VYOTE NDANI GONGA94
MR GENERAL : KUMBE ULINIPENDA EEE SEHEMU YA 9
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Kwa upande mmoja nikahisi ni mchezo, ila kwa upande mwingine nikahisi ni kweli, huyo Bosco alikuwa ni rafiki yangu sana, sasa akazamiaga meli akaenda south Africa, na ile kiutoto utoto akanambia kuwa anaenda kutafuta maisha atarudi baada ya muda flani kunichukua nikaishi nae, akaenda kweli, nani miaka kama minne, sikuwah kumuona wala kumsikia, hivyo kuna namna nafsi yangu ikaanza kupata mashaka, nikajiambia kuwa kukipambazuka nitaenda.
Kweli kumekucha nikanywa chai, kisha nikawa naangaza angaza kuangalia kama kaka mjeda yupo ila sikumuona, nikasema labda ameenda kwenye mambo yake, nikaona nimtumie sms ili asije akaanza kunihoji maswala yake na kunifokea fokea, nikatuma sms kuwa “Natoka na naweza kuchelewa kurudi, nimeona nitoe taarifa, kisha nikaingia zangu chumban kujiandaa…
Sasa wakati natoka nikawa nasikia harufu ya manukato, ila sikujali sana, wakati nafika nje nikasikia,
“Panda kwenye gari nikupeleke..
“Kaka mjeda unataka kunipeleka wapi, kwani unajua ninapoenda…
“Nimesema panda kwenye gari nikupeleke laa sivyo rudi ndani ukalale na hautotoka hapa mpaka nitake, akaendelea kusema nikaona bora nisi hangaike na kubishana nae, nikapanda kwenye gari kisha tukaanza safar, nikamuambia naenda kwa shangazi, basi akanipeleka, sasa ile nafika tu nakutana na Bosco ndio ametoka kwa shangazi, nilishindwa kujizuia na kwenda kumkumbatia kwa nguvu, sio siri nilikuwa nimemkumbuka sana…
Tukabaki tukiwa tumekumbatiana kwa takriban dakika mbili, kisha akaniachia akaanza kuniangalia sana, kumbe huku kaka mjeda anajaa sumu, anataka kuleta vurugu ila hata hajui anaanzia wapi kuleta hizo fujo…
Basi bibi mimi nikawa najiachia zangu na Bosco, sikuwa nataka hata kwenda kumsalimia shangazi yangu, maana nikimuonaga nashikwaga na hasira balaa, kwa mambo ambayo ameshawah kunifanyia, ila Bosco akasisitiza sana nikamuone, basi nikaingia ndani, nikakuta kila kitu kimevurugika, hakufai, alikuwa anaumwa sana, nikajua kuwa nimeitwa kwa sababu shangazi anaumwa…
Nikamuangalia Bosco, akaniambia
“Msamehe shangazi yako na umsaidie walau kidogo maana anayopitia ni makubwa sna…
Sikumjibu, nikafanya usafi, kisha nikapika na kumuuliza ana shida gani, akanambia kuwa anahitaji pesa ya matibabu kama laki mbili tu, basi Bosco akasema kuwa atampa shangazi, na wakti wote huo mjeda amekaa zake kwenye gari hajatoka, mpaka nikaenda kumpelekea chakula, akaniangalia kisha akatabasamu na kusema asante…
Baaadae nikaenda kufata sahani, Bosco akaniuliza kwanini nilipeleka sahani kwenye gari, nikamuambia nimekuja na boss wangu Bosco akataka walau akamsalimie, nikaenda kumpeleka, aisee mjeda alimkata jicho kisha akasema “ Happiness kama umeshamaliza kilichokuleta hapa naomba tuondoke…
“Leo mimi siondoki nalala hapa, nikasema kwa sauti ya kujiamin, aisee mjeda akafunga vioo kisha akawasha gari na kuondoka zake…
Kumbe alikuwa anaondoka lakin akili haikai kabisa, hakufika mbali akarudi, maana ni kama nafsi yake ilikataa kuniacha nikae na Bosco, sasa wakati anakuja akatukuta tunaongea tukiwa tunaangaliana, aisee nilishangaa nabebwa taksi bega kisha akaniingiza kwenye gari, ikabidi Bosco aingilie na kusema “ Wewe ni boss wake tu, kwanini unajifanya kama mume wake…
Mjeda akacheka kisha akasema “Amekudanganya mimi ni mume wake, so ukiendelea kuchekeana na mke wangu utanijua mimi ni nani, kisha akapanda kwenye gari na kuliwasha kwa hasira na kuanza kuondoka…
Yaan tumefika nyumban nilijuta kukutana na Bosco aisee…
ITAENDELEA …………….
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi mr-general-kumbe-ulinipenda-eee-sehemu-ya