MJEDA INAUMA SIWEZI VUMILIA* *SEHEMU YA 1 na 2 "Hebu wewe harakisha basi yaani wewe sijui utakuwa lini yaani jamani dah, hasara hizi jamani watu wanazaa watoto wengine tunazaa magugu maji"
"Sawa harakisha wewe jamani , mhh tupatage sisi hata chochote kitu jamni wewe mtoto sijui upoje yaani muda wote wewe unajiandaa tu mhhh hapana " Mama alizidi kuongea jamani "Mama jamani nakuja mimi unataka niende huko kama vile mtumishi naenda ushuani ujue wee haya huko" nilisema " wee bwana wee hebu harakisha hukoo mwenzio anakusubiri bhana , mimi mwenyew nataka zangu niwahi nikafunguwe hako kamgahawa nipate hata hivyoo vimiambili miambili vya kuendesha maisha" mama alikuwa ana kimgahawa chake ambacho kinampa vimia mbili mia mbili "sawa mama natoka naenda mimi jamani" nilitoka nimevaa zangu kisuruali changu pambee balaa kilijua kunikamata ilikuwa ni cargo na shati moja hii tunayo sare mimi na Aika ndio tulipanga tuvae. Nikavaa na kimtandio changu jamani mhh hapana nilijuaa kupendeza na jinsi nina shepu dodo nilinoga hatarii na kimtandioo kilikaa mahala pake jamani , na vipoda poda kwa mbali
"Haya shangingi langu sasa lishapendezaa hapo linajiona lenyewe ndioo top in town , mwanamke mzima hata mchumba wa kusingiziwa huna dash ila wewe jamani hapana" nilimtizama sana maan alikuwa anaongea ukweli sina hata wa dawa jamani huyu mama hapana mara simu yangu ikaita alikuwa ni Aika anapiga
Aika: hivi unajua kama huku tunakusubiri ni wewe tu?
Me: sawa nakuja nishajiandaaa jamani
Aika: haya chukua hyo boda ntalipia mimi sawa kipenzii?
Me:Jamani tajir wangu hapo pekee ndipo ninapokukubal mhhh haya nafika hapo chap shga angu
"Mama baadae tutaonana shga anguu byee" nulimuaga mama angu , maan nikichelewa hata dakika kumi akuu ntamkwaza rafiki yangu maan ni makasiriko isivyo kawaida
"Haya nirudiee maa usiku hapa utalala njee , me sitaki upuuzi kabisaa kwangu , uwahi tu kurudi na utapitia pale funguoo sawa na kam itatokea emergency ya wewe kulala huko huko kwa akina Aika uniambie mapema sawa?" Nilijibu sawa huku naondoka niliita boda boda maana nilikuwa nina namba yake..
Itaendeleaa......π₯
Ep 02
Nilifika salama tu nikamkuta tayari yeye na kaka yake washajiandaa nilifika getini nikampigia simu akaja kunikaribisha akalipia na nauli tukaanza kupiga story sema huyu ni ana asili ya kujishauaa sana siunajua watu wenye nazo jamani sisi wasafisha njia tukae kimya tuu , maana tunakuwaga tunajisifiaa na kujichangasha ila hawa sasa wenye nazo wanaishia tu kutudharau maan mhhh ni hatari na nusu , ila tunavumilia maan mimi nishamzoea
"Jamani Rahma umechelewa wenzio wamekusubiria kitamboo ujueee?" Alikuwa ni mam yake na Aika "Jamani mama shikamoo , mama yangu mhh nilichelewa si unajua tena kujiandaa kwetu mhh hatunaga hata cha haraka haraka" nilimjibu kwa heshima na mama yake na Aika alikiwa ananipenda sana , maan alikuwa anasema eti nina adaabu na mchangamfuu sana , ndioo maana nimeweza kuwezana na Aika japo yeye kashafikaga chuoo na yupo chuo sasa mpaka sas na leo ilikuwa ni weekend tu " marahaba mwanangu , mhhh ila nyiee nao kama mnaenda kwenye party kumbee ni hapo tu kurefresh mind tu jaman haya , muwahi sasa ili muwahi kurudi sasa" niliitika tu
"Haya mrembo wangu umependeza ila jamani maneno yote haya nimemaliza hata kukuambiaa hongera zako sijakwambiaa umependeza sana mama yangu" nilitabasamu tuu nilipenda jinsi alinisifiaa jamni na vile ninavyopenda sifa sasaa kha " asante mama" nilisema huku nacheka alidakia Aika " mimi sasa cheusi nisifiwe niotee meno ya dhahabu , wanasifiwa wenye rangi tuu haya tuondokee" alisema Aika , yaaani kinginee ni ana wivu huyu jamani hapana yaana hata shule nililkuwa ikimshinda maksi anavyolalalmika jamani utasema kashindwa nini yaani hapana " mbona na wewe umependeza sana, tena hata kunizidi jamni shga anguu Aika " nikamtizama huku nampandishiaa nyusi , alitabasamu tuu akanitizam " haya twendeni sasa warenbo wangu wazuri wazuri sawa" alisema kaka yake anaitwa Swaleh , yeye ni mchangamfu mnoo afuu mzuri kuliko hata dada yake mishauoo ,ni mwnajeshi kam rafiki yake tunaeenda kumuona
"Haya muwahi kurudi sasa sawa eeh?" Alisema mam yake na Aika na tukaondoka tulipanda gari la kaka yake Aika hapo , maan kaka yake Aika ana kaa kwake ila leo alikuja kutembeaa kwao coz ilikuwa ni weekend na ndio ikatokea huoo mtoko sasa tukaondoka hadi kwa rafiki yake na kaka Swaleh, namuita kaka coz ni kaka wa rafiki yangu
Tulifika tukapokelewa jamani hii nyumba ni nzurii mhhh hapana yaani ni nzuri kuliko hata ya kaka yake na bi shgaaa hapa mama kupenda kusifiwa mhhh nilipapenda buree huku ndani full ac , jamani , kwanza njee kuna swimming pool na kulikuwa na wafanyakazi watatu mule ndani yaani inshort ni pazuri mnoo palikua ni ghorofa moja mhhh ni pazuri ,yaani ningekuwa na simu kubwa ningeparekodi kabisa ila ndio hivyoo kiswaswadu gang wenzangu ni wana kazi ya kujiphotoaa tuu , nilitamani ila sikuoneshaa kabisaa...JE NINI KItaendelea....π₯
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
