Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
03 Mar 2026
66 views
VYOTE NDANI GONGA94
Hongera umepata kazi ya kulinda bwawa la samaki usiku huko mkoani Iringa karibu na bonde la mlima Kitonga. Mshahara ni shilingi milioni moja kwa usiku mmoja
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
. Kazi inaanza saa 4 kamili usiku hadi saa 12 alfajiri. Hakuna muda wa majaribio. Ukifika kazini unaanza kazi. Hivyo sikiliza masharti haya kwa makini ili uweze kufika asubuhi. Sharti la kwanza ukifika bwawani pembeni ya bwawa kutakuwa na sinia juu ya kichanja cha mbao ndani yake kuna nyama iliyopikwa vizuri na mchuzi wake. Lazima ule nyama yote na kunywa mchuzi wake. Usiulize
nyama ni ya nini? Ukikataa kula au ukaacha kiasi chochote mwili wako hautaweza kustahimili usiku mzima kwa sababu utachoka mapema. Sharti la pili kuanzia saa tano:30 usiku hutakiwi kusogea karibu na bwawa hata hatua moja. Muda huu maji ya bwawa huwa sio ya kawaida. Yataonekana kuwa meusi sana. Ukikosea na kusogea karibu huwezi kukiona kivuli chako ndani ya maji. Hiyo inamaanisha tayari umeanza kupoteza mwili wako hivyo utapewa mwili wa samaki. Sharti la tatu. Kuanzia saa sita:30 utasikia sauti za
watu wakizungumza kutoka ndani ya bwawa. Usijaribu kusikiliza wala kuelewa wanachokisema. Fumba macho yako na uzibe masikio kwa dakika 10. Ukisikia hata neno moja utajikuta chini ya kina cha bwawa na samaki wenye meno ya binadamu wamekuzunguka huku wakicheka. Sharti la nne, ukihitaji kula samaki unaruhusiwa kuvua. Lakini vua kati ya saa saba hadi saa 8e tu. Vua kadri unavyotaka lakini hutakiwi kabisa kuuza samaki hao au kuwatoa nje ya eneo la bwawa. Ukijaribu kufanya hivyo basi wewe na wote uliowauzia samaki hao mtajikuta
mpo kwenye pango ambalo halijawahi kuwepo duniani. Sharti la tano. Kuanzia saa 8: kamili angalia bwawani kwa makini bila kupepesa macho. Ghafla ukiona kiumbe chochote cha ajabu kisichoeleweka kikijitokeza juu ya maji, chukua mawe yaliyopo pembezoni mwa bwawa na ukirushe kwa nguvu mpaka kitoweke. Samaki wanakiogopa sana hicho na ndio maana uko hapo. Sharti la sita. Saa 9a kamili utaona beseni linaelea katikati ya bwawa. Unatakiwa uingie majini na kuogelea ili kwenda kulitoa. Beseni hilo haliwezi kutoka lenyewe. Ukikataa
kuingia usishangae kuona vyura wenye kucha wakikurukia mgongoni mwako na kubaki hapo bila kutoka hadi asubuhi endapo utafanikiwa kuiona. Sharti la saba. Ukiwa unaogelea, ukihisi mguu wako umeshikwa na kitu kinachofanana na mkono wa binadamu, tulia kabisa. Usipige yowe kutetemeka wala usijaribu kujinasua. Ukifanya hivyo mwanga mkali utamulika bwawani na utakapozima utajikuta mahali ambapo kuna mawimbi makali. Hakuna nchi kavu wala mchana haujawahi kufika. Sharti la mwisho kukubali kazi hii ni lazima. Tangazo hili limekufikia kwa
sababu ulishaomba kazi hii mwenyewe. Najua hukumbuki ni lini. Na hilo sio kosa lako kwa sababu hakuna anayekumbuka. Hii ni kwa sababu baada ya interview kumbukumbu zenu zote tulizifuta. Kazi inaanza leo. Karibu kazini mlinzi wa bwawa letu. Alfajiri ikifika kama bado uko nje ya maji utalipwa.
Maoni
You're not logged in
X
Login
X
signup
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
*AAAAAASH BOSS ENZO* *SEASON TWO* *SEHEMU YA KUMI NA MOJA*
SONGA NAYO. Ila nyie mapenzi konyo Walahi, Yaani ukimuona mtu unayempenda lazima tu Ka moyo kashtuke na kapate amani Fu...
Hongera umepata kazi ya kulinda bwawa la samaki usiku huko mkoani Iringa karibu na bonde la mlima Kitonga. Mshahara ni shilingi milioni moja kwa usiku mmoja
. Kazi inaanza saa 4 kamili usiku hadi saa 12 alfajiri. Hakuna muda wa majaribio. Ukifika kazini unaanza kazi. Hivyo sikiliza masharti haya kwa makini ili uweze kufika asubuhi. Sharti la kwanza ukifika bwawani pembeni ya bwawa kutakuwa na sinia juu ya kichanja cha mbao ndani yake kuna nyama iliyopikwa vizuri na mchuzi wake. Lazima ule nyama yote na kunywa mchuzi wake. Usiulize
nyama ni ya nini? Ukikataa kula au ukaacha kiasi chochote mwili wako hautaweza kustahimili usiku mzima kwa sababu utachoka mapema. Sharti la pili kuanzia saa tano:30 usiku hutakiwi kusogea karibu na bwawa hata hatua moja. Muda huu maji...
👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/hongera-umepata-kazi-ya-kulinda-bwawa-la-samaki-usiku-huko-mkoani-iringa-karibu-na-bonde-la-mlima-ki
Maoni