FROM BANGI TO BABY ππ SEHEMU YA 18
Mama akanambia kuwa Veda alikuwa na huyo mke wake walifunga ndoa kabisaa kanisani, wakati huo Veda alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya mturuki alikuwa kama dereva anamuendesha ile kampuni ilifirisiwa na serikali baada ya kuonekana kuna sheria wanavunja, Basi ukawa mwisho wa ile kampuni Wale waturuki wakarudi kwao na Veda akabaki hana kazi, Huo ndio ulikuwa mwanzo wa maisha magumu kwa sababu Veda ndio kichwa cha familia baada ya baba yake kufariki wakiwa wadogo Veda akaamua kuacha shule ili akimbize nyumbani chochote kitu ...
Baada ya maisha kuwa mabaya yule dada ndio akaanza dharau za wazi sasaa sio kwa Mumewe wala mama mkwe anatoka muda anao taka na anarudi muda anao taka Veda akaanza kukimbiza Boda boda mtaani ili tu kupata chochote lakini mwanamke bado hakuridhika na vile visenti mwanzo alikuwa anapata kila anachotaka kwa veda ila sasa mambo yalibadilika ..
Wakati Veda ameacha kazi yeye alikuwa na mimba ya miezi minne mpaka ikafika miezi 7 Veda bado mambo yalikuwa magumu huyo dada akasema yeye hawezi kuzaa mtoto akute maisha ya hivi Bora atoe mimba kwanza, Hii ilikuwa habari ya kushtusha sana kwetu mimba ya miezi 7 atoe mbona ni mtoto kabisa, Tulimuweka sana vikao lakini aliondoka hapa nyumbani kama wiki akasema anakwenda kwao mara moja na alipo rudi hakurudi na mimba aliitoa tayari yaani tuseme aliuwa tu mtoto kabla hajazaliwa ..
Baada ya hapo ulitokea ugomvi mkubwa kati yao na veda akampa talaka yaani kulikuwa na ugomvi sana kwa sababu mwanamke alitaka wagawane haswa hii nyumba maama aliijenga akiwa yupo nae basi aah yaani mambo yalikuwa mengi hili langu sasa ni tukio la pili kuhusu mimba....
Mmmh nikainama chiniii aibuu na huzuni humo humo nikamwambia mama hata sikujua mie niliwahi kumkuta Veda sehem mbaya na rafiki yake alikuwa na wanawake kibao nikajua na yeye ni wale wale ukweli naogopa sana mie kuumizwa mamaa naogopa"
"Hata kama Veda simjui ila swala la wanawake hapana hapana hapanaa hilo nakataa kabisa huyo sio Veda wangu labda kama ulishamshuhudia na wanawake"
Basi tuliongea mengi sana na mama nikabaki hapo mpaka mchana Veda hakuwa amekuja mama akapika tukala alinikatazaa kabisa kupika et kwakua ni mjamzito, yalikuwa masaa tu lakini mama alijua kunidekeza jamani heee hahaha mpaka rahaa ile siku nilii enjoy sana nikajuta hadi kwanini niliwaza kutoa
Mchana ule tupo tunakula pale nje Veda akawa amekuja yaani amekasirika huyooo akatupita hata hajasalimia , Basi mie nikajisikia tu vibayaa nikamtazama mama akanambia nenda kaongeee nae kama utafanya maamuzi ya kuzaa ila kama bado una wazo la kutoa mwachee"
Mmh nikainuka mie Nampenda sana Veda sanaa ila nilikuwa naogopa tu kuanza kusumbuana sumbuana kuviziana aah ndo sitakii, Basi nikaienda humo chumbani kwa Veda
"Veda naomba tuongee..." nilikuwa mpole mikono nimebana tumboni nachezea nguo yangu, alinikata hilo jichoo wee namie nikamkazia macho akachukua Dawa zangu akanipa
"Kama utatoa ni wewe, Nisamehe kukuingilia ila ukiona huyo mtoto anathamani ya kuishi Tafadhali nishirikishe ukimzaa nitamchukua" akanipa dawa zangu hata nguvu ya kuzichukua nilikuwa nayo sasaa
"Veda lak...."
"Tafadhali Vero Ondoka..." daah yaani amenifukuza tena bila hata kunitazama usoni , nikaondoka kwa hasira mpaka kwa Tinner yaani nililiaaa nililiaaaa akanibembeleza mpaka basi akanambia unamtaka Veda nikasema sana tu sivyo nilivyo kuwa namfikiria mwanzo akanambia sasa si amekubali mimbaa?? Nikasema ndio akanambia hayaa chukua, akanipa begi la nguo nikasema la ninii akanambia hamia kwake sasa utamalizaje hasira zake na upo mbali??
Mmh nikasema si ataniuwa jamani huyo kaka chupu chupu aniuwe akasema we nendaa akikuuwa si tutazika bwana embu nenda ...
Tinner bwana yaani mie nipo serious yeye ananiletea utani wa kijinga ..
Akanambia Nenda kamwambia Sina pa kuishi na hili tupo kama hataki kukaa na wewe akuue tu, Nikasema hili nalo mbona bomba nikabeba mbegi wangu huyo mpaka Kwao Ile nafungua tu geti namuona na yeye anafunga mlango wake pale nje hapakuwa na mtu
"Nimekuja kukaa hapa sina pa kwenda..." akabaki ananishangaa
"Unanifungulia niingie au utabaki unanisimamisha hapa "
Akaufungua mlango akasukuma ukawa wazi mie nikaingia, Ila yeye hakuja nikatulia kama dakika nzima haji
"Veda hivi unakuja au mie niondoke??"
"Vero unataka ninii..." et akaingia amekunja sura
"Nitakaa humu ndani nawewe umtunze mwanao nikizaa utachukua mie nitaondoka kama utaenda nae huko kwenye makasino kununua nae wanawake mtajua wenyewe na uhuni wenu" niliongea kwa hasira na wivu humo humo
Nikamuona ametabasam ila hakusema kitu basi mie ndo nikazidi kupata hasira kwanini sasa hata asikatae mfyuu ...
"Sheria ya kwanza humu ndani marufuku kuvuta mi bange yako Veda staki kabisaa, Sheria ya Pili marufuku kuzurula usiku kwenye makasino Sheria ya Tatu unatakiwa kuwa karibu na mwanao na sio mie " afu nikageukia upande mwingine nikalala zangu nimenuna hatari
Akanitazamaaaaa halafu akaondoka hata hajasema kitu, mie sipendi nataka hata anisemeshe tu mmh ..
Basi nikawa nachat na Tinner namwambia ananipa mbinu niwe namchokonoa chokonoa hivyo hivyo hana mbio kwangu, Tinner akanambia Veda anakupenda sanaaa yaani nilipo mwambia una mimba alifurahi mnoo yaani hata sijui nikuelezee vipi hata nilipo mwambia akuwahi unataka kutoa alichanganyikiwa kusikia hilo Kwahiyo tulia Mume unae dada we tambaaa mmh , kweli kimoyo moyo nilimshukuru Tinner maana sasa hivi ningekuwa naugulia tumbo la kutoa mimba ...
Jioni nikatoka hapo mama alipo niona alifurahiii nikamwambia nimekuja kukaa hapa ila Veda ameninunia akanambia mpe Muda ana hasira bado ila atakuwa sawa mpe tu muda maana humu ndani wote haongei na sie zaidi ya Bangi zake tu, nikacheka akanambia mvumilie kama umeamua kuzaa jamani nimependa sanaa asante Vero nikamwambia mama jamani unafanya nijione nina dhambi hivyoo ...
Basi nikapika mwenyewe chakula cha jioni ila ndo kwa kulazimisha kweli maana mama alikuwa hataki et nipumzike na mie nataka kumpikia cha mibange wangu aah nikapika mtoto ufundi wotee nikaumaliz jikoni Ikafika mpaka sa moja na Nusu Veda hajaja ..
Itaendelea....
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni