JAMANI NIPE CHANCE KIDOGO 4--5 Chapter 4 Abisai alimrudisha mpaka nyumbani kwao. *Hakikisha umeingia ndani maana ukitoa tu mguu wako nitajua mtandao wangu ni mkubwa
kuliko unavyofikiria. Leyna alishuka kwenye gari kwa hasira na
kubamiza mlango. "Uwe na usiku mwema kipenzi changu. Alisema
Abisai huku akimuangalia. Leyna alienda kwenye dirisha la chumba chako na kugonga.
"Leyla nifungulie mlango.
"Wewe nae ni msumbufu siungelala hukohuko. Wewe usiendelee kuichanganya akili yangu
hapa nilipo nimesha changanyikiwa vya kutosha.
Leyla alinyanyuka na kwenda kufungua mlango. Leyna alimpiga kikumbo na kuingia ndani.
*Wewe vipi mbona unanipamia, Leyna hakujibu aliendelea kutembea kwenda.
chumbani kwake. Alijikaza kitandani huku akiwa
anafyonza fyonza.
"Wewe una shida gani?
Leyna alinyanyuka akakaa.
*Yani nimepata mwanaume kichefuchefu yanı mpaka najuta kumfahamu.
Leyla akitabasamu
Kwahiyo unataka kuniambia umepata kiboko yako?
Aaaah wapi hawezi kujiendesha hivi yani nitahakikisha namnyoosha, Hanijui vizuri.. Kwani huyo mwanaume ni nani na umemtoa
wapi? "Si tuliokotaba huko club tukaanza kupendana,
mapenzi motomoto dada ananipa kila kitu na ukimuona ni bonge la bwana, ana sifa zote za kuitwa mwanaume lakini ana wivu hatari kila
ninapoenda nae yupo yani utafikiri shetani kila
muda Anisa nipo wapi? Lakini ulikuwa unataka mwanaume.
mwenye pesa na sasa imempata ndugu sasa. vumilia hayo mambo madogo.
Unaongea nini wewe, siwezi kuvumilia ujinga amenikuta na mambo yangu ataniacga na mambo yangu.
Baada ya wiki moja majira ya saa mbili usiku mama Leyna na Leyla wakiwa kijiweni wakiuza samaki na Leyna alikuwa mtaani na mashoga
zake huku wakiwa wamekaa na wanaume.
Ilikuwa ni kitendo cha ghafla sana Abisai alishuka na kumkuta Leyna akiwa na kikosi cha
sigara mdomoni.
Alimsogelea na kumpiga kibao cha shavu mpaka ile sigara ikaanguka chini.
Wale wenzake walitaka kuingilia,
"Wewe vipi inawania na kuanza kupiga watu. Tafadhali kaeni mbali na hili atakaesogea kibao kitamgeukia. yoyote
Jamani huyu ni mpenzi wake mambo ya
wapendanao hatuingilii. Walisomea nyuma na kumuacha Leyna. akipambana na mwanaume wake.
"Ukanipigia kama nani? "Shhhh unapoongea na mimi jaribu kushusha sauti yako.
Wewe ni nani mpaka niongee na wewe kwa heshima, mama yangu mwenyewe simnyenyekel iweje uwe wewe?
Maneno ya Leyna yalimaanisha hasira Abisai Alimshika mkono na kuondoka nae. Alienda kumkabidhi kwa vijana wawili waliokuwa
wameshiba kwa mazoezi. "Hashim, Yusuph huyu ni shemeji yenu, mpenzi
wangu mimi mke wangu mtarajiwa. Sasa bro mbona shem amekasirika hivyo na
hana viatu? Tulia Yusuph bado sijamaliza utambulisho..
Abisai alimgeukia Leyna Mpenzi, lazizi wangu, mama wa wanangu.
Leyna aliweka midomo yake pembeni, Abisai akaendelea kutambulisha.
"Hawa ni wadogo zangu. Ni wanajeshi wamemaliza mafunzo yao jeshini na sasa ni
waajiriwa Sasa mimi unanisaidia nini? Alijibu Leyna kwa
dharau.
Yusuph, Hashim naombeni mumfunze adabu shemeji yenu ili ajue jinsi ya kuniheshimu..
*Aaaah bro...
Mmegoma nifanye mwenyewe?
Hapana tutafanya.
"Haya kazi kwenu
Usiku ule ule Leyna akaamuliwa akimbie kuzunguka eneo la uwanja wa nyumba.
Siwezi kukimbia na sifanyi adhabu yoyo.....
Kabla hajamaliza kuongea kibao kizito kilishuka
shavuni kwake mpaka akahisi wenge. "Nyanyuka haraka na uanze kukimbia.
Leyna hakuwa na chagua alianza kukimbia akarushwa kichura, kupiga pushapu na
kurukaruka. Leyna alikuwa amechoka sana.
Jamani nisameheni sirudii tena.
Mbona ndio kwanza tunaanza bado kidogo shemeji maliza kupiga pushapu 20.
Siwezi
"Wewe usitutanie.
Leyna alipiga push up huku akiwa analia jasho na machozi vilichanganyikana. Alipomaliza
alilala hapohapo chini.
Shemeji kipenzi bado kidogo nyanyuka. umalizie kukaa hewani. "Sasa nakaaje hewani.
"Hashim muenyeshe shemeji yetu kipenzi. Hashim alimuonyeshea mfano alipanda hewani kama vile amekaa kwenye kiti.
Leyna alifanya mara moja na kuanguka wakimuamuru arudie tena lakini baada ya muda miguu ilitetemeka na kuanguka chini.
"Nyanyuka haraka...
*Basi inatosha kwa leo.
Alisema Abisai huku akinyanyuka kwenye kiti na kwenda kumnyanyua. Alimbeba juu na kuingia naye ndani.
Wakati huo taarifa zilifikia mama Leyna na Leyla. Yani kapigwa kibao na kusombwa kama
mtuhumiwa.
Jamani sasa huyo mwanaume ni nani na kumpeleka wapi? Mama Leyna alionekana kuwa na hofu.
Mama huyo ni mwanaume wake acha kujipandisha presha.
"Huyo mwanaume unamjua?
*Hapana
Daaaah huyu mtoto atakuja kunisabanishia kifo cha ghafla. "Mama tulia atarudi.
Japokuwa Leyna alikuwa akimsimbua mama.
yake lakini alikuwa na wasiwasi juu ya usalama wake sababu mzazi ni mzazi tu
Abisai alipompelekea ndani akamjalisha. kitandani
"Pole kwa mazoezi mke wangu. Aliyoambiwa hivyo Leyna alikuwa kwa hasira.
"Basi mpenzi wangu.
Toka hapa nakuchukia Abisal.
Mimi nakupenda mpenzi wangu sasa ngoja
nikupeleke bafuni ukaoge ilinipate nguvu. Alimchukua tena na kumpeleka bafuni, Leyna
alioga alipomaliza akatoka na kukuta Abisai akiwa anamuangalia abaya zuri tena la bei ghari. Utavaa hii mpenzi alafu utakuja tupate chakula.
pamoja.
Leyna hakuwa mbishi alivaa nguo akiyoandaliwa. na kujitanua vizuri kisha taratibu akitembea huku miguu yake ikiwa inakosa nguvu.
Alifika sebleni akamkuta Abisai akiwa na ndugu
zake wanakula. Shemeji njoo tuungane pamoja, njoo tule. shemeji
Hashim na Yusuph walimchangamkia na. kumuonyesha kumjali wakati huo yeye aliwaona kama mashetani wawili wenye mapembe.
Chapter 5
LEYNA alibaki amesimama akiwaangalia na wao walitolea macho.
"Hapana nataka kwenda nyumbani tu.
Shem chakula lazima kiheshimiwe na kama
hesabu yako ipo hapa ni lazima ule. Aliongea Yusuph huku akiwa kamkazia macho, Leyna alimkata jicho Abisai ambae alikuwa
akimuangalia huku akiendelea kutafuna chakula. Aliona usiwe tabu asije akazua mengine, taratibu alisogea mpaka mezani na kutaka kukaa kwenye
kiti kilichojitenga.
Mmmm mke wangu mpenzi sehemu yako hii hapa, tangia lini umeanza kukaa mbali na mimi? Leyna alisogea taratibu na kukaa karibu na
Abisai
Abisai alichukua sahani ya Leyna na kumpa kulia chakula kisha akachukua kijiko akachoka chakula na kupeleka mdomoni kwa Leyna. Leyna
alikwepesha mdomo wake lakini alipoangalia sura za mashemeji ilimbidi afungue tu mdomo
wake na kila kile chakula. Safi sana huyu ndie mwanamke wangu ninae mtaka.
"Mashaallah mwanamke wako mzuri sana kaka Mungu awabarikie mpate kufunga ndoa.
"Amiin.
Maneno wallyokuwa wakiongea yalikuwa yakimchefua Leyna alichokuwa anataka ni kuondoka tu ile sehemu. Alikula kwa kujilazimisha
akanyanyuka na kutaka kuondoka, "Huagi shem? Leyna aliwakata jicho mashemeji zake kisha akatoka bila kuongea neno Abisal akiwaonyesha alama ya dola ndugu zake kisha
alipomaliza
akamfuata Leyna.
Walipanda kwenye gari huku Leyna akiwa kanuna
"Ukinunua hata haupendezi. Leyna alimkata jicho na kusema
"Abisai sitaki kuongea na wewe na leo hii ndio mwisho wa mimi na wewe huwezi kunitesa kiasi hiki kisa wivu wako wa kimapenzi. Yani kikiendelea kuwa na wewe najlona kabisa kifo changu kipo mikononi mwako.
"Kuachana mimi na wewe ni uwongo mpenzi na wala siwezi kukuzwa ila ukitaka uone mapenzi yangu basi fanya kile ninachotaka mimi.
"Huo ni unyanyasaji bwana.
Kwa haraka utaona hivyo lakini mimi nina mapenzi ya dhati kwako, nakupenda sana Leyna
na lengo langu ni kufunga ndoa na wewe. "Nani? Nani aolewe na wewe kwanza ukoo wenu sijul familia yenu mnaroho mbaya sana,
sithubutu kuingia kwenye familia ya makatili. Abisai hakuwa na hasira alijua anaongea vile sababu ya hasira tu.
Ilikuwa majira ya saa sita na nusu usiku walifika nyumba kwakina Leyna Leyna mpenzi kumbuka kuwa haya
ninayofanyia ni kwa faida yako na kama nitakuwa nimekukosea basi naomba unisamehe. Akiongea Abisai kwa upole huku akiwa kaushikilia mkono wa Leyna.
Leyna aliitoa mkono wake kisha akafungua mlango, akashuka kwenye gari na kuingia ndani kwao.
Wakati huo mama na Leyla walikuwa sebleni wakimsubiri, mama yake alikuwa na wasiwasi
sana.
"Sijui kama mwanangu yupo salama.
"Mama atarudi tu kwani haujamzoea mwanao anaenda kuranda huko na anarudi usiku wa manane?
Sio kwa staili hii ya sasa ya kuchukuliwa na kipigo.
"Kwani mara ngapi anapigana huko. Mmmh Leyla ya safari hii unanitisha mno.
Wakiwa bado wanaongea mara mlango uligongwa
"Leyla nenda haraka kafungue. Alisema mama yao haraka baada ya kusikia mlango unagongwa.
Leyla alienda kufungua mlango huku mama yao macho yakiwa mlangoni.
Aliingia Leyna huku akiwa anachechemea. "Leyna mwana ulikuwa wapi?
Wakati huo Leyla alishindwa kujizuia akajikuta anacheka. Leyna alimkata jicho na mama yake.
akauliza "Na wewe unacheka nini? "Mama huyu ndio ilikuwa na wasiwasi nae, ina
sasa amerudi na abaya kama vile katika kwenye sherehe au mwenzetu ukienda kuolewa ndoa ya
mkeka?
Leyna hakujibu alienda kukaa kwenye kochi huku alihisi maumivu ya miguu, alivua abaya na
mitandio akarushwa kule.. "Wewe ilikotoka ni kwema?
Mama huyu mwanaume king'ang'anizi niliempata najuta kumfahamu sio wakunifanyia hivi na ndugu zake.
Mama alishituka akajua mtoto wake kabakwa. "Amekufa ya nini?
