NILIVYOOLEWA NA SHEMEJI YANGU 1 - - - - - 5
SEHEMU YA 1
ANZA NAYO....
Call me Paaye, oooh Paaye hata sijui hili jina lina maana gani na siijui wazazi wangu walilipatia kwa mkorea yupi maana kwa hili jina saluti kwao
Aaah Paaye ni wa 1998 am me nina miaka 28 japo umri mkubwa lakini kwa muonekano unaweza kuzania nina miaka 20 huko kumbe ni limtu lizima kabisa na kubwa kuliko ninakaa kwa wazazi wangu..
Sio kama napenda no, ni kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu. Katika familia yetu tumezaliwa wawili mimi ndio mkubwa na anafatia mdogo wangu Bruno..
Maisha yetu hapa nyumbani ni maisha ya kawaida sana yes tunaweza kubadili mlo zaidi ya mmoja kwa siku, mama yangu anajishughulisha na biashara ya kuuza karanga hizi za kuweka kwenye mboga na baba yangu yeye ni fundi wa kupaka nyumba rangi pia anaweza kujenga pia..
Na mimi kazi yangu nimeajiriwa kwenye kiwanda kikubwa kilichopo hapa mwanza, kwanza samahani maana nimeanza kujitambulisha bila kuwaambia natokea wapi am ni mzaliwa wa mwanza hapa kisesa wenyeji wa mkoa huu nazani mnapafahamu.
Mimi ni msukuma pure kabisa tena alieshindikana ๐๐ yaani kuongea nimo kwenye kunyimwa shepu napo nimo yani mungu alichonipendelea kwenye mwili wangu basi ni weupe na tako kwa mbali ๐๐๐
Inshallah vyote nimelizika navyo sinaga tabia ya kumkufuru mungu sijui hajanipa shepu mie aka nalizika na mwili wangu japo huwa nachekwa na akina dada wenzangu kuwa sina shape lakini shoga enu kwenye sura nimeumbika ๐๐ฅฐ
Naweza kusema mungu wakati anaumba sura alitulia aisee maana aliumba mpaka na ambavyo havikutakiwa kuwepo kabisa kutokana na umbo langu nikawa naona kama alinipendelea vile usoni.
Nakumbuka siku moja nilipata mkaka flani hivi yuko smart kidogo akawa amenitongoza yule kaka mshenzi sana ndio siku nilipoenda geto akawa anataka tufanye yale mambo kwakuwa mimi nilikuwa nampenda sana na kwa muda huo nilikuwa na miaka 23 nikaona sio mbaya hapa mume nimepata.
Kumbe nilikuwa najidanganya bana baada yakunichezea na kunilegeza pale akaamua kunivua nguo ngoja nicheke kwanza alivyonivyua nguo si akakuta sina shape na ugonjwa wake mkubwa anapenda wanawake wenye shape
Nyege zote zilikata pale pale akaanza kunifokea, nilimuuliza kosa langu nini eti ananijibu kuwa usoni naonekana mzuri ila sina shape.๐ฅน
Nikamuuliza tena kwanini ulinitongoza, akanijibu eti siku aliyoniona aliniona nikiwa na shape na sijui limeenda wapi au ninavaa vigodoro ๐๐๐.
Nilikuwa nimeachwa mchana kweupe lakini hili la kutokuwa na shape lilinifurahisha sana, unajua kwanini yule kaka mpuuzi sana kwahiyo siku zote zile alikuwa ananiona nina shape, sijui mie mzuri ooh ila sina shape hayo maneno me nishazoea na naona kama kawaida na maisha yanasonga.
Na kwa sasa nipo single kinoma yaani nataka mwanaume atakae nipenda mimi atakuja nyumbani ajitambulishe, anitolee mahali na ndoa juu ndio natoka nyumbani ila bila hivyo mniite mbwa.
Basi tuachane na bla bla za hapa na pale twende na story yetu.....
Alfajiri saa kumi na moja niliamka nikaingia bafuni kama kawaida yangu nikakoga baada ya kumaliza kuweka mwili safi niliingia ndani ambako kuna nguo niliziandaa kwaajiri ya kuvaa siku ya Leo.
Basi nilivaa nguo zangu vizuri siku hiyo nilipendeza kuliko siku zote, aah mimi bwana kwenye kupigilia mavazi nipo vizuri sana yaani kila mwisho wa week lazima ninunue nguo ila simu sasa ninatumia kiswaswaduu ๐๐๐
Yaani unakuta nimevaa vizuri nikapendeza ila kwenye simu sasa aibu, kwanza simu yangu haina mfuniko ๐๐ mfuniko wake ulivunjika hivyo simu ikabaki uchi bila kuwa na kifuniko kwa nyuma.
Huwa natumia kwa kujificha ficha japo mama alishaongea mpaka akaamua kukaa kimya akiniangalia tu na me wala sijali chochote ninachojali nikuvaa basi lakini siku ikialibika mbona nitanunua tu mpya..
Basi baada ya kumaliza kujiandaa niliondoka nyumbani hapo ni saa 12 za alfajiri kuelekea saa moja, nilitembea mpaka stand maana kutoka nyumbani mpaka stand kuna kaumbali kidogo ndio maana huwa nawahi kuamka ili nitembee kwa mguu mpaka stand ili pesa yangu itumike vizuri.
Baada ya kufika stand niliita boda ambapo ilinipeleka moja kwa moja mpaka ninapofanyia kazi, nilishuka na kulipa boda kisha nikapiga hatua ili kuingia ndani ya kiwanda hicho lakini nilisimama baada ya kusikia naitwa..
Nikageuka, ngoja kwanza kwenye hii dunia kumbe kuna wakaka wazuri kiasi hiki maana huyu kaka ambae alikuwa mbele yangu ni mwanume pande la mtu na alikuwa amevalia mavazi ya gym akionekana alikuwa akikimbia..
"Habari yako..??"
Nikashindwa hata kumjibu, huyu kaka alikuwa mzuri mpaka mimi nilijiona kinyesi maana sio kwa uzuri ule..
"Aaam aaah salama..."
"Samahani dada kwa usumbufu..."
"Bila samahani...."
Nilimjibu huku anikiangalia chini kwa aibu maana dah huyu kaka alikuwa ๐ฅ
"Unajua sister nilikuwa katika kufanya mazoezi kama unavyoniona hapa, lakini nimepotea njia..."
"Pole kwani ulikuwa unaelekea pande zipi...??"
"Aaah sijui kisesa sijui wapi wapi huko nimesahau kidogo..."
"Hakuna shida kama unaelekea kisesa nitakuelekeza ila ukifika kisesa utaulizia ambapo unaelekea mmmh..."
"Asante sister yani ubarikiwe sana..."
"Ameen.."
Mnaweza kuniita malaya lakini hakuna mtu ambae akiambiwa maneno kama hayo ashindwe kujibu mie mbona fasta tuu ili hizo baraka zije hata kabla siku haijaisha..๐๐
ITAENDELEA.......
SEHEMU YA 2
SONGA NAYO.....
Basi tulisimama pale kwa muda ikapita boda nikaisimamisha kisha nikasogea mpaka alipokuwa yule kaka muendesha boda..
"Habari yako...??"
Nilimsalimu
"Salama, vipi unenda..?"
"Bila shaka, ila sio kwa sasa maana nina kazi kama unavyojua ila hapa kuna kaka angu huyu hapa.."
Nilisema huku nikimnyooshea mkono yule mkaka muhandsome.
"Mmmh...??"
"Nataka umpeleke kisesa ila hakikisha anafika pale ambapo anataka.."
"Usijali dada, buku jero tuu kaka ako anafika bila wasiwasi..."
"Hakuna shida..."
Nilisema kisha nikafungua pochi yangu na kutoa elfu mbili nikampatia yule boda ambapo alinipa jero fasta nikaidumbukiza kwa pochi kisha nikamgeukia yule kaka..
"Sasa kaka huyu atakupeleka mpaka unapoelekea, nakuomba kuwa makini sana na mungu akutangulie huko uendako.."
Mie nae khaa yaani naongea navingine ambavyo havipo kabisa, kuna muda mpaka nilikuwa najiuliza hivi haya maneno ninayoongea ni mimi maana nilikuwa najikuta mtakatifu na huku kanisani sipendi kwenda..
Basi mkaka wa watu hakuwa na maneno zaidi ya kuniambia asante, kisha akapanda boda na kuondoka, upande wangu na mimi nilielekea ndani ya kiwanda..
Baada ya kufika kule niliingia store ambapo tunatumia kuhifadhia vitu vyetu ikiwemo mavazi, basi nilivua nguo zangu na kuziweka sehemu nzuri kisha nikavaa mavazi ya kazi.
Yani kazi ninayoifanya mimi hailingani kabisa na muonekano wangu, nikiwa kazini navaa magwanda makubwa na Mabuti na kofia ambapo naonekana kadogo naanza kusukuma tolori me nimepangwa secta ya kuchukua uchafu na kwenda kumwaga dampo.
Siku hiyo nilipiga kazi maana hapo kazini ukifanya kazi kwa kujituma unaongezwa mshahara na mshahara wa hapo tunalipwa kwa siku ni elfu nane endapo ukiwa kwenye over time unachukua elfu kumi.
Siku hiyo ilikuwa kama bahati kwangu maana nilipewa na over time, kwahiyo nikatoka na elfu kumi siku hiyo bwana meno yote yalikuwa nje kila muda nilikuwa naichungulia pesa yangu maana tangu nianze kazi pale sijawahi kulipwa pesa kubwa kama hiyo.
Nilijiandaa na kuanza kutoka nje ya kiwanda muda umeenda ni saa moja kasoro, baada ya kutoka nje ya geti nilisimama na kuanza kuweka vitu vyangu sawa nisije nikadondosha bure wakati nikiwa nagombania daladala maana muda kama huu boda sijui huwa wanaendaga wapi huwa hawaonekani kabisa na kama ataonekana basi ni wale ambao wanamiliki piki piki zao binafsi yani kwa ajiri ya kutembelea..
Baada ya kuweka vitu sawa, nikaa tayari ili daladala ikipita tuu shwaa naingia, nilisimama pale daladala zinapita lakini bahati haikiwa kwangu kwani kila nikijaribu kudandia naishia kusukumwa.
Nilikaa pale karibia lisaa lizima, nikaanza kumuwaza bi mkubwa huko nyumbani namna atakavyoenda kunigombeza na huku niko kwenye utafutaji kwa kujikatia tamaa nikaa kwenye daraja.
Nikatoa kiswaswaduu changu nikakiwasha maana toka asubuhi naingia kazini nilikizima, nikatafuta namba ya mama na kumtumia message kuwa nitachelewa kufika maana usafiri ni shida kisha nikairuhusu iende, message ilionyesha report kuwa imefika.
Baada ya muda mama akapiga..
"Uko wapi...??"
Bila hata salamu mama akaanza maswali kwakuwa nimeshamzoea na mimi nikaanza kujieleza..
"Mama magari yamejaa kila nikijaribu kudandia nasukumwa hapa unapoona nimenusurika kuvunjika mguu.."
"Ndio ukome na wewe, nimekwambia achana na hizo kazi za kiwandani hazilipi Anza kuuza karanga kama mimi ila hutaki kunisikia, sasa nakwambiaje Leo mimi nimechoka na kiuno kinaniuma kwahiyo fanya lolote uwahi kuja kupika..!!"
"Eeeeh mama bwana laki..."
Mama akakata simu hata hajasikiliza maneno yangu, nikabaki nikiangalia simu labda anaweza kunipigia tena lakini wapi simu ilikuwa inanitazama tuu nikaaumua kuiweka kwenye pochi mara nikamulikwa na mwanga mkali wa tochi.
Katika kuangalia vizuri ilikuwa ni boda hata sikutaka kujishughulisha kusimamisha, ile boda ikaja mpaka nilipokuwa ikakata kona karibu yangu kisha ikageuka uelekeo wa kuelekea kule ninakoelekea mimi..
Ilikiwa ni pikipiki nzuri aina ya Honda na yule anaeiendesha alivaa mavazi meusi tu mpak helmet nyeusi, nikaanza kuhofia labda nijambazi mara yule mtu akaongea..
"Panda twende...!!"
"Twende wapi...??"
"Nyumbani..!!"
"Kwani we nani, au labda umenifananisha...??"
"Binti panda twende, me nimeagizwa na mama yako nije nikuchukue kama hutaki useme.."
Aliongea kwa ukali, niliposikia mama eeeh sikutaka kuchelewa nikadandia na muda huo huo pikipiki ikawashwa, aweee nilibaki nasali kimoyo moyo lolote baya lisitukute maana kwa mwendo ambao tulitoka nao pale sijui niseme tulikuwa kwenye mashindano kama ningekuwa sijamshika vizuri muda huo ningekuwa nipo chini...
Ulikuwa ni mwendo wa shwaaaaa mpaka nikaisi mdomo na masikio yanapeperushwa na upepo ikabidi nimwambie apunguze mwendo yani ni kama nilimwambia ongeza maana aliongeza mpaka speed ya mwisho kabisa.
Huku nilipo mimi nilikuwa hata sielewi nivute hewa au nitoe hewa maana ule upepo ulivyokiwa unanipitia nikawa naomba tuwahi kufika na siku nyingine sirudii tena kupanda Honda.
Kwa uwezo wa mungu nilifika nyumbani salama kabisa, na nilivyokuwa na kisirani sasa nikashuka hata bila kumlipa hela nikapiga hutua kuondoka nilishangaa ni baada ya kuona ile boda inatokomea...
Nikabaki nashangaa tuu hii imekaaje nikiwa bado najiuliza mama huyu hapa..
"Haya tayari umefika kinachokusimamisha hapo ni nini..."
Kwakuwa na mimi nimevurugwa huko nilikotoka nikaamua kumpita tuu, nikaingia ndani nikabadili nguo na kuvaa kijora kisha nikaingia jikoni na kuanza kuandaa chakula cha usiku.
Niliamua kupika chakula chepesi ili niwahi kulala niamke mapema, basi nilipika ugali kwa mrenda na dagaa mchele kwa ajiri ya kutafunia kisha nikaandaa mezani......
ITAENDELEA........
SEHEMU YA 3
SONGA NAYO.....
Baada ya kumaliza kuandaa nilipakua na kuanza kula, nyumbani huwa tuna utaratibu wetu mtu anakuja kula kwa mda wake mwenyewe sio tuivishe na kuanza kukaribisha hilo halipo yani nikupika ukimaliza weka ugali kwa hotpot kama unakula kula wewe hao wengine watakula kwa muda wao ndivyo ilivyo sijui nyie huko makwenu
Baada ya kumaliza kula niliangalia mida ilikuwa saa tatu na nusu bila kupoteza mda niliingia chumbani, ambako niliweka chumba vizuri maana mimi ni mtu msafi machoni kwa watu ila ukiingia chumbani kwangu nguoz zimetapakaa kila sehemu.
Na sina muda wa kukunja maana naweza nikatoka kazini nimechoka najitupia kitandani na kulala, lakini siku hiyo ni kama kuna pepo la usafi liliniingia.
Basi nilifanya usafi ikiwemo kudeki na kupangilia mazingira ya mule chumbani vizuri, muda ulienda ilipofika saa nne nilipanda kitandani na kulala
Huwa sina ratiba ya kusali, na hata kanisani huwa naenda kwa kulazimishwa na mama, mama yangu anaratiba zake kila akitaka kulala lazima amuombe mungu.
Taratibu usingizi ualianza kunichukua, lakini mara simu yangu ililia ni kama kuna ujumbe ulitumwa nilipotezea nikijua ni watu wa mtandao tu.
Siku hiyo ilipita, kesho asubuhi nilichelewa sana kuamka, niliamka saa moja kasoro na natakiwa kuripoti kazini saa moja na dakika kumi na tano, haraka niliamka na kuanza kujiandaa.
Siku hiyo sikuoga maana kwa namna nilivyochelewa hakukuwa na haja ya kuoga, saa moja na dakika kumi nilikuwa kwenye boda nikiiacha mitaa ya kisesa.
Kwa uwezo wa mungu nilifanikiwa kufika kazini salama, lakini nilipofika palikuwa tofauti na siku zote hii ni baada ya kumkuta meneja akiwa na mkutano na wafanyakazi.
Moyo wangu ulikuwa na hofu na kubwa kuliko ni baada ya kuchelewa kazini siku ambayo meneja alikuwa anawasili na hakuweza kutoa taarifa kwa wafanyakazi bali alikuja kwa kushtukiza ili ajue mienendo ya kazi inaendaje
Nikiwa na wasiwasi niliingia lakini sikubahatika kuingia stoo hii ni baada ya kuitwa na kaka mlinzi wa getini.
"Leo kama usipofukizwa kazi basi nyota yako kali.."
"Kwanini.."
"Meneja amekuja na hapa unavyoona wafanyakazi wote wapo sehemu husika hata hao wahindi wapo seriously na kazi.."
Eeeh moyo wangu ulilipuka kwa uwoga zaidi, najua hamjanielewa hapo yani hapa kazini tunasimamiwa na wahindi nao wamewekwa tuu kama sisi wafanyakazi ila wao wanatusimamia sisi kuhakikisha kazi inafanyika vizuri
Nilipiga moyo konde liwalo na liwe, basi nilishika njia mpaka stood ambapo nilibadili nguo na kuchukua tolori langu na kuanza kulisukuma kuingia ndani zaidi ambako kazi ilikuwa inafanyika.
Naweza kusema kwamba siku hiyo mungu alijua kuniokoa maana wakati mie nafika kumbe meneja nae ndio alikuwa ameshatoka hivyo hakuniona kidogo uoga ukanitoka
Mda wa kupata breakfast ulifika nikatoka mpaka kanteen niliagiza chai na chapati nikapiga msosi wangu wa nguvu pale kisha nikaondoka nikihaidi malipo nitalipa jioni.
Nilirudi na kuendelea na kazi, muda ulikimbia ikafika tena mchana, nikenda tena kanteen na kuagiza ugali samaki, nikafakamia pale huku nikipiga mahesabu kwenye hiyo elf nane yangu pesa itakayobaki haitaosha kwa matumizi yangu..
Basi nilimaliza kula na kurudi tena kazini, nilifanya kazi mpaka jioni siku hiyo tuliwahi sana kutoka nikiwa na elfu nane yangu nikasogea mpaka kwa yule mama na kumlipa elfu nne ajabi alikataa
"Paaye wewe tayari umeshalipiwa...!"
"Mmmh kulipiwa mbona sielewi nani ambae anaweza kulipa bila kumwambia mimi...??"
"Kwa kweli hata mie sifahamu kabisa ila ninachojua umelipiwa basi au unataka uniongeze na hiyo nipate faida zaidi..??"
"Basi mama basi, ningekupa sema na mimi maisha yangu mwenyewe ya kuunga unga..!"
Nilisema huku nikirudisha pesa kwenye pochi, huku moyo wangu ukinisaliti kwa kumuongopea mama wa watu.
Nilishika njia na kutoka mpaka nje ya uzio huo, kisha tararibu nilisogelea benchi na kukaa na kuanza kumtafakari huyo mtu ambae amenilipia chakula
"Mmh sasa nani jamani ambae kanilipia chakula..??"
"Au mlinzi wa geti.., aah sasa nani au meneja ametulipia...lakini mbona wengine walikuwa wanalipa..!"
"Sijui kinachonifanya niwaze ni nini, lakini mbona moyo unaenda mbio sana.."
Nikiwa naendelea kuwaza na kuwazua kuna mtu alikuja mbele yangu bila mimi kumuona kisha akatoa chupa ya maji ya kunywa na kunipatia ndio nikainua uso kuangalia ni nani ambae ananipa maji nilistaajabu baada ya kumuona yule kaka ambae nilikutana nae jana.....
ITAENDELEA.....
SEHEMU YA 4
SONGA NAYO.....
Nilinyanyuka kwa uchangamfu, hata maji sikuweza kupokea kabisa.
"Heee kwahiyo Leo tena umekuja huku...??"
Nilimuuliza huki nikimtazama usoni aisee kama mkiniita malaya mniite tuu likaka lizuri hili me nawaambia yani alikuwa kwenye mazoezi lakini bado alikuwa ananunikia adi raha ๐ฅฐ
"Na Leo nimepotea tena.."
Alisema kwa sauti yake ya besi, mh nikaguna kidogo maana kwa huo msauti.
"Usinitanie bana, nambie ukweli.."
"Hahahaha nakutania, anyway chukua maji.."
"Ah hata usijali me niko sawa, ila hayo maji ungetumia wewe ambae uko kwenye mazoezi.."
"Nani aliekwambia niko kwenye mazoezi..??"
"Hata mavazi yanaonyesha wewe ni mtu wa gym sana.."
"Ni kweli laki..."
Simu yake iliita akitoa mfukoni, dah ana simu nzuri afu ni smartphone mpya kabisa sikuona ni aina gani ila kwa mtazamo wangu tu hiyo simu ni million moja ๐ unabisha we ulikuwepo.
Basi shoga enu nilikuwa napiga chabo za chini chini tu, huku tukitembea taratibu, aliongea na simu kisha akakata na kunigeukia mimi.
"Unaitwa nani..??"
Aliniuliza, sasa mimi nikabaki njia panda sijui nimtajie jina au lakini nawaza jina langu ataliweza kweli mbona atanifikiria mie wa kuja, nilifikiria nimdanganye akaona simjibu akaamua kuniuliza tena kwa mara ya pili.
Mdomo koma si nikajikuta nikiropoka..
"Paaye.."
"Nani..?"
"Aaaah ah Paaye..!"
"Anhaaa sawa.."
Alisema lakini nilijua tuu moyoni anajiwazia hili ni jina gani, basi mie muda huo naona aibu hata kumuangalia siwezi, basi tuliendelea kutembea huku kila mtu akiwa kimya upande wa yule kaka yeye alikuwa busy anachart haya uje upande wangu sasa
Nilikuwa nachezea vidole ovyo ovyo, mara nishike pochi mara nijikune ili mradi taflani tu.
Hata sijui tulitumia muda gani katika kutembea na mda wote ule tulikuwa kimya zaidi yeye alikuwa busy na simu, nikaanza kuona kero sasa nikaamua tuu nimuulize hata jina lake
Sasa wakati nainua uso kumuangalia si nikakuta na yeye ananiangalia tukagonganisha macho ewaaa mie haraka nikayahamisha pembeni nikajikuta nauliza swali la kipuuzi..
"Eti kaka wewe umeoa..??"
"Bado, lakini natarajia kuoa hivi karibuni.."
"Ooh vizuri nitafurahi kama na mimi nitakuwa mojawapo wa wageni waalikwa kwenye ndoa yako.."
"Hakuna shida.."
Safari iliendelea huku tukiongea, nilichojua kwa yule mkaka yeye ni mtu poa sana hanaga mambo mengi yani yeye ni mtu wa katabasamu muda wote.
Tuliongea pale na mwisho tukajikuta tumefika kisesa, tukaagana pale huku tukihaidiana kutafutana ili tujuane vizuri tulibadilishiana namba na kila mtu akapita njia yake.
Upande wangu nilienda moja kwa moja mpaka nyumbani, huwa sina tabia ya kupita sehemu sijui sokoni sinaga kabisa kama ni nyumbani basi nanyoosha moja kwa moja.
Nafika nyumbani nakuta pamefurika watu sio wengi sana kivile, kwa kuwa nilikuwa nimechoka nikapitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwangu na kujitupia kitandani na kuanza kufikiria matukio ya siku nzima..
Nikakumbuka kuna mtu nimempa namba yangu haraka nikawasha simu, ile imewaka tuu simu ikaita na namba ni ngeni nikajua tu huyu atakuwa ni yule kaka basi kwa uchangamfu nikapokea
Nilitarajia kukutana na sauti ya yule kaka lakini nilikutana na sauti ngeni kabisa masikioni mwangu..
"Hello naongea na nani..??"
Nikiwa nimepanik niliuliza..
"Najua umechoka, ila utanijua tuu.."
"Usinitishe sawa, nakuuliza tena wewe ni nani..??"
"Me ni mumeo.."
"Mume yani mume kivipi yani..?"
Niliuliza huku nikiwa na hasira kama zote, yule mtu hakujibu zaidi akakata simu, na muda huo mlango wangu wa chumbani ukagongwa nikiwa na hasira nikaamka na kwenda kufungua mlango.
Waliingia shangazi zangu kama watatu hivi wakiwa wameongozana na mama nyuso zao zilionyesha tabasamu Pana kiasi kwamba lilinitisha mpaka mimi ikabidi niwaulize..
"Kulikoni...??"
"Elililililiilili..."
Mama akapiga kigele gele kwangu ikawa kero..
"Mama kulikoni na vigele gele tena vya kazi gani..??"
"Unauliza vya kazi gani, yani unajua umetuheshimisha sana Paaye Hongera binti yangu umepata mume..??"
Shangaz aliongea, jamni hii kitu mnaijua wale ambao mmepitia hali kama yangu, yani sijui nilie au nicheke nikabaki tuu nimetumbua macho nawaangalia namna ambavyo wanafurahi pale lakini mie akili yangu haikuwa hapo kabisa nilikuwa nikimuwaza tu yule kaka.
Mdomo ulikuwa mzito kusema sitaki kuolewa pia moyo ulikuwa mzito kuolewa na huyo mwanaume ambaye amekuja kunichumbia.....
ITAENDELEA...
SEHEMU YA 5
SONGA NAYO.....
Kama mnakumbuka niliwaambia kuwa mwanaume atakaenipenda atakuja nyumbani kujitambulisha na kunichumbia lakini mbona amekuja kwa wakati ambao tayari moyo wangu upo kwa mtu mwingine
Sijaweka hisia zangu wazi lakini ukweli yule kaka nampemda sana japo nimemuona jana lakini nahisi kumpenda kutoka ndani ya moyo wangu na mifupa yangu ๐
Ni lazima nikubali kuolewa maana mkaka mwenyewe aliniambia yupo karibu kuoa anamaanisha yuko na mchumba na sio rahisi kunipenda mimi bali amenitamani
Fikira mbaya ziliutawala ubongo wangu, nirifikilia nikaona sio mbaya acha niolewe maana umri unaenda na sina mtoto wala mume wa kusema labda atarithi Mali zangu.
Basi niliamua kufuata akili yangu, nikatoka na kwenda kumuita mama pembeni ili niweze kuongea nae.
"Mama nimefikiria naona mnipe muda kwanza..!"
"Huo muda ambao unataka tukupe unataka kufanyia nini zaidi..??"
"Mama matani pembeni, nimesema msipokee pesa yoyote mpaka nikamilishe kile ambacho nimepanga.."
"Mh makubwa, sawa ngonja nikaongee na baba yako.."
Mama alisema huku akinyanyuka na kuondoka nikabaki mwenyewe simu yangu ikaingia ujumbe, nikafungua na kukuta umetumwa kwa namba ngeni ulisomeka hivi..
( Hello Paaye I'm Sameer, uko poa...??" )
Nikasahu na habari za ndoa kabisa, nikaaa vizuri na kuandika niko poa sijui wewe kisha nikasend.
( "niko poa niambie..)
( Sina cha kukwambia unafanya nini saivi..??)
( Niko gym..)
( Mpaka muda huu uko gym..?)
( ndio ratiba zangu, hivi kweli una simu..?)
( Hapana sina natumia simu ya mama..)
( Kwani huku simu zinapatikana kuanzia bei gani..)
( efl 25 )
( Sawa usiku mwema )
( nawe pia )
Sasa mtu kanitumia meseji kama nne tu kisha anasema usiku mwema aisee nilichukia nikawa nawaza labda yupo na mkewe ndio kabisa wivu ukawa unanijaa mpaka kifua kilivimba hata chakula cha usiku kilipoiva sikula kabisa nikalala na njaa.
Asubuhi niliamka nikiwa nimechoka mwili unauma, hata sijakaa sawa simu yangu ikaita mpigaji alikuwa Sameer basi haraka nikapokea simu..
" Hallow.."
Niliongea
" Mh bado Umelala ...?"
"Hapana, nimeamka kitambo sana.."
Nilidanganya..
"Okay basi naomba ujiandae kuna mtu anakufata hapo sio mida.."
Kusukia kujiandaa, nikasahau hata kumuitikia, chapu nikaingia bafuni nikaoga dakika nne zilinitosha nikarudi chumbani ambako nilifungua begi na nguo zote nilimwaga kitandani na kuanza kutafuta nguo ambayo itanifaa..
Nilitafuta karibia lisaa maana kila nikichagua hii naona mbaya ikabidi nitoke nje, huko nilimkuta Bruno akiwa anafagia uwanja Bruno ni kijana wa miaka 16 sasa yuko form two.
"We Bruno kuja hapa.."
Mdogo wangu ananiheshimu mimi na ananiogopa kuliko wazazi wake kwa sababu namjali sana, basi akasogea mpaka nilipokuwa.
"Mimi ni dada yako sawa..??"
"Ndio dada najua.."
"Sawa, sasa nataka unaimbie ni nguo gani kati ya nguo zangu zote ambayo nikiivaa huwa napendeza sana..??"
"Aaah dada bwana.."
"Wewe nijibu bana.."
" Gauni.."
"Gauni lipi sasa, maana mimi namagauni mengi sana sasa unasemea gauni gani.."
"Da Paaye we vaa lile gauni ambalo ulinunuliwa na ex wako hilo gauni linakutoa sio poa.."
"Weeee hilo amna kwa kweli.."
"Basi sasa, mimi ninaloona linakufaa ni hilo tuu, kwani unataka kwenda wapi..??"
"Hayakuhusu we fanya kazi yako.."
Niliingia ndani na muda huo meseji ikaingia kwenye simu.
( Umemaliza, kama umemaliza nambie nitume usafiri.." )
( Ndio namalizia..)
Niliachana na simu kisha nikageukia begi la nguo, sikutaka kuichosha akili yangu nilichukua moja ya gauni fupi kiasi langi ya pink na kuvaa nilivaa tuu nikiwa hata sina matumaini ya kupendeza kabisa, miguuni nilitupia raba zangu nyeupe.
Na vile sina shape nguo za kubana huwa sivai kabisa yani mie ni gauni za kumwaga sijui mnaita soro mie sijui.
Usoni nikajipakia ka make up ka buku na wanja kwa mbali kisha nywele nikachana na kuzibana, nikamaliza bila kusahau kiswaswaduu changu nikakichukua na kumtumia meseji kuwa nimemaliza kisha nikakaweka kwa pochi nikaona haitoshi nikakazima kabisa kasije kunisumbua huko mbele...
Je nini KITAENDELEA.......!! "
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi