REAL LOVE* Chapter 8
machozi yalimtoka kwelikweli daktari alimuonea sana huruma, seven aliliona hilo lakini ndo hakuwa na jinsi aliwaza sana afanye nini ili aeleweke kwa binti huyo,
daktari alimaliza kumpima kisha akampa pole fahima na kumwambia yuko sawa ila kinachotakiwa ni uangalizi na kutumia dawa
vizuri kidonda kitatakiwa kisafishwe kila baada
ya siku moja, kwahiyo ni mawili abaki hapo au aende nyumbani baada ya siku moja awe anakuja kusafishwa lakini seven akamwambia daktari nibora kwanza abaki mpaka kidonda kitakapopona kabisa fahima hakupendezwa kabisa na majibu hayo ndipo seven akawaomba wamuache wazungumze na fahima basi wakatoka na kumuacha
seven alisogea na kukaa karibu na binti fahima lakini binti hakutaka hata kumuangalia akageukia pembeni huku machozi yakimtoka, seven alishindwa kujizuia mtoto wa kiume akaanza kulia alilia nyie fahima ikabidi anyamanze na kuanza kumshangaa analia nini,
samahani dada yangu sijui nikuambieje ili unielewe ila samahani naomba unisamehe sana nakuomba unisamehe kwasasa naomba upone kwanza halafu mengine tutaongea tu alisema
seven huku akifuta machozi
sihitaji kukaa hapa nataka kwenda nyumbani nahisi baba atakuwa ananitafuta fahima binti mpole na mzuri sana alisema
"hata mimi natamani utoke hapa lakini nahofia hali yako bado haukp sawa nipe namba ya baba
yako nisingizie ulipata ajali awe anakuja tu kukuona hapa hospitari aliserna seve
navipi kuhusu bili alisema fahima
hilo usijari maana hii ni hospitari yangu usijari inakila kitu kuwa na amani alisema seven
unajuwa nimepoteza vingi sana biashara simu pochi hela yani kiukweli nishakusamehe kabisa lakini sitaki kukuona machoni mwangu hata kwa
sekunde sifuri alisema fahima daaah kauli
hiyo ilimchoma sana seven alijuta kwanini alikutana na cathe kwasababau yeye ndio chanzo cha matatizo yote
najuwa hilo ndomana nikakuomba msamaha hata ningekuwa mimi nisingekuelewa kirahisi
nitalipia fidia zote zilizopotea lakini nilitamani kupata kwanza namba ya mzee na kujuw jina lako alisema seven akijikaza tu ila ndni ya
moyo wake aliumia sana, basi ikabidi fahima
amtajie namba ya baba yake ambayo aliikariri
kichwani, kisha seven akaipiga namba hiyo
wakati huo baba fahima alikuwa anatoka chooni
kuoga ili ajlandae kwenda polisi kutoa taarifa ya kupotelewa na mwanae ndipo aliposikia simu yake inalta akachanganya miguu haraka па kwenda kuipokea simu bila hata kuangalla.
mpigaji nani
hellow aliipokea simu
"shikamoo baba alisalimia kwa heshma sana seven
marhaba bado sijaifahamu sauti yako alisema baba fahima
usijan baba bila shaka wewe ndiye baba yake fahima alisema seven, kauli hiyo ilimshtua sana mzee fahad akahisi huwenda mwanae
atakuwa amepata tatizo alipata wasiwasi sana
oo mimi alisema baba fahima
samahani mzee wangu mimi naitwa seven
nilimgonga na gari fahima kwa bahati mbaya.
sana hakuumia sana ila kwasasa yupo hospitar
salama kabisa na atawekewa uangalizi na
kutibiwa vizuri mpaka atakapopona mnaweza
kuja kumuona alisema seven kwa kujiamnini sana, mzee fahad alishusha pumzi ndefu alishtuliwa sana na taarifa hizo lakini alipata amani baada ya kusikia mwanae yupo katika hali
nzuri sana,
sawa yupo hospitari gani alisema mzee
fahad
"kigamboni ya private kituo cha kwanza alisema seven
sawa nakuja sasahivi alisema mzee fahad na haraka akaanza kuvaa nguo akabeba shati na kuliweka begani akatoka haraka na kumpita
mama fatuma bila kumsemesha kitu, mama fatuma alimshangaa sana ananini mbona haraka hivyo kisha akabinua mdomo wake na
kuendelea kufua nguo,
katika hospitari ambayo walilazwa mama seven
na selina hatimae waliamka na kupimwa vipimo vyote kabisa waliruhusiwa kurudi nyumbani
kwakuwa hawakuwa na hali mbaya sana, basi sarañna pamoja na ndugu wengine wakafanya
jitihada za kuondoka hapo huku wakimtaarifu seven,
upande mwingine walionekana catherine na devi pamoja na mkaka mwingine smart aliyevalla mavazi safi kabisa, wakiwa hotel wanapata
vinywaji
"kwahiyo mr sanju utaweza kabisa kutusaidia
aliserna devi
kahisa hilo ondoeni shaka nitawasaidia mimi
seven ni rafiki yangu mkubwa sana tena tunaongea mambo ya kiutuuzima kwahiyo swala
hilo litaenda vizuri sana alisema mi sanju,
huyu alikuwa ni mwanasheria wa seven ambaye
aliaminika sana na kufanya vizuri leo hii anamsaliti seven kwasababu ya pesa tu, wanasemaga pesa shetani
Tunahitaji uhamishe vizuri yani kila kitu mr sanju nakuamini sana tunataka tumiliki kila kitu
kwa halali kabisa tutakuongezea pesa kama ukiifanya kazi hii vizuri alisema catherine mwanadada anaroho mbaya huyu
msijari kuweni na amani mpo na mr sanju nakazi zake hazipindagi hata mara moja
alisema mr sanju kwa kujisifu sana na kujiamini,
walitabasan na kuendelea kupata kinywaji
upande wa mama fatuma alikuwa anaendelea
kufua ndipo fatuma nae akarudi huku anabinua
midomo yake
kulikoni mbona hivo alisema mama fatuma
"yani mama yule agness yule siku yake moja tu
iposiku nitamuendea kikundi kizima tumpige mana kazidi sana mdomo alisema fatuma
agness rafiki wa fahima yule muuza bia
aliuliza mama fatuma
"ndiyo mama yani namuuliza fahima yuko wapi
anatuambia sisi wachawi tu alisema fatuma
The mtoto hana adabu yule sijui kama hajazaliwa chooni yule alisema mama fatuma
siku yake moja tu yaani nitamuonyesha alisema fatuma
"achana nae mtu mwenyewe muuza gongo unafikiri zimo sasa, umepata vipi alluloza
mama fatuma
"kila naemuuliza anasema hajamuona alijibu
fatuma
mh haya alafu baba yake namuona katoka mbio kaondoka sijui wapi alisema mama
fatuma
"mh baba nae utamuweza hebu nikapumzike mie alisema fatuma huku akiingia ndani, na kumuacha mama yake akiendelea kufua
huku hospitari mzee fahad aliwasili na kufika
hadi kwenye wodi aliyolazwa mwanae fahima
alimkuta mwanae akiwa na seven alifurahi sana alisogea na kumkumbatia mzee fahad machozi yalianza kumtoka na fahima nae pia, ndipo
fahad akaamua kutoka nje ya wodi kuwapisha wawe falagha,
pole sana mwanangu alisema baba
fahima
asante baba alijibu fahima huku akifuta
machozi
"kwasasa unaendeleaje aliuliza babayake
naendelea vizuri sana alisema fahima
kilikukuta nini mpaka ukagongwa
aliuliza
baba fahima, ndipo fahima akaanza kutoa
machozi mfululizo
niambie mwanangu usinifiche alisema
babafahima
nilikuwa navuka barabara ndipo nikagongwa ghafla alisema fahima
"sawa lakini nilisikia uliondoka nyumbani huku unalia shida ilikuwa nini alisema baba fahima
hapana baba hakuna hata shida alijibu fahima huku akifuta mavhozi
fahima kama hautaniambia ukwell basi
nitaondoka hapa na hutoniona teeeeena alisema baba fahima kwa uchungu sana, ndipo
fahima machozi yakaanza tena kumtoka hakuwa na jinsi ikabidi amuelezee maisha halisi
anayoishi nyumbani, yani ndo ikawa kwa mara ya kwanza baba fahima anajuwa kama mwanae
anateseja,
nje ya wodi hiyo mlangoni alisimama seven ambaye alisikia kila kitu kilichoongelewa ndani humo aiseeee seven aliumia sana roho ilimuuma sana alijifikiria kumbe kunawatu wanaishi
maisha ya tabu hivi dah hisia zake zilienda mball sana taratiiiiibu machozi yalimtoka
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi