Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
28 Dec 2025
15 views
VYOTE NDANI GONGA94
JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) NA UKOMBOZI WA COMOROS 2008.
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Machi 25, 2008 itasalia na kumbukumbu kubwa kwa nchi moja wapo ndogo katika bahari ya Hindi ya kutambulika kama Comoros, oparesheni maalum ya Kijeshi ya kumchomoa Kanali Mohamed Bacar aliyejitangazia mamlaka ya kisiwa cha Anjouan.
Jioni moja kabla ya Machi 25, kuta za Mamlaka ndani ya Umoja wa Afrika pale Addis Ababa zilijadili nini kifanyike huko Comoros baada ya mazungumzo ya muda mrefu, bunduki huwa ni option ya mwisho Afrika endapo mazungumzo yatashindikana.
Mwenyekiti wa Umoja Afrika wakati ule alikuwa Luteni Kanali wa JWTZ ambaye ndie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete baada ya mazungumzo ya mdomo kushindikana ikasukwa ramani na Comoros sasa ivamiwe kijeshi chini ya Mwamvuli wa AU.
Dr Hussein Ali Mwinyi kipindi hicho ni Mbunge wa Mkuranga, Pwani ndie alikuwa Waziri wa Ulinzi na JKT, alipokea simu ya upepo kutoka Ikulu ya Magogoni kwa kikao cha haraka kabisa sambamba pia Mkuu wa Majeshi, Mnyakyusa Jenerali Davis Mwamnyange, escort na ving’ora kwa ajili ya emergency gathering.
Makubaliano baada ya kuisoma Comoros vizuri kwanza Mission ile ilipewa code name “Operation Democracy in Comoros” hapo Umoja wa Afrika ukiwa umebariki, nchi kama Tanzania, Sudan na Senegal kutoa vikosi vyao kuelekea Mashariki mwa Bahari ya Hindi wapatao Askari 1,500.
Simu ya upepo ilisikika ikiita Makao Makuu ya JWTZ eneo moja tulivu Jijini Dar Es Salaam ambapo walitakiwa kuandaliwa Wanajeshi wapatao 750 tayari kwa ajili ya kuelekea kwenye Mission ya kuweka heshima, nakala kwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ yes Chief of Staff Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, maelekezo yote yakapokelewa.
Machi ilikuwa ya kawaida Tanzania ila kwenye ulimwengu wa Medani ulikuwa Mwezi busy sana, wakati kikosi kipo tayari Comoros ilipaswa kushambuliwa kutoka maeneo matatu muhimu nayo ni Bandarini, Uwanja wa Ndege na eneo la kulinda raia, haikuwa rahisi maana wanayepambana nae ni Mwanajeshi pia ana uelewa wa kivita.
Route ngumu ya Bandari na hatarishi wakapewa JWTZ, kikosi chetu kiliongozwa na Meja Jenerali Daniel Igoti akisaidiwa na Luteni Kanali Shaban Lissu.
ITAENDELEA.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
Waarusha ni kabila la watu linalopatikana kaskazini mwa Tanzania katika eneo la mlima Meru, Mkoa wa Arusha
. Lugha yao ni Kiarusha inayohesabiwa kama lahaja ya Kimaasai[1]. Wakati wa kuja kwa wakoloni hao walikuwa wakazi wa ene...
JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) NA UKOMBOZI WA COMOROS 2008.
Machi 25, 2008 itasalia na kumbukumbu kubwa kwa nchi moja wapo ndogo katika bahari ya Hindi ya kutambulika kama Comoros, oparesheni maalum ya Kijeshi ya kumchomoa Kanali Mohamed Bacar aliyejitangazia mamlaka ya kisiwa cha Anjouan.
Jioni moja kabla ya Machi 25, kuta za Mamlaka ndani ya Umoja wa Afrika pale Addis Ababa zilijadili nini kifanyike huko Comoros baada ya mazungumzo ya muda mrefu, bunduki huwa ni option ya mwisho Afrika endapo mazungumzo yatashindikana.
Mwenyekiti wa Umoja Afrika wakati ule alikuwa Luteni Kanali wa JWTZ ambaye ndie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete baada ya mazungumzo ya...
👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/jeshi-la-wananchi-wa-tanzania-jwtz-na-ukombozi-wa-comoros-2008