Wamenifundisha mazoezi ya kijeshi.
nimepigiwa sauti, vichura mama pamoja na
pushapu yani hapa nilipo sina hali.
Mmmmh unelitafuta umekipata, kongole zimfikie huyo baba Mama yao alinyanyuka akaenda kulala.
"Unajua mama alikuwa na wasiwasi na presha yake imepanda ujue
Bora atakunywa dawa itashuka ila haya maumivu ya mwili wangu ni kama vile uchukue maji ya moto unisaidie kunikanda. Usiku huu mwenzangu uongo wewe nenda Kameze panado ukalale..
Usiku kucha Leyna alikuwa akiugulia maumivu ya mwili Kesho yake kutwa nzima alikuwa ndani hakuweza hata kutoka nje ya geti. Abisal alikuwa akituma msg hazikujibiwa, alipiga simu hazikupokelewa
Ilipofika Mida ya saa sita mchana Leyla alikuwa akiandaa samaki mara alisikia geti likigongwa..
"Leyla kafungue geti labda wateja wa samaki hao. Leyla alinyanyuka na kwenda kufungua geti alikutana na kijana aliekuwa kwenye pikipiki. Habari
Salama "Samahani naweza kuonana na Leyna?
Leyna yupo lakini haltaweza kuonana nae sababu hayupo sawa anaumwa. "Wewe ni nani yake?
Dada yake.
Basi sawa nina mzogo wake hapa natumai utamfikia.
"Usijali utamfikia..
Ilikuwa mifuko mitatu mikubwa ilikuwa imejaa
vitu. "Kwanza hii mizigo imetoka wapi?
Kwa boss Abisai mwenyewe ataelewa. "Sawa. wewe mwambie hivyo
Leyla alibeba ile mizigo mmoja akamuacha maana ilikuwa mizito.
Mama yake alipomuona akauliza.
*Huyo mitmzogo inatoka wapi?
Niya Leyna mama, tena kuna mwingine nimeuacha huko.
Huko chumbani Leyna akiwa anaperuzi mtandaoni mara simu yake iliita iliyokuwa Inapiga ni namba mpya, Leyna alipokea.
hallow.
"Vipi mapenzi wangu unaendeleaje? "Abisai niache bado nina hasira za jana.
Najua mama ila hayo yote yataisha baada ya kuona nilichokutumia hapo nyumbani kwenu. "Umetuma niniChapter 6
Leyna alipofika nje akakuta mifukoni imesheheni bidhaa.
*Hivi ni vitu vyangu.
Ndio vimetoka kwa.....
Abisai
Ndio huyo huyo.
Leyla nipe kiti maana siwezi kukaa chini.
Leyla alisogeza kitu leyna akakaa na kuanza kukagua vitu.
Mfuko mmoja ulikuwa na nguo, viatu, pochi na vito vya thamani.
Mwenyewe alimuangalia vile vitu huku akitabasamu.
Kwa hapa kaniweza, hivi ndio viti vyangu sasa.
Mfuko wa pili na watatu ulikuwa na vitu vya kula pamoja na nyama kwaajili ya kunywa supu.
Haya ni mambo ya jikoni Leyla peleka kule.
Katika kuangalia mara ikadondika bahasha
ambayo ilikuwa umetuma.
Mama naomba unipe hiyo bahasha.
Huyu ndio mwanaume alie iutangldika jana.
Ndio huyu huyu na ndugu zake.
Kumbe mnajuana mambo yenu, sasa kwanini
usimlete nyumbani nikawafungisha ndoa. Nani wa kuolewa na yule mwanaume?
Wewe.
Aaaah wapi siwezi kuishi na mwanaume mwenye masharti na wivu.
Leyna alifungua ile bahasha akakuta kuna pesa alipiga kelele za furaha kisha akatoa zile pesa na kuwaacha mdomo wazi Leyla na mama yake.
Sasa ukisikia Abisai ndio huyu, mwanaume na
nusu, mwanaume mwenye pesa sio vijisenti. Mmmmmh Mama yao aliishia kuguna hakuwa na neno la kuongea.
Leyla shika hizi hela leo pia pilau tamu lenye nyama za kutosha alafu friji lijae vinywaji leo ni siku yenu.
'unapenda sana hela nakwambia nitakuja kukuzula kwasababu ya hizo pesa.
Mama pesa ndio kila kitu. Wewe mwenyewe nikikupa utachukua.
Mfyuuuuuu, yani mimi nakala ndani roho juu nawaza mwanangu kapatwa na nini kumbe unapendekeza ujinga tu. Yani wewe ni bora ungeenda kukaa kwa baba yako mdogo Mama yao alifyonza kisha akanyanyuka na kuingia ndani.
Baada ya siku mbili tatu kupita Leyna akipata nafuu akaanza kutoka mitaani. Abisai alikuwa akikutana nae na kwenda nae sehemu za starehe kisha alimrudisha nyumbani. Hivyo ndivyo alivyokuwa akitaka Abisai yani alipo Leyna nae awepo pembeni yake.
Siku moja Abisai alimtunia pesa na kumtaka akafanye shopping ili jioni amsindikize kwenye harusi ya rafiki yake.
Leyna alienda dukani kufanya manunuzi ya nguo jioni nilipofika leyn akijiandaa na kuvalia nguo yake. Ilikuwa gauni iliyoachwa mgongo wazi na maeneo ya kifuani palikuwa wazi kidogo, ilishika kiuno huku chini iliachia lakini ilikuwa na mpasuko mrefu mpaka sehemu ya paja. Jioni Abisai alifika kwaajili ya kumchukua
alimuangalia tangia alipotoka getini mpaka alipofika kwenye gari. Alipanda kwenye gari na ile mpasuko ukajiachia sehemu ya paja ikawa wazi.
"Vipi baby nimependeza ?
Umependeza kiasi ila ingependeza sana kama ungeziba mgongo kifua na huo mpasuo ungeziba, sijapendezwa na hiyo nguo.
Jamani Abisai hivi kwanini hatujawahi kuendana hata siku moja yani wewe ni mwanaume inaonekana Mjanja sana lakini unamambo ya kizee.
Sawa kufananishwa na kitu chochote unachotaka ila kwenye mali zangu huwa sitaki kabisa watu wengine wazione.
Ulitaka nivae baibui au abaya?
Hata kama isingekuwa hayo mavazi lakini ingekuwa nguo ya kiziba hizo sehemu nyeti. Basi sawa iwe kwa leo tu.
Abisai alikubali wakaondoka na kuelekea kwenye ukumbi wa sherehe.
Walifika na kuingia pamoja huku wakiwa wameshikana wakionekana kama watu
walipoenda na sana. Walifika kwenye meza wakaungana na wenzao
wengine.
Shuhuri iliendelea huku watu wakinywa na kula. Kwenye meza waliyokuwa wamekaa kulikuwa kuna mwanaume alikuwa anamuangalia sana
Leyna, Abisai alimuona yule mwanaume taratibu alisimama akavua kiti lake na kumvakisha Leyna.
*Vipi baby? Leyna aliuliza kwa sauti ya chini. Tulia naona wadhenzi wameshaanza
kukutokea macho. Asante baby, sasa unanisikia nilikuwa nahisi
baridi.
Leyna alizuga kwa kusema hivyo ili watu wasije wanaelewa vibaya.
Licha ya kufanya hivyo lakini bado yule mwanaume aliendelea kumuangalia na safari hii Abisai alishuhudia mwanamke wake akiwa snakonyezwa. Aliporudisha macho yake kwa
Leyna, Leyna aliangalia pembeni Abisai alisimama. na kumuangalia yule mwanaume.
Haina aibu, imeumbwa hauna haya wewe? Umekuja na mwanamke wako lakini macho kodi kwa wanawake wa wenzako. Kaka jiangalie sana
watu tunagharamia.
Bro mbona kama sikuelewi? Alijitetea yule mwanaume.
Chunga sana kijana. Abisai aliendelea kumuonya.
Jamani baby hivi kwanini unapenda kuniaminisha mbele za watu? Aliongea Leyna Wewe nyanyuka tuondoke.
*Lakini....
Hakuna lakini simama. Abisai alisogea karibu na Leyna akamshika mkono na kutoka nje ya ukumbi huku sherehe ya harusi ilikuwa inaendelea.
Full 1000
0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni