VYOTE NDANI GONGA94
MY TRUE LOVE STORY SEHEMU YA 1
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Ni mwaka 1997 ndio mwaka niliokuwa naanza darasa la kwanza katika kijiji cha nduruma, shule ya msingi mlangarini..
Nilikuwa natoka kwenye familia yenye uafadhali wa maisha kidogo pale kijijini, kwa sababu kwanza nilienda shuleni nikiwa nina nguo za shule zote, na viatu vyeusi ambavyo vilikuwa vimepigwa kiwi vizuri na guo yangu ya shule iliyopasiwa kwenye pasi ya mkaa…
Ingawa tulikuwa bado tunaishi kwenye nyumba ya udongo, ila angalau nyumban kwetu kulikuwa na solar, hivyo ndio nyumba pekee ambayo ilikuwa inawaka taa tena vizuri sana, kuna baadhi ya watu wakawa wanatuita matajiri, kwa sababu baba ilikuwa kila jumapili analeta jenerator analiwasha kisha wanakijiji wanakuja kuangalia tamthili, kwa kipindi hicho zilikuwa zile za kina muhogo mchungu na mama kai za Itv, na matangazo yaliokuwa yanapita ni yale ya jambo, yaan watoto wa kijiji kizima nyimbo zao kuu zilikuwa ni chai jaba kikombe cha ubora, na ile ya mimi naitwa jambo kubwa, na wewe je, mimi naitwa jambo ndogo na wewe je, mimi naitwa jambo kati kati, yaan hizo nyimbo mbili zilikuwa kama nyimbo za kijiji na ulikuwa usipozijua unaonekana mshamba kwa sababu hauangaliag tv, yaan mpaka wale ambao hawakuwa wanakuja nyumban kwetu iliwalazimu kushika hizo nyimbo ili wasije kuchekwa na watoto wenzao..
Sasa Wakati naanza kusoma darasa la kwanza , kuna mwanafunzi wa kiume alikuwa anatoka kijiji jirani, alikuwa anaonekana kama anatoka kwenye maisha duni kuliko hata ambayo nilikuwa natoka mimi, kwa sababu sisi tunaanza la kwanza na viatu, angalau kidogo wasafi, ila yeye alikuwa anakuja peku…
Alikuwa mchangamfu sana, na kila mtu pale darasan alimpenda, licha ya kuwa na maisha duni, ila alihakikisha kuwa kila aliekuwa karibu yake ni lazima awe na furaha, alikuwa anaitwa omary ..
Katika kipindi kifupi toka tumeanza shule, tulijikuta tunakuwa marafiki wakubwa sana na omary kutokana na uchangamfu wake na upendo wake kwa watu wengine na adabu aliokuwa nayo kutoka kwa mkubwa na mdogo, yaan kila ambae alikaa karibu nae alijihisi amani na furaha ya kweli…
Nilikuwa naumia anavyotembea peku, zile hela zangu ambazo nilikuwa napewa kwa ajili ya kula shule, na wakati huo nilikuwa napewa shilling 50, nilikuwa sili, naweka mpaka ikajaga kufika shilling 750 kwa enzi hizo nikamnunulia viatu…
Yaan alilia kwa uchungu na kunambia hakika zinura sitakaa nikusahau kwenye maisha yangu yote..
Miaka ikaenda na sisi tukawa tunaendelea kukuwa kama kawaida, hatimae tukamaliza elimu ya msingi na urafiki wetu ukakuwa zaidi, na tukaanza kujihisi wenyewe kuwa hatukuwa na hisia za kawaida bali tulishaanza kutengeneza hisia za mapenzi kati yetu…
Hatukuwa na uhakika kwa sababu ya umri kuwa mdogo ila binafsi nilianza kujisikia vibayua kila nikiona ameongea na mwanafunzi wa kike, au mtu yoyote Yule wa kike, nay eye vile vile hakuwa anapenda kunona hata nikimsalimia mwanaume kwa bahati mbaya…
Miaka ikaenda, tukaanza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya mlangarini, na mwaka ambao tulianza kidato cha kwanza ndio mwaka ambao nilivunja ungo, hivyo nikaanza kupendeza, kangozi kakaanza kuteleza, hips na tutako tukaanza kutoka, mvuto ukaanza kunijia, nikawa ni binti mwenye mvuto mno, nadhan katika shule ya mlangarin mimi ndio nilikuwa binti mrembo kuliko mabinti wote pale, na wivu kwa omary ndio ukazidi mara dufu, maana mara kadhaa alikuwa akinikuta naongea na mwanaume atanuna balaa…
Basi maisha yakaenda, na namshkuru Mungu mapenzi yetu yalikuwa ni yakuhamasishana kwenye mambo mazuri, na kusema ukweli pale shuleni sikuwa na rafiki wa kweli zaidi ya omari, kwa sababu nilitembea nae kila mahali, na hakuwah kutaka nikae pekee yangu kama yupo shuleni, na tukawa tunafundishana na hata waliokuwa wanatuona tupo karibu ni wanafunzi wenzetu walikuwa wanatufikiria vibaya ila watu wengine wote walikuwa wanadhan tulikuwa na ukaribu wa kusoma tu maana matokeo yalijieleza vyema…
Miaka ikaenda na hatimae tukaingia kidato cha nne mimi na omari wangu, na tulisoma mchepuo mmoja, na masomo sawa, hivyo tulikuwa tunakaa pamoja mpaka darasani, na tulikuwa tunakaa mbele kabisa yaan…
Nilivyofika kidato cha nne ndio kama uzuri wangu ulizidi mara dufu, usumbufu haukuwa wa kawaida, na wale vijana wa babe wa shule na mtaani wakaanza kumtishia omari kuwa akae mbali na mimi, ila haikuwa rahisi, kwa sababu kwa namna nilivyokuwa nampenda kukaa mbali na omari wangu ilikuwa kama adhabu kali sana yenye kuumiza vibaya sana…
Maneno na vitisho vya watu havikuwah kututeteresha hata kwa bahati mbaya, bali ndio kama vilizidi kutupa nguvu na kuchochea kwa kasi moto wa penzi letu, kwa sababu hatukutishiana hata kwa utani kuachana na omari wangu…
Maisha yakawa yanaendelea kama kawaida, na siku ya mahafali ya kuhitimu kidato cha nne ikafika, wazaz wa omari hawakuwa na uwezo wa kumfantia mahafali, ila nikakubali tufanye pamoja, na kwwa kuwa familia yangu ilikuwa inajua kuwa tulikuwa ni marafiki tu wa kawaida hakuna mtu hata mmoja ambae alishangaa…
Sasa kama tunavyojua mambo ya mahafali, kuna muda wa kucheza mziki ukafika, kuna muhuni mmoja wa pale kijiji akanifata na kutaka kucheza na mimi, nikakata akanilazimisha sana ila nikamsukuma huko na kumfata omari na kumueleza kilichonikuta…
Omary akanishika mkono kisha tukasogea pemben kidogo na shule, sehemu moja ambayo kulikuwa na mto nduruma, tukawa tumekaa kule mtoni tunapiga zetu story, na omary akawa ananiapia kuwa akija kufanikiwa atanijengea nyumba kubwa sana, na kuninunulia gari, anaamin atakuwa tajiri sana baadae na utajiri wake utakuwa ndio utajiri wangu…
Nilikubali maana ni kawaida yake kutoa ahadi kila siku na sikujua ni lini hizo ahadi zitaanza kutekelezwa…
Basi tukakaa hapo mtoni mpaka kagiza kalipoanza kuingia, tukaona turudi zetu nyumban, ila wakati tunajiinua maana tulikuwa tumekaa chini, tukasikia sauti inasema “ hawa huku…
Mara tukashangaa tunaona kundi la wahuni, walikuwa kama kumi hivi, wote nawajua ni vijana wa mtaani tu, basi wakaja mpaka tulipo, walimpiga sana omari, kisha wakaanza kuniingilia kwa fujo, mungu anisaidie mimi…’
Yaan vijana wote walinifanyia huo ukatili, sitaki kuamin kama usichana wangu ndio ulikuwa unatolewa kikatili namna ile, nilipiga kelele sana ila waliniweka mavitambaa mdomoni ili nisiweze kupiga kelele, na nikimuangalia omari kwa namna alivyochapika hakuwa anaweza kufanya jambo lolote lile zaidi ya kupepesa macho tu…
Alikuwa anaonekana kuumia sana kwa kitendo ambacho nilikuwa nafanyiwa, mpaka akawa anajikuta anatokwa na machozi bila kutegemea…
Wale ambao walimaliza kunifanyia ukatili wakamshika omari na kwenda kumtupa kwenye mto nduruma, na kipindi hicho kilikuwa ni kipindi cha mvua, hivyo mto ulikuwa umejaa, nikawa naona mwili wa omari wangu ukiwa unaenda na maji, nikajikuta nimepoteza fahamu
NAKUJA
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi my-true-love-story-sehemu-ya
