UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 08
SONGA NAYO.................
Mama mtu kuona nimesimama tu akaniongelesha kwa hasira "we mpuuzi mbona umesimama kama sanamu embu toa vitu kwenye gari haraka"
Niliitikia sawa na kufungua buti nikaanza kushusha mizigo wao wakaingia ndani ,,basi nikapeleka yote ndani kisha nikaenda sebleni ili niulize wanahitaji kinywaji gani .
Ajabu nikashangaa kuona Shuu anawaletea🤔 , sikutaka kusimama nikapita na kuingia jikoni dakika mbili nyingi akaja na kuniuliza .
"Ulikuwa na ratiba ya kupika nini leo?"
Nikajibu " wali na samaki "
"Hapana achana na samaki ,tutapika wali kuku alafu tutengeze na juice ya matunda"
🤔tu!!huyu kuingiwa na jini mpenda kazi au nini kimempata mbona anaanza kujishughulisha hivi🤨🤔.
Niliwaza na kuitikia sawa ,nikaona anafungua friza na kuanza kuchagua kuku mkubwa kuliko wote, alipompata akamtoa na kusema.
"Utaanza kuandaa viungo mapema na akiyeyuka tu niite, alafu kingine nisikuone ukijipitisha sebleni maana mnakuwaga kama wachawi😒."
Nikajibu sawa akaondoka ,nikabaki nawaza nipitie wapi ili niingie chumbani nikakunje nguo maana nishapewa onyo nisipite sebleni na hakuna sehemu nyingine ninayoweza kupita tofauti na sebleni.
Niliwaza mwisho nikaona eeeh nisiichoshe akili yangu embu nitulie mie ☺️, basi nikaka mda ulivyo sogea kidogo nikaanza kuandaa viungo.
Bibie heka heka kwake zikawa haziishi mara aje achukue tissue mara hiki mara kile yaani ikawa ni full mizunguko😁.
Basi bwana mda wa kupika ulifika nikamuita akaja ,hapo najua anakuja kupika yeye ajabu anafika anasimama pembeni🤨.
Nikamuuliza " utaanza kupika nini?"
Akajibu "nitaanza kupika nini ukimaanisha nini ,we pika hapo "
Eeeh hii kali ,sasa anakuja huku kujifanya anapika ili iweje kwa mfano 😒, niliwaza na kuanza kupika akawa na kazi ya kunambia kuwa makini usije kupika vibaya.
Nilipata hasira nikajikuta namjibu " we kwani shida yako nini kama unataka kizuri siushike chungu 😒"
Kujibiwa hivyo akachukia ila kuongea ndo akawa hawezi yaani akitaka kufoka anafoka kwa vitendo😁nikaona ahaaa nimeshaona huyu anataka huyo baba sijui kaka ajue kuwa yeye ndo kapika😁.
Sasa ngoja nicheze michezo ya kitoto 😊,nikaanza kujiongelesha hiki chakula cha leo sijui kama kitakuwa kizuri , akasema jitahidi kiwe kizuri.
Nikamwambia si hadi kiwe maana mikono imechoka na hivi vyakula vya kiswahili me hata sivijui ila haina shida mgeni mwenyewe anaonekana mtu poa sana .
Kusikia hivyo akaanza kujishughulisha kwanza akachukua juice akamimina glass mbili moja akanipa ,akawa anajaribu kunipigisha story ,naona alitaka kunifanya nisahau kama ananifanyiaga uduanzi. 😒
Nikawaza sijui nimfanyie ujinga nitoe vyakula vibaya ila nikaona hapana sio vizuri kucheza na chakula, basi nikapika kwa moyo safi kabisa.
Na kilipokuwa tayari ,akaenda kuoga mda huo wageni wake wakafika nikawapa vinywaji kisha na mimi nikaenda kuoga .
Sasa nilivyo maliza tu ile nataka nivae akaja na kunipa gauni na kunitaka niivae , nikapokea akaondoka nibaki naangalia hilo gauni alilonipa .
Jamani ilikuwa kubwa alafu rangi yake mbayaa 😐 nikataka nisivae ila nikaona haina haja ya kutibuana mtu usiku huu maana najua nisipovaa ataniletea maneno mengi.
Basi nikavaa kichwani nikafunga kitambaa changu safi na kwenda jikon, nikamkuta tayari kashaweka chakula kwenye mahotpot.
Si nikataka nipeleke dining wee nilirudishwa haraka na kuambiwa nikae jikoni humo humo , bila kubisha nikakaa akafanya kila kitu mwenyewe.
Na alivyo maliza watu wote wakasogea mezani ,nikasikia yule mwanaume ananiulizia Shuu akamjibu kuwa nimeshiba ,basi wakapakua chakula na kuanza kula .
Alvin alivyo na makusudi akaniita ,ile nimeitika tu Shuu akamuuliza "amepumzika vipi unataka nini nikuletee?"
Alvin akajibu " ningetaka uniletee nisinge muita " baada ya kumjibu vile akaniita tena ,nikainuka na kwenda kufika akanambia naomba uniletee glass nyingine hii rudisha"
Nikajibu sawa na kuchukua ile aliyotaka niirudishe kisha nikaenda kumletea nyingine, kufika nikampatia ,sasa ile nimegeuka niondoke yule mwanaume akaniita "Wardah"
Nikageuka na kuitikia "abee "
Akasema " kwanini tunakula wewe ukiwa umejificha unajua sio vizuri eeh??"
Nilitabasamu na kumjibu"samahani kama itakuwa ni kosa ila huwa nakula mapema sana"
"Ooh ni mambo ya diet, ila kuwa makini usije kupata shida "
"Sawa asante " nilijibu na kuondoka huku nyuma akabaki ananiangalia Shuu akamshtua kwa kumuuliza anakionaje chakula.
Basi waliendelea kula na baada ya kumaliza nikaenda kutoa vyombo, Shuu akanizuia kuwa atatoa mwenyewe mie ninani nikatae kusaidiwa😊
Bila kuongeza neno nikarudi jikoni na kutulia akatoa vyote na kusafisha meza alivyomaliza akaungana na wageni wake wakapiga story baadae mda ulivuo enda wakaaga kuondoka.
Sasa yule mwanaume si akaniita tena bhna , me nae nikainuka na kwenda kufika pale akanambia" me naondoka bhna nikaona si vyema niondoke bila kukuaga "
Nikatabasamu na kumwambia "Asante na karibu tena "
Akajibu " Asante na kabla sijaondoka naomba nikwambie kitu "
Shuu kusikia hivyo mishipa ya shingo ikamsimama nikaona ananiangalia kwa jicho Kali, me nikaishia kutabasamu tu sa ningefanyaje eti hata kama unge kuwa wewe ungefanyaje.
Hakuna chakufanya zaidi nikasubiri kuwambiwa hicho kitu , mwanaume yule akasema "una rangi nzuri sana itunze usije iharibu "
'"Asante " nilijibu akaondoka mimi nikarudi jikoni ,Shuu na mama yake wakamsindikiza hadi nje akaingia kwenye gari na kuondoka.
Sasa kitendo cha yule mwanaume kuondoka tu Shuu alikuja kuniwashia moto balaa , sikuwa na chakujibu zaidi ya kuinamisha kichwa chini .
Akafokaa wee alivyo choka akaondoka na mimi nikaingia chumbani kwangu na kulala, siku ikaisha ilipofika kesho yake jioni Aunt Vero nae akarudi .
Nikampokea mizigo na kupeleka chumbani kwake, kurudi sebleni nikakuta anaongea na boss mama shuu na maongezi yao yalikuwa ni kuhusu kazi zao.
Sikuwa na kitu cha kufanya nikae pale hivyo nikaenda zangu jikoni , mda ukaenda saa zikakatika siku hiyo nayo ikapita .
Sasa kesho yake mida ya jioni tukapokea ugeni wa mdada ,ambae nilikuja kufahamu kuwa ameletwa kwaajili ya kule kazini kwao maana binti aliekuwepo kaondoka.
Basi nilifanya majukumu yangu na baada ya chakula kila mtu akaingia chumbani kwake , sasa mimi kabla ya kulala nikakumbuka sijashusha pazia ya jikoni.
Hivyo nikatoka kwenda jikoni ,ile nafika karibu na chumba cha boss nikasikia wanaongea na kutaja jina langu ,nikawaza hawa watakuwa wanaongea nini.
Embu ngoja nisikilize usikute wananipangia mbinu za kuniangamiza maana sio kwa kunong'ona huku, bwana we nikajibana .
Aunt Vero akasema " hapana sidhani kama Wardah atafaa kwa kazi ile "
Boss akamjibu " kwanini asifae na kuliko apelekwe huyu bora aende Wardah maana huyu aliekuja hana muonekano hata kidogo.
Zaidi tukimpeleka tutapoteza wateja kitu ambacho sitaki kitokee "
"Kuhusu Wardah hapana ,we kama unaona huyu hafai basi arudi kwao tutatafuta mwingine "
"Arudi kwao na hela yangu ya nauli iishie chini ? Na kwanini unamkingia kifua Wardah kwasababu hii si mara ya kwanza nataka kumpeleka unakataa .
Kwani shida iko wapi ?"
"Shida ipo shoga angu Wardah bado ni mdogo na pia anaonekana amelelewa kwenye misingi ya dini sana hivyo ningeomba umuache tu"
"Mdogo , msingi ya dini? Yote hayo yanahusiana nini na mimi au yeye sio mwanamke? Maana tunachokitaka ni mtu mwanamke tena mwenye muonekano wa kuvutia kama alivyo yeye.
Sasa nashangaa unapinga ,we sikia kwanzia kesho nitaanza kutoka na Wardah, huyo aliekuja ndie atabaki na majukumu ya humu ndani basi "
"Kama umeamua haya ila mi naona angebaki tu "
"Abaki iliiweje bwana wewe ,yaani mtu anakila sifa ya kazi alafu abaki si ushamba huo ,embu nipishe nilale zangu mie"
Walimaliza kuongea haraka nikarudi chumbani kwangu kwa kunyata nikafika na kufunga mlango taratibu kisha nikaka kitandani, kichwani nikabaki najiuliza maswali watanaka kunipekea wapi.
Na hiyo kazi ni kazi gani ambayo huyo alieletwa haimfai ila mimi🤔, niliwaza mara mlango ukafunguliwa akaingia...........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi