MIMI NERIA💃💃❤️❤️❤️ 1___5
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Mapenzi jamani ni kitu cha ajabu🤦♀️, ni bahati sana kwa mtu kumpata kirahisi yule aliepangiwa nae, yani unakutana kwanza na vichwa ngumu🤣 wanakuumiza weee then mwishoni ndo anakuja yuleee spesho kwa ajili yako.
Hellow peoples🙋♀️ Naitwa Neria. Nilikua nasoma chuo Mbeya wakati Mama na mdogo wangu walikua wanaishi Dar. Icho kipindi ndo nilikua namalizia malizia chuo nikawa nina raha😊 sana. Sisi Mama ndo alikua anatulea yaani kila kitu nikitaka napata toka kwa Mama. Baba yangu alifariki nipo mdogo, Kwaiyo Mama akaja kuolewa na mume mwingine ndo akampata mdogo wangu Steve.
Ila ile 💍ndoa yao haikua ya baraka, Baba yangu wa Kambo alienda akaoa tena mwanamke mwingine kwaiyo Akawa katutelekeza kiaina. Sasa kuna siku nilikua zangu discussion na rafiki yangu ndo nikapokea simu📱 kua mama anaumwa sana hali yake sio nzuri.
Ukiangalia nyumbani🏠 hakuna mtu mwingine wa kumuhudumia zaidi ya Steve ambae ndo kwanza yupo darasa la pili, na majirani hawawezi kuacha kazi zao na kumuangalia kila siku. Nikaomba ruhusu chuo nikafunga safari Mpaka Dar kwenda kumuona Mama.
Nakumbuka Siku ya safari sasa niliwahi stand mapema kabisaa nikakata tiketi asubuhi ile ile pale stand. Nikapewa tiketi yangu nikapanda basi🚌, sasa nimefika kwenye siti yangu nakuta kuna mtu kakaa. Tena alikua ni mkaka kalala😴 kajifunika na koti usoni.
Ukiangalia siti zote zimejaa hakuna hata siti moja iliyokua wazi.
"oya bro, umekalia siti yangu" nilianza kumuamsha yule kaka aliekua kalala.
"Broo!" nikaanza kumsukuma maana alikua anajifanya hata hasikii😒. Yule kaka alitoa koti usoni akaniangalia kama dakika mbili nzima kisha akarudisha koti lake usoni akaendelea kulala.
Daah mda huo huo konda akasema watu wakae chini tayari safari inataka kuanza na ukiangalia ni mimi mwenyewe nilikua nimesimama basi nzima.
Nilichukia😠, nikazidi kumwamsha yule kaka akawa bado anajifanya anisikii, Nikamtoa koti lake usoni, nikachukua maji kwenye chupa nikammwagia usoni.
Weee yule Kaka alishtuka akasimama kwa hasira😡, tukawa tuna tizama sasa kila mmoja ana hasira na mwenzake.
"husikii ninavyo kuambia nipishe nikae"
"una wazimu eee? kwaiyo ulidhani mimi ni kichaa nitatoka uko kote nije kukaa kwenye siti yako. Wewe ni nani kwanza?" Wee jamaa ana dharau😫 huyoo. Alifungua waleti yake akatoa tiketi akanionyesha na mimi nikampa ya kwangu.
Tiketi zetu zilikua zinafanana namba ya siti. Ikabidi konda aitwe, tulipomuelezea akasema mmoja Abaki pale mwingine aende akakae mbele na dereva.
"Mimi nitabaki hapa, huyu ataenda kukaa na dereva" Nilidakia
"huyu nani! Si umenikuta hapa, peleka miguu yako ukakae na dereva"🤣
"mbona huna huruma wewe kaka kwani ukienda kukaa na dereva utapungukiwa nini?"
"wewe ulivyo nimwagia maji usoni ulikua na huruma! Nenda kakae na dereva kule mbele acha kutupigia kelele" Yule kaka akarudi kukaa kwenye siti nikawa nimesimama namtizama kwa hasira😡
"Dada tupishe basi" Kuna kadada kalikua kamekaa nae pembeni kakawa kana leta shobo naisi sababu yule kaka alikua handsome.
Basi nikatoka kwa aibu🙈 mpaka mbele karibu na dereva nikawa nimekaa pale. Safari ikaanza vizuri, hasira zikawa zimeniisha baada ya kumkumbuka Mama yangu🥹.
Dereva alikanyaga mafuta mwishoni tukafika sehemu ya kula. Wakashuka wote mimi nikawa wamwisho nikaenda kununua chakula ila wakati narudi nikakutana na yule kaka ambae tulikua tuna gombania nae siti.
"Sista nisaidie kumwambia konda anipe dakika tano nimepata shida kidogo" Nikamkubalia, akatoka pale nduki sijui alikimbilia wapi.
Nikasema hunijui, yani siti yangu ukalie wewe alafu unataka nimwambie konda akusubirie? Subutuuu🤣.
Basi nikarudi kwenye basi🚌 na chakula changu nikawa nimekaa pale pale kwa dereva nakula. Konda akaja ,nae dereva akaja akawasha gari, mimi kimya sijaongea kitu. Kweli Dereva akaanza safari, tukawa tumemuacha yule jamaa kule hotelini🏩 ila jamani mimi🤣.
"Konda mwenzangu simuoni, tumemuacha" kale kadada kakaanza kulalamika hata kabla hatujafika mbali😒.
Kabla konda hajamjibu ghafla yule kaka akawa kashafika, jasho likawa linamtoka mpaka la meno🤣 maana alikimbia sana.
Konda akamfungulia mlango akaingia maskini🤣 nyiee. Ila aliniangalia kwa hasira😡 mimi nikawa namchekea tu, akapita zake kwenda kukaa kwenye siti yake.
Majira ya usiku tukawa tumefika Dar, tukaanza kushuka stendi, nikakimbilia kwenye buti nikachukua begi langu, nikaita boda boda ile nataka kupanda akaja yule kaka akapanda yeye🤣. Nilimtazama kwa hasira😡, yeye akacheka kisha akanikonyeza
"i hope sitakuja kukutana na wewe hata kwa bahati mbaya, bro tuondoke" Alinambia huku boda boda ikianza kuondoka.
"Mpuuuzi wewee nani anataka kukutana na wewe sasa! mjinga kabisaa" weee🗣 nilimpiga kelele za hasira😡 mpaka boda boda ikapotea kwenye usawa wa macho yangu.
Nilichukua usafiri mwingine nikaenda mpaka nyumbani🏠. Kufika namkuta mama yangu na yeye ndo alikua karuhusiwa kutoka hospitali🏥 ila hali yake haikua nzuri.
"Mama yako anatakiwa kufanyiwa operation, na milioni 10 inahitajika" Jirani yetu Mama Getu alinivuta pembeni
"Daah sasa iyo hela💵 natoa wapi mimi wakati hali yetu ndo hii" nilichoka, nikaanza kulia😭
"Sasa unalia nini Neria? Badala ya kupambana na wewe unaanza kulia, unadhani mama yako akikuona katika hali hii atajiskiaje? Si ataona amekua mzigo kwenu? Embu acha kulia" Mama Getu akawa ananibembeleza pale nikawa nimenyamaza.
Aliondoka akarudi nyumbani kwake nikawa nimebaki sasa mimi nikiwaza🤔 iyo milioni 10 natoa wapi si nitaenda kumpoteza mama yangu jamani😭.
Niliingia chumbani kwangu, nikaoga nilipomaliza nikafungua begi langu nivae nguo. Nashangaa nakutana na boksa za kiume, mara spider! Heee nikashtuka😳
Inamaana nimebeba begi la mtu nikaacha langu, uwiii mbona balaa linaniandama kwanzia asubuhi😭.
Kukagua lile begi vizuri nakutana na kitambulisho cha NIDA pamoja na kadi ya mpiga kura. Kuangalia ni vya Imran yulee kaka ambae nilikua nagombania nae siti🤦♀️.
JE NINI KITAENDELEA
MIMI NERIA
Sehemu ya : 2
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Tulipoishia......
kukagua lile begi vizuri nakutana na kitambulisho cha NIDA pamoja na kadi ya mpiga kura. Kuangalia ni vya Imran yule kaka ambae nilikua nagombania nae siti.
Tuendelee........
Aisee mbona nina mkosi na huyu kijana. Nilichukia😠 nikachukua lile begi nikalitupa pembeni. Hasira zilipoisha nikachua vitu vyake nikaanza kuvipanga upya🤣.
Siku iliyofatia niliamka nikamwandaa mdogo wangu akaenda shule nikawa nimebaki na Mama.
Bado hali yake haikua nzuri hata kidogo kwanza siku zilivyozidi kwenda ndivyo hali yake ilizidi kua mbaya.
"Mama milioni 10 tutatoa wapi" niliongea kwa huzuni, Mama akiwa kajilaza nje kwenye mkeka.
"mwanangu acha tu nife" mama aliongea kwa tabu, machozi yakashuka😭 yenyewee nikawa najikaza nisilie mbele ya Mama. Alikua kashakata tamaa maskini😭 ya kuendelea kuishi maana kulikua hakuna hata tumaini lingine lililobaki.
Ukiangalia ndani kwenye hakuna hata chakula kilichobaki zaidi ya unga tu, tena kodi ndo ilikua inakaribia kuisha aisee😭.
Nilienda dukani nikanunua sukari maana nilikua na visenti vyangu nilibana. Kisha nikapika uji, nikamnywesha Mama nilipomaliza, Mama Getu na yeye alikua kaja kumuona, nikamwomba amuangalie mimi nikatoka.
Nilibeba begi🎒 la Imran mpaka kwenye ofisi za Lile basi tulilopanda, nimefika nikakuta begi langu lisha letwa alikua kalichukua Imran, yani kifupi tulikua tumebadilishana😠.
Mbali na kulirudisha, alikua kaniachia ujumbe jamani huyu kaka🤣 eti anasema
"nisione ukijipitisha mbele yangu hata kwa bahati mbaya"
Angejua ninavyo mchukia tu asinge jisumbua kuniandikia hata uo ujumbe, kwanza nani anampango wa kujipitisha mbele yake mfeeew😒.
Baada ya kuchukua begi langu, nilienda moja kwa moja kwa Baba mdogo. Alikua ni mdogo wa Baba na yeye ndo alichukua mali za baba zote na jukumu la kunisimamia akawa kamuachia Mama. Alivunja kabisa undugu na sisi.
Nilifika nyumbani kwake nikakuta anamfanyia mwanae wa mwisho Birthday party, wanachoma nyama na kucheza mziki kama kuna harusi vile🥹.
"Unafanya nini hapa?" Baba mdogo alinipokea na maneno makali tena mbele za watu mpaka nikaanza kuona aibu
"Baba mdogo, mama anaumwa sana please naomba utusaidie!"
"Mimi ni Daktari? Sina msaada na wewe"
"Baba mdogo tafadhali mama atakufa etu please msaidie afanyiwe operation!" na kiburi changu chote lakini mtoto wa kike nikapiga hadi goti🧎♀️ na kumshika mguu ili anisaidie😭
"Hahaha kwanza sina undugu na wewe Neria! Mama yako alikua Malaya, kila mwanaume alilala nae, kwaiyo sidhani kama wewe ni mtoto wa Kaka angu"
Aiseee weeee yale maneno yaliniuma, nilimrukia baba mdogo nikaanza kumkaba. Disco likawa limeingia mmasai🤣.
Hata kama ni wewe jamani, mtu amtolee mama yako maneno machafu sidhani kama utamuacha salama.
Niliikamata ile shingo ya baba mdogo kisawa sawa kama sina akili nzuri. Watu wakanikamata iyoo ndo ikawa pona pona ya Baba mdogo.
Baba mdogo alisimama kwa hasira😡, alinizaba vibao👋 vya kufa mtu mpaka mashavu yakaanza kua mekundu. Kisha akanibeba na kwenda kunitupa nje ya geti lake😭.
Daah nililia😭 pale getini weee mpaka hasira zikaisha nikanyanyuka na kuondoka.
Barabarani mvua ikawa imeanza kunyesha ila hata sikua naisikia.
Watu waliokua wanapita na magari🚗 wakawa wana nishangaa😳 ninavyo tembea kama zombi.
Nilitembea mawazo yakiwa mbali. Nilishakata tamaa kabisa nikawa naona mama anakufa mbele ya macho yangu na mimi nimeshindwa kumsaidia😭.
Nilisikia honi ya gari🚗 piiiiiiiiii kuja kugeuka, kumbe nilishafika mpaka katikati ya barabara pasipo kujua aiseee.
Dereva wa lile gari alichuna breki kali ikawa imebaki kidogo tu anigonge🙆♀️. Weew chezea kufa ukiwa unajiona nini.
Dereva alishuka akiwa hana hata hasira tofauti na nilivyo tegemea, hakua mwenyewe alikua ana mtu kambeba nae akashuka alikua ni Imran bhana, yeye sasa ndo alikua kakasirika😡 utadhani ndo dereva.
"Upo sawa?" Kaka wa watu akaanza kunikagua kama nipo sawa apo bado mvua inaendelea kunyesha.
"nipo sawa"
"angekua mtu mwingine ningesema ni bahati mbaya ila kama ni huyu mwehu ni maksudi tu" Imran alifoka kwa hasira😡 mpaka mwenzake akawa ana mshangaa.
"Nani mwehu? wewe ndo mwehu tena una bahati siko kwenye mudi lasivyo ningekufinyanga nitoe ayo macho"🤣 na mimi sikua nyuma
"nini wewe? unajua mimi ni nani?"
"na wewe unanijua mimi nani? Alafu kwanza mbona una kihere here, dereva asilalamike ila wewe kajamba nani unaleta mdomo! Gari🚗 yenyewe umepewa Lifti unataka kupiga na honi" 🤣 nyie mimi
"Unasemaje wewe! Nini?" Imran alianza kunisogelea kwa hasira😡
"Stop Imran unataka kufanya nini?" Kaka Dereva Alimuwahi Imran akawa anamtuliza hasira, kidogo akawa amepoa.
"Sorry! Naitwa Fahami!" Kaka dereva alinipa mkono huku mvua inaendelea kunyesha.
"Naitwa Neria" na mimi nikapokea mkoni wake🤝
"Fahami kama umemaliza tuondoke, nishachoka kunyeshewa kisa huyu mwehu" Imran alitukatisha😒
"Okay, Neria mama naomba nikupe lifti" Wee Fahami akaaniita mamaa kwani lifti nili ikataa sasa🤣 nikakubali.
"Bro kama unampakiza huyu mwehu kwenye hii gari mimi sipandi" Imran akaanza kuleta drama🤦♀️.
"usipande kwani umelazimishwa!" nyie mimi huyu na kihere here changu.
Kuna bodaboda ilikua inapita, Imran akaisimamisha akapanda huyoo akaishia, yani jamaa alikua ana nichukia kweli kweli😒.
JE NINI KITAENDELEA?
MIMI NERIA
Sehemu ya : 3
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Tulipoishia......
Kuna bodaboda ilikua inapita, Imran akaisimamisha akapanda huyooo akaishia, yani jamaa alikua ananichukia kweli kweli😒.
Tuendelee......
Fahami akanifungulia mlango nikakaa siti ya mbele, na yeye akapanda akawasha gari tukaondoka.
"Jana Imran alinambia stori yako, alikua ana kuongelea siku nzima kwa hasira😡, nikajua ni demu wake" Fahami aliongea huku akicheka🤣
"weeee nooo! Siwezi kua na yule kichwa kibovu ana roho mbaya sana na makasiriko juu" Basi Fahami akawa anacheka🤣 sana kutokana na majibu yangu.
"ila ugomvi wenu unazidi kua mkubwa wakati ilikua ni kutoelewana kidogo tu ila mnaukuza"
"Mimi sina shida naye ila yeye ndo anazidi kuukuza sana, mfeew"😒
"anyways, Neria unafanya kazi gani?"
"mimi bado nasoma chuo!"
"ohhh nice, unasoma wapi?"
"Arusha"
"mbona uko hu...." kabla Imran hajamalizia sentensi simu📱 yangu ikawa inaita kwenye pochi👝. Nikaitoa ilikua ni mama Getu ananipigia. Nilipopokea akanambia hali ya Mama imezidi kua mbaya kwaiyo wamempeleka hospitali🏥. Aiii nikaanza kulia😭 mbele ya Fahami. Ikabidi jamaa asimamishe kwanza gari aniulize shida nini ndo nikamwambia Mama kazidiwa yupo hospitali🏥.
Basi Fahami akakimbiza gari🚗 mpaka hospitali🏥, kufika namkuta Mama yupo ICU.
"binti lipa haraka tuanze operation" Dokta alinambia
"lakini Dokta bado sijafanikisha kupata kiasi cha hela ila naomba umsaidie mama yangu" nilikua naomba maskini mimi😭
"Namsaidiaje bila operation? Kama huna kiasi cha pesa ulicho agizwa basi nasikitika kukuambia sina msaada zaidi" Dokta aliondoka na kuniacha nimesimama kama mshumaa huku machozi 😭yakizidi kushuka. Mda huo Fahami alikuja maana alikua kaenda kubadilisha zile nguo zilizolowa ndo akanikuta nipo kwenye hali ile. Nilianza kumuhadithia Kuanzia mwanzo mpaka mwisho huku nalia😭 maskini akawa ananionea huruma.
"Neria nina weza kukusaidia" Fahamu alinikazia macho
"kweli?" nilipata tabasamu😊 la ghafla nikafuta mpaka na machozi
"ila na mimi nitaitaji msaada wako"
"unamaana gani Fahami? Kama mwili wangu siwezi kukupa!" niliongea kwa kujiamini😒
"No! No! Sipo ivyo Neria. My God kwanini umefikiria ivyo?"🤦♀️
"Hata kama ni wewe lazima uwaze ivyo!"
"ni jambo kubwa kidogo ila naomba unihaidi baada ya operation na mama yako naomba unisaidie jambo langu Neria please🙏"
"kwaajili ya Mama yangu nipo tayari kufanya kila kitu but naomba tu mama yangu atibiwe kwanza"
"okay" Fahami alichukua simu📱 yake akafanya mawasiliano, mda sio mrefu pesa yote milioni 10 ikawa ishalipwa bila kucheleweshwa.
Mama akapelekwa chumba cha operation sisi tukabaki nje kusubiri, sasa ndo akili ikanijia Je Fahami atataka nini kama malipo ya kumsaidia Mama yangu🙆♀️ mbona nimechukua maamuzi ya kukubali tu pasipo kujua nini nitafanya.
Masaa matano yalipoisha, Daktari akatoka akatupa habari njema kua Mama ametoka kwenye hatari kwa mda ule hali yake ilikua inaendelea vizuri😊 ila hatukuruhusiwa kumuona mpaka kesho yake. Mda wote huo Fahami alikua bega kwa bega na mimi. Alituchukua akaturudisha nyumbani, akashuka Mama Getu na Steve nikawa nimebaki na Fahami kwenye gari🚗.
"Neria!" aliniita
"abee!"
"unakumbuka ahadi yako?"
"ndio!" "Naomba usiache kuitimiza"
"nataka kujua ni nini hasa natakiwa kufanya mbona unaniweka njia panda?"😰
"Ni hivi....... Mimi ni mtoto pekee kwenye familia yetu. Sina Kaka wala Dada, Nina Binamu tu ambaye ni Imran. Kwa mda mrefu sana Mama alikua ana sisitiza nione lakini sina mpango huo. Ameshajaribu kuniletea wanawake wa kila aina"
"Kwanini hutaki kuoa?" nikamkatiza, mimi kwa umbea😅
"unajua ndoa ni process, sio kitu cha mchezo mchezo alafu mpaka now bado sijapata mwanamke atakae nipelekesha!"
"okay endelea..."
"so, ningependa uigize kama mke wangu! Hii ni njia pekee ya kumfanya Mama aache kunifatilia."
Patamuuu apo....... JE NINI KITAENDELEA?
MIMI NERIA
Sehemu ya : 4
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Tulipoishia.........
"so, ningependa uigize kama mke wangu! Hii ni njia pekee ya kumfanya mama aache kunifatilia."
Tuendelee.....
"Mmhhhh" nilivuta pumzi ndefu nikijiuliza kwanini nilikubali tu pasipo kujua jambo lenyewe
"Neria ulikubali please usiniangushe" Fahami aliweka sura ya huzuni😔. Kama kanisaidia bila kusita sita kwanini na mimi nisirudishe asante kwa kukubali jambo lake.
"okay sawa" Fahami alifurahi😊, alinipa laki mbili💵 kisha akanambia atakuja kumuona mama hospitali🏥, akaondoka zake.
Moyoni nikawa najiuliza mbona Imran hayupo kama Fahami yani ni mtu na binamu yake ila Imran ana makasiriko kama nini.
Kesho yake nikawahi hospitali🏥 nikamkuta Mama kashafungua macho jamani🥳, nilishangilia aiiiiiiiiiiiiii. Alikua hawezi kuongea vizuri ila alikua na yeye anafurahi mpaka anatoa machozi.
Alipokuja Fahami nikamtambulisha kwa Mama kama Mchumba wangu. Mama akatabasamu😊 nikajua tu kamkubali Fahami kumbe wenzake tuna igiza.
Siku zilizidi kusonga mbele Mama akawa fresh kabisa akarudi mpaka nyumbani🏠. Siku moja tukiwa tumekaa sebuleni akaanza kuniuliza habari za Fahami.
"Unampenda Fahami?" Mama aliuliza swali ambalo likanifanya nipaliwe na mate, angejua tu mimi na Fahami ni mtu na best ake.
"ndio" nikawa naogopa kumtazama machoni😞
"mbona huonyeshi kama mnapendana, nawaona mpo kama marafiki tu! Una uhakika hamdanganyani?"
"Mama jamani sasa tudanganyane ili iweje. Fahami angekua ana nidanganya angekulipia hela ya operation si ungekuta kashakimbia ila kwa kuonyesha yupo bega kwa bega na mimi ndo maana yupo hadi leo ana vumilia shida zetu" nikawa namdanganya Mama😰
"Sawa kama umesema ivyo!" Jioni Fahami alikuja kunichukua akiwa na furaha sana, alinipa pete💍 nikavaa. Akanichukua kunipeleka nyumbani kwao kwa mara ya kwanza.
"Nimeongea video call na mama nikamwambia nishaoa!"
"Heeee!" nikashtuka😳
"unashangaa nini au ulitaka twende kanisani kabisa tule kiapo mbele yao wakati ni maigizo"
"Hawajakugombeza umeoa bila wao kuwepo?"
"Mama yangu ni mzungu hana shida kabisa. nimemwambia nina mke tayari akasema anataka kukuona kwaiyo apa ndo nakupeleka ukaongee nae kwenye video call"
"Na baba yako?"
"Hana shida na yeye, mwenye shida sana sana ni Mama!"
"Mhh na vipi kuhusu Mama yangu maana anachojua sisi ni wachumba"
"Haina shida, Tutajua baadae cha kufanya kuhusu yeye"
Tulifika kwenye jumba🏠 kwao yanii ni bonge la jumba kweli kweli. Macho yalinitoka kama nimebanwa na mlango.
"Imran kaenda gym kwaiyo ni mda mzuri maana angekuwepo angeharibu kila kitu"
Fahami alinipeleka mpaka chumbani kwake, aliwasha pc💻 yake akampigia Mama yake. Haikupita mda mrefu mama yake akapokea akawa amefurahi kuniona.
"Mwanangu umeoa mke mzuri👌" Mama Fahami alikua ana shangilia
"See! Nilikuambia nipe mda nitakuletea mkwe mwenye viwango" Fahami akaanza kujitapa
"Naona mwanangu! aisee embu nione pete yako Mwali wangu" Nilinyanyua mkono nikamuonyesha pete💍 akazidi kufurahi😊
Niliongea na Mama Fahami kwa mda mrefu mpaka akatosheka kabisa. Tulipomaliza kuongea na Wazazi wa Fahami, nilivua pete💍 nikamrudishia Fahami.
"Asante Neria, kila kitu kimeisha. Mama kashajua nimeoa kwaiyo hata nisumbua tena"
"Woow bora! Nitaenda kumuambia Mama tumeachana kisha nirudi zangu Mbeya kusoma"
"Yeah Asante sana!" Fahami alinikumbatia🫂kunishukuru saa ngapi Baba yenu Imran asiingie na kutukuta.
"woow kwaiyo unamleta huyu mwehu mpaka ndani sio?" Imran alikua kachukia😡
"Koma mimi sio mwehu! Tena unikome"
"siongei na wewe funga domo lako"
"Broo embu cool basi, Neria ni rafiki yangu please muache" Fahami akanitetea
"huo urafiki umeanza lini? Yani kati ya marafiki wote Bongo ukaona huyu ndo rafiki? Kweli hujui kuchagua!" Imran alicheka kwa dharau
"kwanini mimi nipoje mpaka siwezi kua rafiki yake?" nilikua nishaanza kushikwa na huzuni😞
"Haupo level zetu kabisa. Bora hata Fahami, mimi ndo kabisa hata nusu huingii!" Nyie niliumia zaidi na dharau za Imran.
Nilibeba pochi👛 yangu nikatoka nje pasipo hata kufukuzwa😩. Nilichukua boda mpaka nyumbani🏠.
Nimefika Mama akanipokea nikaanza kulia😭.
"unalia nini mwanangu, umeondoka hapa kwa furaha una rudi unalia😭"
"Mama nimeachana na Fahami" nilidanganya ila hicho sicho kilicho kua kina niliza bali maneno ya Imran
"mmeachana?" Mama alishangaa😳
"ndio"😭
"Mbona hii ni nuksi mwanangu! Jamani kwanini" Mama alipatwa na huzuni tayari hakudhani kama ningeweza kuachana na Fahami.
Patamu apo.......
JE NINI KITAENDELEA?
MIMI NERIA
Sehemu ya : 5
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Tulipoishia......
"Mbona hii ni nuksi mwanangu, jamani kwanini?" Mama alipatwa na huzuni tayari hakudhani kama ninge weza kuachana na Fahami.
Tuendelee.....
Basi ile siku ikapita vizuri hatimaye na wiki ikakatika kabisa Mama akawa na huzuni😔 ya uchumba wangu feki kuvunjika wakati mwenzake nilikua nina Full Amani.
Nilianza kujiandaa kurudi chuo na kila kitu nikawa nimepanga ili kesho yake nirudi zangu chuoni. Sasa nikawa kuna vitu baadhi sijanunua, nikawa nimekumbuka usiku ivyo nikaenda dukani.
Wakati narudi niliona gari🚗 ya Fahami nikawa nimepotezea. Kumbe na yeye alikua kaniona, ivyo akarudisha gari🚗 nyuma.
"Daah Neria nilikua nakufata wewe rafiki yangu"
"Mpaka upate shida ndo unitafute, Ndugu yako aliniabisha wewe ukawa tu unamwangalia" nilianza kulalamika😒
"nisamee Neria, panda basi kwenye gari🚗 naomba kuongea na wewe!" Kwakua aliniomba kinyenyekevu nikapanda. Aliegesha gari 🚗 sehemu yenye utulivu ili anieleze shida yake vizuri.
"sijui hata nianzie wapi Neria"
"anzia popote tu!"
"Mama na Baba wanarudi toka Italy🇮🇹"
"mbona hushangilii hujawa miss?"
"Neria acha kujitoa ufahamu basi, umesahau kwamba wewe ni mke wangu feki na lengo la Mama kuja Tanzania🇹🇿 ni kutaka kukuona sasa unafikri asipo kukuta itakuaje?"
"si ulinambia kila kitu tumeshamaliza? Na hivi unavyo ona nimetoka kununua vitu kesho narudi chuo, sidhani kama nitaweza tena kukusaidia wewe mwambie mama yako tumeachana kama mimi nilivyo fanya"
"mhh hapana! Unadhani ingekua rahisi ivyo ningekufata mpaka huku usiku huu? Yanii this time nakuhitaji haswaa uniokoe kwenye hii shida"
"vipi na mimi masomo yangu? siwezi kubaki tena huku Fahami na mama angu akijua je wakati anajua tumeachana na kibaya zaidi anajua sisi tulikua wachumba na sio mke na mume"
"Mama yako haitaji kujua haya yote. Utamwambia unarudi Mbeya lakini utakuja nyumbani🏠 kwangu, na kuhusu chuo utahamia huku Neria nipo tayari kugharamia"
"Heee unataka nidanganye tena? Dah Fahami hapana bhana! Tulikubaliana baada ya operation niigize kama mkeo na nikaigiza tena ukasema tumemalizana! Kwa sasa hapana sitaki kuongeza uongo mwingine"
"Neria nitakulipa pia! nitakupa milioni 10 nyingine please nisaidie rafiki yako🙏" Fahami kwa kutia huruma hajambo, na kama sio kusema milioni 10 hata moyo wangu usinge tetemeka, chezea hela💵 nini
"Na Imran?" "hahahahaha hayupo! Harudi leo wala kesho kwaiyo hakuna kikwazo" Basi nikawa nimekubali ombi la Fahami.
Alinirudisha nyumbani🏠 nikamalizia kujiandaa ila kichwani najua kabisa siendi chuo. Kesho yake asubuhi, Mama akanisindikiza mpaka stand, akahakikisha nimepanda basi🚌
"mwanangu usome! si unaona hali yangu jinsi ilivyo? Hakikisha unasoma kweli kweli"
"Sawa Mama" Alinikumbatia akanikiss💋 mwanae, kisha akashuka akawa ana angalia basi linavyo ondoka stendi.
Basi🚌 lilivyo fika mbele kidogo nikashuka, nikamkuta Fahami ananisubiri, nikapakia haoo tukaondoka. Alinifikisha mpaka nyumbani🏠 , nikashusha virago vyangu mpaka chumbani. Ila mwenzenu moyo ukawa unanisuta ile mbaya acheni tu.
Yani mama anajua upo chuo unasoma kumbe mtu hata safari hukuanza ulishukia njiani🤦♀️. Mimi na Fahami tulifanya maandalizi, wazazi wake wakawa wamerudi kutoka Italy🇮🇹.
Mama Fahami alikua ana nipenda huyo. Kwanza alikuja na zawadi za kila aina kwa ajili ya mkwe wake nikawa nasema siku akijua ukweli sijui itakuaje. Na mimi sikua nyuma dada yenu nikawa naigiza kama mke bora kwa Fahami yani kila mtu alie tuona alisema Kapo sindo hii sasa yani burudani🤣.
Mbali na hayo yote, Fahami aliniamishia chuo cha Dar, nikawa namalizia degree yangu ya uhasibu bila shida yoyote ila kumbukeni Mama yangu anajua mwanae nipo Mbeya🤣🤣. Mwezi ulipoisha nikawa nimemaliza chuo, nikapata degree yangu, Mama Fahami akawa kanifanyia party ya kunipongeza.
"Mwanangu kwaiyo hautaki kabisa kurudi nyumbani" Mama alilalamika baada ya kupokea simu📱 yake apo bado party inaendelea
"Sio ivyo Mama, ni kwamba nimepata kazi huku tena mshahara ni mkubwa sana, please naomba niache nifanye kazi huku kwa siku chache alafu nitarudi"
"Kama ndo ivyo, Mungu akutangulie mwanangu natamani ningekuja kwenye mahafali yako"
"usijali Mama"
"Sawa mwanangu" Nilimaliza kuongea na Mama roho ikawa inaniuma💔, ila ndo ivyo milioni kumi bado naitaka sana.
JE NINI KITAENDELEA?
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi