VYOTE NDANI GONGA94
MR GENERAL : KUMBE ULINIPENDA EEE SEHEMU YA 7
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Sijui ni kwanini maneno yake yaliniumiza sana, nilijua kuwa amefanya ya kufanya kwa sababu ananipenda sana, kumbe anajifanya kuwa alikuwa ananisaidia, sikuwa nataka kusaidiwa kabisa mimi, ila nilikuwa nataka anipende ili nikatambishie watu ambao walijua nitakuja kuteseka, na pia kwa sababu moyo wangu ulikuwa unamuhitaji sana….
“Kwanza sikukuomba unisaidie, nilikuwa nimeridhika kabisa kuolewa na Yule mzee, kwanza anamvuto sana, nina uhakika ningezaa vitoto vizuri sana, na kingine umesema kuwa umenisaidia kwa sababu unataman nije kuolewa na mwanaume ambae namtaka, basi mwanaume ninae mtaka ni mjeda sio wewe kwanza, anakaa huko mtaani kwetu, nikajibu kwa kujiamin, nikashangaa mwamba amenywea kama amemwagiwa maji vile kisha akaondoka zake…
Kumbe hapo amejaa sumu balaa, yaan alikuwa na hasira kiasi kwamba hata hakulala nyumban, roho ilikuwa inaniuma sana, maana nilikuwa nampenda sana, ila nilimuona kama ana madharau flani hivi, nikataka kama kuyakomesha yale madharau yake na kutengeneza heshima yangu binafsi…
Maisha yakawa yanaendelea kama kawaida, alikuwa ananipa kila kitu, yaan nikisema kila kitu namaanisha, ila hakuwa ana muda na mimi kabisa, nilikuwa najisikia vibaya sana, na kuanza kujilaumu kwa mdomo wangu mrefu, huenda labda mwenyezi Mungu alipanga aje kuwa mume wangu, ila nilivyo na bichwa bovu maskin ya Mungu nimeshaharibu kila kitu mimi…
Nilipendeza nikanawiri, shangazi alikuwa ananipigia simu sana akitaka nirudishe gharama za watu za harusi ety Yule baba anamdai, nikawa hata sipokei simu zake wala kujibu sms zake, niliona kama anataka kunipa stress na wakati nilikuwa nakula kuku kwa mrija huku…
Mwisho nikamblock kabisa asiniletee utani, sasa kwa kipindi chote hicho ambacho nilikuwa naishi na mjeda sikuwah hata mara moja kumuuliza jina lake, tulikuwa hatupigi story wala kuonge kitu chochote kile yaan alikuwa hata akinikuta nimekaa ukumbin basi anapitiliza zake ndani moja kwa moja…
Kweli nilinawiri na kupendeza sana, ila nilikuwa nina upweke wa hali ya juu, nilikuwa najihisi mpweke kuliko kawaida yaan, siku moja nilimfata na kuomba kuongea nae…
“Unataka nini?..
“Kwanini tusikae hata tupige story hata kidogo, yaan tupo wawili tu humu ndani na kila mtu anaishi maisha yake, na jambo la kushangaza hata jina sikujui, kweli, nikaanza kulalamika…
Akarudi na kunigeukia kisha akasema
“Ulisema kuwa kuna mwanaume ambae unampenda, sasa kwanini usingeenda kukaa na huyu mwanaume unaempenda na uachana na mimi, nitakulisha maana nimekuwa kama malaika kwenye maisha yako, ila siwez kukugusa tena, kisha akaondoka zake…
Yale maneno yake yalinifanya nijisikie vibaya sana, na nikasahau kama mimi ndio nimesababisha yote hayo…
Niliingia ndani na kujifungia kisha nikaanza kujiuliza ananichukuliaje huyu, yaan anaishi na mwanamke nyumba nzima kama anaishi na mwanaume mwenzake, ngoja nitamfundisha adabu..
Kesho yake nikaamka mapema sana, ila hata sikumkuta ukumbin, mara akaingia ndani kana kwamba kuna kitu anaenda kuchukua, kisha akatoka na kunambia
“Sitakuwepo kwa mwezi mzima, hela zipo kwenye kabati la vyombo na nina uhakika kila kitu kipo vizuri, kisha akaanza kuondoka zake..
Nikajikuta nimeropoka na kusema “Asante Mungu, aisee alinigeukia na kunikata jicho kisha na yeye akaondoka zake..
ITAENDELEA …
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi mr-general-kumbe-ulinipenda-eee-sehemu-ya