ABEE SHEMEJI….(1)
MTUNZI…EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
WatsApp…+255718 862176
AGE…(18+)
*******
“No Kassim. Hapana! Si..wezi, Mungu wangu….”
“Hajrath, nisikilize. Huwezi kufanya nini? Ndio ishatokea sasa”
“Ni mme wangu lakini”
“Namimi ni Kaka yangu, Hajrath. Niangalie usoni”
“N..o Siwezi, Eeeh Mungu wangu. Ahmed Ahmed amka basi”
Kila mtu alionekana kupigwa na butwaa usiku wa siku hiyo, siyo Hajrath wala Kassim.
Kila mtu alipagawa vya kutosha. Lakini mmoja wapo kati ya watu hao wawili, alionekana kuchanganyikiwa zaidi, huyu ni Hajrath alikuwa mara azunguke mara ashike hiki. Hakuamini kama mme wake wa ndoa yupo chini, amelala katulia. Kichwani kwake ilikuja taswira ya milango ya gereza, inafunguka nayeye kutupwa ndani, jambo hilo lilionekana kumchanganya zaidi. Sio yeye tu, hata Mwanamme huyo Kassim, aliyekuwa pembeni yake.
Aliyekuwa amelala chini ni kaka yake, tumbo moja! Ni wazi kwamba endapo siri hiyo ingevuja wasingetoka salama, ndiyo maana walikuwa wanahaha, kutafakari ni kitu gani wakifanye.
“We..we ndio umesababisha, shemeji”
“Huu, sio muda wa kulaumiana. Wewe ndio chanzo”
“Hapana wewe ndio umemuua”
“Sasa tutafanya ni..ni?”
“Siju..i”
Haikuwa kazi rahisi kutoa maamuzi, mtu aliyekuwa amelala chini alikuwa ahemi wala hajigusi.
“No, Ahmed please. Wake up mme wan..ngu”
Hajrath, bado hakuamini kama mmewe amelala sakafuni haongei kitu, ndio maana alikuwa akimwaga machozi, anaongea kwa kwikwi.
Alitamani walau mwanamme huyo aseme japo neno la mwisho, wakati mwingine alijilaumu kwa upumbavu wake ikapelekea mpaka mmewe kufariki dunia, kifupi yeye ndio alikuwa mkandarasi wa kila kitu kutokea.
“Shemeji”
Kassim akamuita Hajrath huku akimuangalia kaka yake, aliyekuwa chini sakafuni amelala. Badala ya Hajrath, kuitikia alimuangalia tu kumaanisha kwamba anamsikiliza, anaweza kuongea.
“Inabidi hii ibaki kuwa siri yetu”
“Kassim, sijakuelewa…Hili swal..a lazima nilipeleke polis..i”
“Polisi? Ukaseme nini? Wewe ndio chanzo”
“Kwanini umemuua kaka yako?”
“Mimi, sijamuuwa wewe ndio umemuua”
Hajrath na Kassim walizidi kubishana, juu ya kitu gani wakifanye.
Ki ukweli ulikuwa ni msala mkubwa endapo jambo hilo lingefika kituo cha polisi. Ni dhahiri kwamba hakuna hata mmoja kati yao angeachwa salama, kutokana na tukio hilo lililotokea, hiyo ilifanya kila mtu amtupie mpira mwenzake. Baada ya kulumbana sana, wakiwa seblen wakaamua kutoka na wazo kwamba wakaitupe maiti hiyo mbali, ili kupoteza ushahidi.
“Kassi..m, Oooh My God, kwanini mimi?”
Hajrath alilalamika huku akiweka mikono yake kichwani na kupiga piga miguu yake chini, baada ya kumuona Shemeji yake anatoka nje na funguo za gari.
Roho ilimuuma vilevile, mwanamme huyo kwa kitendo alichomfanyia kaka yake, sambamba na kuumia moyo alimlaumu sana Shetani. Licha ya yote hayo hakuwa na jinsi zaidi ya kuingia ndani ya gari na kulirudisha kinyumenyume kwa kasi mpaka karibu na mlango kabisa, akaretemka na kuliacha linaunguruma. Alivyoingia ndani, akatembea kwa kasi mpaka karibu na maiti ya kaka yake.
Akaitizama maiti hiyo iliyokuwa chini sakafuni, moyo ukamuuma ajabu, lakini hakuwa na jinsi ilikuwa ni lazima apige moyo konde kwani maji yalikuwa tayari yashamwagika, ni vigumu kuzoleka!
“Nisaidie tum-bebe”
Hapo, ndipo Hajrath alipozidi kuchanganyikiwa zaidi. Ilikuwa ni lazima wakubali kilichotokea ili wasonge mbele kwani hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa tayari kuingia kwenye matatizo makubwa na ilikuwa ni lazima wafanye jambo hilo wasionekane na wabaki na siri hiyo nzito mpaka kifo chao.
“Mnyanyue kwa huko.” Kassim, akaamuru.
Hajrath akapiga moyo konde, akamnyanyua mme wake wakambeba. Yeye akamshika kwa upande wa kichwani, Kassim chini upande wa miguu wakaanza kumtoa nje. Walivyofika huko wakasaidiana kumuingiza ndani ya gari.
“Shem”
Kassim, akaita kabla ya kuingia ndani ya gari.
“ABEE SHEMEJI”
“Hatuwezi kumtupa hivi, inabidi tumuweke ndani ya gunia. Una gunia lolote? Ama mfuko mkubwa?”
“Ngoja, nikaangalie stoo. Nisubiri”
Roho ya uwoga ikamtoka Hajrath, akavaa ujasiri ambao hata yeye mwenyewe alijishangaa kabisa.
Akatembea mpaka jikoni. Huko aliingia stoo, akaanza kutupa macho yake huku na kule, akaona gunia alivyolishika na kulifunua akaona kuna viazi, akavimwaga chini vyote kwa haraka na kutoka mbiombio mpaka nje.
“Liweke gunia hilo ndani, fanya haraka ingia twende”
Kitendo cha Hajrath kuingia, gari ikapigwa moto na safari ikaanza mara moja.
“Tunaenda wapi?”
Hajrath, akauliza huku akimuangalia shemeji yake, bado hakuamini kama mmewe amekufa tayari na yeye pamoja na Kassim walikuwa wakandarasi wa jambo hilo kutokea, wakati mwingine alidhani yu ndotoni japokuwa alitamani iwe hivyo ashtuke ili amkute Ahmed wake, yupo hai lakini jambo hilo halikuwezekana kwani kilichokuwa kimetokea kilikuwa ni ukweli, sio siri usiku huo kwake ulikuwa ni sawa na Jehanam.
“Bado sijajua”
Ni kweli Kassim, alikuwa katika dimbwi la mawazo mengi sana!
Hakutaka kuamini kama Kaka yake kipenzi amekufa kisa Mwanamke huyo shetani aliyekuwa kushoto kwake, mara ghafla roho chafu ikamvaa ikamwambia ammalize pia na Hajrath kwani bila mwanamke huyo wenda asingejikuta katika matatizo makubwa namna hiyo.
“Kwanini uliniita? Kwanini umenifanya nimuuwe kaka yangu? Wewe Malaya naongea nawewe”Kassim, akauliza kwa ukali na kufoka.
“Kwa sababu nakupenda”
“Nyamaza, Kahaba wewe. Tena funga bakuli lako!Wema wangu umeniponza, bora ningemuacha akuuwe tu, ona sasa ulichokifanya”
“Kassim, lakini in..”
“Lakini nini? Lakini nini? Yote umetaka wewe? Kwanini lakini, umetumwa au? Najuta kukufahamu. Yaa…”
Ghafla ukazuka ugomvi mkubwa, Kassim alifoka kwa sauti ya juu, akionekana kujuta.
Akatamani muda urudi nyuma, arekebishe kilichotokea lakini muujiza huo kamwe usingetokea, hata angeenda kwa Mganga yoyote yule! Kifupi maisha yake yasingekuwa na amani hata kidogo kuanzia siku hiyo. Damu ya kaka yake ilikuwa mikononi mwake, kilichomfanya akatishe sentensi yake ni baada ya kuangalia ‘site mirror’ za pembeni, akaona gari linamulika mulika taa, kuashiria kwamba asimame, alivyoangalia vizuri akagundua ni gari ndogo aina ya Vitz.
“Kuna gari inatuwashia taa nyuma, unaifahamu?”
Kassim, akauliza. Hiyo ilimfanya Hajrath ageuke nyuma.
“Mungu wangu!”
“Nini?”
“Gari ya Tonny hiyo”
“Tonny! Ndo nani?”
“Rafiki yake Ahmed, please simama”
“Nisimame!? Hivi una wazimu wewe mwanamke?”
“Hapana, nakuomba simama. Alafu niachie mimi, nakuomba.”
Kwa hofu na mashaka ilibidi Kassim, aweke mguu kati na kuweka gari kando.
Gari la nyuma yake pia likasimama, akashuka mwanamme mmoja mrefu kiasi, mwenye rangi ya maji ya kunde. Akatembea mpaka karibu kabisa na gari ndogo aina ya Verrosa, kwa kuwa vioo vilikuwa vyeusi sana hakuweza kujua ni nani anaendesha gari. Akagonga kioo! Kikashushwa taratibu, sura ya Kassim ikaonekana, pembeni kushoto yupo Hajrath.
“Tonny, mambo”
Hajrath akawa wa kwanza kusalimia.
“Poa shem, nilijua upo na Ahmed. Yuko wapi?”
“Ndio tunaenda kumchukua, amenipigia simu. Si unajua mimi siwezi kudrive usiku. By the way. Huyu ni shemeji yangu, mdogo wake na Ahmed, anaitwa Kassim”
Hajrath aliongea kwa pupa, kwaniya ya kutaka Tonny aondoke ili yeye na Kassim wamalize walichokianza.
“Niaje broo”
Tonny, akamsalimia Kassim.
“Poa”
“Anywei. Nitamcheki kwenye simu kesho. Msalimie sana”
Hata kabla ya Tonny kumalizia kuaga vizuri, Kassim akawa tayari amepiga gari moto na kuliondosha mahali hapo kwa kasi.
Aliamini kuendelea kubaki eneo hilo, wenda ungeibuka msala mwingine kwani Tonny angechungulia kidogo ndani angeuona mwili wa Ahmed na huo ndio ungekuwa mwisho wao! Ndani ya gari kukatokea ukimya wa ajabu, Kassim alikuwa akitafakari ni wapi, akautupe mwili huo ili mtu yoyote yule asijue ulipo. Hapo ndipo alipopata wazo la kwamba waende kumtupa katika pori lenye miti lililokuwa Mbweni, kwa kufanya hivyo waliamini hakuna mtu yoyote Yule angejua ni wapi Ahmed alipo.
Dakika kumi baadaye, wakawa tayari wamelifikia pori hilo, wakazima taa na kushuka, wakateremsha gunia na kuushusha mwili wa Ahmed chini, hapo ndipo walipoanza kuuweka ndani ya gunia huku wakitizama huku na kule kama wanaonwa.
Walivyohakikisha wamemaliza shughuli hiyo nzito, wakalifunga gunia kwa juu na kamba, wakalibeba gunia. Wakatembea nalo mpaka katikati kabisa ya pori, lililokuwa lina giza kuliko kawaida, wakamtupa chini.
“Naomba hii ibaki kuwa siri yetu”
“Sasa tutasema nini? Akiuliziwa?”
“Nitakwambia cha kufanya, tuondoke”
Hakuna hata mmoja kati yao aliyekubali kuamini kwamba Ahmed, amefariki tayari.
Mbali na hapo wao ndio walikuwa wakandarasi wa kila kitu kutokea, kwa haraka wakatembea mpaka walipoacha gari, wakaingia na kuondoka zao kwa kasi!
Gunia, lililokuwa limetupwa porini ndani yupo Ahmed, lilianza kutingishika kwa nje, baada ya dakika thelathini kupita tangu liwekwe eneo hilo, kumaanisha ya kwamba, Ahmed hakuwa
amekufa kama walivyodhani.
********
TANZANIA ARUSHA(Ngulelo) 1999.
“Darling, unajua wewe ni mzuri sana”
“Ahsante baby”
“Nakupenda, naomba usije ukaniumiza”
“Siwezi mpenzi”
Haukuwa utani hata kidogo, ungebahatika kumuona mwanamke anayesifiwa wallah, usingebisha.
Ungekiri kwamba mwanamke huyo hana kasoro yoyote ile, ni wazi kabisa Mungu alimpendelea katika uumbaji wake. Rangi yake haikuwa ya kung’aa, bali maji ya kunde, hakuwa mwenye macho makubwa wala madogo bali ya wastani lakini wakati wote yalikuwa yamelegea, midomo yake ndio usiseme, alikua ana ‘lips’ pana. Zilizofanya mwanamme yoyote Yule atamani kuzinyonya.
Kuongezea hapo, alikuwa amejaaliwa katika maumbile. Hiyo ndio ilifanya mwanamme yoyote rijali ageuze shingo yake nyuma, endapo akipita mbele yake. Ahmed, alikuwa amelala kitandani, anamuangalia Mpenzi wake jinsi alivyoumbika, mbaya zaidi alikuwa ametoka kuoga, amevaa kanga moja tena imelowana. Hiyo ikafanya damu yake ianze kumwenda mbio kwa mara nyingine.
“Hajrath”
Ahmed, akaita huku akimeza mate ya uchu.
Japokuwa alikuwa ndege ni wake lakini alionekana kuwa na ugwadu kana kwamba ndio siku yake ya kwanza kukutana naye kitandani!
“Abee Mpenzi”
Hajrath, akaitikia. Namna alivyozungumza ni wazi kabisa ungedhani ana mapozi ama maringo, kumbe ndivyo alivyo. Akamuangalia Mpenzi wake aliyekuwa bado yupo kitandani, amejifunika na shuka hana nguo hata moja.
“Njoo nikwambie kitu”
“Uniambie nini? Huna lolote, najua unachokitaka”
Kwa hali ilivyokuwa na jinsi ambavyo Ahmed, alivyokuwa akimuangalia Mpenzi wake, ilionekana wazi kabisa kuna zoezi pevu anataka kulifanya.
Hajrath aliligundua hilo, baada ya kuona shuka alilojifunika Ahmed limetuna kwa mbele, kama mwanamke mtu mzima akajua ni kitu gani, anatakiwa kukifanya. Akadondosha kanga chini na kupanda kitandani, akamsogelea Ahmed midomoni wakaanza kulana denda. Ilikuwa ni wazi kabisa kila mtu, alikuwa ana moto kwani walianza kushikana huku na kule taratibu sana, wakabinuana kitandani huku wakikwaruzana migongoni. Hajrath, akawekwa chali, akawa anaangalia juu kwenye paa. Hapohapo, Ahmed, akajisogeza kidogo na kutoa ulimi wake, akaugusisha kwenye chuchu za Hajrath.
“Yeeees Beeeeibiii”
Kilichosikika hapo ni miguno na Hajrath hakuwa anajielewa tena, zaidi ya kufumba macho na kuvuta vuta mashuka, ni dhahiri kwamba alikuwa yupo katika dunia nyingine ya huba!
Je nini kitaendelea?
Usikose toleo lijalo.
ITAENDELEA.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi