*MIMI SIKUACHIπ₯°* *26 *SEASON TWO*
*SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA*
Basi bwana mie nikamuoa fatuma na nilikaa nae nyumbani kama weeek. Kwa uo mda lemi ye alinishanitangulia . Yani alishaondoka baada ya mimi kuoa tu. Basi mie nikatulia nyumbani na mke wangu nakula saba kwanza. Basi apo mama alituhusiana sana . Juu ya ndoa . Walitueleza mengi kuwa ndoa ni kuvumilana kupendana na kuheshimiana. Asa mama alinisihi sana kuwa nikawe makini na mtoto wa watu kwenye miji ya watu uko . Nikasema sawa mama. Basii mama akawa anamwambia fatuma.yani akikutesa uyu we nipigie simu. Mama bwana asa mm naanzaje kumtesa fatuma ninavyompenda uyu mwanamke dunia ya mwisho. Nampenda sana. Yani sanaaa . Mama anashindwa kuelewa tu.
Basi bwana . Baada ya week . Mimi nikaaaga nyumbani sasa kuwa naludi chuo kuendelea na masomo. Nikabeba na mke wangu. Basi tulisafir siku nzima akawa ananalalamika miguu inamuuma sana .nikawa namuelewa ni mimba ndo mana inakuwa hivi. Basi nampa ple. Namshika shika miguuu hivyo mpaka tumefika morogoro. Na tukapanda gari mpaka mkongeni tukashuka.mana iko ndo kijiji nilichopanga. Basi tumefika jioni kabisa. Mimi nilichoka ila fatuma alizidi alikuwa kachoka mnooo. Akafikia kulala tu. Basi bwana mie nikaenda kumtafutia chakura kwanza. Kisha nikaludi .nikamuasha akaoge.akanmbia nimechoka sana mume wangu. Ila nikambembeleza sana kuwa akaoge bdi akajivuta tu. Mie nikaenda kumuwekea maji chooni. Mana choo ni cha njee. Basi akaenda kuoga alipotoka. Akala. Akapanda kwenye godoro kupumzika. Na mm wala sikumshika kumsumbua mana nilishaelewa mke wangu kachoka.
Kesho yake asubuh sana nilimuamsha na nikamuelekeza mazingira yote ya pale. Na uzuri ile nyumba tulipanga wanafunzi 3 wote yani. So nyumbani anakuwa anabaki mwenyewe . So hakuna umbea umbea wala maneno. Mi nikamuachia elfu 10. Nikamwambia naingia chuo. Akanmbia sawa hakuna shida. Basi kweli mwanaume nikaingia chuo. Washikaji wakanipongeza sana matani kwa sana. Mi nikawa nacheka tu .na ratiba za class zikaendelea kama kawaida. Mda wa mchana sasa.kwanza nilimpigia simu mke wangu kujua anaendeleaje mana ni mgeni. Akanmbia naendelea vizur na yupo powa na ameamka vziri tu. Nikamuuliza umepika . Akanmbia ndio na sokoni nimepajua. Nikacheka nikasema pow tutaonana jioni. Basi ile nataka simu na princess anapita mbele yangu. Mh kanuna uyo akanipita shwaa ata hajanisalimia. Yani ni fyaaaaa. Ila kapendeza kawaka mtoto anajua kuvaaa uyu na lile figaa uko nyuma acha kabisa .mie nikaludi kukaa na mwanangu lemi tukisubili kipindi cha jioni
Lemi akanmbia daah unajua princess mpaka mm kaninunia .kanambia et mimi ni shemeji mnafiki mwanangu. Nikacheka.nikasema yule demu ana shida sana. Alikubali mwenyewe oooh ntakuwa na wewe uku ukiwa na mwanamke wako. Mala kaghairi anaitaka peke yake anaanza kujinunisha asa ata akinuna nani ana mjali ana hisi aende zake uko. Lemi akanmbia ila yule demu mwanangu umemuacha we una moyo. Ahaaaa acha tu ninyamaze mie nikacheka mana lemo nae ana tamaa msenge uyu basi bwana mimi ndo nikaanza maisha ya ndoa uku nikipambana na shule.mi sikuw na kikubwa sana. Pesa ya kuendesha maisha ni ya boom.ila nashukuru tu fatuma alikuwa ni mwanamke muelewa sana hakuwa na tamaa kabisa. Yan ananjua tunaishije .nilishamwambia anivumilie . Tupambane mpaka nitakapopata lazi kila kitu kitakaaa sawa.
Basi bwana siku zikawa zinaend na maisha yanasogea. Apo mm na princess ni tulikaushiana kabisa. Nikaanza kusikia tu scandal zake mala kuna leacture anatembea nae. Mala anatembea na mwanafunzi mwenzie wa mwaka wa pili . Ila mie wala.sikujalai nikawa busy na mambo yangu. Siku iyo sas nakumbuka ilikiwa mida kama ya saa 1 .nilikuwa natoka class nipo na lemi. Asa tunatoka hivi. Namuona princess amesimama anaongea na mwanaume. Ila ni kama wanabishana hivi. Mh mi nikasimama kwanza. Nikawa namsikia princes anamwambia kwani nn huelewi hujui kukataliwa nimeshakwambia sikutaki ebu niache. Alafu yule mwanaume ni kama anabembeleza ila anabembeleza kwa fujo na kufosi. Aseee nikasogea mpaka pale .nikauliza nn apa. Kuna nn yani. Princess akanyamaza kimya yule jamaa namjua ni mwaka wa 3. Na yeye uwa anakujaga na gari apa chuo anaitwa jeff. Akasema.we bwana mdogo nn ebu acha mi naongea na mwanamke wangu apa. Nikasema.asa mbona kama unafosi broo. Mwanamke si anakwambia hakutaki ama..hujui kukataliwa . Yule jamaaa akanambia dogo ebu sepa bwnaa nn sasa unaingialia visivyokuhusu. Nikamuanagalia sana uyu jamaa. Kisha nikamshika mkono princess nikamvuta. Akawa hataki. Nilimkata jicho moja tu. Akajinyamazisha kimya .nikamvuta mpaka pembeni. Nikamwambia unajifanya unakaataa nini kimaraya maraya . Akanmbia kwani yanakuhusu unaingilia nn sasa si ungeniachia tu
Nikasemaa unazani kukutoa pale kwamba mimi nakuhitaji ww. Ebu acha upumbavu wako. Wewe. Nimeona unapata shida alafu ww ni mtoto wakike .angekubaka bule. Akaningalia kisha akanisonyaaa .kisha uyo akaondoka zake. Mie nikaludi kwa lemi tukasepa .ila lemi akanmbia mh we bado unamtaka princess mbona imekuwa vile.nikasema mm sipendi kuona mwanamke anaonewa mbele yangu .lemi akanmbia fresh mwanagu. Kisha uyo mie nikakudi kwangu. Kwa fatima wangu. Na mda uo fatuma mimba yake ilikuwa na miezi 3. Ila ilikuwa inamsumbua sumbua aswaa vyakula anachagua chagua namuelewa ni hali yake basi napambana nae tu. Basi ikakata kama week sikuonana na princess kabisa . Na nikawa busy na mambo yangu tu. Siku iyo sasa nimekaa zangu classs nachezea simu. Nikaona kuna mtu kampost princess anavalishwa pete. Alafu kaweka captain kaandika nikiwa mkubwa nataka kuwa kama ww da princess. Mh uyu alopost ni alikuwa mdada nasom nae . Asa si ile kuview status ndo naona mh nikaangalia vizur mna sikuelewa nimepatwa na hali gani. Kwanza alipendeza kinoma alafu na ata uyo mwanaume niliona alikuwa njema ndo kamvisha pete sasa. Nilikuwa na lemi nimamuonesha ile picha .nikamuuliza oyaa mwanagu uyu sio princess kweli. Lemi akanmbia mh ndo mwenyewe mbona kama.anavishwa pete ya ndoa na nani tena? Nikasema sijuh nimeona kapostiwa tu. Mh lemi akaningalia akanmbia kwani umeumia. Nikasema kwannn niumie sasa .si ni moja ya maisha yake jamani. Lemi.akanmbia powa kaka. Ila sio siri mi niliumia kinoma kuona uyu demu kavalishwa pete. Yani moyo uliuma kisenge yani petee tena..alafu ana furaha mnoo.
Mh nikajikuta nimemtumia sms. Nikamwmbia hongrra kwa kuvalishwa pete .akanmbia thanks. Daaah yani anasema kabisa thanks. Nikamuuliza so ndoa lini. Akanijibu soon tu. Mh nikamjibu powa kisha nikakausha aseee nilihis kamoyo kanauma mnooo. Badi tumetoka class na yeye namuona kwa mbali . Yupo na rafiki zake anacheka sanaa na wenzie. Aseeeee sielewi ata kwa nn na wakati nna mke nyumbani. Ila moyo ukauma kisenge mpaka nikachange lemi akaniuliza we vp huendi kwako leo. Nikasema sikia nataka kuongea na princess. Lemi akanishangaa kasem princess tena. Unataka kuongea nae nini sasa na humtaki. Nikasema lemi muite princess aje room kwako mwambie una maongezi nae muhimu nataka kuongea nae . Mh lemi akaningalia akacheka akanmbia ahaaa kumbe unampenda sio. We demu yule mkari sio masihara kumuacha demu kisenge senge kama yule kama vipi wewe kuwa nao wote kwani sh ngapi. Mmoja yupo chuo mwengine yupo nyumbani. Nikasema sikia acha maneno mengi mpigie. KWeli lemi akampigia aikuchukua mda princess akapokea . Lemi akasema princess sikia bwana unajua nn kun issue nataka tuongee kidogo achana na mambo ya zamani. Princess akasema sitaki drama zenu naomba mniache. Lemi mimi na ww tuna cha kuongea kipi. Lemi akasema kipo bwana ni issue zengine wala sio za kuhusu haji no. Njooo hostels ni issye ambayo inataka wote tuwe tumetulia. Princes akasema hapana siwezi kuja kisha akakata simu daah roho ikauma. Yani anajikuta nani. Lemi akaniangalia akanambia si umemsikia mchumba kakataaa kuja.nikasema powaa
π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
