Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo

*KOMANDO NIOE NTAKUWEZA TU* *1-5* *__________________________________________*  *SEHEMU YA KWANZA*  "Weee Maa yaani kila mtu ameamka kuchota maji ni wewe unajifungia ndani tu kwamba utaoga na kufulia mate yako"
Gonga94 · Stories

*KOMANDO NIOE NTAKUWEZA TU* *1-5* *__________________________________________* *SEHEMU YA KWANZA* "Weee Maa yaani kila mtu ameamka kuchota maji ni wewe unajifungia ndani tu kwamba utaoga na kufulia mate yako"

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.


"Jamani mimi bado nna usingizi, nichotee bhasi undugu wangu"
"Wewe ushanigeuza mimi kikaragos chako au umenioa kila siku nikuchotee tu maji nakwambiaje amka tukachote maji, mimi sikuchotei hata tone moja"
rafiki angu Jemma alikazana nitoke nje niende bombani nikachote maji, mtaa tuliohamia ulikua na tabu ya maji, maji hutoka baada ya siku tatu, kwahiyo ili uwe na akiba ya kutosha ilibidi kuchota maji mengi na kuyaweka ndani, ilibidi niamke tu.

Ilibidi nivae nilikusanya ndoo za maji, nilipita nyumba kadhaa kwani bomba la maji lilikua huko, nilipofika niliweka foleni kulikua na watu wengi ambao wengi wao walikua wamama, niliwajua wamama wa mtaa huyo ni wambea sana hivyo sikutaka kukaa nao karibu nikaenda kukaa kibaraza flani kilikua nyumba nyingine, nilikaa hapo nikibonyeza bonyeza simu yangu.

"Hello mambo?" Kijana mmoja ambae alitokea huko aliponiona mimi nimekaa, akaamua kunifuata, nikajua kumekucha kweli kweli.

"Poa za wewe?" niliitikia huku nikimtazama huyo kaka alienisalimia.
"Fureshi naitwa Twalib sijui unaitwa nani?"
"Manka hapa" nilimjibu.
"Jina limekaa kipesa pesa tu hata mwonekano wako unasadifu yaliyomo"
"Hahaha punguza fix bro"
"Yaah true nakwambia kwani huko kwenu huwa hawakuiti bosslady maana mwonekano wako mmmh ni mikosho kinouma"
"Wacha weee" niliona Twalib anatoa sifa nyingi ambazo sikua naendana nazo hata kidogo eti mimi bosslady wapi na wapi hahahaha nilijikuta nacheka tu.

"Nimependa kuona ukitabasamu, naomba unirekodi hapa nipate video za ukumbusho"
Nilimkubalia Twalib alitoa simu yake macho matatu, aliweka kwenye camera na kuchagua filter nzuri nikajisemea ila wanaume wa dar kwa kupenda filter nikajua hizo zote atataka kutamba nazo huko tiktok.

Bila kutia neno nikaanza kumrekodi hiyo ongea yake ya kimapozi sasa ilikua inaniacha hoi, nikajikaza kucheka sana ili nisiharibu mambo, nikasema huo ubuyu wote nitampa Jemma ili tucheke kwa pamoja maana kaka alikua na mapozi kunizidi hata mimi mwanamke.

Nilimrekodi video kama tatu na zote anaramba lips baada ya kumaliza alinijia na kunipa chocolate, nikaguna na kuipokea.
"Nilijua nikipita njia hii, lazima nitakutana na mrembo kama wewe nikaona si vibaya kubeba chochote kitu cha kukufurahisha"
"Sawa nashukuru" tuliendelea kuongea mambo mengi ambayo yalikua ya kufurahisha maana Twalib alikua mcheshi kweli, aliniomba namba ya simu nami nikampatia kwani sikuona kama kuna ugumu wowote wa kumnyima mtu namba, kuona wepesi wa kupata namba si akaanza kunitongoza.

"Unajua siku ya leo kitu kizuri ambacho kimepita mbele ya macho yangu ni uzuri wako. Udongo uliokuumba wewe ulikua na utofauti sana pia muumbaji alipata utulivu wa kina kulikata kata umbo lako katika usahihi wa namna yake yaani kila kimoja kimepangiliwa vizuri mahali pake, sitaki kukufuru ila sioni ulichoninywa labda tumshukuru aliekuumba kwa kukupendelea, mimi nimekupenda, si ajabu moyo kupenda mara ya kwanza unapomwona mtu maana hata adamu alimpenda Hawa siku ya kwanza kumwona katika upendo huo huo nami nimekuzimikia mazima, haijalishi jimbo lako likoje ila ni furaha yangu kupata kivuli na utulivu kwako unasemaje mama angu" Twalib alishusha swaga zake pale na kunitazama usoni nami bila woga nilimtazama ajabu macho yake yalikua kama yamelegea hivi yaani ananitongoza mpaka macho yake yamelegea nilianza kucheka sio kwasababu aliongea vibaya hapana ila nimezoea tu mtu akiwa ananitongoza huwa nashindwa kukaza hujikuta katika hali ya kucheka sana nadhani ndo ambapo huwa naitafuta confidence yangu hivyo kama mwanaume atakua na moyo legelege ule wa kuwahi kukasirika unaweza jikuta unakata tamaa na kukimbia kwa kuniona labda nna dharau sana.


"Mbona unanicheka yaani mnyamwezi kukusifia kote huko na bado unanicheka wee manzi umenichukuliaje kwani?" Twalib akaanza kupandisha hivi hasira hakujua kwamba mimi ndo nilivyo.
"Hahaha subiri kwanza nakusikiliza bado, wewe endelea tu" nilimtuliza kwanza sasa mtu unanitongoza sijakupa jibu ndo unawahi kudhira ndo nini hiyo.

"Ooh bhasi sana mrembo naendekea, Kama nilivyo kwambia mimi nataka kuishi nawewe nitakuzingatia kwa mambo mengi, vizawadi, pesa, kutoka kwenda maeneo mazuri, tutakwenda vacation ndani na nje ya nchi, yaani mambo matam matam yote ambayo mdada mrembo kama wewe unayastahii mimi nitapita nayo na kutisha kabisa" Twalib aliongea mambo mengi ambayo kwa asilimia kubwa nilijua ni uongo kutokana na mwonekano wake, sikuona kama anayo hiyo pesa ya kunipeleka nje ya nchi, nilimweka kwenye kundi la kunihadaa tu, sawasawa na wale wanaume ambao hutumia magari ya watu ya kuazima anahakikisha anampata mdada kwa ahadi za uongo akishakula na kupata vitu vyake vyote anakimbia na wakati huo labda anakuacha na mimba kabisa.

Wakati namtafakari nikaona watu wanaanza kukimbia kwa kasi mara si nikaona mbwa kichaa anakimbiza watu waliokua bombani, kumtazama Twalib aliesema atanilinda kwa upendo hee hayupo ameshanikimbia ila nyie wanadamu, mimi kuanza kukimbia hatua ya kwanza ya tatu nikajikuta niko chini, nimejikwaa vibaya na kuanguka, nikawa napata wakati mgumu kusimama mguu wangu wa kulia ulikua na maumivu makali, kutazama namwona mbwa kichaa anakuja upande wangu.

"Mamaaaaa nakufa mimi, nakufa mwenzenu msaadaaaaa" nilipiga kelele kuomba msaada kwani mbwa kichaa alikua karibu kunirarua na meno yake makali, nilikua naogopa hata nguvu za kusimama nilikosa.


Itaendelea.......

EP 2.

Mbwa kabla ya kunifikia alipigwa rungu la kichwa.
"Wuuuu wuuuuuuuuh" alibweka huku anazunguka zunguka, alitokea mwanaume mmoja akiwa kwenye mavazi ya jeshi ndie aliempiga mbwa kichaa na rungu la kichwa, mbwa alipotaka kumvamia alichezea marungu ya kutosha mpaka akakimbia kuyaokoa maisha yake, hapo nilipata ahueni kidogo kwani nilijiona niko salama, nilimshukuru Mungu pia nilimshukuru huyo mwanajeshi.
"Ahsante sana kaka angu kwani umeniokoa Mungu akubariki sana"

"Niite komando, unaweza kwenda kwako, huyu mbwa ameshaondoka hapa" Komando alitoa sauti ya mamlaka nami niliipata vyema, nilitamani kukimbia ila nisingeweza kwakua mguu wangu bado ulikua unapata shida kwa maumivu hivyo nilikimbia kwa mguu mmoja huku nikiruka ruka juu.
"Simamaaa" sauti ya amri ilisikika tena nyuma yangu, mamaaa nimeisha mie yaani mjeda anataka nisimame ningekua na uzima wangu wala nisingesimama ningekimbia zangu ila kwakua nilikua na maumivu ya mguu ikabidi nisimame huku natetemeka jamani hawa wajeda ukutane nao kawaida tu huwa balaa mtu unawaogopa, sijui lini nitakua na ujasiri wa kutowaogopa mimi.

Nilisimama bila kugeuka nyuma kumuangalia hiyo nguvu ningetoa wapi mimi.

"Unakaa wapi?"
"Ha hapo mbele" nilijibu huku nikiendelea kutetemeka huyo komando mwenyewe nilikua sijamwona sura kabisa ni sauti ya amri amri tu ndio nilikua naisikia, sijui kwanini aliuficha uso wake kwa kitambaa na kichwani kavalia kofia.

Mbali na ukali wa sauti yake angalau kuna jambo lilinipa faraja ni namna mikono yake imara ilivyokua imenibeba sikuona dalili ya kuniangusha kitu kingine alichokua nacho komando ni kwamba alikua ananukia vizuri, hiyo perfume yake ilikua inaziburudisha pua zangu, watu waliokua vichochoroni wakichungulia walishangazwa kila walipokua wanatuona mimi na komando tunakuja, nilimwonesha nyumba yangu tulipofika mlangoni nilifungua mlango nikajua anaishia hapo si akanibeba tena na kuniweka kwenye kochi hapo sebleni.

"Una dawa ya kuchua?"
"Ndi ndio mezani pale" nilimjibu alikwenda kuchukua hiyo dawa na kurejea, alinipandisha traki juu bahati nzuri traki ilikua bwanga hivyo alipandisha mpaka mapajani, nilichoombea asiyatamani mapaja yangu maana ni meupe na mazuri, mwanaume akiwa na tamaa anaweza kudata nayo na kutamani yatomasa zaidi na nilijua jambo hilo haliwezi kuishia hapo kwani atataka kunila kabisa, nikawaza huyu komando akitaka kunifanya vibaya nitamkatalia kweli, maana alikua na nguvu kunizidi yaani niliona kwa mazingira nisingeweza kuchomoka kabisa.

Kumbe komando wawatu hakua na hata hayo mawazo alianza kuninyoosha mguu kwa mikono yake nilikua naugulia maumivu eti akanipa pole mpaka nikashangaa kumbe makomando nao wanahuruma mimi nilikuaga najua hawana huruma kabisa kutokana na kazi yao, baada ya kuninyoosha akaanza kunipaka dawa kwenye goti langu alinipaka mpaka mwisho alirudisha traki mahali pake kisha akasimama.

"Usifanye mijongeo isiyo na lazima utajitonesha mguu wako"
"Sa sawa" niliitikia bado nilikua namwogopa mwogopa hivi.

"Naweka simu yangu chaji hapa, unilindie nitaifuata badae"
Niliitikia kukubali japo moyoni mwangu sikutamani hata aiache hiyo simu na kurudi badae kwani angeendelea kunitia hofu tu, aliaga na kuondoka zake.

Kutokana na maumivu ya goti niliona kulala isingewezekana kwanza usingizi ungetokea wapi kwa namna nilivyokua naugulia mguu wangu.

Nikasogea kwenye meza ya Tv ili niweze kuwasha na kuweka movie kwa sauti ya juu ili kupunguza kusikia stori za majirani kwani nilijua wataongelea mbwa au wataniongelea mimi kubebwa na komando niliwajua vizuri majirani walivyo na umbea wa asili.

Kabla ya kuondoka meza ya tv kurudi kochini, nikaona ni kheri niicheki simu ya komando kama inapitisha chaji au laa maana isijekua haiingizi afu badae mwamba anarudi anakuta simu yake haina chaji ningekua natafuta vita nyingine na komando na mabalaa siyataki mimi, nikagusa kioo cha simu nikaona simu inapeleka moto ila kuna jambo lingine lilinishangaza kwenye kioo cha simu.

Nikajikuta naduwaa kwelikweli yaani sikuamini.

Itaendelea.............

EP 3.
"Nilimwona mwanaume akiwa kwenye mavazi ya jeshi yale ya kiofsa yanakuawaga ya kijani hivi yamemkaa vizuri sana mwilini, niliganda kwenye sura yake alikua mzuri sana, hakua mweusi wala mweupe alikua na rangi flani hivi ya katikati, kwa ujumla alikua na mwonekano mzuri nadhani nikisema mwanaume mzuri unaelewa sio ule wa vijana wa TikTok waramba lips hapana nazungumzia tu mwanaume mzuri bhasi kuna mikosho ako nayo ilinipiga bumbuwazi kwa muda.

Likaja wazo huenda simu ikanipiga picha wakati nimeigusa na kuitazama kwa muda mrefu, kimbembe akirudi mwenye simu, wee nikabofya kibonyezeo cha pembeni na kurudi kwenye kochi mara si nikajitonesha "mamaaaa" nikapiga ukelele ila mimi.

Nikatulia kutazama movie pale mara simu yangu ikaanza kuita mpigaji alikua mdogo angu nikaipokea na kuiweka sikioni.

"Dada duka wamevunja wameiba kila kitu aaaaaaaah aaaaah" mdogo angu alinipa taarifa ambayo aliushtua moyo wangu, kusikia kwamba duka langu limevunjwa walikua wanavunja maisha yangu kwa ujumla kwani maisha yangu jijini yalitegemea uwepo wa hilo duka sasa kama wanalivunja ili nirudi sifuri nilikua kwenye wakati mgumu sana, wezi ni watu wabaya sana jamani, kama hujawahi ibiwa ukaona mwizi anapigwa unaweza mwonea huruma ila siku akikuibia ile yenyewe yenyewe ndo unajua kwamba mwizi sio wa kumwonea huruma hata kidogo.

ilibidi nijikaze kidogo nijari usalama wa mdogo angu kwanza.

"Tulia mdogo angu mali zinatafutwa tu wewe uko wapi?"
"Niko hapa kwenye duka nje ila sina nguvu kabisa, dada naumia napata mawazo mfululizo tutakua wageni wa nani sisi dada aaaah dada tumeisha sisi, dada tumeumbuka aaaagh dada sina nguvu hata za kutembea njoo unichukue tafadhali napata mawazo mabaya mimi nakuomba njoo"
mdogo angu alitoa kauli ya kunitoa machozi kabisa yaani aliomba msaada kwangu kilichoniuma zaidi sikua na nguvu ya kwenda kumsaidia mdogo angu kwenye maisha inauma sana pale mtu mwingine anapoona wewe ni msaada kwake halafu wewe huna hiyo nguvu ya kutoa msaada nyie inauma sana, hiyo nguvu sikuipata kwakua na mimi hali yangu haikua shwari nilianza kukosa pumzi, huwa nasumbuliwa na pumu hivyo nilianza kupata pumzi kwa tabu sana.


Mlango ulianza kugongwa kwa fujo sana nilikosa nguvu hata ya kwenda kufungua nilikua vibaya mno jamani.

"Ni mimi naomba nifungulie nimefuata simu yangu, tafadhali usiogope" mgongaji alinitoa hofu nikaitambua sauti ya mgongaji kuwa ni yule komando ila sina nguvu za kumjibu akafungua mlango na kuingia ndani alinikuta mimi nahangaika kwa haraka akajua hiyo ni pumu akaniuliza wapi ilipo dawa yangu, mimi nikaonesha mkono kilipo chumba changu akaenda haraka aliporudi alinipa nilivuta nilivuta kwa muda ndipo nikapata uafadhali.
Aliniuliza naendeleaje nilimjibu tu niko sawa, akafungua mapazia yote ili kufanya hewa izunguke vizuri ndani.

alinitazama mimi nikawa nakwepesha macho yangu asiniangalie kwani angejua kwamba nilikua nalia ila mwamba alifanikiwa kujua kwamba nilikua nalia na sikua sawa.

"Vipi mbona kama ulikua unalia au maumivu ya mguu yamezidi au kifua kinauma bado" Komando aliniuliza.
"Ha hapana hauumi"
"Pole na utulie kila kitu kitakua sawa" kila akiniambia sawa ndo machozi yalizidi kunitoka mimi nilikua nawaza hali ya mdogo wangu tu.

Komando alinibmbeleza huku akitoa kitambaa na kofia aliyovalia kwa muda mrefu nikaweza kumwona vile vile alivyoonekana kwenye picha ndivyo alivyokua anaonekana hapo mbele ya macho yangu, kweli kaka komando alikua mzuri wa sura na mwili wake ulikua upo vizuri, aliitazama simu yake na kuona inapeleka chaji kisha alinigeukia mimi na kuniuliza kwanini bado nalia, kwakua sikua nimempa sababu mpaka wakati huo, ikabidi nimwambie kila kitu kuhusu mdogo angu na mahali alipo, nilitamani kwenda kumchukua akaniomba mimi nitulie nyumbani halafu yeye atakwenda kumchukua mdogo angu na kurudi nae nyumbani, aliniuliza kama ninae rafiki nikamwelekeza kwa Jemma akaenda kumchukua ili aje akae na mimi kuniangalia hali yangu kisha yeye akaondoka kwenda lilipokua duka langu ili kumchukua mdogo angu, niliombea dogo awe salama asije akajifanyia kitu kibaya kwa stress za kuibiwa vitu dukani kwetu.
Itaendelea......

EP 4.

Nilitulia kwangu baada ya lisaa hivi nilipigiwa simu na mdogo angu kwamba komando ameshamchukua na tayari wapo njiani anamrudisha nyumbani, nilimshukuru sana Mungu kwa jambo hilo maana sikutamani kumpoteza mdogo angu kwa namna hiyo, niliwapigia wazazi na kuwaondoa hofu kwamba ninae rafiki angu amekwenda kumchukua dogo na wapo njiani wanarudi home.

Wazazi nao walimshukuru Mungu kwa hatua hiyo, niliendelea kutazama movie huku tunaongea ongea na Jemma, nilikua nampa mipasho ya kijana Twalib namna alivyokua ananitongoza na kunifanyia vituko pia nikamwambia alivyokimbia na kuniacha mwenyewe nikiwa kwenye hatari ya kung'atwa na mbwa, tulimcheka sana hapo Jemma akakumbuka kumbe kuna vyombo tuliviacha bombani pia kuna maji ya kuchota akaamua yeye aende bombani kwa muda kuchota maji yake na yangu kwani akiyakosa maji siku hiyo ilibidi tungojee mpaka siku tatu zipite hapo tungejuta kabisa, Jemma alipoondoka tu.

Mara nikaona namba mpya inaingia nikaona nipokee kwani huenda ni komando ananipigia na mimi sikua na namba yake.
"Halooo kaka" nilianza kuongea.
"Weee mbwa nimeona clip video namna wanavyolifanya duka lako, wewe ulijua utakaa nalo milele sio, yaani wale wezi wamenifurahisha sana hiyo ndo karma mbwa wewe, ulizani mali yangu itakupa utajiri labda kama mimi sio mkinga, kenge maji wewe hilooooo limefilisika pyeeeee lichekeni hahahahahah nenda kadange tena ili upate hizo pesa nakwambia na huwezi pata mwanaume akakufungulia duka kama mimi hahahaha lazima urudi kijijini kwenu ukalimie migomba na kukatia mifugo nyasi mbwa wewe" maneno makali yalizidi ikabidi nikate simu na kuiblock namba kabisa, niliitambua hiyo sauti ni sauti ya Sanga aliekua ex wangu.

Ni mwanaume ambae tulikua kwenye mapenzi mazito nikiwa chuoni na hata nilipomaliza chuo kwakua kupata kazi ni mtiti na mimi sikutaka kurudi nyumbani kwetu Moshi.

Sanga kwa mapenzi yake bila kulazimishwa na mtu, akaamua kunifungulia duka la nguo kila kitu kiliandikwa kwa jina langu hivyo nilikua na umiliki asilimia mia moja ya duka hilo.

Siku zikasogea ila nikaja kubaini kwamba Sanga ni mshenzi zaidi ya neno lenyewe sababu alikua na wanawake wengi sana halafu nilipomuuliza bila aibu akanijibu kuwa yupo nao ila mimi ananifanya kama main chick ndio maana alikua huru kunifungulia mpaka duka, halafu wengine ni ma side chick hawatopata chochote cha maana kwahiyo nitulie tu ili nirambe maisha, mwanzoni nikakubali ila siku zilivyozidi kwenda nikajiona nitapata magonjwa bure ni kheri nijiachie nisiendelee kuwa nae, kiutu uzima nikamwambia akajifanya kupanick eti anataka duka lake, mimi nikajiuliza huyu anamjua mchaga au anamsikia nikakaza nikasema sitoi hata pin, akapeleka shauri mahakamani bahati nzuri nilikua na rafiki angu flani ni mwanasheria akanipambania mpaka ushindi ukaridi kwangu kwahiyo akabaki na ile chuki ya moyoni tu kwani nilimpiga huko mahakamani.

Kwahiyo alipoona duka langu linavunjwa na vitu kuchukuliwa ndipo akaanza kunitumia maneno ya kejeli kwamba nitarudi kwenye sifuri na kweli sikua na akiba yeyote ndani ya kujaza mzigo upya kwani nguvu yangu kamili nilitegemea kwenye hilo duka peke ake.

Kidogo aliingia mdogo angu Oliva alikua peke ake alipoingia ndani tulikumbatiana kwa nguvu sana, tulilia kwa pamoja huku tunamshukuru Mungu kwa namna alivyokua ametuvusha kwenye jambo hilo kubwa kwakua kalikua kamechoka na tulikua na kawaida ya kwenda kuoga pamoja nilimwambia
"Twende nikakuogeshe totoo" kanavyopenda kudeka sasa kakakubali haraka tukabadili nguo tukaingia bafuni nikamwogesha kulikua na kiporo cha wali tukapasha pale na kula kwa pamoja huku tunaendelea kuongea.

"Hivi dada yule mjeda ako mmeanza kudet lini maana anajali hatari, nilikua naogopa sana njiani maana dereva wa gari alikua anakimbiza sana gari yaani, ila alivyokua ananitoa hofu sasa, utasikia shem tulia mimi nakulinda usiogope kama kufa nitaanza kufa mimi halafu wewe utawahi kumwambia dada ako namna nnavyompenda" mdogo angu aliongea maneno mageni ambayo yalinishangaza kabisa kwani mimi na komando hatukua wapenzi ndo siku ya kwanza kuonana nilijitahidi kujitetea kwa mdogo angu lakini hakuonesha kunielewa kabisa nikaona hii ngoma nzito sitoweza kujitetea zaidi.

"Kaniambia kwamba nikwambie mke wake badae atakuja kula na rafiki ake mmoja kwahiyo upike chakula kizuri kabisa"
"Heeee mbona kasheshe huyu komando kaniganda sasa anakuja na mtu mwingine duuh" mdogo angu akazidi kunitania tu tena alionesha kunipa mamoto kwamba amempitisha komando awe shemeji yake mimi naishia kucheka tu.

Muda ulisogea ilipofika jioni tulikua ndani ikabidi tupike chakula pale, pilau nyama maana kulikua na nyama ambazo zilikua kwenye friji, tukajitahidi kupika vizuri zaidi na mimi kwenye kipengele cha kupika sina dogo huwa napika balaa.

Muda ukasogea mdogo angu akasema anakula yeye maana njaa imemkamata, mimi nikadai nawasubiri wageni huo ukawa mwanya mwingine wa mdogo angu kuendelea kunitania kwamba nimenogewa sana na komando, kwenye utani mdogo angu alikua ananizidi ikabidi nitulie tu.

Muda ukazidi kwenda ila komando wala rafiki ake hakutokea na sikua na namba yake nikazidi kumsubiri tu hapo nimejinunisha balaaa, naandaa maneno ya kumwambia akija ili ajue nimekasirika ila nisimuuzi asije akanivunja vunja bure, mpaka saa tano usiku mdogo angu alikwenda kulala chumbani kwake, mimi nikaendelea kuwasubiri hao wageni. Kidogo simu yangu ilitetemeka kuonesha ujumbe umeingia, nilijua atakua komando tu sababu yeye alikua na namba yangu ila mimi sikua na namba yake, niliifungua meseji kwa bashaha lote ili nijue komando katuma kutu gani?.

Itaendelea................

EP 5.
"Hello beautiful" jumbe ilikua ya salamu ndiyo iliyoingia kwenye simu yangu nami niliijibu kwa bashasha lote, baada ya mazungumzo ya dakika kumi nilijua alietuma meseji ni Twalib yule kijana alienitongoza asubuhi, alipotokea mbwa kichaa akanikimbia, mshenzi yule alijilengesha kwenye kumi na nane zangu nikampelekea moto wa maneno makali ambayo alijuta kunifahamu mpaka akaniomba msamaha ndipo hasira yangu ilitulia, nikaona komando nae ananizingua tu kwani hakua amefika mpaka wakati huo, nikadokoa nyama hapo mbili tatu maana sikua na mzuka na pilau lenyewe sijui hali ya kukasirika ilitoka wapi, nikahifadhi chakula kwenye friji ndipo nikaenda zangu kulala chumbani kwangu kwani nyumba tuliyokua tunakaa ilikua na vyumba viwili, sebule, jiko na choo, kwa kiasi fulani ilikua na uzuri wake, nilijitahidi kutafuta lepe la usingizi nilikosa kwakua nilikua nawaza maisha ya mjini yatakwendaje bila kuwa na duka pia sikua na kipato kingine kikubwa cha kuendelea kuniweka mjini. Kichwa changu kiliwaka moto niliyatafakari maisha ya kwetu moshi nikaona siwezi kutoboa kabisa mpaka usingizi unanichukua sikupata njia mbadala ya kuishi mjini.

Siku mpya ilipoingia kama kawaida hatua na kwenda dukani, tunaenda kuuza vitu gani wakati wezi wametufanyia kitu mbaya kwa kuiba kila kitu mpaka pesa walikomba yaani.

Nikitazamana ndani hatukua na chakula cha kutosha ndani na pesa ilikua kipengele, tukawaza tutaishi vipi ila tukaamua kutulia kwani mambo huenda yakarudi kwenye hali yake ya kawaida, mdogo angu alipofungua friji na kukuta chakula cha jana akajikuta anacheka na kuanza kunitania, sikua sawa hivyo aliamua kuachana na huo utani kwani kufanya hivyo ni kunikera zaidi.

Tulikula hiko kiporo na wali hatukua na matumaini tena kama komando atakuja kwa namna alivyokua ametuzingua usiku uliopita.

Tukakaa na tunapiga piga stori huku tunacheza karata mara mlango ukaanza kugongwa ile kufungua mlango komando huyu hapa tena kavaa mavazi yake kabisa ya kijeshi.
Mdogo angu alimpokea mzigo aliokua ameubeba, mdogo angu asivyo na dogo jamani akaanza kumwita shemeji eti komando akaanza kucheka kwa mara ya kwanza namwona anacheka, maana kwangu mimi siku iliyopita hakucheka hata mara moja.

"Unaendeleaje na huo mguu?" Aliniuliza nami nilimjibu kwamba niko poa, alijitetea kwamba hakuja usiku uliopita kwakua alibanwa na kazi sana hivyo alituletea vitu tupike na baadae atakuja na huyo rafiki ake, tulimshukuru na yeye kuondoka tulipofungua mfuko aliobeba ulikua na mchele kama kilo nne hivi, nyama nyingi ya ng'ombe pamoja na viungo mbalimbali vya pilau, tukajua komando alikua mpenzi wa pilau huyo.

"Yaani limtu linasababisha tunakula pilau siku mbili mfululizo halafu hiyo samahani yake linaomba taratibu anabahati yale mavazi tu leo ningemchezesha vibao ndo angejua kichaa changu cha kichaka kimekaaje"


"Hahahaha namwambia kwamba unataka kumpiga shemeji" Oliva aliongea kama utani nikaona anatoa simu na kumpigia Komando, nikaona huyu mtoto anataka kuweuka nikataka kumfikia ila maumivu ya mguu yalikua makubwa hivyo alikua ananikwepa kwepa, simu ikapokelewa upande wa pili ili aweze kunishtaki mbele ya komando jamani, simu ilivyopokelewa tu Oliva akaanza kuongea pale.

"Shem, dada anasema kwamba umeondoka bila kumkumbatia wala kumbusu hajapenda kabisa" Oliva aliongea kitu cha tofauti kabisa angalau niliweza kupumua vizuri, sijui komando aliongea nini ila nilimwona Oliva anacheka huku akishangilia nikama walizoeana ndani ya muda mfupi kwa haraka sana, simu ilipokwatwa pale nikamdadisi sana Oliva aniambie komando kasema nini ila hakuweza kufungua kinywa chake na kudai nitaona mwenyewe alichosema.

Tukaendelea kupika pale kidogo mlango ukaanza kugongwa si akaingia komando akiwa na mfuko wenye soda ndani yake. Oliva alienda kumpokea huku anafuraha kweli mpaka nikawa namshangaa huyu mtoto amewehuka au vipi mbona huyu komando kamkaa sana akilini gafla kuzoeana hiyo vipi.

Komando hakukaa kwenye kochi badala yake akanibeba kwa mikono yake, nikaanza kumwomba aniachie.
"Komando niachie jamani sikupigi mimi, nilikua natania tu wala sijanuna" wakati naomba hivyo mdogo angu alikua anacheka na kushangilia ni kama alikua anapendezwa na kitendo hiko, akanipeleka mpaka chumbani kwangu, akanisimamisha na kunikumbatia kwa nguvu.

"Manka nakupenda sana, nataka kuishi maisha yangu yote na wewe, mimi naitwa Fredy, sina mke wala sina mpenzi, mdogo ako kanambia kila kitu kuhusu wewe kwamba huna mpenzi wala mtu wa karibu hivyo nataka kuziba nafasi ya upendo kwenye moyo wako niko tayari kuja kwenu na kukulipia mahari nikubalie mama angu nakupenda sana nimeshindwa kuficha hisia zangu nakupenda kweli kabisa" Komando Fredy alijimimina maneno yake ya hisia zilizokua moyoni mwake.

"Sasa mbona haraka hivyo" kabla sijamalizia sentesi yangu alinisogezea mdomo wake karibu yangu hapo sikuweza kujizuia tena kwani midomo yake ilianza kucheza na midomo yangu kwa ufundi sana alikua kama anataka kuning'ata na haning'ati nilihisi msisimko wa ajabu ukilinganisha na muda mrefu umepita sikua nimeshikwa namna hiyo, nilitamani kumwomba komando aniachie ila hata kutamka neno moja nilishindwa alinisukuma kitandani nilienda mzima mzima, akaja juu yangu na kuanza kunitumasa, sasa hiyo tomasa yake mmmmmh, si nikaanza ku..

Tangazo - Distro kid Upload your music To day
Distro kid Upload your music To day
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*KOMANDO NIOE NTAKUWEZA TU* *1-5* *__________________________________________* *SEHEMU YA KWANZA* "Weee Maa yaani kila mtu ameamka kuchota maji ni wewe unajifungia ndani tu kwamba utaoga na kufulia mate yako"



"Jamani mimi bado nna usingizi, nichotee bhasi undugu wangu"
"Wewe ushanigeuza mimi kikaragos chako au umenioa kila siku nikuchotee tu maji nakwambiaje amka tukachote maji, mimi sikuchotei hata tone moja"
rafiki angu Jemma alikazana nitoke nje niende bombani nikachote maji, mtaa tuliohamia ulikua na tabu ya maji, maji hutoka baada ya siku tatu, kwahiyo ili uwe na akiba ya kutosha ilibidi kuchota maji mengi na kuyaweka ndani, ilibidi niamke tu.

Ilibidi nivae nilikusanya ndoo za maji, nilipita nyumba kadhaa kwani bomba la maji lilikua huko, nilipofika niliweka foleni kulikua na watu wengi ambao wengi wao walikua wamama, niliwajua wamama wa mtaa...

👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/komando-nioe-ntakuweza-tu-1-5-__________________________________________-sehemu-ya-kwanza-weee-maa-y

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi komando-nioe-ntakuweza-tu
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

MY WANGU❤️ sehemu ya 68

MY WANGU❤️ sehemu ya 68

542
MY WANGU❤️ sehemu ya 69 na 70

MY WANGU❤️ sehemu ya 69 na 70

474
AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 45💘💘

AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 45💘💘

438
AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘  N0 46💘💘

AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 46💘💘

351
MIMI SIKUACHI🥰 19 MPAKA 20

MIMI SIKUACHI🥰 19 MPAKA 20

164
AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 47💘💘

AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 47💘💘

134
MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 12 na 13

MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 12 na 13

89
MIMI SIKUACHI🥰 16 MPAKA 18

MIMI SIKUACHI🥰 16 MPAKA 18

85
MIMI SIKUACHI🥰 21 MPAKA 23

MIMI SIKUACHI🥰 21 MPAKA 23

82
MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 10 na 11

MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 10 na 11

76

ZIMESOMWA ZAIDI

‎TUNDA LA  DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

‎TUNDA LA DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

11.01K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

6.8K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya tisa.  👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya tisa. 👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

3.65K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya sita.  👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇  Shemeji inauma utanichana.

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya sita. 👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇 Shemeji inauma utanichana.

3.01K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 20.  👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 20. 👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

2.43K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya tatu.  👉 Sitaki sitaki mimi mdogo niache sitaki...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya tatu. 👉 Sitaki sitaki mimi mdogo niache sitaki...👇

2.4K
I LOVE YOU DADY 💘❤️💘10

I LOVE YOU DADY 💘❤️💘10

2.27K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 16.  👉 nakupenda pia...👇

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 16. 👉 nakupenda pia...👇

2.25K
❤❤ MTOTO WA MKE WANGU😛😛  Sehemu ya tisa.  Sasa jamaa akaupitisha ulimi kwenye mdomo wa  hawa na hawa kaachama

❤❤ MTOTO WA MKE WANGU😛😛 Sehemu ya tisa. Sasa jamaa akaupitisha ulimi kwenye mdomo wa hawa na hawa kaachama

2.24K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya nane.  👉 Mimi Nalia ndio tayari bikra imetolewa...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya nane. 👉 Mimi Nalia ndio tayari bikra imetolewa...👇

2.15K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

Hakuna Ratiba kwa sasa

Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 47💘💘 Post Mpya
AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 47💘💘
@majario LIVE

Baada ya kumaliza kupeana ule utamu wa alfajir hemed alinikumbatia tena tukalala tuliamka saa tatu za asubuhi tukaingia bafuni kuoga baada ya hapo tulipata breakfast tulivyomaliza kula nilimuaga hemed nikamwambia...

MIMI SIKUACHI🥰 21 MPAKA 23 Post Mpya
MIMI SIKUACHI🥰 21 MPAKA 23
@majario LIVE

🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡 Sehemu ya 21 Basi mie nikaendelea na vipindi na jioni sana ndo tukaludi getoo. Basi tukiwa tunaendelea na story zetu mi na lemi. Oyaaaaa kufika saa nne jsiku mtoto...

MIMI SIKUACHI🥰 19 MPAKA 20 Post Mpya
MIMI SIKUACHI🥰 19 MPAKA 20
@majario LIVE

🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡 Sehemu ya 19 Daah nikasema.mwanangu iyo chupi.nimemnunulia fatuma.natka nikampelekee si unjaua bado week 3 tunaenda likizo. Lemi akaniangalia akasema mh . Aya bwana hkuna noma.mi nikaivuta ile chupi. Nikaweka chini...

MIMI SIKUACHI🥰 16 MPAKA 18 Post Mpya
MIMI SIKUACHI🥰 16 MPAKA 18
@majario LIVE

🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡 Sehemu ya 16 Basi nikapata kaumarufu kweli kweli pale chooni. Yani ata wadada wakawa wananishobokea sana. Naomba unifundishe nifundishe kama zote. Wadada full shobo na mimi. Ata washikaji wakawa...

AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘  N0 46💘💘 Post Mpya
AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 46💘💘
@majario LIVE

Moyo wangu ulianza kudata juu yaHemed🥹🥹 nilijaribu kuongea nao lakini wala haukunisikia niliuambia moyo tulia hukuhuku kwa boo tayari tushasolve tatizo lililokuwepo Acha kuhamahama😟😟 lakini moyo bado ulizidi kung'ang'ania kwa...

MY WANGU❤️ sehemu ya 69 na 70 Post Mpya
MY WANGU❤️ sehemu ya 69 na 70
@majario LIVE

Basi nilipata kafuraha mno. Nikachukua pesa yangu .nikarudi darasani kuendelea na ratiba zangu. Uwiiiiii nilifurahi sana. Yani sana tu. Na prepo ilivyoisha tukarudi darasani. Mie nikampa tu yule mwanafunzi...

MIMI SIKUACHI🥰 14 MPAKA 15 Post Mpya
MIMI SIKUACHI🥰 14 MPAKA 15
@majario LIVE

🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡 Sehemu ya 14 Aseee mi nilimuangalia sana uyu demu. Nikamuona jau . Yani yupo very serious ananitongoza .mnajua kuna jinsi nilimdharau . Nikaona uyu demu daaah. Alivyoona namshangaa na sijamjibu...

MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 12 na 13 Post Mpya
MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 12 na 13
@majario LIVE

12 MPAKA 13 🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡 Nikasema vp mbona huniachii mkono. Akanmbia ahaa sory haji. Kisha akaachia mkono wangu. Na mda uo uo ndo lemi akawa analudi pale. Akasema ahaaa mrembo upo...

MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 10 na 11 Post Mpya
MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 10 na 11
@majario LIVE

10 MPAKA 11 🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡 Aseeeee uyu demu ni mzuri bwana. Mi. Mwenyewe nilikubali. Ila sio kwamba nilimtamani no. Mi ni mwanaime ninayejielewa sana. Wanaume tuna tamani mno. Ila unakuwa na msimamo wako...

MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 7 na 8 Post Mpya
MIMI SIKUACHI🥰 Sehemu ya 7 na 8
@majario LIVE

7 MPAKA 9 🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡🟡 Basi bwana tukivyotoka kula sasa. Mi nikaludi ndani ila lemi akanmbia kuna mtu anakutana nae kidogo nikasema powa so nikamuacha mimi nikaludi hostel.aseeee chuo kimechangamka iki sana. Yani...

MY WANGU❤️ sehemu ya 68 Post Mpya
MY WANGU❤️ sehemu ya 68
@majario LIVE

Basi akashuka. Akamsalimia mama pale. Mama akamuitikia. Akaniuliza. Ushakuwa tayari. Mie nikasema ndio . Akanmbia kachukue nilivyokwambia tupakie. Nikasema sawa. Kweli nikaenda kuchukua. Vilikuwa vidogo. Kweli. Vyengine niliviona kashanunua yeye...

AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 45💘💘 Post Mpya
AAAAH IMETOSHA BOSS 💘💘 N0 45💘💘
@majario LIVE

0742133100 Babie Love Niliipokea ile simu huku nikiwa natetemeka kwa uoga..... hello daddy.... pendo what's going on 🤷‍♂️ taarifa gani hizi nazoambiwa kwani hamkumaliza tofauti zenu inatakiwa muache drama mtakuja kunitesea...

MY WANGU❤️ sehemu ya 66 na 67 Post Mpya
MY WANGU❤️ sehemu ya 66 na 67
@majario LIVE

Aseeee nilikuwa na maumivu kwa kila sehemu ya mwili wangu. Nilikuwa na maumivu makali mnoo. Asa mkono . Yani sikuwa sawa kabisa. Namsikia mlige akiwa ndani .anasema yani nikitoka njeee...

PILOT SITAKI INANIOGOPESHA  SEHEMU YA 19 - 20 Post Mpya
PILOT SITAKI INANIOGOPESHA SEHEMU YA 19 - 20
@majario LIVE

Nilikuwa najilazimisha hata kucheka mama aliniona ila akajua labda ni uoga tuu akaniambia mwanangu usijali bhana Kila kitu kutakuwa sawa na ndoa yako itapita vizuri tu nikawa namjibu kwakichwa saw,...

MY WANGU❤️ sehemu ya 64 na 65 Post Mpya
MY WANGU❤️ sehemu ya 64 na 65
@majario LIVE

Basi mie nikaingia chumbani nikajilaza kitandani.nikalia mnoo .niklia aswaaa.mana mi.mwenyewe mlige nampenda.nampenda sana.na kweli nimemkosea ila hataki ata kuongea na mie ni ananifanyia hasira tu. Basi shoga yenu nikawa nalia...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest