UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 06
SONGA NAYO..................
Nilibaki namuangalia huku nikijiuliza ana maana gani kusema vile ?,🤔na nitakosaje amani eti kisa kutokuwa karibu yake 🤔na niukaribi gani anaoutaka kutoka kwangu na kwanini atake ukaribu na mimi?.🤔
Niliwaza sana mwisho nikageuka na kuendelea na kazi zangu, dakika zikakata nikamaliza kuandaa vitafunwa bila kupoteza mda nikaandaa meza na kuita wote waliokuwa chumbani .
Siku hii madam boss pamoja na aunt Vero walikuwa hawapo hivyo Shuu pamoja na rafiki zake wakasogea mezani Alvin nae hakuwa nyuma .
Sasa kwakua huwa siungani nao mezani nikapiga hatua kuelekea jikoni maana huko ndiko ninapopatiaga chakula, ila kabla sijafika Shuu akaniita nami bila kusita nikaitika na kurudi mezani.
Kufika akanambia " kwa hiyo unataka tujipakulie ?" Swali lake lilinifanya nikamuangalia usoni kwa mshangao sana, maana hakuna siku niliyowahi kufanya kitu kama hicho.
Nilitamani kumuuliza huenda labda anatania ila nikapotezea na kusema " samahani nilihisi mtapakua wenyewe " niliongea huku nikivuta chupa la chai na kumimina kwenye vikombe vyao.
Akabaki ananiangalia kwa jicho la hasira sana, me sikutaka hata kuongea au kufanya chochote kitakacho mpa nafasi ya kuongea ,zaidi niliwahudumia kisha nikauliza kama kuna lingine.
Wakajibu hapana nikageuka na kuondoka ,kufika jikoni nikamimina chai na kukaa chini nikaanza kunywa taratibu, sekunde zilisogea nikawa natazama chai na vitafunwa .
Nikajikuta nikizama kuwafikilia ndugu zangu ,ni siku zimepita sasa sijaongea nao sijui hali yao ikoje na sijui kama wanapata chakula kwa wakati 😪
Kwa mara nyingine niliangalia kikombe cha chai na kukumbuka namna mdogo wangu Shamsa anavyopenda chai ,nikatamani walau ningekuwa nae nikamuona namna anavyo kunywa huku akitabasamu 😪.
Lakini niko mbali na hata kama ningekuwa karibu sijui kama tungeipata maana maisha yetu ni duni sana 😪, niliendelea kunywa chai huku nikiwafikilia zaidi ndugu zangu.
Hadi pale nilipomaliza nikainuka na kufuta machozi kisha nikaenda kutoa vyombo, bila kuongea neno nilianza kukusanya sahani kwa pamoja kisha nikabeba ili nipeleke jikoni mara Shuu akaniita na kusema.
"Kwa mara nyingine kichwa kubwa unataka uwe unakumbushwa kila kitu, kwa hiyo watu tuinuke bila kunawa ili tuwe wachafu kama wewe?"
Nilisimama kwa sekunde kadhaa bila kugeuka , kinyonge nikageuka huku uso ukiwa unaangalia chini na kusema " samahani ngoja nipeleke hivi vyombo jikoni kwanza alafu nakuja ."
"We bwege nini,,kwa hiyo tukae kukusubiri wewe hadi upeleke hivyo vyombo kwamba huwezi kutunawisha ndo ukavipeleka au umeanza kuota pamembe.
Maana hamchelewagi, mkishaona mnaanza kung'aa tu kosa vichwa vinaanza kuwavimba embu rudisha kwako zako hapa utunawishe kwanza ,lione kubwa zima akili zero."
Bila kuongea neno nilirudi nikaweka vyombo mezani na kutaka kwenda jikoni kuchukua jagi pamoja na kibeseni kidogo kwaajili ya kuwanawisha .
Kwa sauti ya ukali Shuu akaniita " we mbwa wewe unaenda wapi😡 !?"
"Samahani naonda kuchukua jagi na beseni ili niwanawishe "
"Kwa hiyo unaenda jikoni na bado unarudisha hivi vyombo hapa kwamba tupige navyo picha ama ubongo wako umeingia maji?😡"
"Samahani 😔" niliongea na kuvichukua vile vyombo Kisha nikaingia jikoni huku nyuma akabaki anasema " yaani miwatu mingine kama mitahira ,eti linatuachia mivyombo michafu lione lilivyo kama nguruwe pori mfyuuu😏"
Alvin hali akiwa kimya aliinuka taratibu na kusogea lilipo sink la kunawia akanawa na kurudia simu yake mezani kisha akapiga hatua kuelekea kilipo chumba chake .
Kabla hajafika mbali Shuu akasema " eeeh uendelee kukaa kimya hivyo hivyo sio ujifanye baba mwenye nyumba kuingiliwa mambo ya kike "
Alvin aligeuka akamuangalia Shuu kwa sekunde kadhaa bila hata kuongea kitu akaondoka na kuingia chumbani kwake .
Mnyonge mie nilichukua maji na kwenda nikaanza kuwanawisha mmoja baada ya mwingine , nilivyo mfikia Shuu akanyoosha mikono huku akiniangalia usoni kwa jicho la dharau.
Bila kuongea neno nilizidi kuinamisha uso wangu chini ,taratibu nikamsogezea zaidi na kumiminia maji akawa ananiangalia tu bila hata kunawa .
Nikainua macho yangu na kumuangalia usoni akanambia " unaniangalia nini nisafishe kwa mikono yako na sio kunimwagia maji tu"
Bila kuongea niliweka chombo mezani nikashika mikono yake na kuanza kumuosha taratibu, akawa ananiangalia usoni huku akitabasamu 😔.
Sikuonesha kuchukia hata kidogo zaidi nikawa bize kufanya kile alichotaka na nilivyo maliza nikamfuta mikono vizuri kisha nikamuuliza " kuna kingine ambacho unahitaji nikufanyie!?"
Alitabasamu kwa dharau na kunambia "yeah kipo" aliongea huku akirudisha kiti nyuma na kusimama , nikahisi anataka kuondoka hivyo nikarudi nyuma kumpisha apite .
Ajabu alichukua maji machafu ambayo walishakwisha nawa akanimwagia nayo usoni na kunitupia kibeseni😔, niliinama chini na kukiokota akanikanyanga na mguu wake huku akisema.
" Nataka siku zote unapokuwa mbele yangu uwe hivi hivi unanielewa ??"
Nilishindwa kuzuia machozi ,nikajikuta nautazama ule mguu wake kwa sekunde kadhaa huku machozi yakinitoka , kwa sauti iliyojaa uchungu nikasema "sawa"
"Vizuri na kuna nguo chafu chumbani kwangu hakikisha unazifua na kuzikunja vizuri ,sasa jifanye chizi nirudi nikute hujafua uone nitakavyo ichakaza hiyo sura yako mbovu"
Aliongea na kutoa mguu wake kisha wakaondoka , sikuinuka nikabaki nimeshika chini vile vile macho yangu yakawa kuangalia namna anavyofurahia .
Moyoni nikasema iko siku haya machozi utakuja kuyarudisha, sijui itakuwa lini na nitafanyaje ila hii ni ahadi UTAJALIPIA .😡
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi