Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo

MIRANDA (Binti Yangu) 1 - - - - - 5
Gonga94 Β· Stories

MIRANDA (Binti Yangu) 1 - - - - - 5

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.


SEHEMU YA 1
ANZA NAYO SASA......

Kuna ule msemo kuwa mpende yule anaekupenda na mthamini yule anaekuthamini,yes naweza kusema kuwa mimi nilibahatika kupendwa na kuthaminiwa bwana 😊

Yaani binti yenu kwenye kupendwa sijui niseme nilizaliwa na ka nyota flani hivi ka kupendwa😍 , yani nilipozaliwa mama aliwahi kuniambia nilipokuwa mdogo nilikuwa napendwa jamaniπŸ€—

Haipiti siku watoto kutoka nyumba za jirani wanajazana nyumbani ili kunibeba πŸ˜… kuna wale msioamini ila kuna wachache sana wataamini maana wao walikuwa kama mimi

Okay loves, tuachane na bla bla za hapa na pale kwanza twende na utambulisho rasmi sasa, unaweza kuniita Mira ikiwa ni kifupi cha jina langu, jina langu ni Miranda yes Miranda never and ever nalipenda hili jina πŸ₯°

Katika familia yetu mie ndio mkubwa wakifuatia wadogo zangu saba πŸ˜…πŸ˜… mpaka naona aibu hata kuwatambulisha hawa wadogo zangu maana sijui wazazi walipania kuzaa aisee 🀣🀣ukifika nyumbani unakuta vitoto vimefuatana balaaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œ

Okay kwa sasa mimi naishi huku Oman πŸ‡΄πŸ‡², na naishi kama mfanyakazi wa ndani katika familia moja hivi ya kitajiri sana, yani hii familia sijui hata niielezeeje maana wanajua kujali na kuthamin haki ya mtu

Wakati nilipokuwa tanzania niliwahi kusikia kuwa waarabu ni watu wa baya sijui ukienda huko wanaenda kukufanyisha kazi za ngono mara ufanye mapenzi na mbwa πŸ˜‚ my zangu naweza kusema sio wote wapo hivi

Msije mkasema nawatetea maana kwanza lazima niwatetee hawa ninaoishi nao maana hawa watu wananipenda zaidi ya hata hilo neno πŸ€— hivi unajua maana ya kupendwa na familia nzima wewe πŸ˜ƒ yani napendwa mpaka kuna muda naogopa sasa 🫣 maana huku kwenye kupendwa aweee πŸ”₯

Sababu kuu ya mimi kupendwa ni kwa uchapakazi wangu lakini pia mimi niko na heshima kama zote, hivi mnaelewa maana ya kuwa na heshima zote iko hivi mimi naheshimu watu wa rika zote awe mkubwa au mdogo sijawahi kumzarau mtu kabisa

Basi nazani mmejua ka story kangu kafupi twende na story yetu,

Ni majira ya mchana jua lilikuwa kali sana, siku hiyo nilikuwa zangu jikoni nikiwa nimejiachia na sijali lolote, binti nilikuwa nimevaa nguo za stara yaani ikitokea umeona upaja wangu basi niite mbwa nimekaa pale πŸ˜‚πŸ˜‚

Mimi kwenye kuvaa nguo za stara huko uarabuni naweza kusema niko kwenye orodha ya watu wanaojistiri aisee, mimi ni mkristo pure kabisa lakini mavazi ninayovaa ni ya kiislam yani mpaka ushungi nafunga nabaki nimeonyesha macho tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œ

Mie bwana nimetokea kupenda sana dini ya kiislam kutokana na watu wengi wa huku kujistri sana, lakini uje hapa kwa boss wangu eeeh hawa watu wanajiachia aisee yani nusu ya miili yao iko wazi na hawajali lolote kama yupo baba or mama yao mabinti wao ni kujiachia tuu na vinguo vifupi imefikia muda mpaka mapaja yao yamenikinai sasa hata kuyaangalia πŸ˜‚πŸ˜‚

Basi bwana niliendelea kupika na muda huo hapo nyumbani nilikuwa nimebaki mimi na mtoto mdogo wa madam ambaye bado mdogo sana ana miezi sita.

Mtoto huyu anitwa Nasrat na hili jina nilimpa mimi mwenyewe, najua mnajiuliza kwanini waruhusu mimi nimpe jina mtoto wao na ikiwa wao wapo, shoga enu kama nilivyowaambia mie napendwa na ninaaminiwa sana kwahiyo hakuna shida kitendo cha kuambiwa naletewa mtoto wa kumlea awee chapu nikampa jina akiwa bado tumboni πŸ˜‚

Nasrat nimemfanya kama mtoto wangu, yani imefikia hatua Nasrat ananiita mimi mama, kuna ka furaha huwa nakapata na upande wa mama yake yeye hajali lolote kuhusu mtoto yani hii familia naweza kusema kuwa huyu mtoto ni kama wamenizalia awe wangu

Nikiwa bize napika nikasikia sauti ya mtoto wangu analia, chapu nikaacha kupika na kwenda kumuangalia mwanangu, nilimkuta akiwa analia sana πŸ₯Ή yani mtoto alikuwa analia na haikuwa kawaida yake

Nikiwa kama mlezi nilihisi kuchanganyikiwa haraka nilikimbia mpaka seblen na kumpigia simu doctor na kumuomba aje nyumbani haraka doctor alinihaidi atakuwa hapo baada ya nusu saa.

Nilikuwa nazunguka kama chizi nyie huyu mtoto nampenda kama nimemzaa mimi, nilitafuta namba ya mdam na kumpigia nikimuomba aje nyumbani mtoto wake anaumwa.

"Madam pleas Nasrar analia sana na sielewi shida nini..."

Nilisema huku machozi yakinitoka kabisa.

"Ila Mira, hivi umesahau kuwa huyo mtoto nimekuzalia wewe namaanisha kuwa huyo mtoto ni wako mie watoto watatu wamenitosha naweza kusema kuwa Nasrat alizaliwa kwa bahati mbaya maana sikuwa kwenye mpango wa kuongeza mtoto mwingine kwa kuwa sikutaka kuonekana mbaya kwa kukatili kiumbe kisichokuwa na hatia niliamua kumzaa na kukukabidhi wewe kwahiyo huyo ni mtoto wako na sio wangu

Kama ni shida kama zilivyo shida niko tayari kukusaidia kwa lolote lile lakini ni kwamba Nasrat sio mtoto wangu.."

"Madam huu sio muda wa kuongelea hayo mambo, tafadhali kama mzazi njoo umuone binti yako.."

"Mira, hivi wewe ni mtu gani usienielewa umeanza lini kunipandishia sauti nimesema hivi huyo ni mtoto wako kwahiyo pambana kuhakikisha anakuwa sawa na kuhusu gharama usisite kunijulisha.."

Alisema madam na kukata simu, nyie huyu mama hata simuelewi kabisa mara ya kwanza wakati wananiambia haya yeye na mume wake nilizani wananitania bwana lakini leo ndio nimejua wako serious aisee nilichoka.

Nikiwa nazunguka hapo sebleni huku nimembeba Nasrat doctor aliweza kufika pale, basi kwa haraka alianza kumfanyia matibabu, hali ya mtoto haikuwa nzuri hivyo ilimbidi kupelekwa hospitali kubwa ili kwenda kuangaliwa zaidi

Mkumbuke muda wote huo sikuweza kuingia jikoni hata kuzima jiko nilisahau kutokana na kuchanganyikiwa nilishindwa kukumbuka kama sikuzima jiko.

Basi tulibeba mtoto na kuelekea hospital, njia nzima nilikuwa nikimuomba mungu amuepushe Nasrat maana bado mdogo sana tena anamuhitaji mama yake na kama mlikuwa hamjui Nasrat toka azaliwe hajawahi kunyonya maziwa ya mama yake πŸ₯Ή jambo hili linaniuma sana zaidi amekuwa akitumia maziwa ya ng'ombe.

Safari yetu ilienda kuishia hospital kubwa sana, tena ilikuwa hospital ya private haraka mtoto walianza kumfanyia matibabu, wakati huo nilishapiga karibia simu zote za ndugu zake lakini hata hawakujali lolote kuhusu mtoto zaidi ya Naina huyu ni dada mkubwa ndio wa kwanza kuzaliwa

Anafuata mvulana hata sijui anaishi wapi ila nasikiaga tu habari zake kuwa kuna mtoto wao wa pili ambaye anafahamika kama Anfrey sijawahi kumuona na sijui yupo wapi mie sijui

Kuna mwingine anaemfuata Anfrey huyu ni mdada anaitwa Swatii, binti huyu ni mcharuko yani binti hatulii na mwanaume mmoja kila mkaka anapita nae aisee huyu binti ni kiwembe

Na mtoto wao wa mwisho ndio Nasrat kama Nasrat binti yangu mzuri nyie πŸ₯° yani ukikaaangalia hutaacha kukatazama lakini ndio hivyo binti hana bahati ya kupendwa na wazazi wake......

ITAENDELEA......
SEHEMU YA 2
SONGA NAYO.......

Basi baada ya muda Naina akawa amewasili pale, na kuniuliza habari za mtoto mie basi hata kuongea siwezi nilikuwa nalia tu ikabidi Naina achukue jukumu la kunituliza kwanza..

"Mira, najua wewe ndio umekuwa kama mzazi lazima hili likuume lakini nikutoe hofu hali ya Nasrat itakuwa nzuri kikubwa tumuombe Allah..."

"Lakini..."

"Kaa kimya Mira, hutakiwi kunieleza chochote vyote najua na sio kwamba sifahamu najua kabisa na usione mie nipo hapa kwa kupenda no nafanya hivi kwa sababu wewe umekuwa mtu mhimu katika familia yetu ndio maana nimeamua kuja ili kukupa moyo

Sihitaji kusikia ukinieleza chochote kuhusu mama or baba naomba focus na mtoto kwanza.."

Hata sikutaka kubishana nae nikakaa kimya huku nikijiinamia tuu nalia mwenyewe kwenye moyo wangu, basi matibabu yaliendelea hatiame kila kitu kilikamlika na doctor alitoka ili kuja kutupa majibu zaidi.

"Nahitaji kuonana na mama wa huyu mtoto..."

Alisema doctor, basi mie hata sielewi zaidi nikabaki namwangalia Naina.

"Unaniangalia nini, wewe nenda kaangalie afya ya mwanao..."

Nikawa hata sijamuelewa hapo.

"Unaongea kuhusu nini..??"

Nilimuuliza.

"Eeh Mira hivi siku hizi umekuaje wewe, kwani wewe sio mama mzazi wa Nasrat..??"

Eeh hapo kidogo kwanza nikamuangalia doctor, kisha nikamfuata maana kukaa nikibishana na watu ambao haiwaijali damu yao ni sawa na kuumiza Figo.

"Mwanao uliwahi kumnyonyesha mara ngapi toka umzae..??"

Baada ya kufika tuu kwenye chumba cha doctor, doctor alinitupia swali ambalo kwangu lilikuwa gumu kulijibu nikabaki nimetumbua macho nikimuangalia doctor

"Nafikiri haupo sawa kwa saivi nikuache upumzike kwanza.."

Doctor alisema huku akinyanyuka, nilimuwahi na kumuomba akae tuzungumze.

"Dr, kwanza nitangulize samahani, huyu mtoto mimi nilimuokota na kumlea kama mtoto wangu.."

Niliamua kudanganya sasa maana ningethubutu kuongea kuhusu madam basi ni kama naiweka familia kwenye matatizo makubwa.

"Oooho ndio maana, maziwa unayompa mtoto sio mazuri kwa afya yake hivyo itabidi kwanza nikupe dawa ya kuua vijidudu vya magonjwa kisha nitakuagizia mlo kamili wa watoto ambao wana miezi kuanzia miwili na kuendelea hii nakupa offer maana una moyo wa kipekee sana.."

"Asante, vipi hali ya mtoto kwa saivi..??"

"Anaendelea vizuri, ila kwa Leo hamtaweza kutoka hapa labda kesho.."

Alisema Dr huku akinyanyuka na kutoka ndani ya chumba hicho akaniacha mwenyewe kichwa kikiwa kizito kwa mawazo basi doctor aliweza kurudia akiwa amebeba dawa pamoja na chakula cha mtoto.

Alinipa maelekezo pale baada ya hapo aliniruhusu kwenda kumuona mtoto, sikupoteza muda yani ile naruhusiwa tu ni shwaa nikawa nimefika wodi aliyolazwa Nasrat.

Baada ya kufika mule wodini nilikakuta kakiwa macho, kanaangalia tuu juu ya dari yani kamepoa hata uso wa nuru hakana kabisa kalionekana hakana hata furaha maskini..πŸ₯Ή

"Nasrat.."

Nilkaita kakaniangalia, baada ya kuniona kakatabasamu nyie nilifurahi nikakashika vidole vyake kakawa kanacheka basi namie nacheka furaha yangu ni kumuona Nasrat akiwa na tabasamu

Nikiwa nacheka hapo na mtoto aliingia Naina, alipofika alikaa pembeni yangu na kuanza kuniangalia namna nilivyokuwa namcare mtoto.

"Wooow nakuona mwenyewe..."

Alisema Naina..

"Yaah kwanza hapa afadhali maana nilikuwa nawaza sio poa..."

Nilizungumza

"Inaonekana unampenda sana mtoto wako.."

"Yaap lazima nimpende kwa sababu ni mtoto wangu.."

Nilimjibu huku nikionekana kuchukizwa sana naaswali yake yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Hakusema neno zaidi alibaki akiniangalia tu na simu yake iliita akanyanyuka

"Naenda kupokea simu.."

"Sawa..."

Akatoka, mie nikabaki nasonya tuu watu sijui wana roho gani hawa yani ndio nimeamini kuwa kuna watu huwa wanatupa watoto wao wa kuwazaa maana siku zote zile nilikuwa nakataa kabisa ila kwa hili aaah niseme tuu nimeamini.

Basi baada ya muda Naina alirudi mule wodini na kunikuta nampa mtoto chakula

"Mira, najua unasumbuka kwa ajiri ya mtoto lakini kwanini usingezima kwanza jiko ndio hayo mengine yakafuata..??"

"Unaongea kuhusu nini..??"

Nilimuuliza maana hata sikuwa naelwa kabisa eti

"Kwanini hukuzima jiko wakati unaondoka.."

Hapo kidogo ndio nikakumbuka kuwa nilikuwa napika na jiko sikuweza kuzima, kwa hofu nilinyanyuka na kumuangalia Naina nawaza kama nyumba itakuwa imeungua yote nitafanyaje mimi.

"Eeeh Naina nilipitiwa tuu bahati mbaya, kwani nyumba imeungua au..??"

Hapo nauliza huku jasho likiwa linanitoka mwili mzima.

"Hapana.."

"Ila, nambie basi mbona unaniambia maneno nusu nusu sasa nitaelewa nini..."

"Hakuna chochote kilichotokea, maana mlinzi alienda kuzima jiko ila nikwambie kitu shoga angu kuwa makini na mali za watu..."

Naina aliongea kisha akaondoka, nikabaki nawaza kama nyumba ingeungua sijui ningefanyaje, sina hela labda ya kusema nirudishe mali za watu zilizoteketea ndio nikakumbuka na maneno ya Naina ndio kabisa nikaona hapa niwe makini naweza kutolewa Figo......

ITAENDELEA.........
SEHEMU YA 3
SONGA NAYO.......

Basi siku hiyo nilishinda hospital nikimuangalia mtoto, ilipofika jioni ilinibidi nirudi nyumbani kufuata mahitaji ya mtoto kama pampazi na vitu vingine.

Basi nilichukua usafiri mpaka nyumbani, baada ya kufika nyumbani nilikuta familia nzima ikiwa inapata chakula cha jioni yani inafutru

Nilifika na kusalimia pale, kisha nikamsogelea madam.

"Madam nilikuwa nao..."

"Kama kuhusu Nasra naomba usiniambie chochote.."

Eeh nikabaki namuangalia huyu mama huku nikimpima tuu kwenye mizani ya jicho, yani nilishindwa kumuelewa kabisa et

Imagine umebeba mimba miezi tisa na ukaumwa uchungu sijui masaa mangapi na tena ukajifungua kwa op ukauguza kidonda kwa miezi sita leo hii mtoto unamkana kabisa sio wako kweli hii inawezekana au mie niko ndotoni.

Niliona kama naota aisee nikajizaba kofi la shavu kwanza labda nilikuwa naota lakini ni uhalisia kabisa kwanza nilivyojipiga tuu madam akacheka kisha akantazama kwa umakini mkubwa

"It's the truth, sijawahi kupendezwa na Nasrat kwa sababu zangu binafsi, kama nilivyokwambia awali nilitaka kumtupa Laki..."

"Inatosha sasa inatosha..."

Nilizungumza huku nikilia kabisa, madam alinyanyuka kwenye kiti na kunifuata mapaka nilipokuwa alipofika akanikumbatia πŸ₯Ή huku akinituliza yani kwangu niliona kama amenizarau kabisa huyu mama

Kwa hasira nilisukuma huko, nilitamani kumzaba kibao ila nikatulia

"Wewe ni mama wa aina gani ambaye hujali lolote kuhusu mtoto, hujui binti yako kule ana hali gani mtoto anaumwa kwa sababu yako mtoto anapitia kipindi kigumu ile hali mama upo hapa hivi nikuulize wakati unapan..."

"Binti taratibu sawa, umesahau kuwa mimi ni boss wako..??:

"Uwe boss au nani yangu lakini lazima nikwambie ukweli, nasema hivi kuanzia leo sitamujali tena Nasrat bora nimuache tuu apumzike kwa amani.."

Nyie nilikuwa nimechafukwa balaa huyu mama alikuwa ananiona mie kama matako yake, muda wote ule tunajibizana baba wa familia yeye alikuwa kimya akinywa supu huku anachezea simu yake.

"Mira..."

Madam aliniita baada ya kuona nimekasirika sana ukweli nilikuwa nimechukia na macho yalikuwa mekundu kama nilivuta bangi aisee πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œ

Nilimuangalia bila kumuitikia.

"Mira, kuna machaguo mawili.."

Aliniambia madam, mie nilikuwa kimya huku mdomoni nikitafuna karafuu πŸ˜‚πŸ˜‚ eeh nilikuwa natafuna ili kuepuka kupiga mtu maana mie hasira zangu nazijua mwenyewe

"Chagua kuondoka hapa na unilipe milioni 50 kwa sababu umekiuka mkataba tulioweka baina yangu mimi na wewe either ubakie hapa na uendelee kumlea Nasrat sio kumlea tuu bali kumfanya kama mtoto wako na hutanilipa chochote mpaka Nasrat afikishe miaka 15 ndio utaondoka hapa na hutaondoka naye yaani utaondoka wewe kama wewe na Nasrat ndio utakuwa mwisho wake wa kuishi..."

Nilikuwa natafuna karafuu lakini mpaka niliitema maana nilisikia utamu na uchungu kwa pamoja, nilimuangalia madamu kisha nikamuuliza.

"Yani itakuwa mwisho wake kivipi.."

"Kama ulikuwa hujui, ngoja nikuambie kitu, Mira umeishi kwenye hii nyumba zaidi ya miaka mitatu si ndio..??"

Sikumjibu

"Usione huu utajiri unapatikana kwa nguvu zetu, hapana Mira bali tumejiunga na chama kikubwa cha freemason na tunatakiwa kutoa kafara ya mtoto wetu wa mwisho na hatutakiwi kumpenda ndio maana unaona mie mzazi sijali lolote kuhusu Nasrat lakini ukweli naumia sana tena sana kuona binti yangu anateseka vil..."

"Komea hapo hapo.."

Nilimwambia na sikutaka kusubiri neno jingine kutoka kwake nilishika njia na kuingia chumbani, yani kichwa kilikuwa kizito hii siku nilihisi chungu, nilikuwa nazunguka tu mle ndani na nisijue kipi nichague

Siku hiyo ilikuwa ndefu, kila nikikumbuka kuna mtoto kule hospital na ananitegemea mimi moyo ulikuwa unauma, basi nilichukua pampazi na nguo nyingine za kubadili nilitoka moja kwa moja

Nilipofika sebleni niliwakuta wakiwa wamekaa wanaangalia TV mie nikawapita kama siwaoni vile, nilitoka mpaka nje nilisimamisha usafiri nikapannda na safari ya hospital ikaanza.

Njia nzima nilikuwa nawaza kiasi kwamba nilipitilizwa kituo, basi nilishuka na kuchukua gari nyingine tena safari hii nilichukua ile ya kipeke yangu

Namshukuru mungu niliweza kufika salama na niliweza kumkuta Nasrat wangu anendelea vizuri, siku hiyo ilipita kwa mbinde sana na sikubahatika kurudi nyumbani kwa sababu ya mgonjwa.

Kesho yake majira ya mchana tuliweza kuruhusiwa huku doctor akinihimiza sana kumuangalia mtoto, basi nilichukua usafiri mpaka nyumbani nilikuta nyumba ikiwa kimya nilijua watu walikuwa hawapo

Nilimchukua Nasrat na kwenda kumlaza chumbani kwangu, baada ya hapo niliingia jikoni na kuanza kuandaa chakula cha mtoto maana nilitaka ale kwanza yeye harafu mambo mengine yaendelee

Baada ya kumaliza kuandaa nilimlisha kisha nikamuogesha, nilimbembeleza hadi akalala na mimi ndio nikapika chakula cha wote kisha nikala na kupumzika maana usiku mzima sikulala nilikuwa namuangalia mtoto.

Majira ya jioni nilianza kusikia milio ya gari ikimaanisha wana familia walianza kurejea nyumbani kwa kuwa sikuwa sawa sikujishughulisha kutoka.......

ITAENDELEA........
SEHEMU YA 4
SONGA NAYO.....

Nikaendelea kulala bila kujisumbua kwenda kusalimia huko sebleni

Nikiwa nimelala nilisikia nikigongewa mlango, basi kichovu nilinyanyuka na kwenda kufungua mlango nikakutana na madam, nilitamani kufunga mlango kila nikiiona hii sura moyo wangu unahisi hasira

"Umeshindaje..??"

Aliniuliza

"Salama..."

Nilimjibu kwa mkato siku hii sikumchangamkia kama zilivyo siku nyingine sijui pole na kazi aka siku hiyo nilikuwa mkavu

"Aaah nimekuja kukuita hapa kuna kitu nataka kukuonyesha.."

"Kitu gani..??"

"Mira bwana, nimekuletea wadada wa kazi wawili watakuwa wanakusaidia kwenye kufanya usafi na kuandaa chakula ila wewe jukumu lako ni kumlea mtoto basi.."

"Nashukru.."

Nilisema huku nikifunga mlango, akanizuia tena

"Arafu nimesahau, leo ndio unapokea mshahara wako so nikitoka hapa nitaenda kukuwekea kwenye account yako.."

"Asante.."

Hakuongea chochote aliondoka na mimi nikafunga mlango ila sikufunga mlango bali niliuegesha tuu kisha nikaanza kumchungulia madam namna alivyokuwa anaondoka.

"Cheki yale matako, lanamke lijinga tuu hata shape halina kazi kujaza minyama tuu.."

Nilijiongelesha, πŸ˜‚ ila mimi mara ya kwanza wakati nafika kwenye hii nyumba nilikuwa namsifia madamu kuwa yeye ni mzuri sana ila leo ndio nimeanza kumchunguza sasa na kumdadisi mwili wake.

Basi nilihakikisha nafunga mlango vizuri ili mtu yoyote asiingie chumbani maana nilikuwa na mashaka sana kuliko kawaida tena nilifunga na funguo kabisa kisha funguo nikaziweka kwenye nyoyo zanguπŸ˜‚, baadae nikatoka ili kwenda kuona hao wadada wapya wa kazi.

Kweli bana kama alivyoniambia madam niliwakuta wakiwa wamekaa kishamba kishamba yani macho meupe wanashangaa tu.

"Shikamooo..."

Walinisalimia ndio nikajua kuwa ni watanzania wenzangu bwana maana waliongea kiswahili kabisa tena kilichonyooka, basi mimi ili nisionekane na mie nimekaa kizembe ikabidi niongee kiinglishi maana watu wote hapa tunaongea kingreza tu

"Habari zenu...??"

Niliwasalimia kingreza, wakabaki wananiangalia tuu wasinielewe, najua mioyoni walikuwa wanajiuliza huyu nae kumbe ni mwarabu bana πŸ˜†πŸ˜†

Sikutaka kuichosha akili yangu ukizingatia nilikuwa namawazo yangu nikawaambia wanifuate basi bila ubishi walinifuata niliwapeleka mpaka jikoni.

Nilikuwa na kazi ya kuwaeleza namna ya kutumia jiko na ratiba za humu ndani, hivyo ilinilazimu kuongea kiswahili kama nilivyowaambia mie naheshimu watu wa lika zote basi taratibu nialianza kuwafundisha ili waweze kunielewa kirahisi.

"Ratiba za humu ndani mnatakiwa kupika chakula mara mbili kwa siku..."

Niliongea kisha nikawatazama, kwa mbali nilisikia sauti za nyayo ikionyesha mtu alikuwa akija jikoni kweli Swatii aliweza kufika mle jikoni..

"Da Mira..."

Swatii aliniita nawaambia huyu dogo ni kiwembe mjini ila ako na adabu kama zote yani ninachompendea Swatii ananijali sana na haipiti siku bila kuniletea zawadi.

Hata jana nilipokosana na mama yake yeye hakuwepo alikuwa kwa mabwana zake na alilala huko leo ndio amerudi sasa.

"Swatii mambo..??"

"Poa tu, mh naona vitu vipya..."

"Yaap.."

"Da Mira mbona jana ulinipigia sana simu yani mimi simu yangu niliweka silent hivyo sikusikia kabisa maana nilikuwa kwenye party, party ilipoisha ndio kuangalia simu nikakuta missed calls zako vipi ulikuwa na shida..??"

"Aaah nilikumiss tu si unajua tena wizo.."

"Wewe tena ila kuna zawadi yako nimekuletea..."

"Zawadi gani...??"

"Sikwambii mpaka umalize mambo yako, utakuja chumbani uchukue.."

"Sawa love ndio maana nakupenda mwaya.."

Nilimwambia.....

ITAENDELEA........
SEHEMU YA 5
SONGA NAYO.....

Basi tuliongea pale na swatii akaondoka, nikawageukia wale mabinti na kuendelea kuwafundisha pale baada ya kuelewa kila kitu niliondoka na kuelekea chumbani kwangu kumuangalia kipenzi cha roho yangu kama ameamka.

Nilimkuta akiwa bado kalala, basi niliingia bafuni nikaweka mwili safi baada ya kumaliza kila kitu nikatoka sikusahau kufunga mlango nikaelekea chumbani kwa Swatii

Nilimkuta akiwa amekaa kitandani anachezea laptop kwa kuwa mimi na yeye ni ma bff nilifika na kujitupia kitandani.

"Nipe zawadi yangu.."

Nilimwambia bila kujua anaongea na mtu kwenye laptop baada ya kuona sijibiwi ikabidi nisogee nione nini anafanya bwana bwana nilibaki nimekodoa macho yangu kiasi kwamba nililitoa mpaka nyuzi 100 za jicho

Nilikuwa nashangaa baada ya kuona likaka lizuri likiwa linaongea na swatii kwa mawazo yangu nikajua ni mpenzi wake hivyo nikamuuliza..

"Swatii, bwana ako mbona mzuri hivi...??"

"Hahahaha we toka lini ukaanza kusifia mwanaume...??"

"Toka zamani mbon, arafu naona hata hunizuii mimi kumtazama.."

"Weee naomba uniache Swatii mimi, yani mimi nina wivu balaa siwezi ruhusu rafiki yangu au hata dada yangu kuwa karibu na bwana yangu maana nitaumia sio poa..."

"Mbona mimi hujanizuia kumtazama au mimi sio mwanamke..??"

"Kwa sababu huyu sio bwana angu.."

"Ni nani...??"

Niliuliza huku macho yakiwa yamenitoka..

"Ni kaka angu..."

Kusikia kaka niliruka na kwenda kujibamiza kwenye furniture iliyokuwa mle chumbani bahati mbaya niliangukia mkono hivyo ukateguka, maumivu niliyoyapata yalisababisha Swatii afunike laptop na kuja kuniangalia mimi..

"Umeumia..??"

Swatii alinuliza baada ya kunifikia.

"Sio sana ila mkono umeteguka.."

"Dah leo ndio nimeamini kuwa hujawahi kuwa na mchumba, maana siku zote unaniambia huna mpenzi nikajua unanitania bana.."

"Tuachane na hayo bwan, hivi hajaniona..??"

"Nani..??"

Swatii dishi lake limeyumba, yani huyu binti ni mwepesi kusahau.

"Si kaka yako..."

"Sizani kama amekuona maana alikuwa busy na kazi, wakati mimi naongea nae macho yake yalikuwa pembeni.."

Hapo kidogo presha ikanishuka.

"Sawa.."

"Basi njoo nikukande.."

Swatii aliniambia huku akinisogeza kitandani na mara mlango ulifunguliwa akaingia madam

"Mira umeumia..??"

Madam aliniuliza kwa kujali yani nilitamani amjali binti yake na sio mimi..

"Sio sana mkono umeteguka tu.."

"Hapana kwa kweli nampigia simu doctor.."

Alisema kweli akatoa simu na kumpigia doctor kabla simu haijapokelewa niliichukua na kuikata kisha nikampa simu yake na kuzungumza.

"Niko sawa mama we unaweza kwenda Swatii atanihudumia.."

Niliongea kwa upole ili swatii asihisi kitu, basi madam hakuwa na lakufanya zaidi ya kutoka, baada ya madam kuondoka niliweza kusikia sauti ya Nasra akiwa analia basi niliachana na uzungu nikanyoosha mkono kwa nguvu ukalia kaaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œ

Swatii akabaki haelewi, mie nikatoka zangu mbio mbio kumuwahi mtoto.

Kwa uwezo wa Allah siku hiyo ilipita na siku nyingine ikashika nafasi, siku hiyo nilikuwa na ufuaji wa nguvu maana mimi napenda kufua kwa mkono kuliko kutumia mashine

Nilikuwa na ufuaji wa nguo zangu na za mwanagu basi hao wengi wanatumia mashine, basi nilifanikiwa kumaliza mida ya saa tatu na muda huu Nasra wangu alikuwa bado kalala

Nasra ni mtoto mtulivu sana, yani hanaga makelele na hata sijui huko nje wanajua kama madam anamtoto maana Nasra huwa hasumbui.

Basi nilipomaliza kufua niliingia ndani ambapo nilimkuta madame akiwa anaongea na simu yani kwa namna alivyokuwa hatulii ilionyesha alikuwa akiongea na mtu ambaye alimpa taarifa za kufurahisha sana......

ITAENDELEA.......

Maoni

You're not logged in


Tangazo - Elton John - Sacrifice
Elton John - Sacrifice
Elton John - Sacrifice
Elton John - Sacrifice
Sikiliza Wimbo Kamili
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MIRANDA (Binti Yangu) 1 - - - - - 5



SEHEMU YA 1
ANZA NAYO SASA......

Kuna ule msemo kuwa mpende yule anaekupenda na mthamini yule anaekuthamini,yes naweza kusema kuwa mimi nilibahatika kupendwa na kuthaminiwa bwana 😊

Yaani binti yenu kwenye kupendwa sijui niseme nilizaliwa na ka nyota flani hivi ka kupendwa😍 , yani nilipozaliwa mama aliwahi kuniambia nilipokuwa mdogo nilikuwa napendwa jamaniπŸ€—

Haipiti siku watoto kutoka nyumba za jirani wanajazana nyumbani ili kunibeba πŸ˜… kuna wale msioamini ila kuna wachache sana wataamini maana wao walikuwa kama mimi

Okay loves, tuachane na bla bla za hapa na pale kwanza twende na utambulisho rasmi sasa, unaweza kuniita Mira ikiwa ni kifupi cha jina langu, jina langu...

πŸ‘‰ Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/miranda-binti-yangu-1-5

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral #fictionwriter
#ShortDrama #fblifestyle

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu Β· dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi miranda-binti-yangu
MIRANDA (Binti Yangu) 12 to 13
MIRANDA (Binti Yangu) 12 to 13
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 7
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 7
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 6
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 6
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 11
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 11
MIRANDA (Binti Yangu)   SEHEMU YA 19 - 20
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 19 - 20
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 8
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 8
MIRANDA (Binti Yangu)     SEHEMU YA 9
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 9
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 10
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 10
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 16
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 16
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 17 - 18
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 17 - 18
MIRANDA (Binti Yangu)   SEHEMU YA 15
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 15
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 14
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 14
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50

1.15K
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 48 na 49

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 48 na 49

1.1K
*AFANDE MILLAN😎* *Sehemu ya 51 na 52*

*AFANDE MILLAN😎* *Sehemu ya 51 na 52*

355
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 39  na 40

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 39 na 40

233
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 38  na 39.

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 38 na 39.

209
SHAMIRA Sehemu ya 48

SHAMIRA Sehemu ya 48

62
BARUA ZA KAKA YANGU; Nikikupenda Mimi Inatosha!

BARUA ZA KAKA YANGU; Nikikupenda Mimi Inatosha!

25
Enzi zetu Radio Free Africa ilikuwa ndiyo bonge moja la station yani unapata full vibe hakuna kubadilisha station.

Enzi zetu Radio Free Africa ilikuwa ndiyo bonge moja la station yani unapata full vibe hakuna kubadilisha station.

10
#TBT 2014 nilijiunga na SAHARA MEDIA GROUP LTD. January niliripoti ofisi za Adda

#TBT 2014 nilijiunga na SAHARA MEDIA GROUP LTD. January niliripoti ofisi za Adda

3
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50

ZIMESOMWA ZAIDI

β€ŽTUNDA LA  DADA β€Ž β€ŽSEHEMU YA KWANZA

β€ŽTUNDA LA DADA β€Ž β€ŽSEHEMU YA KWANZA

11.68K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

7.4K
πŸ™„ NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWAπŸ”₯  sehemu ya tisa.  πŸ‘‰ Akaanza kunipamp sasa...πŸ‘‡

πŸ™„ NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWAπŸ”₯ sehemu ya tisa. πŸ‘‰ Akaanza kunipamp sasa...πŸ‘‡

3.82K
πŸ”₯ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoaπŸ”₯  Sehemu ya sita.  πŸ‘‰ Aaaaaaaaa chomoa...πŸ‘‡  Shemeji inauma utanichana.

πŸ”₯ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoaπŸ”₯ Sehemu ya sita. πŸ‘‰ Aaaaaaaaa chomoa...πŸ‘‡ Shemeji inauma utanichana.

3.31K
MY WANGU❀️ sehemu ya 119 na 120.

MY WANGU❀️ sehemu ya 119 na 120.

2.9K
MY WANGU❀️ sehemu ya 108

MY WANGU❀️ sehemu ya 108

2.84K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoaπŸ”₯  Sehemu ya 20.  πŸ‘‰ Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...πŸ‘‡

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoaπŸ”₯ Sehemu ya 20. πŸ‘‰ Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...πŸ‘‡

2.69K
MY WANGU❀️ sehemu ya 116 na 117

MY WANGU❀️ sehemu ya 116 na 117

2.68K
MY WANGU❀️ sehemu ya 106 na 107

MY WANGU❀️ sehemu ya 106 na 107

2.63K
πŸ”₯ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoaπŸ”₯  Sehemu ya 16.  πŸ‘‰ nakupenda pia...πŸ‘‡

πŸ”₯ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoaπŸ”₯ Sehemu ya 16. πŸ‘‰ nakupenda pia...πŸ‘‡

2.57K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

Hakuna Ratiba kwa sasa

Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
#TBT 2014 nilijiunga na SAHARA MEDIA GROUP LTD. January niliripoti ofisi za Adda Post Mpya
#TBT 2014 nilijiunga na SAHARA MEDIA GROUP LTD. January niliripoti ofisi za Adda
@majario LIVE

Estaste, Kinondoni baada ya HR Mkuu Mzee Shilatu na msimamizi Steven Diallo kuning'oa kutoka Ebony FM, Iringa. Nikapokelewa na Tom Chilala, Wiltrudies Mutembei @wiltrudiesmutembei kisha wakanikabidhi kwa "Semaji"...

*AFANDE MILLAN😎* *Sehemu ya 51 na 52* Post Mpya
*AFANDE MILLAN😎* *Sehemu ya 51 na 52*
@majario LIVE

Daaaah nilishangaaaa sana kwamba aya mambo yamekujaje kujaje, na mbona sielewi, nikasema mama sijaelewa yani kwamba umesema? , mama akanmbia nilishaongea sana na wewe millan, juu ya suala la wewe...

SHAMIRA Sehemu ya 48 Post Mpya
SHAMIRA Sehemu ya 48
@majario LIVE

Wassap;0742443214 Mwandishi; lissa wa huru media Akasema mimi pia nimekula njoga nikaoge basi chapi chapu. nikase​ma sawa. Kweli mwanaume akaenda kuoga nikabaki nimetulia tu na baada ya mda akatoka akanifata...

Enzi zetu Radio Free Africa ilikuwa ndiyo bonge moja la station yani unapata full vibe hakuna kubadilisha station. Post Mpya
Enzi zetu Radio Free Africa ilikuwa ndiyo bonge moja la station yani unapata full vibe hakuna kubadilisha station.
@majario LIVE

Binafsi nilikuwa napenda sana vipindi vitatu pale RFA , 1 - Sindano 3 za moto, asubuhi na Fredwaa...!! 2 - Sitosahau na Sky Woker 3 - Showtime bongo moja ya show za...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 39  na 40 Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 39 na 40
@majario LIVE

39 MPAKA 40 🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼 Mwandishi; lissa wa huru media Nilitukana kweli kweli kwemye gari umo. Ila barka hakunijibu alikuwa busy na kuendesha gari. Akawa ananipeleka mlandizi ukoo. Nikasema wewe mjinga unaenfa...

BARUA ZA KAKA YANGU; Nikikupenda Mimi Inatosha! Post Mpya
BARUA ZA KAKA YANGU; Nikikupenda Mimi Inatosha!
@majario LIVE

Nikikupenda mimi inatosha, acha kuwa na presha, acha kuhangaika na ndugu zangu, kama wakikupenda ni ziada tu lakini haibadilishi chochote! Nani alikudanganya kuwa wanapaswa kukupenda! Mimi mwenyewe sina uhakika kama...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50
@majario LIVE

🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈 Basi bwana penzi likanoga mpaka mwezi ukakata, apo zena alikuwa na wasi wasi kuwa ntamuacha ,ila mi wala sikuwa na ayo mawazo kichwani kwangu ata kidogo, kila siku namuona...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 50
@majario LIVE

🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈 Basi bwana penzi likanoga mpaka mwezi ukakata, apo zena alikuwa na wasi wasi kuwa ntamuacha ,ila mi wala sikuwa na ayo mawazo kichwani kwangu ata kidogo, kila siku namuona...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 48 na 49 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 48 na 49
@majario LIVE

Daaah mchumba ndo kashanikatia simu mi nafanyaje sasa ,basi nikaweka simu pembeni tu, kisha nikapanda kitandani, nikavuta shuka , nikapumzika na asubih sana nikaamkia kazin na mwanangu lbraa,ibra akaniuliza...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 38  na 39. Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 38 na 39.
@majario LIVE

kipande cha 38 🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼 Mwandishi; lissa wa huru media Basi ndo hivyo . Nikaikosa ndoa na bwana barka.na nikawa busy na maisha yangu . Na mambo yangu. Na nikazidisha mapenzi tu kwa...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 36 na 37 namba zilikosewa endelea kusoma. Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 36 na 37 namba zilikosewa endelea kusoma.
@majario LIVE

36 MPAKA 37 🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼 Mwandishi; lissa wa huru media Maua akasema khaaa yani unanitukana mimi. Kwaiyo mimi naweza kuolewa na kaka yangu. Nikasema yaa unaweza sasa kisebengo cha nini. Nakuona sana tangu...

SHAMIRA Sehemu ya 47 Post Mpya
SHAMIRA Sehemu ya 47
@majario LIVE

Wassap; 0742443214 Mwandishi; lissa wa huru media Basi shost alivyotoka kuoga akanmbia shamira shoga yangu nisamehe kwa yale maneno nilokwambia basi. Nikasema yapi? Akasem si yale ya kukwambia ukatoe mimba...

SHAMIRA Sehemu ya 46 Post Mpya
SHAMIRA Sehemu ya 46
@majario LIVE

πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€ Mwandishi; lissa wa huru media Nikaona aisha kakasirika akanambia sawa kama unataka kulea iyo mimba na kuzaa. Ile kulea mtoto ni gharama umae ukielewa hilo suala mapema . Mana sio...

*AFANDE MILLAN😎* *46&47* Post Mpya
*AFANDE MILLAN😎* *46&47*
@majario LIVE

Nakumbuka kuna kipindi ,nilisafiri na ibraa kikazi kwenda moro , apo nilishamuaga zena kuwa mm nasafari naenda moro kikazi, ntakaa siku 2, akanmbia hakuna shida, basi mm nikawa...

SHAMIRA 44 kwa 45 Post Mpya
SHAMIRA 44 kwa 45
@majario LIVE

πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€ Sehemu ya 44 Mwandishi; lissa wa huru media Aseeee tulichoka mno na shoga yangu asa mimi jamani.nafanya nini na hili tumbo na mwanaume hanitaki. Na ameshakana kuwa hii mimba sio yake...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest