SHEMEJI UNAINGIZA YOTE KWANGU? xxxxxx======xxxxxx======xxxxxx 1 - - - - - - 5 SEHEMU YA 1
Huwenda wengu hamjawahi kupitia hili jipya nililopitia mimi kwenye hiki kitu kiitwacho maisha.....wanaume hawa🙌🙌nawaita mara mbili. Si mara moja tena........
😁manake kwanza nicheke halafu nipoze them niendelee...sasa...
Nilipokuwa na miaka mitano niliweza kumuokota mtoto mdogo mwenye miaka minne akiwa katika mazingira ya kutelekezwa.
Isingekuwa rahisi kumuacha katika mazingira magumu namna hii. Nilimpa amri dreva wangu amchukue.
Nilipomfikisha nyumbani Mama yangu alitaka kunigomea kumpokea mtu niliyemsaidia. Lakini nilionesha msimamo wangu kuwa ni lazima tumsaidie.
Alikuwa na jina baya eti Shida, niliamua kumuita Manuu....kwa kifupi nilikuwa kama Mama yake.
Nilimlazimisha Baba yangu amuweke darasa moja na Mimi. Katika mambo yote sikuacha kumkumbusha aina ya uhusiano wetu
"Sisi siyo ndugu ni marafiki....kamwe usije kusahau hili"
"Sawa Vailet" Hili ndilo lilikuwa jibu lake
Tulipokuwa darasani watu wote tulimchukulia poa lakini ghafla tulianza kumuogopa....alikuwa anajua kila kitu. Kuna muda alikuwa ana mkosoa hadi Mwalimu.
Matokeo yake yalikuwa mazuri sana ukilinganisha na Mimi.
Hali hii iliendelea hadi tulipofika Chuo kikuu. Hakuwa mtu wa kusoma lakini kwa jinsi alivyokuwa anafanya vizuri kila mtu alitamani kuwa karibu yake. Alifamika kama Manuu kipanga.
Kuna muda alikaa na Wakufunzi kushauriana ni mbinu gani itumike kuleta ufahulu mzuri kwa wanachuo wote.
Sikujali sana kwa sababu niliamini hata nikifeli darasani ajira kwangu ni uhakika. Si unajua tena sisi wengine wazazi wetu wameanza kujitafuta kitambo sana.
Siku moja nikiwa Supermarket niliitwa na Mkaka mzuri sana mfano wake sijawahi kuona.
Tulibadilishana namba, alikuwa ananijali sana asikuambie mtu. Kitu kilichonivutia kutoka kwake alikuwa ni mtu wa mafanikio sana. Alikuwa ana fahamiana na watu maarufu duniani na hata kuna wengine walikuwa wanakopa pesa. Na hapa ndipo nilipata kujifunza unaweza kuwa maarufu na usiwe na kibunda.
Jioni moja aliniomba tupate wote dinner, hata kama ningekuwa na sumbuliwa na kuhara nisingekataa.
Ule msemo usemao mkataa pema kubaya kunamuita niliuzingatia sana.
Nilipendeza kuliko kawaida, kama ungeniona namna nilivyokuwa na ng'aa basi ungenifananisha na mwali wa kizaramo.
Niliachia tabasamu pana baada ya kumuona, Mwanaume huyu alikuwa ananukia kiasi kwamba aliyazima manukato yangu mfano wa mshumaa.
"Naomba unisaidie kufikisha ujumbe wangu kwa Manuu, mueleze ukweli kuwa nampenda" Fredo aliniambia hii kauli bila kupepesa macho yake
Sikutaka kuonesha kuchanganyikiwa, niliachia tabasamu la uongo ili hali ndani ya moyo wangu nikiumia
"Kwahiyo wewe hapo unataka ni kusaidie kumpata Manuu?...kwanini usimkabili kwa macho yako mwenyewe. Pengine hujijui tu lakini katika ulimwengu huu sidhani kama kuna mwanamke anayeweza kusema hapana mbele yako" Niliongea
"Siyo kwamba sina ujasiri wa kumkabili Manuu. Lakini najikuta najiona kama punje ya mchele kwake. Sijui ni muelezeeje tu lakini Manuu ni tishio machoni kwa Wanaume. Siku ya kwanza namuona moyo wangu ulilipuka mithili ya mafuta ya taa na kiberiti. Nilihitaji kukuzoea wewe kwanza ili iwe rahisi kutimiza ndoto zangu" Fredo aliongea akiwa kazama katika hisia kabisa
"Mueleze kuwa Manuu ana kifafa uone ni kitu gani atafanya" Wazo hili lilikuja kichwani mwangu. Nilitaka kulifanyia kazi lakini nafsi ilinisuta
"Sawa Fredo, nitakufikishia ujumbe wako....jibu lolote atakalo nipatia nitakujulisha hivyo itapendeza kama utajiandaa kiakili" Niliongea
Fredo alinyanyua glass juu kuashiria yupo tayari kwa lolote.
Basi baada ya dinner kumalizika alinipeleka mpaka nyumbani.
"Usiku mwema" Alizungumza baada ya kuubusu mkono wangu
"Usiku mwema pia..." Niliongea ilihali nikihisi hali ya utofauti mwilini mwangu, fikiria ni busu tu kama angenishika nyonyo hata kwa bahati huenda ningeiona pepo si kwa kuchanganywa huku na uzuri wake.
Baada ya kuingia ndani, nilielekea moja kwa moja chumbani kwa Manuu.
"Dinner yako imeendaje na bwana Fredo" Manuu aliniuliza kwa sababu nilikuwa nishamtambia kuwa Mwanaume huyu ananitaka ni vile tu anapita njia za panya kunieleza ya moyoni
Niliweka pochi yangu mezani nikiwa sijui hata ni kitu gani namueleza.
Tukutane sehemu ya pili kila kitu kitafahamika.
🍭
SEHEMU YA 2
"Kila kitu kimeenda vizuri, Fredo ana tabia za kizungu bado anaendelea kupiga kona huku na kule...." Niliongopa kiasi cha kujihurumia
"Anatumia mbinu ya tatu katika saba zitumiwazo na Wanaume" Manuu aliongea huku akitabasamu
"Una maanisha nini"
"Ana tengeneza ukaribu kwanza ili iwe rahisi kuwasilisha jambo lake. Na hata hivyo mambo mazuri hayahitaji haraka"
"Ahsante kwa maneno yako mazuri....naona upo unasoma kitabu wacha nikaongee na Mama kwanza..." Nilimuaga Manuu
Mlango wa chumbani kwa Mama ulikuwa umeegeshwa tu, bila shaka aliuacha wazi kwa ajili ya Baba.
Sijui ni kitu gani Mama yangu alikuwa anafikiria, mpaka nakaa karibu naye hakushtuka kabisa kama nipo karibu yake.
Macho yake yalikuwa kwenye bahasha kumi zilizojipanga, sikuelewa ni mchezo gani anafanya. Niliamua kumfahamisha uwepo wangu kwa kumshika mkono
"Wee kapanya kadogo umefikaje hapa" Aliniuliza
"Nimepita hapo mlangoni, inaonekana akili yako ilikuwa Uturuki, na hiki mezani ni nini namaanisha hizi bahasha" Niliuliza
"Hizi ni bahasha kutoka kwa Vijana Wasomi na maarufu hapa Tanzania. Wote hawa wanaomba kumuoa Manuu pindi atakapo maliza Chuo mwaka huu. Hakuna barua hata moja inayojieleza kuhusu wewe" Mama aliongea
Nilikodoa macho nisijue niseme nini
"Miaka 20 iliyopita ulimsaidia Manuu kwa wema tu. Nakumbuka alikuwa anaitwa Shida lakini wewe huyo uliona anafaa kupewa jina zuri ukamuita Manuu. Mwanangu ulikosea sana kumsaidia....yaani majanga yake yote na mikosi yake yote imehamia kwako."
"Sikuelewi Mama...."
"Ndiyo, wewe huyo huwezi kunielewa Mimi kwa sababu akili yako yote inafikiria kuhusu maisha ya Manuu na siyo yako. Kesho nitakupeleka nyumbani kwa Nabii atakufafanulia vizuri namna ulivyofanya kosa kumsaidia Manuu" Mama aliongea
Nilizikusanya barua zote kumi kisha ni kaanza kusoma moja baada ya nyingine.
Wanaume wote waliokuwa wamejieleza kwenye barua tofauti nilikuwa na wafahamu. Ni watu maarufu sana na wote hawa bado hawajaoa.....
"Fredo ni wa kumi na moja" Nilijisemea ndani ya moyo wangu. Sikutaka kuonesha kuvurugika, nilimshika Mama mkono
"Nabii ni binadamu kama wewe, kila kitu kina muda wake....naumia kuona unamuonea wivu mtu ambaye kama siyo Mimi hata asingefika hapo alipo" Nilijiongelesha
"Sawa, unaweza kwenda....nina uhakika muda si mrefu utakuja kuniuliza ni kitu gani ufanye kuhusiana na Manuu" Mama aliongea
Nilimkabidhi bahasha zote kisha ni kaenda chumbani kwangu kulala.
Saa kumi na mbili alfajiri Fredo alinipigia simu kusikia kuhusiana na kazi aliyonipatia
"Kasema nipe muda atanijibu naomba uwe mvumilivu" Niliongopa
Basi Fredo alinipigisha stori za hapa na pale, aliendelea kuniweka karibu kama ungetuona basi ungehisi tupo kwenye uhusiano lakini ukweli ni kwamba tulikuwa marafiki tu.
"Kwa wakati huu naomba usikatae wala kujieleza. Kuna barua hapa imeletwa kwa ajili yako inahusiana na ndoa" Mama aliongea kiasi cha machozi kumtiririka
Niliishika barua pamoja na picha iliyokuwa kwenye bahasha nyingine. Moyo wangu ulishtuka baada ya kumuona Fredo....
"Unasema huyu ni mtoto wa rafiki yako?...yeye ndio ametaka kuoa au Wazazi wake ndio wameona inafaa kwake kuoa" Niliuliza
"Wazazi wake ndio wameamua, ni watu wa sheria sana kiasi kwamba hata kama ana mchumba wake hawezi kumuoa atafuata chaguo la Wazazi" Mama aliongea
Nilirudia kuisoma barua kwa umakini ndipo niligundua Mama yangu hakuisoma vizuri.
Barua ilimtaka rafiki wa Vailet na si Vailet.
Kama nitamsahihisha katika hili basi atavunjika moyo. Niliondoka hadi chumbani kwangu. Nilianza kuichapa upya.....niliondoa neno rafiki wa Vailet ni kaacha Vailet. Nilihakikisha barua ya kwanza na ya pili zinafanana.
"Nisamehe Manuu" Nilijisemea moyoni mwangu huku ni kiiteketeza barua ya kwanza.
Nilimrudishia barua Mama ni kiamini atakuja kumkabidhi Baba
"Mama, hakukuwa na haja ya kufikiria kuhusu Nabii. Nadhani sasa umejionea kwa macho yako kuwa wakati wangu haukuwa umefika...." Niliongea
Mama yangu alitikisa kichwa kuashiria ndiyo lakini ukweli ulibakia ndani ya moyo wangu.
Usikose kipande cha tatu
🍭
SEHEMU YA 3
Zilikuwa zimesalia wiki tatu tufanye mitihani ya UE.
Manuu alikuwa bize sana na kujisomea, huwa si mtu wa kujisomea ila kwa wakati huu alijisomea.
Sikutaka kusumbuka, unajua bhana kuna sehemu za kutumia nguvu nyingi kusoma kama sekondari au advance lakini si Chuo. Nadhani mliopita huku mnaelewa nini naongelea.
Zikiwa zimebakia siku mbili tufanye mitihani ya kumaliza Chuo. Baba yangu aliniletea mitihani yote mitano....alinisisitiza nimuoneshe na Manuu lakini sikutaka kufanya hivyo.
Swala la Chuo liliisha, na hapo ndipo nilifungiwa ndani kwa wiki nzima. Kila sehemu ya mwili wangu ilikuwa inanogeshwa.... nilikuwa kama Mtoto jamani.
"Kwanini mikono yako inatetemeka" Mama yangu aliniuliza ikiwa ni siku yangu ya harusi
"Sijawahi kuvaa hili vazi Mama" Niliongea
Mama yangu ni kutabasamu tu, ilikuwa ni sheria ya Wakwe zangu kunifuata.
Walikuwa makini sana hawakuweza kuchelewa walifika kwa wakati.
Nilimuona Mama yake Fredo akishtuka, aliniangalia kwa sekunde kadhaa.
Alipiga hatua akanisogelea tukawa pua na mdomo. Hakuishia kunitazama alinikumbatia.
"Bila shaka ilitokea dosari wakati wa kuchapa barua, siyo wewe tulikutaka. Lakini kwa heshima iliyopo kati wetu na Wazazi wako nitakupokea nikiamini utakuwa mwema kwa Fredo" Alininong'oneza
Nilijitia kushangaa kusikia eti kuna dosari ilijitokeza wakati wa kuchapa barua.
Basi niliingizwa kwenye gari, Wazazi wangu pamoja na Manuu waliingia kwenye gari lao pia.
Nilipofika Kanisani moyo ulishtuka baada ya kukutana macho na Fredo.
Macho yake yaliguswa na mshtuko pia bila shaka alikuwa anategemea kumuona Manuu na si Mimi.
Nilikaza moyo kwa kuwa Mimi ndio nilibadili barua basi natakiwa kuvumilia kila kitu.
Taratibu za ndoa zilifuatwa, tulikula kiapo na kuvikana pete.
Ile Mchungaji anataka kufunga kila kitu watu tuende ukumbini Manuu alinyoosha mkono.
Mmmh anataka kusema nini tena!
"Naomba niongee maneno machache tu..." Manuu aliongea kisha akamtazama Fredo
Cha ajabu alikosa cha kuongea wakabakia kutazamana.
"Manuu...." Nilimrudisha dunia baada ya kuona akili yake ni kama imehama hivi
"Fredo hakikisha unakuwa Mume bora kwa Vailet na si Bora Mume" Manuu aliongea haya maneno
Watu wote walifurahia lakini kwa upande wangu nilikataa kuamini haya maneno. Nina uhakika kuna jambo Manuu alitaka kulimwaga hadharani.
Nilijiahidi kumuuliza kwa njia yoyote ile, basi tulielekea ukumbini kumalizia sherehe.
Muda wote macho ya Fredo yalikuwa kwa Manuu. Ni kama walikuwa wanaangaliana hivi kwa kuibia.
"Ni lini na saa ngapi watu hawa wameanza kutazamana namna hii" Nilijiuliza kwa sababu muda wote Manuu alikuwa ni mtu wa vitabu.
"Samahani huu ni ujumbe wako...." Mwenyekiti wa kamati aliniletea
Isingekuwa rahisi kuvumilia hadi sherehe iishe eti ndio niusome.
Nilielekea chooni nikiwa na matron wangu.
Yeye alibakia kwa nje kisha Mimi nikaingia ndani
Nilijikuta ni kiogopa kuifungua bahasha. Na hata mikono yangu ilianza kutetemeka bila sababu ya msingi.
Nilijipiga moyo konde ni kaifungua bahasha.
Nilishangaa kukutana na ile barua ya kwanza iliyoletwa nyumbani kwetu kwa ajili ya Manuu.
Sikuelewa huu ujumbe umetoka kwa nani maana kama ni familia ya Fredo wanajua changamoto ilikuwa ni wao kukosea barua ingawa Mimi ndio nilibadilisha.
Niliinusa barua kwa umakini kuna harufu ya marashi niliyanusa yalikuwa ni kama ya Manuu...
Ina maana Manuu anaijua hii siri au kuna mtu anataka kutuchonganisha, sikupata majibu niliiflash karatasi chooni. Ile nafungua mlango nitoke nilikutana na Manuu akiwa kashika bahasha sawa na niliyokuwa nayo Mimi. Tena siyo kuishika tu alionekana kuusoma ujumbe pia.
Usikose sehemu ya nne
🍭
SEHEMU YA 4
Manuu hakuongea chochote badala yake alinikumbatia.
"Mbona unanikumbatia katika mazingira haya..." Nilijiongelesha huku ni kijaribu kuichungulia barua ya Manuu
"Ombi lako limepita, nitakuwa house girl nyumbani kwako mpaka pale utakapopata mtu mwingine unayemuamini, hukuwa na haja ya kuniandikia barua" Manuu aliongea
Mmmh sikujua hata nisemeje, kumbe karatasi aliyokuwa ameshika Manuu ilikuwa tofauti na niliyotumiwa. Kidogo nilipata amani ya moyo.
Japo barua ilikuwa imechapwa lakini niligundua ni akili ya Mama. Ni mtu ambaye amekuwa na hofu kuhusu kesho yangu kupita kiasi
Matron alinisihi nirudi ukumbini kuepusha minong'ono.
Nilikaa kama dakika 10 hivi ndipo Manuu alirejea tena. Hali ya yeye kutazamana na Fredo ilinikwaza....niliamua kufatilia kwa ukaribu ndipo niligundua Manuu ananiangalia Mimi na si Fredo.
Presha la moyo wangu lilishuka baada ya kugundua Manuu hana muda na Fredo.
Hatimaye kila kitu kilifikia tamati, isingekuwa rahisi kuelekea moja kwa moja nyumbani kwa Fredo kutokana na utaratibu.
Tulilala hotelini, Fredo alitaka tuzungumze na si kufanya tendo la ndoa.
"Mimi na familia yangu tulikuwa tunamtaka Manuu.....siwezi kulaumu sana. Wakati Mama yangu anachapa barua alifanya makosa. Ilikuwa ni fedheha kubwa kwao kuieleza familia yako kuwa walikosea barua..... nachotaka kusema huenda hili jambo limeenda hivi kwa sababu maalumu, mwanzo nilikupenda kama rafiki lakini nitajitahidi kukupenda kama mke wangu. Nitamuondoa haraka sana Manuu ndani ya moyo wangu...." Fredo aliongea akiwa kanikazia macho
Nilijisogeza tararibu nikamkumbatia, yalikuwa ni maneno mazuri sana.
Kulivyo pambazuka asubuhi tulioga kisha tukaelekea kwetu. Japo sikuhusika kutoa hata shilingi mia lakini kwa kuwa nimekuwa mkewe chake ni changu.
Nilifarijika baada ya kumuona Manuu akifagia uwanja.
Bila shaka Mama yangu anataka nimchunge Manuu asije kuniletea uhuni.
Kitu kingine kilicho ni furahisha ni pale Fredo alipovunga kama hajamuona hivi.
Kazi yangu kubwa ilikuwa ni kula na kwenda chooni. Wafanyakazi walikuwa na jukumu la kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.
Asubuhi moja nikiwa bado kitandani nilishangaa kuona Fredo yupo dirishani. Alionekana kuchungulia.... niliamka tararibu ni kasogea dirishani.
Nilitaka kuona ni kitu gani hicho anaangalia kiasi cha kushindwa kusikia navyo tembea taratibu.
Nilishangaa kuona ana muangalia Manuu tena alikuwa hadi anacheka
"Huyu ni kichaa kweli kweli, anawezaje kuzungumza na ndege na hata wakasikilizana..." Fredo aliongea pekee yake
"Nani kichaa..." Nilimuuliza
"Si Manuu..." Fredo alijibu bila shaka akili yake ilikuwa mbali bado.
"Mwanaumeeeee" Nilimshtua
Eeh alishtuka balaa, sikutaka kuzungumza kuhusu ujinga wake. Nilimkumbusha ni muda wa kuoga
Nilitarajia atachangamka lakini haikuwa hivyo aliendelea kumtazama Manuu
Hii kitu ilinikera sana
Usikose kipande cha nne
🍭
SEHEMU YA 5
Sikutaka kumlazimisha tena kuhusu kuoga.
Mbinu ya Mama kumuweka karibu yangu Manuu siyo sahihi.
Ni msomi mzuri anatakiwa kutoka nje ajitegemee.
Niliingia bafuni kuoga baada ya kumaliza kila kitu nilimfuata Manuu
"Unatakiwa kukaa ofisini na si hapa, haiwezekani ufuate ndoto yangu. Sijui hata ni kitu gani niliwaza kukuita hapa" Niliongea
"Mumeo pia kaniahidi kunitafutia kazi, kadai si busara Mimi kukaa hapa..."
"Mume wangu kazungumza na wewe hizi habari?" Niliuliza kwa uso wa tabasamu ilihali ndani ya moyo wangu nikiwa na mshangao mkubwa
Manuu alitikisa kichwa kuashiria ndiyo.
"Fredo ni mtu wa kujali sana natumaini atatimiza maneno yake. Nitamzuia Baba kuingilia kati kuhusu hili....ni muda wa Mume wangu kujikusanyia sifa" Niliongea
Kwa pamoja tulicheka, lakini amani ya moyo wangu ilikuwa ni ndogo sana. Ingawa na umiliki mwili wa mume lakini nilipoteza kujiamini
"Nitaenda nyumbani kwenu muda wa mchana, Mama yako kaniita" Nilimuambia Mume wangu tukiwa tunapata chai
"Sawa, nadhani kesho nitaanza kuingia kazini nimepumzika vya kutosha...." Fredo aliongea huku akinishika shika nyonyo, nilijikuta ni kisisimka balaa na hata nikasahau kuhusu wasiwasi wangu.
Muda ulipofika nilijiandaa ni kaenda zangu kuonana na Mama mkwe wangu.
"Umekuja kwa wakati sahihi, kama ungechelewa kidogo tungepishana karibu sana" Mama mkwe wangu aliongea huku akinipokea mkoba, hadi niliona aibu aiseee
Hakuishia hapo aliniletea stuli sofa ni kanyoosha miguu yangu
"Unajua kuna siku nilitembelea Chuoni kwenu enzi hizo mnasoma, sikuwa pekee yangu niliambatana na Fredo pamoja na Baba yake. Na hiyo ndio siku tulimuona Manuu, hakika alituvutia sana lakini ndiyo hivyo hakuwa ridhiki yetu. Nimempa Fredo jukumu la kumtafutia kazi nzuri hivyo usije kufikiria tofauti" Mama mkwe wangu aliongea
"Nafurahi kuona mnajali kuhusu Manuu, Mimi na yeye tumetoka mbali sana.. " Niliongea
"Akili zako za kiutu uzima ndio zinanifanya niendelee kuvutiwa na wewe ingawa hukuwa chaguo letu. Utakula chakula gani," Mamkwe aliniuliza, si mnajua tena familia za kishua kama hizi kila mtu huwa na chakula chake
Nilikaa hapa mpaka mida ya jioni, ulikuwa ni wakati sasa wa kurudi kwa Mume wangu.
"Hii ni zawadi kwa ajili ya Manuu, usimuambie kama imetoka kwangu" Mama Fredo aliongea kwa nia njema kabisa nasema hivi kwa sababu macho yake ndio yalizungumza na maneno
Niliipokea kwa mikono miwili kisha ni kaingia kwenye gari langu.
Safari ya kwenda nyumbani ilianza, tamaa ya kumpigia simu Fredo ilinijia ghafla....cha ajabu simu yake iliita na kuita bila kupokelewa.
Niliachana naye huku nikiwa na hofu, nilipofika nyumbani niliuliza kuhusu Manuu na Fredo.
Jibu nililopatiwa lilinifanya nikimbie kuelekea bustanini na si kutembea.
Nilishangaa sana kuona wamekumbatiana, tena wote wakiwa wanalia.
Moyo wangu ulivunjika sana hasa baada kuona glass moja ya juisi ikiwa na mirija miwili....hii ni kumaanisha kwamba walikunywa kinywaji kimoja?? vipi je wamebadilishana mate??.......ni mtu na shemeji yake ila hii 🙌🙌........
Utamu kama huu si wa kukosa kabisa
Tukutane sehemu ya sita
🍭
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi