TIPWA TIPWA NA MR MARVEL 1 - - - - - - 5
SEHEMU YA 1
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Kila alipokua akipita mtaani kwao utasikia watu wakimuita tipwa tipwa huku wakimtania, lakini yeye hajali hata kidogo. Karidhika na mwili wake, hana mda wa kuhifadhi maneno ya watu moyoni😒.
Huyu jina lake ni Noela, familia yake hupendelea kumuita Nunu lakini mtaani hujulikana kama tipwa tipwa pro max. Yaani kajazia mpaka kajazia tena. Amezaliwa na kukulia Arusha kwenye familia ya watoto watano huku yeye akiwa mtoto wa nne.
Stori yake inaanza rasmi alipohamia Dar es salaam kwaajili ya chuo. Ilikua ngumu kwake sababu hakuwai kabisa kutoka nje ya mkoa wa Arusha. Na hata ivyo alihofia mno upweke kwa maana baadhi ya watu walikua wakimtenga hata marafiki hakua nao😭
Lakini alipofika huko mambo yalikua tofauti kabisaa, Alipata shosti kindaki kindaki kwa jina la Iris na wakaivana mno, yani alipo Iris humkosi Noela na alipo Noela humkosi Iris. Waliambiana siri hata ambazo hawakuwai kuzisema maana huo ndo urafiki💞
Basi bhana pale chuoni kulikua na kijana mmoja huyo ambae alikua anawakosesha wadada usingizi kwa uhandsome wake. Ukiachana na muonekano, pesa pia alikua nao maana kuanzia uvaaji wake mpaka magari anayo tembelea aisee ni balaa🔥
Jina lake huyu mwamba ni Salmon, mtoto wa engineer mkubwa sana hapa Tanzania. Sasa Noela nae alikua kwenye kundi la wadada wanao zimika na Salmon ila sasa hakua na matumaini ya kua nae. Kwa jinsi Salmon alivyo handsome na yeye alivyo tipwa tipwa, ni ngumu kuwa pamoja.
Kwaiyo mara nyingi alikua akiishia kumuangalia kwa mbali au mda mwingine akipata kaupenyo basi anampiga Salmon picha kisiri siri na ku save kwenye simu yake. Kabla hajalala usiku, anaziangalia weeeh mpaka usingizi unampitia.
Alikua anafanya ivyo mara kwa mara mpaka siku moja Iris akamshtukia.
''na wewe umezimika na Salmon'' Iris alichekaa😂
''hapana..... mimi? akuuu.....'' Noela alikana ila machoni anaonyesha kabisa kafa kaoza hata haelewi somo.
Basi Iris akamvizia na kumyang'anya simu yake, alienda mpaka upande wa picha akakuta picha karibia 60 niza Salmon, apo Noela anaona aibu mpaka kumuangalia Iris machoni hawezi.
''khaaa shosti yangu kweli umekufa umeoza, picha zote hizi?''
''ongea taratibu jamani mpaka watu wasikie?'' Noela alijibu kwa uoga😞
''embu na wewe acha uoga, utaficha mpaka lini? mwambie unavyo hisi''
''ili anitukane sio, wee Iris naona kabisa hunitakii mema''
''unacho ogopa kitu gani?''
''naogopa kuoga mvua ya matusi. Ona kwanza jinsi nilivyo na Salom alivyo, mfano tukiingia kwenye mahusiano hata kutembea wote barabarani itakua ngumu coz nitaonekana kama mama yake wa kambo''😂
''labda nikukumbushe kua mapenzi hayachagui ndugu yangu, shauri yako! we kaa hapo ukinung'unika ukisubiria miujiza''
''acha iwe ivo ivo sitaki aibu ndogo ndogo mimi''
Noela aliridhika kabisa kumuangalia Salmon kwa mbali na sio kumfuata kumuambia anavyo jihisi. Basi bhana siku moja Proffessor aliwaachia kazi ambayo walitakiwa waifanye kwenye makundi, bahati nzuri Noela alipangwa kwenye kundi lenye wanaume watupu akiwemo Salmon🔥.
Yani alifurai sio mchezo maana hatimae angepata nafasi ya kuwa na Salmon kwa ukaribu zaidi. Na Kadri walivyokua kwenye group pamoja ndivyo jinsi walivyo anza kuzoeana. Imagine Wote kwenye group walikua wana m-treat Noela vibaya isipokua Salmon tu. Nadhani ndio sababu ya wao kuzoeana mapema😌.
Basi bhana urafiki ukakolea wakawa mpaka wanatoka pamoja weekend, wanaenda kuangalia movie, kuogelea na mda mwingine shopping. Salmon hakuwai kumfanya Noela ajihisi vibaya kwavile alivyo, sema sasa wasichana pale chuo hawakupenda kabisa urafiki wao💔.
Yani alikua anapitia wakati mgumu sana kama Salmon hayupo, akipita tu wanamsonya, mara wamcheke kuna time alikua anakuta kitanda chake hostel kimemwagiwa maji, akianika nguo kambani anakuta zina matope. Walifanya kila kitu ili wamnyime amani binti wa watu, uzuri Noela hakua akijali😭.
Sasa siku moja Noela akamuambia Iris kua anapanga kumuambia Salmon kuwa anampenda, ajabu ni kwamba Iris alibadilika mno
''unamuambia ya nini? we kausha''
''mmmmh nimevumilia sana nimeshindwa, acha nimuambie tu kama kunikataa anikatae ili niwe na amani''😞
''Noela utaishia kuumia wewe shauri yako, kwani urafiki haukutoshi? unataka na mapenzi juu?''
''acha nijaribu bahati yangu huwezi jua, leo tukitoka namuambia huko huko'' Noela alitabasamu akifungua kabati na kuanza kuchagua nguo za kuvaa.
Apo Iris alikua anamuangalia vibaya mno sababu alikua akimuonea wivu. Japo hakua akionyesha, Iris nae alikua kazimika kwa Salmon, tena roho ilimuuma pale kuona Noela yupo na Salmon karibu mpaka out wanatoka pamoja💔.
Ila kuna kitu kimoja kilichokua kinampa moyo, ni kuwa Salmon hawezi kuingia kwenye mahusiano na tipwa tipwa kama Noela. Kwaiyo alijua wazi lazima jioni Noela arudi akiwa analia sababu atakua amekataliwa, basi akawa anamsubiri kwa hamu ili amcheke. Binti ana roho chachu huyu...😠
Anyways, Kweli jioni Noela akarudi na mazawadi kedekede tena akiwa anatabasamu vibaya mno. Sasa Iris akashangaa imekuaje tena wakati yeye alikua anasubiria vilio
''shosti, mbona tabasamu haliishi? vipi, umefanikiwa'' Iris alianza kuingiwa na wasiwasi
''huwezi amini Iris.........hapa nilipo nina furaha mbayaaaa......uwiiiiiiiiiii nilikua najiuliza nitafika saa ngapi ili nikupe hizi habari'' Noela aliruka ruka🥳
''niambie sasa''
''Salmon kanikubalia! now mimi ni girlfriend wake official'' Noela akamkimbilia Iris akimkumbatia asijue mwenzake moyo unamchoma nusu ya kutoboka! weeeeh
Nakuja.........
SEHEMU YA 2
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
''hongera.....''😠
''mbona kama hujafuraia'' Noela alimshangaa rafiki yake😲
''nina wasiwasi na uyo Salmon. Unajua mimi sitaki kabisa uumie''
''una maana gani Iris?''😲
''nina wajua vijana kama Salmon jinsi walivyo. Noela utalia kama ambulance shauri yako''
''Salmon yupo tofauti sana mbona, hana hayo mambo kabisa''
''vijana mahandsome lazima wana shida mahali usije ukasema sikukuambia'' Iris alikua anajaribu kumtisha tisha Noela ila napo ilishindikana kwaiyo akatoka kwa hasira bila kusema chochote.
Kuna namna Noela mwenyewe akawa hamuelewi rafiki yake kwanini kakasirika. Alishusha pumzi huku akiingia bafuni kuoga baada ya hapo akampigia Salmon simu wakiongea kwa mda mrefu kweli. Si mnajua jinsi gani penzi jipyaa lina motoo? enheeeee ndo ivo ivo....💕.
Basi bhana taarifa zikasambaa chuo kizima kuwa handsome wao ana mahusiano na tipwa tipwa. Kuna waliofurai na kuna waliochukia mno tena walio chukia walikua wengi sana. Kwa kuwakomesha wambea Salmon alikua anatembea na Noela kila mahali wakiwa wameshikana mikono, embu fanya kama unaona nyuso za wanafki zilivyo jaa wivu😂.
Yani penzi lao lilikua tamu kama asali asikuambie mtu. Kila mahali walikua pamoja bila kujali maneno ya watu. Na kwa kipindi cha miezi mitatu waliokua pamoja hawakuwai kukulana zaidi ya ku-kiss na kukumbatiana tu.
Uzuri Salmon alikua muelewa na alikubali kuvumilia mpaka siku ambayo tipwa tipwa wetu angeamua kumtunuku, ukizingatia bado alikua bikra🙈.
Basi bhana mwezi mwingine ukakatika bado wakiwa pamoja, na hiko kipindi ndo kilikua kipindi cha valentines kwaiyo kulichangamka balaa. Hapo sasa Noela akaona kuna haja ya kumtunuku msela kama zawadi ya Valentines
Na kama mnavyojua chochote anacho fanya lazima amshirikishe Iris ili amshauri na ndivyo ivyo alivyo fanya.
''Nini?? Unataka kufanya nae???" Macho yakamtoka Iris😲
"Ndio, sasa nitamnyima mpaka lini?"
"Mmmhhhhh Noela unafika mbali sasa"
"Sifiki mbali Iris, Salmon ni mpenzi wangu kwaiyo ni kitu cha kawaida alafu amekua mvumilivu sana, huoni kama hii zawadi itamfaa zaidi?"
"Sioni! Iyo bikra baki nayo utakuja kumpa mumeo mkisha oana! Kwa sasa tulia binti"🙄
"mimi ndo nisha amua ivyo" Noela alisimamia msimamo wake
"Okay, kwaiyo utafanyaje sasa?"
"Hata sielewi"
"Usijali mimi nina idea, u book hoteli, then upambe icho chumba kwa maua, baloons na mishumaa! Yani chumba kiwe romantic mpaka jamaa apagawe au unaonaje??"
"Woow Iris idea nzuri" Noela alifurai
"Na usijali kuhusu gharama, kila kitu nitashughulikia mimi"
"Ooooohh asante sana Iris!" Walikumbatiana pale pasipo Noela kujua kama shoga ake huyoo kuna jambo kabambe kampangia💔
Kweli Iris alianza maandalizi na siku yenyewe ya Valentines day ilipofika, kila kitu kilikua tayari, kuanzia room hadi mapambo.
"Ushamuambia Sasa Salmon zawadi uliyo muandalia?"
"No! Nataka iwe suprise! Hapa nataka kumuandikia meseji kuwa jioni tunatoka" alijibu Noela
"Nooo!!.. Ilo swala niachie mimi, wewe unatakiwa uende mapema, ukajiandae ili akifika akute mtoto umeiva upo tayari kwa kuliwa! Mimi nitafanya kazi ya kumuambia upo hoteli gani na room namba ngapi"
"Wazo zuri sana ilo"
"Ndio, tangu lini mimi nikakupa wazo baya???........em ngoja kwanza kuna kitu nimesahau kukupa" Iris alisogea mpaka kabatini, akatoa kagauni kekundu kafupi ka kukalia akampa Noela
"Mbona lipo wazi namna hii, yani ukivaa haka unakua uchi kabisa"
"Kheeee! Kwaiyo unataka akija akukute umevaa ile sketi yako ya solo kama muimba Kwaya??? Unatakiwa ujiachie ili kusudi akikuona tu adate! Nikufundishe vitu vingapi Noela? Mbona unanichosha kungwi wako????
"hahahahhhh sawa basi nimekuelewa!"
"Hoteli ni Pacific View room 77, tena naona uwahi sasa ivi ili ukajiandae vizuri na utoe uoga wotee"
"Hakuna shida! Ndo usisahau kumuambia jamani"
"Siwezi sahau" Iris akatabasamu
Basi Noela akajiandaa haraka haraka kisha akaelekea Hotelini. Alipofika alielekezwa room 77 ilipo, akaenda mpaka huko na kukuta pame pendeza sana yani Iris hakumuangusha hata kidogo. Kwa mbali alikua na hofu akijiuliza je anafanya jambo sahihi ama ni mapenzi yanampelekesha??🤔
"Sina namna, inabidi nimpe tu nisije kusalitiwa bureee" alijiambia huku akielekea bafuni kwenda kuvaa kale kagauni alichopewa na Iris.
Upande wa Iris alitakiwa amuambie Salmon kua Noela kamuandalia suprise ivyo aende Pacific View hotel, room no 77, badala yake alimtajia hoteli tofauti kabisa na hoteli ambayo Noela alikuwepo. Alimtajia D & D hotel, room no 17. Mnaona mambo hayooooo........
Yani ni bora Noela angemuambia Salmon mwenyewe kuliko kumuamini huyu shetani Iris💔
Em kwanza nakuja................
SEHEMU YA 3
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Baada ya kuvaa kale kagauni Noela alijitazama kwenye kioo kuona jinsi gani alivyo noga vibaya mno. Alijua kabisa hapa, Salmon hachomoki hata kidogo. Alipomaliza kujitazama alirudi chumbani na kuangalia saa, ilikuaa saa mbili usiku.
Mda huo Salmon alipaswa kuwa kashafika ika bado hakuona mtu. Akaamua kutulia kidogo huenda jamaa yupo kwenye foleni asijue kuwa Salmon ndo kashafika D & D akiwa hana hili wala lile😞
Yeye aliambiwa akifika pale aulize room no 17 na kweli akaulizia na kuelekezwa ilipo. Taratibu akatembea hadi chumba namba 17, alipofika akagonga mlango. Hakukaa sana mlango ukafunguliwa na Iris akiwa kajifunga kataulo kafupiii mno, sijui nika mtoto kale??
Salmon akatoa macho akiwa haamini anacho kiona vile😲
"Iris..... Unafanya nini hapa???..... Noela yupo wapi!?"
"Noela wa nini wakati mimi ndo nilie kuita hapa???.... Em njooo huku bhana" Iris alimkamata Salmon na kumuingiza ndani kwa nguvu
"Iris ni nini unafanya??" Macho yalimtoka Salmon😲
"We kwani unaona nafanya nini???? Acha utoto basi......mimi mwenzio nakutaka ama we huoni! Tena najua hata wewe unanitaka pia maana kuna namna hua unaniangalia"
"Kabla sijakujibu Noela yupo wapi?"
"Yupo hoteli nyingine kabisa hata hajui hata kama nimelichezea mchezo"🙄
"kwaiyo hapa tupo wawili tu?" Salmon akamsogelea Iris na kumvutia kifuani kwake bila aibu. Alishaanza kumtamani Iris kitambo sana na Noela hakua akijua ilo
"Taratibu basi jamani nitadondosha taulo....." Noela alilegeza sauti
"Itakua unyama sana kama likidondoka mamaa, wewe ni mzuri sanaaa aiseee"
"Mzuri kushinda yule tipwa tipwa wako??? Hana hata kiuno maskini ya Mungu! Kajazia kama pipaa! Hujui mgongo ni upi tumbo ni lipi, sijui hata ulimpendea nini"🙄
"Achana na Noela, deal na mimi"
"Nataka nikupe yote mpaka akili ikukae sawa kuwa mtoto mzuri nipo na sio yule nguruwe pori wako"
Iris akamsukumia Salmon kitandani na kumkalia kwa juu, baada ya hapo wakaanza kukiss huku mechi ikichezwa kama hawana akili nzuri. Yote haya yakiwa yanaendelea, Noela yeye alikua busy kumsubiri Salmon afike.
Alipoona hafiki na mda unazidi kwenda akapiga simu yake zaidi ya mara 5 bila kupokelewa. Akahisi pengine Iris alisahau kumuambia ndo maana hakua amefika
"Itakua Iris hajamuambia nini? Ngoja nimuulize" aliachana na namba za Salmon, akatafuta za Iris akampigia. Kwa bahati mbaya Iris alikua amezima simu maana hakutaka usumbufu mda ambao angekua ana mshughulikia shemeji yake💔
Maskini Noela alikata tamaa kabisa mpaka akawa anaona kama ile siku niya mkosi. Ajabu ni kwamba bado roho yake ilikua inamuambia aendelee kusubiri pengine Salmon atafika.
Basi acha aendelee kusubiri binti wa watu, subiri.....subiri na wewe! Mpaka saa sita na nusu inafika Salmon hakua kafika. Mwishoni baada ya kukata tamaa kabisa, akasikia mlango unagongwa.
Weeeeh aliachia tabasamu zito akikimbilia kufungua mlango. Alitegemea atakutana na Salmon ila alikutana na sura tofauti kabisa na Salmon wake.
Alikua ni jamaa flanii ivii kapanda hewani, chocolate colour anavutia hatari. Kwa haraka unaweza sema ana miaka 50 ila weeeh body ya kijana wa miaka 25! Sio kama hawa wababa wetu wa mtaani wenye tumbo kama pakacha??? NO! Huyuuu anavutia vibaya mno👌
Yule jamaa alimuangalia sana Noela kwa macho ya matamanio kutokana na kale kagauni alichokua kavaa! Kabla hata Noela hajamuuliza chochote alishangaa anavamiwa na mabusu pamoja mipapaso isiyo kuwa na idadi.
"Niachie......... Niache............" Noela alilalamika akijitoa kwa yule jamaa ambae aligundua alikua kalewa ila hakuweza kwani alimshinda nguvu.
Kadri alivyokua analeta vurugu ndivyo yule jamaa alivyokua anazidi kumshika sehemu zilizo mmaliza nguvu. Kwakua Noela alikua ni mgeni wa yale mambo, alishangaa anazidi kulegea kwa msisimko.
Mbali na yote hayo Noela hakua tayari kabisa kulala na mwanaume ambae sio Salmon lakini ilo hakufanikiwa. Kwaiyo badala ya kupoteza usichana wake kwa mwanaume anae mpenda, akapoteza kwa mwanaume ambae hamjui kabisa na hata hajawai kumuona.
Baada ya vuta nikuvute na kumaliza haja zake, yule jamaa akageuka upande wa pili akipitiwa na usingizi huku Noela akilia tu bila kituo😭
Alijiona kama mkosaji na kujilaumu kuwa pengine hakutumia nguvu za kutosha ndo maana alibakwa. Haraka haraka alitoka pale kitandani, akaingia bafuni akaoga upesi kisha akavaa na kuondoka kwa huzuni😭
Yani njia nzima mpaka anafika hostel ulikua mwendo wa kilio kama kafiwa vile. Alitegemea kumkuta Iris japo amtulize ila palikua kimyaa..... Kwa uchungu akapanda kitandani akijaribu kujifariji.
Je nini kitaendelea.
Nakuja..........
SEHEMU YA 4
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Siku iliyofuata asubui na mapema kwenye hoteli ya Pacific view, simu ya yule jamaa iliita. Kwa uchovu bila ya hata kuangalia ni nani aliekua anapiga, alivuta simu na kuipeleka sikioni
“Hellow Mr Marvel….” Sauti ya mwanamke upande wa pili ilisikika
“Yes…..Good Morning…..” aliitikia yule jamaa ambae sasa ndo tunamjua kama Mr Marvel mwenyewe
“Nakupigia kuhusu ile issue ya jana…”
“Yeah! Pongezi zako Madam Joe maana jana usiku nili enjoy sana! I don’t know msichana kama huyu ulimtoa wapi but kajua kuni fanya ni enjoy” 😊
“Msichana gani tena Mr Marvel maana msichana nilie kuandalia hukuja kulala nae” Madam Joe mwenyewe akashtuka
“What??? Aaaah Madam Joe bhana hujaniandalia dada flanii ivii kibonge??”
“Noo!! Mimi katika wasichana wangu sina vibonge! Wote nima model”
“What embu subiri kwanza” Mr Marvel aligeuka upande wa pili hakuona mtu. Haraka akanyanyuka na kwenda bafuni napo hakuona mtu.
Akabaki anashangaa na kujiuliza msichana alie lala nae ni nani na ameenda wapi maana hamuoni!
Alishusha pumzi kidogo akiangaza huku na kule ndipo alipoona kitu kitandani.
Kuangalia kwa makini akagundua ni matone ya damu kuashiria kuwa, alie lala nae jana ni bikra. Bila kutegemea Mr Marvel akatabasamu😊
“Madam Joe una hakika kabisa yule msichana sio wako?!”
“Hapana Mr Marvel… sio wangu!”
“Basi sorry i think kuna mistake imetokea mahali”
“Kwani Upo chumba namba ngapi?” Madam Joe akauliza
“I think 77”
“Oooh hapo ndipo kosa lilipo anzia! Mimi nilikuelekeza room no 67 Boss wangu!”
“Usijali Joe hakuna kilicho haribika! Nitakulipa kama kawaida maana kosa ni langu coz nilikua nimekunywa pombe”
“Hakuna shida Boss wangu”
Madam Joe alikata simu akimuacha Mr Marvel akijiuliza maswali mengi sana. Ila kilichokua kinamuuma ni kukumbuka kuwa alitumia nguvu kulala na Noela mpaka kumtoa Bikra💔.
Alitamani sana kumpata amuombe msamaha maana alichokifanya hakikua kizuri. Lakini mbali ya yote hayo Mr Marvel anakubali kuwa toka azaliwe hajawai enjoy namna iyo. Na hio ndo sababu iliyofanya ashindwe kabisa kumsahau binti alie lala nae usiku kucha.
Tukija upande wa pili kwa Noela bado hali ilikua mbaya sana kwa stress. Kila alipokumbuka tukio la jana usiku, chozi lilimtoka😭
Hakuelewa atamtazamaje tena Salmon ama atamuambia nini tena iwapo hatakuta bikra??
Mbaya zaidi kilichokua kinamuuma ni kupoteza usichana wake kwa mtu ambae hastahili kabisa. Alitamani angekuwa na uwezo arudishe masaa nyuma ili lile tukio lisitokee.
Basi akafuta machozi akijitaidi asiendelee kulia. Akiwa pale mlango ulifunguliwa, akaingia Iris akiwa ana raha kama zote.
Yani alijiona mshindi kwa kufanikisha mpango wake wa siku nyingi. Sasa anashangaa kumuona Noela akiwa kavimba uso kwa kulia.
Kwa haraka akaanza kupata wasiwasi labda siri yake imevuja. Kwaiyo kwa uoga akamsogelea na kumuuliza
“Bi dada upo sawa?? Mbona umevimba kama donati??”😳
“Iris ulikua wapi usiku mzima??? Nimekupigia hukua unapatikana??”
“Aaaaah…. Si unajua nilijipatia kijibaba ndo kalinitoa out! Nimekula bata usiku mzima hapa nilipo sina hali, viungo vyote vya mwili vinauma! Vipi wewe mbona huzuni tena”
“Acha tu, kilicho tokea huko ni kibaya sana”
“Kuna nini?? Embu nambie?”
Noela alitamani kumuambia Iris kuwa kalala na mwanaume ambae sio Salmon ila ni kama roho wa Mungu alimuingia akaona ni heri aendelee kufanya lile tukio kuwa siri yake🤐.
Hapa kuna cha kujifunza ndugu zangu, sio kila siri unampa shoga akoo! Ohoooo mtaumbuka watu wangu🥱
Basi, Noela akaamua kumwambia Iris kuwa kinacho mliza ni kwasababu Salmon hakufika mbali ya kumuandalia suprise kubwa kama ile.
“Kheeeeee hakuja??? Makubwaaa…” Iris ndo anajifanya eti kushangaa
“Hajaja huwezi amini! Nampigia simu hapokei! Unajua mpaka nimechoka sasa. We hujui ni jinsi gani kaniumiza Salmon”
“Na gharama zote nilizoingia na bado hajaja, kuna kitu Noela sio bure! Ila usimlaumu sana pengine alipata tatizo”
“Apate tatizo ndo ashindwe kuniambia??? Mhhhh sio Salmon ninae mjua mimi”
“Mimi nahisi itakua alipata emergency bhana usilie na kumkasirikia buree”
“Mbona unamtetea leo wakati siku nyingine huwa unamponda??” Noela alimshangaa Iris😳
“Amna bhana kuna mda unaweka kuponda pembeni, unaangalia na situation jinsi ilivyo” Iris alijishtukia maana toka apewe shoo nzuri na Salmon basi amekua akimuwaza kila wakati
“Ok”
Noela hakutaka mambo mengi, aligeuka upande wa pili akiendelea kujilaza kitu ambacho bado kilimpa mashaka Iris.
Noela hakua kachangamka kabisa, hata kama Salmon hakufika ndo awe vile?? Alie kiasi kile?? Ama alishawashtukia kuwa walikua pamoja ila kakausha???🤔
Iris aliogopa sana, alichukua simu yake akatoka nje ili pindi atakapo mpigia Salmon basi Noela asiweze kusikia.
Alipohakikisha kuna usalama ndipo akazipiga namba za Salmon.
“Yes Iris…”
“Nime kumiss jamani, natamani turudi tena kule tukajifungie”😊
“No! Nipo busy”
“Au huku enjoy?? Maana usingekataa turudi tena kule”
“Kwani umepiga simu kuniambia ilo, ama kuna lingine???”
“Skia, hili tipwa tipwa lako linajiliza kama halina akili nzuri. Eti anasema hukufika hotelini ndo maana analia, ila kwa jinsi ninavyo mjua mimi Noela, hapa kuna issue nyingine! Nina wasiwasi atakua anajua ukweli”
“Ukweli gani??? Kajuaje???? Ama wewe umemuambia Iris” Salmon alipaniki😰
“Mimi nimwambie nina kichaaa??? Ila bhana sina uhakika! Nimekupigia tu ili nikufahamishe”
“Poa nakuja apo sasa ivi”
“Sasa unakuja kufanya nini?? We si umesema upo busy!”
“Nakuja kumuona mpenzi wangu jana nilimkosea” Salmon hakutaka kutoa maelezo mengi, akakata simu.
Apo Iris akachukia akaona anatakiwa aongeze utundu ili Salmon awe wake kabisa. Yani hata kama ni kuroga alikua yupo tayari ili penzi la Salmon asilikose.
Je nini kitaendelea????
Nakuja…………
SEHEMU YA 5
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Haya, Noela aliendelea kulala mpaka mda wa saa tano ambapo Salmon alikua kafika. Ingawa hakutokea kwenye suprise aliyo muandalia, Noela hakuacha kabisa kumkumbatia mpenzi wake maana anampenda vibaya mno.
“Baby uko poa? Mbona kama umelia sana??? What happened???”
“Nipo sawa”
“Hauko sawa momy mimi nakujua vizuri! Please usije ukanambia kwakua mimi sikuja basi ndo unalia mpaka sasa ivi?”
“Yes iyo ndo sababu! Na kwanini hukuja?”
“Aaaah…. Baby unajua…. Jana nikiwa njiani nikapata call kuwa Dad kapata ajali! So nikapaniki na kupitiliza moja kwa moja hospitali! I am sorry kwani sikukupa taarifa ila akili yangu haikua imetulia kabisa” Salmon akadanganya bila hata kupepesa jicho
“Kweli??? Jamani… anaendeleaje?”🥺
“Now yupo okay maana hata hakuumia sana”
“Basi mimi nikawaza mengi labda pengine haunipendi”
“No! Nakupenda sana Nunu wangu. I am sorry maana ilo halitatokea tena”
“Naelewa Salmon”
“Sasa mbona nishakuomba msamaha ila bado haupo sawa??? Are you sure umenisamehe?”
“Nimekusamehe kweli vile” Noela akafosi tabasamu😊
“Unaonaje ukajiandaa then tukatoka?? Twende sehemu tuka relax kufidia jana?? Au unasemaje my love??”
“Sawa hakuna shida”
Noela alinyanyuka na kuingia bafuni ili aoge then watoke. Alimuacha Salmon akiwa kakaa kitandani kwake akiwa anachezea chezea simu bila pressure.
Sasa saa ngapi Iris asifike?? Alikua katoka kwenda canteen kutafuta chai ndipo kurudi na kumkuta Salmon.
Weeeh alimkimbilia akamrukia na kuanza kumbusu. Naweza sema Iris alikua kama kichaa kwa Salmon yani kichaa kweli kweli.
“Wewe vipi?? Una wazimu” Salmon akamsukuma pembeni akiwa kashachukia😡
“sasa una vimba nini wakati nime kumiss?”
“Ndo ufanye huo ujinga hapa??? Ama hujui kama Noela yupo bafuni??”
“Najua sana na huyo akiingia bafuni hatoki leo!! Anaogaga masaa mia! Mpaka asugue mgongo wake na alivyo kibonge sio leo”
“Kwaiyo??”
“Tuna mda mwingi wa kukulana tena mpaka tutosheke!”😊
“Ndo maana nakupenda! Huna uoga kabisa” Salmon alianza kumshambulia Iris kwa mabusu pekee sababu hakua comfortable kufanya kitu kingine zaidi ya mabusu. Aliogopa sana Wanaweza kukutwa.
Basi wali kiss kwa mda mrefu walipotosheka ndipo Iris akamuachia mwenzake. Ilikua kama bahati maana mda ule ule nae Noela akatoka bafuni.
Alichukua nguo zake toka kabatini, akazivaa haraka kisha yeye na Salmon wakatoka na kwenda zao ku-enjoy.
Kweli siku iyo Salmon aliweza kumfanya Noela atabasamu tena, huwezi amini ile huzuni ikaisha na akarudi kama zamani.
Lakini kwa Salmon hata hakua ana enjoy sana maana kila dakika Iris alituma meseji akitaka kujua wanafanya nini. Tena Iris alimuonya sana Salmon kuwa asithubutu kumbusu Noela kwani ana wivu🥱
Ndo kwanza Salmon hakua anaelewa somo, alipo pata nafasi ali mbusu Noela wake na kumuambia jinsi gani anampenda kwa dhati!………..Mhhhhhhh haya embu ngoja tuone🥱.
Sasa basi siku zilivyokua zina songa ndipo Noela akaanza kuhisi kama Salmon kabadilika kabisa. Kuna namna attention na mapenzi aliyokua anampa mwanzo yalipungua.
Na mwanaume hawezi kubadilika tu pasipo uwepo wa mwanamke mwingine. Noela alianza kuhisi hapa huenda Salmon ana mwanamke mwingine.
Ile hofu aliyokua nayo akamuambia Iris ili ampe mawazo
“Amna bhana! Hakusaliti” Iris alijifanya kumuonea huruma ila ndani ya moyo alikua anashangilia kuwa, hatimaye anakwenda kufanikiwa kummiliki Salmon kama wake
“Nina hisi tu! Lazima atakua na mwanamke”
“Kwanini unasema ivo??”
“Naona tu jinsi alivyo, kapunguza kabisa mapenzi sio kama zamani! Muda mwingi tukiwa pamoja huwa ana ishia kuchati ama kuongea na simu kisiri siri”🥺
“Utakua una elewa vibaya”
“Huo ndo ukweli Iris, na nikigundua Salmon anani chiti kweli aisee naweza kuzimia kwa presha! Nampenda mno jamani”😭
“Tulia bhana Noela! Sio kama unavyo fikiria”
“Nasubiri nimuulize kesho kutwa maana uvumilivu unanishinda”
“Kesho kutwa si birthday yake??” Iris akajikuta anaropoka
“We umejuaje???” Alimkata jicho😒
“Aaaah…..nani….. alipost instagram niliona post yake. Alisema atafanya party nyumbani kwao” alijichekesha
“Anhaa!”
Noela aliishia kunung’unika na kujiambia kuwa lazima amuulize Salmon ni kipi kilichosababisha mpaka yeye akabadilika.
Haya, siku ya Birthday ya Salmon ikafika. Kwanza alialika marafiki zake wengi wa chuo maana alitaka kuhakikisha anafanya birthday ambayo ita trend sana.
Kwaiyo aliandaa vinywaji, nyama za kuchoma za kutosha na pia party ilitakiwa iwe ni pool party.
Iris na Noela nao walikuwepo kwenye party. Iris yeye alivaa ka swimming suit (nguo ya kuogelea) kalicho mbana bila kujali watu. Yeye alichotaka ni kuonekana mzuri mbele ya Salmon🤦♀.
Kwa Noela kuvaa swimming suit ilikua ngumu maana angeonekana kama kituko! Badala ya kujiaibisha yeye alikaa pembeni tu anakunywa juice ya embe na sio pombe kama wenzake.
“Mbona hubadilishi nguo??” Salmon akamfuata kumuuliza
“Nibadilishe nivae nini??”
“Si uvae swimming suit kama wengine! Wote hapa wamevaa ivyo kasoro wewe tu, nani mpenzi wangu! Unadhani watu watanionaje??” Alichukia😤
“Basi usichukie, ningekua nimekuja na swimming suit basi ningeenda kubadilisha”
“No problem nishakununulia! Nenda chumbani kwangu utaikuta kitandani! Chumba changu ni cha tatu ukitoka sitting room! Fanya haraka nakusubiria”
“Sawa”
Noela alinyanyuka na kuingia ndani! Palikua pametulia tuli alafu pasafi balaa. Kweli Salmon alikua akiishi maisha mazuri.
Alitembea moja kwa moja mpaka chumba cha tatu, akafungua mlango na kuingia ndani. Alikuta kitandani kuna nguo ya kuogelea alio andaliwa.
Sema sasa hako kanguo kalikua kadogo alafu alipokavaa kalimbana balaaa akawa kitu cha ajabu. Kama kimondo vile🤣.
Kwa kuogopa asimkere Salmon siku ya birthday yake, Noela akatoka akiwa kavaa vile vile na kufanya awe kichekesho. Aisee watu walimcheka mno tena Salmon mwenyewe ndo alikua wa kwanza kucheka🤣.
Yani ni bora angechekwa na wote na sio kuchekwa na Salmon maana yeye ndo kamnunulia ile nguo. Na hata kukubali kuivaa nikwa sababu yake😔.
Basi Wakati party ikiwa inaendelea upande wa ndani, huku nje Kuna magari manne expensive yalikua yanaingizana.
Kwenye gari moja alishuka Mr Marvel akiwa na walinzi wake wanne. Kwanza alishangaa kusikia kelee na kuona kuna baadhi ya magari yamepakiwa nje ya nyumba yake ambayo hayakua yake.
“Whats going on here?? (Kuna nini kinacho endelea)” alimuuliza mlinzi akiwa kashakunja sura😡
“Boss, Sir Salmon anafanya party kule kwenye pool! Leo ni birthday yake”
“Ndo afanye nyumbani bila ruhusa yangu! He knows very well nikirudi nyumbani huwa sitaki kelele zaidi ya kupumzika”🗣️
“Nisamee Boss sikukuambia”
Mr Marvel hakujibu, kwa hasira aliingia ndani ili aende kustopisha ile party ya mwanae. Akiwa kafika koridoni akapishana na Noela ambae alikua akikimbilia chooni akiwa analia.
Na hii ni baada ya kuchekwa sana na Salmon na rafiki zake ndio sababu ya kulia kwake. Sasa alipopishana na Mr Marvel hakumjua, ila Mr Marvel yeye alimjua maana taswira ya Noela huwa haitoki kabisa kichwani kwake.
Je nini kitaendelea? ....!! "
…