭😭😭
“Ilitokea kwa sababu hatukuwahi kufanya mapenzi. Kama mwanaume, sikuweza kujizuia ndio ikatokea” ivyo ndivyo Salmon alijitetea
“Lakini uliniambia utanisubiri mpaka nikiwa tayari. Haya yote yasingetokea kama ungekuja hotelini siku ile ya Valentines. Nilikuwa tayari kukupa mwili wangu but hukuja! Na tangu siku ile hukuwai kuomba tena mapenzi, nikajua huna haraka na icho kitu kumbe una sehemu unapewa for free”
Salmon kusikia vile akashangaa kwa sababu hakuwai kujua kwamba ile siku ya Valentine, Noela alikuwa amemuandalia kitu maalum.
“Noela sikujua kama…..sikujua…..! I am sorry Noela mama nisameee! Please baby……”
“Too late!…..mimi nimenawa mikono sitaki tena chochote kutoka kwako! Si Iris ndo alikua anakupa kichaaa??? Haya huyo hapo baki nae, mimi na wewe tayari tumeshamalizana”
Baada ya kusema hayo Noela akageuka na kuondoka huku Salmon akikimbia kumfuata. Alijua amefanya kosa kubwa sana, na hakuwa tayari kumuacha Noela aondoke akiwa kwenye hali ya kilio kama ile.
Weeeh Iris kuona vile akasema usinitanie unamkimbilia Noela wa nini???? Alimuwahi Salmon akamzuia kwa mbele Akamuuliza “Kwa nini unamkimbilia?”😡
“Pisha nipite Iris Nahitaji kuongea naye”
“Kuongea naye kuhusu nini? Mimi nipo hapa. Ongea na mimi mwanamke wako na sio yeye”
Salmon akamtazama kwa hasira “Ulijua vizuri Noela aliniandalia nini siku ya Valentine, lakini ukaamua kunyamaza na kunitega kwa mitego yako ya kipuuzi”❤️
“Nilifanya nilichopaswa kufanya kwa sababu nakupenda. Kama ungefanya mapenzi na Noela siku ile, mngeanza uhusiano serious na mimi nisingepata nafasi. Ndiyo maana nilitumia nafasi ile kufanya nilicho fanya Na nimefanikiwa”
“Wewe ni mwanamke hatari sana Iris. Najuta kwa yote yaliyotokea kati yetu!” Salmon akaingia ndani taratibu akiwa na huzuni😔
Unajua nini kitatokea baadaye?
Nakuja………
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni